Mshambuliaji wa timu ya FC Lupopo ya DRC, Ntombo Lutete akiipangua ngome ya Yanga katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar leo. Kushoto ni Wisdom Dhlovu na Geofrey Bonny. FC Lupopo ilishinda bao 3-2
FC Lupopo wakishangilia ushindi wao wa 3-2 dhidi ya Yanga leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Congo wapo juu kimpira kuliko tanzania mimi nadhani ifike wakati mfumo wa ligi ubadilishwe na makombe ya FA na taifa cup yarudishe ninaposema mfumo wa ligi ubadilishwe nataka ligi iwe na timu kuanzia 16 mpaka 20 ligi ya sasa hv timu ni 12 tu na haina ushindani kabisa kwa sababu mkoa wa dar tu unatimu 6 na tanzania ina mikoa 21 bara na 5 visiwani so kuna vipaji vya baadhi ya mikoa tunashindwa kuviona pia hata serikali irudishe michezo ya UMISAVUTA,UMISETA na UMITASHUMTA yaani tunaomba mambo yarudi tu kama zamani tulipokuwa tunaona timu kama RTC kigoma,Reli ya morogoro,bandari mtwara.mecco na tukuyu stars mbeya,kariakoo ya lindi,ujenzi rukwa,lipuli ya iringa,CDA ya dodoma,mirambo ya Tabora ,coastal union na african sport za tanga,TAMCO ya kibaha,majimaji ya songea,kariakoo ya njombe na wachezaji kama kina juma mgunda,razack yusuph careka,juma mgunda,peter tino,sikinde mbunga,lunyamila,edifonce amlima,said sued scud,sanifu razaro,george masatu,fumo felisian na kadharika yaani tanza nia enzi za mwanakatwe mwenyekiti wa FAT na chini ya utawala wa mzee ruksa mambo yalikuwa tambarare sana upande wa michezo ila kwa sasa hata akaja kocha toka ulaya kama viongozi wetu hawabadiliki soka la tanzania litazidi kuteketea tu!!!

    ReplyDelete
  2. MDAU WA ELIMUFebruary 13, 2010

    Giza limetanda mbele hatuoni!kweli Yanga Daima?napata wasiwasi!!!!!

    ReplyDelete
  3. CONGO WANAVITA VYA HAPA NA PALE LAKINI "MPUTU" TP MAZEMBE WAKO JUU. WATANZANIA TUNAPENDA {SHOO KUPITA KIASI}.

    ReplyDelete
  4. haya sasa mlaumuni Maximo,siku zote mkiambiwa football ni lazima iwepo ktk clubs kwanza ndio timu ya taifa itakuwa na uhai mnakataa haya sasa,bora hata Miembeni ya zenji wame-droo tena na wa-misri

    ReplyDelete
  5. Hao jamaa wamepiga magoti wanashukuru support ya ushangiliaji toka kwa washabiki wa Simba. Madega alishatangaza rasmi kwamba Yanga na Simba sio ndugu kimpira hivyo maana yake alishatangaza uadui na Simba.Ilikuaje waliomba washabiki wote waishangilie Yanga bila kujali itikadi za kitimu? Na vipi waliposawazisha kwanini waliikebehi Simba? Poleni wana Yanga ila mlizidi kidomodomo

    ReplyDelete
  6. kipa wa congo ni Fally Ipupa? naona amewafunga goli moja, kwi kwi kwi, poleni Yanga, tatizo hamtaki kumsikiliza sangoma wenu.

    ReplyDelete
  7. Yanga wamePOPOlewa? Wameingiliwa na POPObawa? Noma sana.
    Naungana na mdau anayesema mlaumuni Maximo.

    ReplyDelete
  8. Makamba, DodomaFebruary 14, 2010

    aAh!!! Jamani Yanga mbona mmejilegeza kupita kiasi?? Haya jitayarisheni kupokea kipigo kingine kwenye mechi ya marudiano wiki mbili zijazo.

    ReplyDelete
  9. Tatizo la kandambili ni maneno meeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeengi mpira hakuna. Wakishashinda ligi ya mchangani wanajiona wamefika. Yako wapi sasa? Na bado wakienda huko Lubumbashi lazima watapigwa si chini ya nne. Tulieni mhangaikie nafasi ya pili ambayo nayo ni bahati kuipata.

    ReplyDelete
  10. Kitu cha kushangaza ktk Tanzania kuna mikoa haina timu sasa huo mpira wa maana wenye ushindani uko wapi?

    Nakumbuka zamani kila mkoa karibu kulikuwa na timu lakini leo wakuu wa mikoa hawana wazo kabisa la kuhamasisha maendeleo ya michezo ktk mikoa yao

    Jk una kazi kubwa.

    ReplyDelete
  11. Mnaolaumu uchache wa timu kwenye Ligi si mnajua tatizo siku hizi kila kitu hutegemea udhamini? Sasa kuongeza idadi ya timu kama mtakumbuka ndicho kilichowafukizisha Safari lager that time(kumbukumbu yangu inaniambia hivyo)
    Ni kweli timu zipo chache sana na hata zilizopo zote zinalilia kucheza Dar es Salaam kama Mtibwa Moro na JKT Ruvu na kufanya jumla ya timu kuwa 6 toka Dar pekee. Udhamini wandugu

    ReplyDelete
  12. Mnategemea bingwa wa ligi Tanzania acheze jumla ya mechi 13 kwa mwaka na kutangazwa bingwa, apambane na mabingwa wa nchi zingine waliopata ubingwa baada ya mechi 40 ya ligi ya kwao?

    Ipo haja kuongeza ushindani ligi ya Tanzania iwe angalau timu 20. Pia kuboresha timu ktk usajili na kulea vipaji bora.

    Mdau
    Bendera

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...