Shoto ni katibu siasa na uenezi Bw. M Katega akiwakabidhi katiba ya chama cha Mapinduzi viongozi wa tawi la South London Mwenyekiti Bw. Kassim Hassan na katikati mjumbe wa tawi hilo Bw. Seth Mdendemi
katibu siasa na uenezi Bw. M Katega akiwakabidhi katiba ya chama cha Mapinduzi viongozi wa tawi la East london Katibu wa tawi Bi Mariamu Mungula na Mjumbe Bw. Iddy Mwanga

kushoto Bw. Frank Mukiza, Kassim Hassan, Mariamu Mungula, M Katega, Seth Mdendeni na aliyekaa ni Pashency Linus
kutoka shoto ni Neema Kumba, mwandishi wa Tanzaniaone UK Bw. Ally Muhdin na Katibu wa tawi la East London Bi. Mariamu Mungula

Chama cha Mapinduzi CCM jana jumamosi ya tarehe 27 mwezi wa pili mwaka 2010 kilifungua mashina mawili na kuchagua viongozi wa kuongoza mashina hayo jijini London Uingereza. Mashina hayo yalifunguliwa na katibu siasa na uenezi Bw. Katega. Mashina yaliyofunguliwa ni sina la South London na Shina la East London.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Ndugu wangwana hapo tawi la ccm huko UK mimi ni mkereketwa wa ccm haoa ujerumani

    nilikuwa naomba simu kama kontakti za Bwana Seth Mdendemi na mimi ni mjumbe wa taiw la ccm hapa ujerumani naitwa Edward

    ReplyDelete
  2. Nawapa pongezi na kueleza mshikamano wetu na nyinyi. Hata hivyo sisi wana-CCM, ambao ni wanachama wa chama pekee Tanzania inaowaunganisha Watanzania wa makabila, rangi na dini zote, hatuna budi kukaza buti na kujipanga ili kutekeleza wajibu wetu wa kihistoria. (Yes we can accomplish our party's historic mission towards our country). Mwana-CCM Arusha.

    ReplyDelete
  3. Sasa nimeamini unaweza kumtoa mtu Ghetto lakini kuitoa Ghetto ndani ya mtu ni Kazi!!!!!

    ReplyDelete
  4. Kidumu chama cha mapinduzi!
    tunaomba muje mfungue matawi na huku Liverpool,au mtuambie tufanyeje ili tuweze kufungua.

    ReplyDelete
  5. Hongera Mariam Mungula nakumbuka wewe ndio muasisi wa CCM UK, mkiwa wewe,Mr.Maajar,Said John,Juma Pinto,Mzee Mpopo.

    ReplyDelete
  6. Aisee watu hawana aibu aisee... Duh!!!

    ReplyDelete
  7. Mzizi wa noma watu washaukata.

    ReplyDelete
  8. Kweli uogope sana ufisadi, yaani umepenyeza mpaka ulaya????? Nasisi pamoja na shule zetu na xposure zetu tumekubali watanzania wenzetu wafe masikini....

    may be its about time to rethink deeper, this time even deeper

    ReplyDelete
  9. Wewe Anon wa 08:03:00 p.m. (1) Huna exposure yoyote ya nchi nyingine za kiafrika. (2) Ukiondoa watu wachache sana, wengi wa hao viongozi wa upinzani ndio mafisadi wakubwa sana, both waliojitajirisha serikalini na nje ya serikali. (3)Toeni constructive suggestions za kuiendeleza nchi badala ya kutukana ovyo. Mtu yeyote anaweza kutukana, ulimi hauna mfupa. CCM tunajizuia kutukana na hatutaki kujifanya eti ni wajuaji kwa sababu uungwana wetu si matusi wala si fujo. (4)Eti ooh, we need to rethink deeper...toa thoughts zako zenye kichwa na miguu. Hatutaki hollow sound bites. Sisi Wana CCM tuyafanyie kazi mapungufu yetu na kuimarisha umoja wetu. Na wapinzani pia mfanye hivyo hivyo bila arrogance yoyote. Mdau wa CCM kiboroloni, Moshi.

    ReplyDelete
  10. ama kweli wabongo nuksi!!!! yani hata mkiwa UK mnafikiria ufisadi??? sasa CCM na UK wapi na wapi? jamani siasa zingeachwa zifanyike bongo huku ulaya pigeni boksi...kha

    ReplyDelete
  11. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

    JAMANI NAOMBENI KONTAKT ZA SETH MDENDEMI .. EMAIL YANGU NI : rlimited@ymail.com

    AKSANTENI SANA

    EDWARD

    ReplyDelete
  12. Watanzania tunachekesha kweli. Ukiwa ndani ya nchi..CCM...ukiwa nje ya nchi... CCM. Watanzania hawana jipya. Siajabu Manyoya sasa yakahamia huku huku ulaya!!!! To heck with Power, give me Freedom!

    ReplyDelete
  13. michuzi wacha kubania,waeleze hawa wanaojiita wakereketwa kuwa chama kinafungua matawi nje ya nchi pale tu nchi ikiwa haina demokrasia na kuzuiliwa kisiasa kuendeleza kazi za chama ndani ya nchi.sasa nyinyi ccm ndio wenye serikali mnafanya shughuli zenu ndani ya tanzania bila tatizo lolote nini mnafungua matawi nje ya nchi,na kama ccm inaongoza vizu
    ri kwanini hamrudi nyumbani acheni kudanganya watu.
    mnasapoti ufisadi tu ,mkae mkijua kila kitu kina mwisho

    ReplyDelete
  14. Duh shamba la bibi tambalare kabisa. USA utapumulia wapi kupata nafasi ya kufurukuta CCM zaidi ya Republican na Democratic?

    ReplyDelete
  15. Wewe anon Sun Feb 28, 10:01:00 PM, kwanza nimefurahi kwamba umeguswa ukaamua kujibu. Vya bule vinauma ahhh...

    Sasa ngojea nikueleze "Mdau wa CCM kiboroloni"; kitu cha kwanza vijana walio wengi Ulaya wanajiunga na CCM si kwasababu wanaipenda bali kwasababu wanatafuta sehemu ya kukimbilia wakirudi TZ. Basically their brain isn't creative at all, dead.

    Unasema CCM "mnajizuia kutukana" what u mean...kuna matusi yanayozidi ufisadi, wizi??? Basically, unapoona picha za watoto wanatafuta chakula kwenye dampo la uchafu Dar au Moshi, hayo ndo matusi ya CCM. Unapoona asilimia 18 tu ndo wanafaulu form four na asilimia 72 wanapoteza ndoto zao maisha, basi hayo ndo matusi ya CCM. CCM imetutukana, imetuibia na sasa imetupumbaza, obviously imekumpaza zaidi wewe.

    Eti unataka "constructive ideas" how u gonna distinguish btn contructive and destructive if you don't know the difference btn right and wrong??
    Mdau get a life man..vya bule vinauma.

    Talk about how to challenge the status quo and not support something that isn't working...

    ReplyDelete
  16. Mkiwa nje ya nchi na eposure mliyopata mna mikakati gani kuwashari CCM wenzenu hapa nyumbani kutawala nchi kwa misingi bora kama mnayoiona huko ili angalau nasi tupate mabadiliko. Tuache unafiki je utawala wa CCM na maendeleo ya nchi mnauonaje ulinganisha na nchi mlizoko?

    ReplyDelete
  17. Anon 08:53:00, Ni vizuri kuwa wewe pia umetoa maoni yako na ndani yake kuna ambayo yako valid. Ninachokisema ni kuwa si sawa kuwatukana watu ambao hukubaliani nao. Wapinzani watoe ilani zinazoeleweka badala ya kutukana tu. Mwaka huu kuna uchaguzi, itakuwa vizuri mkinadi sera zenu hadharani kidemokrasia. Msimamo wangu ni ule ule : I cannot trust most of the so-called opposition leaders because I know many of them too much. Na CCM ndicho chama pekee kinachotuunganisha Watanzania wote. Mwana CCM Kiboroloni.

    ReplyDelete
  18. Mimi sina mengi ila ndugu zangu mshika mawili moja umponyoka. Amua moja Siasa --->> Rudi BONGO ama BOX --->> Jilipue kaa ULAYA. Hakuna yote hapa, mtafulia kote kote Shauri zenu.

    MDAU OBSERVER

    ReplyDelete
  19. poleni sana wana UK haya ndio madhala makubwa ya mtu wa masterz ametoka bongo kwenda ulaya kutafuta elimu hili arudi kudaoidia nduguze matokeo yake anamaliza chuo vizuri kufanya kazi za ajabux2, wenyewe wanaitata kubeba mabox mi najua kazi zao hasa ni kuosha wazee wzito wanaosubiri kufa,kufagia mitaro,kuchunga vichaa nk matokeo yake wanaona ni kzi za maana kweli mpaka akili inakuwa domnant wanashindwa kufikiria na kuamua mambo ya maisha yako wanakazana tu kufungua matawi yasiyopiga kula za kumchagua kiongozi wowote baadae wanataka urai wa nchi mbili
    this is tanzania youth?
    km munauchungu na CCM tafuteni hizo degree murudi kuendeleza nchi yenu

    ReplyDelete
  20. Kwa kweli matawi ya CCM huku nje yatasaidia sana wakati wa uraia wa nchi mbili. sisi wana CCM tutasaidia sana chaguzi za huko nyumbani na pia tuta organize michongo mbalimbali ya pesa. Kuingiza na kutoa pesa nchini. Kidumu chama cha Mapinduzi

    ReplyDelete
  21. mdau wa kiboroloni acha comments zako, CCM na wachaga wapi na wapi wewe, WACHAGA WALIENDELELEA HATA KABLA CCM HAIJAFIKIRIA KUZALIWA, MAZAO YETU KAMA KAHAWA TULIKUWA TUNAPATA DAWA ZAKE BURE, KILIMANJARO ILISTAWI SANA BILA CCM, SASA DAWA ZA KAHAWA ZIMEIBIWA NA SIASA ZENU, KAMA ASILI YAKO SIO MGOMBANI NA UNATUMIA JINA LA KIBOROLONI ACHA KABISA, TUNAHITAJI DAWA ZA KAHAWA NA SIO CCM.TULIA HUKO WEWE.

    ReplyDelete
  22. Mzee Misupu.Naomba umpe salamu zangu mdau Panshency.

    Panshency mimi Baraka tulikuwa tunapiga mzigo wote Kings College Hospital kwa Wajam mitaa ya Camberwell enzi hizo za early 2000.

    Nigongee hapa 075 1909 7330.

    ReplyDelete
  23. We anon wa Mon Mar 01, 10:24:00 AM, nimekupata vizuri. Katika maelezo yangu sijasema kwamba nasupport kambi ya upinzani kwasababu wote ni wavuta bangi...

    Tatizo langu ni kwamba sisi watu walioko nje nilihisi tutakuwa mwanga kwa wale waliobaki nyumbani...Ila wote tunapokimbilia CCM, of which we know is rotten with ufisadi then tunahalalisha wizi na matokeo yake hatuwezi kuendelea.

    Hata kama CCM ina watu wa maana kuliko upinzani, hawawezi kufanya chochote kwani ni sawa mwanasiasa mwenye akili sana lakini kazaliwa Cuba...usitegemee afanye chochote cha maana

    u can take this to the bank: unless CCM igawanyike vinginevyo maendeleo hayawezekani..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...