Youtube na mtandao:
Tanzania is more than bongo flava......
Habari ya kazi Ankal,
Habari ya kazi Ankal,
Naomba lau nafasi nipate kuwakilisha mawazo yangu kupitia tovuti ya jamii. Nilikuwa naperuzi peruzi ndani ya youtube na nikagundua kuwa unapofanya search ya tanzania kikubwa utakachopata katika youtube ni bongo flavas na video za watu binafsi ambazo zinahusiana na utalii,nikimaanisha kuwa watu katika kutembelea kwao mbuga za wanyama basi walichukua baadhi ya video na kuziweka katika youtube.
Yaani hakuna official videos zozote ambazo kwa kweli zinatuonyesha kuwa watu serious.hata ukisearch kikwete unachopata ni videos ambazo zimewekwa na watu wa nje na sio watanzania hasa anapokuwa kwenye mikutano ya kimataifa.
Its really a shame kwamba katika kipindi hiki ambapo tunajidai kuwa tunataka kuwa mstari wa mbele kwenye utalii tunashindwa kutumia nafasi hii ya kujitangaza kwa bure kabisa kwa kutumia njia ambayo ni rahisi na ya bure kama mtandao wa youtube.
Idara ya utalii wangeweza kutumia njia hii kwa kujinufaisha na kufikia watu wengi dunia nzima,kwani kama tunavyojua kwa dunia ya sasa kitu cha kwanza mtu anachofanya anaposikia kitu ni kwenda kugoogle,badala ya kupoteza mamilioni ya fedha kwenda kutangaza nchi kupitia kwenye mabasi ya London tumeshindwa kuweka official video ya promotion ya nchi mtandaoni hasa katika youtube amabayo tunajua kuwa mamilioni ya watu wanatembelea kila siku.
Tulichoishia kufanya ni bongo flavas tu.i mean dont get me wrong,i love bongo flava,but we're more than that.kwa wenzetu wakenya unaweza kufuatilaia habari zakila siku zinazorushwa na vituo vya televisoin kwa kutembelea youtube kwani karibu vituo vyote vya tv vya Kenya vina ukurasa wao hapa na kila siku wanaweka video za habari zao kila siku.huwezi kupata hata habari moja si ya ITV wala TBC au kituo chochote cha Bongo mtandaoni,tumebaki kulala tu
its time that we wake up.......
Naomba kuwakilisha..
Mdau Ugiriki
its time that we wake up.......
Naomba kuwakilisha..
Mdau Ugiriki


shida ni kuwa wewe unataka kila kitu kiende kwa mtazamo wako na vinginevyo basi unaona kuna tatizo. Jaribu kuwa na mtazamo ulio mpana zaidi wa kuelewa mambo
ReplyDeletesamahani lakini ukweli ndio huo
nawasilisha
Unashangaa hilo hebu fungua website ya ubalozi wa Tanzania USA, unadai Zouk na Ndombolo ni ngoma zetu za asili, and thats a goverment site
ReplyDeleteMdau Ugiriki nimekubaliana na wewe 100%, kwa kweli inasikitisha, naomba vyombo husika waliangalie hili jambo kwani sidhani kwamba itakuwa vigumu kumpa kijana mmoja kazi ya kuweka hizi video's amabazo tayari ziko hewani kwenye youtube and social networking sites kama facebook. It's easy and straightforward, theses sites are free, lets make use of them.
ReplyDeleteNasupport maoni ya mwenzetu wa Ugiriki 100%. Tz always wana- dragg miguu katika many things. si utalii tu. Hakuna hata state house website. Ni vigumu kweli kusaka information za TZ katika mitandao.
ReplyDeleteNdo hivo "mchelea mwana kulia utamkuta si wako". waache wangine wasonge mbele kisha sisi tuna-desa tu, Kama uonavyo wanamziki "wa kizazi kipya" wanavyo-desa kutoka kwa wamarekani weusi.
kwanini wewe usiwe unapost?
ReplyDeletewatz wengi wanachukulia internet kama anasa na sehemu ya kujaza upuuzi, mfano social networks nyingi utakuta wabongo wameweka majina ya ajabu ajabu tuu na picha za wanamuziki wa marekani au picha za ngono, mfano mtu anajiita john cena, t.i, 50cent nk..mimi huwa ninajudge kwa kuangalia jina na picha sina muda wakupoteza kuchat na watu wanamna hii
au mfano mwingine angalia eastafricantube.com yaani ni danguro.. akina mapuka na wenzake 85% ya contents ni ngono na video za kutikisa makalio makubwa, hata ukiangalia frquenty watched videos ni hizo za akina mapuka. AIBU TUBADILIKE WATANZANIA.
Unachosema ni kweli, lakini watanzania tunachonga sana... yaani sana tu...Wewe mwenyewe umeshafanya nini kama mfano?? Ufinyu wa namna ya kusearch kwako ndio kunakufanya uone hakuna kitu kingine zaidi ya Bongo flava, ndio umejua leo kutumia youtube?? naomba nikwambie kuna mengi kuhusu Tanzania kwenye youtube kuliko uliyoyaona. Almost national parks zote zipo ndani ya Youtube. Hata kama hizo video ulizoziona zimewekwa na wadau wa nje, yes nao ni part ya jamii yetu, wewe unataka video za Tanzania au unataka video zilizowekwa na watanzania walioko Tanzania??...Mdomo mpana kuongea mikono mifupi kiutendaji..
ReplyDeletekuna documentary ya andrew young kuhusu tanzania inaitwa TANZANIA THE STORY OF LIFE, tutaipataje tuliokuwa europe naona inapatikana marekani tu ukitaka kununua online.serikali ijaribu kuongea na waandaji waiweke japo amazon tuweze kununua
ReplyDeletewabongo kazi yao ni siasa za kuzima kashfa za rushwa tu, hakuna kitu cha maendeleo.
ReplyDeleteMdau ni kweli hata mm nilishaliona hilo,ila si siri tupo nyuma kwa mambo mengi sana!real we have to change.coutly
ReplyDeleteMjomba unaelalamika a2na ata video moja ya utalii youtube. Mi nadhani wewe uko biz ktk mitandao 2. Unaangalia Tv kweli? CNN ya USA kuna clip ya Utalii inaonyeshwa kila cku, TZ mambo makubwa wewe, yuotube aende nani. 100% ya wa2 wakisearch ki2 kwanza wanaenda yahoo, google na nk. sio youtube. Angalia tv sana utaona tangazo la Tz. Tena nikiwaga na msela wangu 2naangalia newz on CNN wanasema msela huyo ndo kwao, clip inaonyesha wanyama na kisiwa kizuri cha ZNZ, majamaa mpaka leo wanaplani watimbe bongo sababu ya hiyo clip. Si mwingine mdau from Kigogo
ReplyDeleteNi kweli Mdau wa Ugiriki.Makampuni ya kitanzania wanaweza kutengeneza video clips za ubora wa juu na kuitangaza Tanzania
ReplyDeleteClip za usafiri za Azam Marine DSM to ZNB, TAZARA, PecisionAir, Coaches(Buses), Reli ya Kati, Viwanda vya bidhaa, Biashara za malori ya usafiri SuperDoll, Wakulima wakubwa, Viwanja vya Ndege,BANDARI n.k n.k zingekuza muonekano wa maendeleo yaliyofikiwa na Tanzania ktk YouTube.
Mimi au Mdau wa Ugiriki na vikamera vyetu havitakidhi zana ya kutoa clip bora kutangaza maendeleo ya Tanzania yaliyofikiwa sasa hivi.
Naamini kampuni kama NAHOZA media ya hapo Tanzania inaweza kufanya kazi bora kwa kutumia uzoefu wa kutengeneza filamu wakatoa clips bora za video kuhusu shughuli za huduma, biashara, usafiri wa anga, majini na barabara n.k na gharama zitakuwa ndogo kuliko za CNN, MSBN, BBCworld n.k
Mdau
Jijini London
mdau wa kwanza naona umefilisika..hoja ya huyu bwana ni kweli na amevipa changamoto vyombo vikubwa vya habari na wengine walioko katika fani hizo kutransfer habari zao kuziweka hapo ili watu wengine ambao wanataka kuijua nchi yetu wazione kwa urahisi kisichoeleweka hapo nini???!!!
ReplyDeleteuwezo wako wa kuelewa ni mdogo, unapo search site kama youtube results zake hutolewa kwa number of views. so ukisearch neno tanzania haispecify ni kitu gani unasearch kuhusu TZ.so youtube itakupa the most popular video searches about TZ, and that happens to be bongoflava.
ReplyDeleteMmiliki wa youtube ni mbongo?
ReplyDeleteMchizi naona unaiabuse YouTube, unasechi bongo flava halafu unalalama hauoni kitu kingine!
ReplyDeleteKama unataka video za utalii serch utalii, Kama unataka video za serikali, dalala za bongo, mamodel na mamiss, bunge, kanumba, hata kesi ya Muro imo kwenye yotube.
Nadhani unachoitaji ni elimu tu namna ya kuserch. Au labda pengine upo kwenye slow dial up connection browser zinachukua forever kufunguka basi ulichoona ni bongo flava tu kabla hujagiveup.
Na mwanakoment unayelalamika kuwa matako ya akina dada yanatikisika ndio vimejaa youtube-umejuaje Kama wewe mwenyewe hupendi kuangalia! Wenzako wanaburudika na hizo shows tafadhali peleka interest zako mahala pake. Kwani cha kuitangaza nchi ni wanyama tu!
Ali kiba anaitangaza nchi kupitia hiyo hiyo bongo flava, sasa yuko viwanja anakula mkwanja. Akiwa bongo anawalipa mafundi wajenzi wa nyumba yake pale mbezi, pesa ya nje inaingia kwenye mzunguko wa uchumi wetu bongo.
Anyway achaniishie hapa
Nakushauri
Nakubaliana Na Mdau Wa Ugiriki Kwa asilimia 100%.Watanzania Tubadilike,Tunashindwa hata kutumia Facebook na Twitter kuitangaza nnchi, hatukatai kuhusu kutangaza kupitia Vituo Kama CNN, ila Kwa nini Tusitangaze na kwenye Youtube pia..After all ni Free..mimi nadhani vitengo vimekaliwa na wazee wenye mawzo mgando.Hizi ni Zama Mpya, tunahitajika Vijana Tutoe changamoto..Online Marketing..Kitu 360 ..Haya Kwenye Nyimbo Ya Akon na Keri Hilson inayoitwa Oh Africa..Kuna mtu kajipaka bendera ya Tanzania(Let us Capitalize on it)
ReplyDeleteHuyu Mdau Ugiriki ni Zoba kabisa. Yaani analalamikia Youtube na kwingineko hakuna video nzuri za Kibongo...Sasa anamlalamikia nani?! Kama wewe ni mtanzania halisi kwa nini usiweke basi hizo video ambazo unaona zinafaa. unalalamika unataka nani aweke??!! Youtube, facebook, Twitter, nk ni za kila mtu tena wewe huko Uliko una nafasi kubwa zaidi ya ya mtandao maana uko kila mahali sasa unalalamikia wamatumbi wenzako tulieko Tandahimba.....Mbusi mkubwa wee Tenda mwenyewe usingoje kutendewa????
ReplyDeleteBora hata hauko Tanzania maana ungekuwepo ungezidi kuturudisha nyuma......AMA KWELI NYANI HAONI.....!!
Mzawa
kabla ya kuposti habari yako jiulize je ni watanzania wangapi wanauwezo wa kumiliki hizo camera?Je ni watanzania wangapi wanatembelea sehemu za utalii?.wewe mwenyewe kabala hujawa mkimbizi ulikua na tabia ya kutembelea vivutio mbali mbali tanzania?..bongo fleva ni nyingi kwa kwakua video ambazo zimesharekodiwa na watu wanazitoa kwenye sites tofauti.Mimi nadhani watanzania wengi wanapenda kuweka picha na video za sehemu mbali mbali lakini tatizo uwezo wengi hawana.
ReplyDeleteWote mmetoa mawazo mazuri na mna imani na uchungu wa nchi yeni lakini mundishi wa Topic hii lazima aelewe kwamba sio kila kitu anataka afanyiwe ,
ReplyDeleteHivi yeye hajawahi kwenda kwenye mbuga za wanyama (Utalii ) na kwanini asichukue hizo Video na kuzipost mwenyewe kwenye You Tube
Tanzania inakuwa kila siku ,kitu ambacho hakijafanyika usingoje mwine afanye ," Wewe pia ni Mtanzania, post them videos pls
Wabongo hebu acheni ulimbukeni, jamaa wa ugiriki yoko right kabisa. Watanzania tuko nyuma sana kujitangaza. Ndio kuna website za utalii lakini hiyo ni sehemu moja tu. unapo dhamiria kujitangaza unatakiwa uweke matangazo yako sehemu ambayo watu watayaona. kuna watu ambao hawakuwa wameplan kuja tanzania, hawataweza kutafuta tovuti ya utalii ili waweze kuja,ila kwenye youtube wakiiona then wanaweza kubadilisha mawazo na kuja. kuhusu cnn, hiyo ni tv ya marekani inaonekana marekani tu na baadhi ya nchi tu. ila unapo weka online dunia nzima itaona.
ReplyDeletekitoroli
Mtoa maada ni muhimu ila hajui kueleza,Usiseme official video ziwekwe na wenyewe,ok Naomba kumuliza je nyinyi watanzania ugiriki hamna website yenu?Je nini zaidi mlichoweka kuh:nchi yenu,website za wenzetu zote ukifungua unaanza kuona historia ya tanzania japo kwa kifupi,sasa kama mtu hajui nini tanzania atajuaje kama ni nchi au jina tu,ok nimesearch You tube GREECE nikakuta following results: That
ReplyDelete1.That is Greece !
video by liondani,
2.Macedonia is Greece,by makedoniatruth
3.monty python footbal by meskalino
NIKASEARCH
NIKACHEKI UK
1.ferari 450 by autocar
2.Manian by zoolandmusic
3.UK BEST FREE by Captain Rabb
NIkasearch Tanzania
1.Serengeti national park by timsmithdv
2.Lion vs Hyena by the tanzaniaOdysssey
Tanzanian albino by theindependent
HAPO NIMEKUTA RESULT BORA NI ZA TANZANIA KWANI IMEANZA NA UTALII IJAPOKUA NI WATU BINAFSI NA SIJAKUTA HATA OFFICIAL VIDEO KWA HIZO NCHI ZA WAZUNGU PIA NI WATU BINAFSI
WALA SIJAKUTA BONGO FLAVA PIA KAMA ULIVOSEMA sasa ukisikia internet sio unavotaka wewe tu ikutii andika TANZANIA+UTALI AU TANZANIA+TOURISM basi itakupa na ndio inavotakiwa kwani ukiandika TANZANIA TU kuna mambo mengi sasa itakupa option gani NENDA SHULE NDUGU YANGU,ACHA UONGO
http://tembeatz.blogspot.com/
ReplyDeleteNenda ukaone moja ya initiatives za wachache.
Ni kweli hata mimi namuunga mkono huyu jamaa na maelezo yake ni kweli tunahitaji kuonyesha utalii na utamaduni wetu kama vile ngoma za kiasili nafikiri watu wengi watafurahia sana kuona utamaduni wa nchi yetu.Maana sehemu zingine zinajivunia sana na maadili ya nchi zao.
ReplyDelete