Ankal, na mimi ningependa kutoa dukuduku langu kama ifuatavyo kuhusu hii kitu 'Syrian Exhibition'

Hawa jamaa wanaotoa vibali kwa Exhibition wanajua tafsiri ya Exhibition? Naomba waende kwenye kamusi ya bure katika tovuti ya Wikipedia waangalie 'Commercial Exhibitions' ina maana gani, ili wajue nini maana ya Exhibition. Kwanza hawa wa Syria inaelekea hawalipi kodi, pili wanauza bidhaa za China na Dubai na kusema zimetengenzwa Syria. Pia bidhaa wanazouza ni hafifu sana na hazileti thamani yeyote katika kujenga uchumi wa nchi yetu zaidi ya kuwanufaisha raia wa nchi zao tena binafsi.

WaTanzania wanaoajiriwa kuuza katika booth zao hulipwa pesa ndogo sana kulingana na manufaa wanayoyapata. Tuseme Syria ndio bidhaa hizo za nguo, viatu na urembo tu wanazotengeneza? Na iweje Exhibition ifanyike kila baada ya mwezi mmoja? Hii ni Tanzania yetu tu mimi naona. Hivi kule kwao wanaruhusu kutoa vibali kutangaza mitaani kama wanavyofanya kuwaibia watu? Hiyo biashara wanayofanya sio Exhibition ni biashara za wamachinga wa hapa kwetu.

Naomba waondoke wawaachie vijana wafanye biashara hizo wao walete bidhaa zao wakati wa Sabasaba trade fair. Nakuambia kweli watu wanalubuniwa na kuuziwa bidhaa zao kwa bei ghali mno! Ingekuwa bora wauze bei poa kwa kuwa hawalipi kodi.

Naomba anayehusika katika kutoa kibali cha hawa jamaa atoe kwa kuzingatia haya na pia hiyo wanayoitwa wao Exhition itafutiwe jina jingine, either "Syrian Wamachinga Show" na ifanyike mara moja au mbili kwa mwaka, sio kila mwezi. Maana yake nini hasa? Na India wafanye hivyo, na Turkey wapewe kibali pia, na South Africa nao wapewe kibali, tutafika kweli?

Nawasilisha
Mdau Millenium Tower

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Si kweli kwamba eti wanafanya exhibition hiyo kila mwezi: ni mara moja kwa mwaka. Mbona mimi nimekwenda huko sikuona vitu made in China? Wewe sema tu una chuki zako za binafsi unazizijua, halafu unajitia kutoa hoja uchwara za uongo. Inadhihirisha kuwa chuki ni adui mkubwa wa ukweli. Doto Kasanga.

    ReplyDelete
  2. Mdau wa Millenium Towers pole najua inaweza ikawa ni ushindani wa biashara, hizo bidhaa za China zimejaa kibao hata nisiponunua kwa wa Syria nitazikuta Kariakoo. Kwahio kununua bihdaa za wa Syria ni kuchagua tu sio lazima kwa kweli, mimi ni mteja wao mkubwa na sitegemei kama nitarudi nyuma una vitu ambavyo hata nikitembea Kariakoo mwezi mzima sitavipata kwahio naona anaevutiwa kwenda kwenye maonyesho aende tu kwa sababu sio lazima kununua bidhaa zao wala kwenda. Perfume zao yaani ni nzuri saaana. Biashara ushindani jamani tusianze kupakaza vitu vibaya, wachina mbona wamejaa Kariakoo hatuwafukuzi C'mon.

    ReplyDelete
  3. Mkuu umeandika ukweli kabisa! Nakuunga mkono! Na wala siyo protectionism ila ni kupigania haki ya soko la usawa na uhuru (free and fair trade) ambapo siyo mmoja anatumia mamlaka ya nchi kuuza bidhaa zake wakati mwingine anatumia jasho lake. Chonde chonde viongozi wetu, msiigeuza Tanzania jalala jamani. Wekeni utu wenu mbele kabla hamjakaribisha watu.
    Mdau
    Japan

    ReplyDelete
  4. hivi watanzania mbona lazima tulalamike ktk kila kitu? hivi kuna ubaya gani wakiwa wanauza kila mwezi, hata kama bidhaa ni hafifu... bora hawa waliyokuwa sehemu moja ama hao wamachinga wako. hii ni chuki tu... na pia kwanini michuzi anapost hizi habari za chuki ... mimi huwa nakuja hapa kupata habari za nyumbani badala yake sometimes naona habari zisizo na maana kama hizi au basidei ya kuzaliwa au harusi mtu... wat the hell

    ReplyDelete
  5. chuki binafsi hio, mimi nakataa kubaliana na wazo lako kabisa,tanzania ina karibisha kila nchi kufanya biasha ni ujanja wa mtu tu, hataka kama wanunua kariako ni akatika kutafuta maisha bora ya kila binadamu, nini ujanja ,wacha chuki sio nzuri unaumea wewe bila sababu yoyote,wenyewe wanaraha zao wewe una umea ,pole sana,,,

    ReplyDelete
  6. inakuhusu nini wewe..chuki binafsi tu hizo hasa chuki dhidi ya waarabu.

    ReplyDelete
  7. FITNA kama hii ndiyo inayokubalika....simply because ni ya kujenga na si kubomoa....na aliyeandika ana uchungu wa inji yake. Manake hii mitambaa myeusi inayotangaza the bloody exhibition mimi naliona kila siku na inawezekana imeshapita miezi sita sasa .....sasa hii ni EXHIBITION KWELI au UKWEPAJI WA KODI?

    ReplyDelete
  8. Ni kweli Mtoa hoja unalosema, ujinga huu hauwezi kufanyika katika nchi zenye wenyewe.Ila si wote tunajua bongo haina wenyewe? kama kungekuwa na wenyewe tungeibiwa kuanzia 1996(IPTL) mapaka 2010(TRL)?

    ReplyDelete
  9. HILO NALO NENO mdau kama veile ulikuwa akilini kwangu jamani kama sikosei kwa muda usiopungua miezi minne 4 wameshafanya hiyo wanayoita exhibition mara nne 4 Golden tulip, Pale Mikocheni opp TM hopital na leo Diamond Jubilee.ukweli nimepata hisia kuwa hakuna Syria wala nini ni kuna mfanyabiashara amabaye ameamua kuijpatia pesa zake kiulaini kama unavyojua bongo, hivi ni nani ndie anayetoa kibali cha exhibition? mbona saba saba tumezoea mara moja kwa mwaka iweje hawa mara 10 kwa mwaka? wahusika tusaidie.

    ReplyDelete
  10. tuthibitishie kama hawalipi kodi, sio unapayuka tuu!

    ReplyDelete
  11. Acha Ubaguzi na wewe ni nani mpaka uwachagulie wananchi bidhaa? Una data gani kuwa hawalipi kodi? Hao waajiriwa wa bidhaa za 'wananchi' wanalipwa vizuri? Hizo bidhaa za 'wananchi' zina ubora gani?

    Waache wananchi wajichagulie wenyewe. Ikiwa wataona bidhaa duni au ghali si wataacha? Kama una data kwamba wanakwepa kodi kwa mujibu wa sheria, nakushauri utoe taarifa TRA, polisi au Takukuru.

    ReplyDelete
  12. kama ni kweli ndio wanavyofanya! basi atuna watumishi wa selikali! na hii yote ni matokeo ya rushwa kuanzia selikali za mitaa,wilaya na mkoa pamoja na mamlaka husika! mpaka mje kushtuka watu washapiga bao! sikuhizi tbs wanachoma moto bidhaa feki,kwahiyo hao wamekuja na stahili mpya!

    ReplyDelete
  13. hii ni noma! tatizo la wabongo wanaendekeza sana njaa! serikali za mitaa mpaka mkoa na mamlaka husika washakatiwa hapo!

    ReplyDelete
  14. ur very right...hii nchi sa nyingine kama haina watendaji wa TRA wala JIJI vibali vinapotoka

    ReplyDelete
  15. Mtoa mada, tatizo lako ni nini hasa? Ni kufanyika kwa exhibition kila mwezi, tafsiri ya neno exhibition, watanzania kulipwa ujira mdogo, bidhaa zinazouzwa si za Syria na hazina ubora, au nini?
    Kama Syria wanafanya exhibition kila mwezi, vipi wale wachina waliohamia kabisa pale kariakoo? Kuuzwa kwa bidhaa za china na wa-syria hilo nalo unataka serikali iingilie kati? Ujira mdogo, hili ni tatizo kwa wa-syria tu, je wahindi tulio nao hapa bongo toka uhuru wanalipa ujira mkubwa?
    Kama exhibitions zao zinafanywa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo sidhani kama ni busara kulalama hapa kwa Michuzi.
    Mdau, Kariakoo

    ReplyDelete
  16. Hivi ile Machinga Complex pale Ilala imeishafunguliwa au bado? Mara ya mwisho nilipokuwa Dar las October ilikuwa bado nini hasa tatizo?

    ReplyDelete
  17. Tukipata Raia million moja kama huyu jamaa wenye uchungu wa nchi yake tungpata maendeleo makubwa sana injii hii

    ReplyDelete
  18. ndugu na jamaa inabidi mambo kama haya yahangaliwe sisi wa tanzania tunalipa kodi kubwa sana kufanya biashara kwenye nchi yetu hao watu sio syria ni mtanzania kuna baadhi ya viongozi wamekula teyari bila kubisha na raisi wenu yupo humo pili hacha mambo ya kijinga unapo leta mambo ya kidini eti kwa sababu ni waharabu ndio maana unararamika wara sio hivyo mtanzania ina bidi tatu raia wetu tujipange sawa kuomba serikali yetu kuivunja hiyo tukururu pia na TRA make ina bidi tuingilie hata kama ni kuchoma nyumba zao za mbezi zichomwe moto mie niko njiani kama mtanzania wa kwanza kuanzisha nitadili na watu wa TRA kama osama tanzania subuli ni rudi home tatu viongozi wa serikali mie kama ni u mafia ndio huu mie wangu ni uchungu na wezi wa pesa za wananchi tanzania 75% wanaishi kwenye nyumba za udongo wakati kikwete anashinda ulaya nimechoka raia naomba watu wa kujitolea tuanzishe fagia uchafu wa serikalini jera sio kitu tutakwenda tu make atanyumbani ni kama jela sioni tofauti niamini jamii yangu

    ReplyDelete
  19. Tatizo nchi hii tuna akina Doto Kasanga wengi mno(na wengine ndio wako wizarani huko)! Yaani wa-tz wengi tuna ufahamu mdogo. Exhibition maana yake ni kuonyesha bidhaa kwa nia ya kupata mikataba ya ku-supply kwa muda mrefu, au kuingia ubia kuwekeza pamoja. n.k, sio kuuza rejareja. Infact ukienda exhibitins nchi zenye wenyewe, kuuza rejareja hairuhusiwi mpaka siku za mwishi kabisa za exhibition, na kunakuwa na kiasi cha bidhaa ambazo zinaruhusiwa kuingizwa.

    Kwanini? Kwasababu exhibitors au waonyeshaji hawana leseni kufanya biashara nchini, hawalipi kodi maana ni bidhaa za "maonyesho". Kwa hiyo kwa kawaida maonyesho yanakuwa mara chache, kwa mfano mara moja kwa mwaka. Sasa wakifanya kila mwezi, au kila baada ya mwezi si wamefungua maduka?

    Sisi watanzania pia hatuna utamaduni wa usawa, au fairness, AU HAKI. Ni maneno marahisi sana, ila yana maana kubwa na kwa sisi sidhani hata kuyaelewa ni rahisi kwasababu si utamaduni wetu.

    Msingi mkubwa wa kuwakatalia hawa wa Syria na Exhibitions zao zisizoisha ni kwamba si HAKI wala hakuna FAIRNESS kwa wafanya biashara wa kitanzania ambao inawabidi wakate leseni, walipe kodi, ilhali hawa wageni wakiachiwa kila kitu bure. Achilia mbali kwamba kutolipa kodi na leseni ni kuvunja sheria kwasababu sio exhibition bali ni maduka, lakini lazima utambue kwamba si haki kwa wale ambao wanalipa.

    Kuwa na utaifa wa kiuchumi(au economic nationalism)ni muhimu kulinda maslahi ya watanzania.

    Nitatoa mfano mmoja unaoonyesha umuhimu na uzito wa haki wenzetu wanavyoujali. Hivi karibuni kampuni ya BAE Systems ya Uingereza ilipigwa faini na serikali ya marekani(na uk pia) kwa kuuza silaha na rada Uarabuni na huku kwetu Tanzania, hata inatulazimu turudishiwe"chenji" yetu. Jiulize, kwanini USA iipige faini kampuni ya UK kwa kutumia rushwa kuuza silaha nchi za nje?

    Sababu ni HAKI, FAIRNESS. Kwa kutumia hongo kupata tenda ya kuuza ndege za kivita na rada(hata kama ni ya zamani), kumewanyima haki wauzaji wengine wa USA na kwingineko. Kama wasingehonga na wakafuata sheria waziwazi, inawezekana wamarekani nao wangeuza angalau kiasi, lakini kwa kutumia hongo, hawakuwatendea haki wauzaji wengine na hivyo kuwakosesha mapato. Haya wameyatungia sheria, ili yakitokea HAKI itendeke, wakapigwa faini.

    Kwa hiyo mnaoshindwa kumulewa mwandishi wa hii jiulizeni: mimi leo niende Kenya nilete makontainer kila baada ya miezi miwili nasema exhibitions, kwa hiyo sina leseni hapa ni haki kwa wengine?. Haki hii ni ya kiuchumu, ya kuweza kufanya biashara bila ya upendeleo na bila kuwafanya wengine wawe na wakati mgumu.

    Nadhani itafika mahali wafanya bishara watalalamika kwa "fair competition commission" ambao ni moja ya kazi yao kuhakikisha kunakuwa na fair competition.

    Waambie hao wa-Syria wakafanye "exhibitions" kila baada ya miezi miwili SWEDEN ndio utajua nchi zenye wenyewe.

    Mungu Ibariki Tanzania.

    DMK

    ReplyDelete
  20. Nakubaliana na wewe Ndugu Dotto Kasanga. Huyo anayejitia eti ni wa millenium tower si mkweli. Kuna jumba moja la ibada si mbali na millenium tower linalodhaminiwa na wafadhili fulani mafashisti kutoka nchi moja kubwa ambapo wa-TZ wenzetu wanafunzwa siasa na hao wahubiri na kuelezwa wamkubali nani na wamkatae nani. Sitashangaa kama huyo hater ni mmojawapo. Nakumbuka hata siku moja Novemba 2008 walifanya maombi maalum kumuombea Mccain ashinde uchaguzi USA. Lakini walidorora!!! Brother wetu mpendwa Obama alichaguliwa!!! Ukichanganya njaa, ujinga na chuki ni hatari tupu...

    ReplyDelete
  21. machinga complex tatizo ni ushuru wataotozwa pale,,,wanainchi wanaona NO

    na hapatoshi padogo sana kwa uwingi wa wafanyabiashara

    ata cjui itakuweje,mwisho liwe gofu

    kodi yetu iyo alafu,,,

    ReplyDelete
  22. Naunga mkono mada hii. Kwa kusema kweli hata mimi nimechoshwa na hizo exhibitions. Yani unakuta tangazo la previous exhibition halijaondolewa barabarani, tayari kuna jingine. Hizo ni biashara ndogondogo na sio exhibitions.Halafu bidhaa zao hazina kiwango hata kidogo pia bei yake iko juu.HAWANA MAANA!

    ReplyDelete
  23. we mdau wa Tarehe Wed Feb 24, 11:31:00 AM.
    Unayetaka kuthibitishiwa kama jamaa hawalipi kodi au wanalipa, Unaelewa maana ya EXHIBITION? naona we ndio unapayuka, sasa ikishakuwa exhibition hiyo kodi utailipa kwa mtindo gani? usikurupuke na kuwaambia wenziyo wanakurupuka. In case you dont understand, Exhibition ni display; show; public presentation of work or skills; trade fair. Its not a business per se.

    ReplyDelete
  24. jamani watanzani, hakuna mtu anaye hate humu ndani. Hata kama ana hate lakini si he has a point au?. Unajua mtu akileta hoja ifikirieni kwanza kabla ya kubwabwaja tu.
    Yes hao watu hii sio exhibiton yao ya kwanza. Na wanarudia rudia sana. Na kama ni exhibiton kwanini wameconcentrate kwenye kuuza kwa reja reja?
    Mimi sijui kuhusu quality ya products zao lakini kama sisi tunakosea kwanini wasitoe ufafanuzi hiyo exhibition ni ya aina gani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...