TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ameondoka nchini leo, Jumatano, Februari 17, 2010, kwenda Uturuki na Jordan, kwa ziara rasmi za kiserikali kwa mwaliko wa viongozi wa nchi hizo mbili.

Rais Kikwete ambaye anaandamana na Mama Salma Kikwete, pamoja na wafanyabiashara wa Tanzania, anatarajiwa kuwasili Ankara, Uturuki, usiku huu tayari kuanza kwa ziara ya siku tatu nchini humu kwa mwaliko wa Mheshimiwa Rais Abdallah Gul.

Rais Kikwete alipokea na kukubali mwaliko wa kutembelea Uturuki tokea Februari mwaka jana wakati Mheshimiwa Rais Gul alipotembelea Tanzania kwa ziara ya pili kwa mwaliko wa Rais Kikwete.

Wakati wa ziara hiyo ya Uturuki, Rais Kikwete anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, na pia kukutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan.

Miongoni mwa shughuli zake wakati wa ziara hiyo, Rais Kikwete pia atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Uturuki, pamoja na mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao katika Uturuki.

Tanzania na Uturuki zinatarajiwa kutiliana saini mikataba sita ya ushirikiano kati ya nchi hizo wakati wa ziara ya Mheshimiwa Rais Kikwete.

Aidha, Rais Kikwete atatunukiwa shahada ya juu kabisa (PHD) ya heshima na Chuo Kikuu cha Faith cha Fatih cha mjini Istanbul.

Rais Kikwete anatarajiwa kuondoka Uturuki Jumapili, Februari 21, 2010, kwenda Jordan kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa MfalmeAbdullah wa Pili.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Februari, 2009

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Asante kwa taarifa. Lakini nataka kufahamu shahada anayopata Raisi ni ya mkondo gani? Pili, tunaomba tupewe majina ya wafanyabiashara wanao andamana na Rais katika ziara kama hizi za kibiashara na pia biashara wanazofanya nyumbani.

    ReplyDelete
  2. ISIJE WAKALIPIWA NA PESA YETU YA KODI HAO WANAOJIITA WAFANYA BIASHARA

    ReplyDelete
  3. Upendeleo wa watu fulani tuu!!!! Kwani si unajua awamu hii ni yetu tu!!!!

    ReplyDelete
  4. Sawa mkuu tufungulie njia na tuboreshee mazingira, tunakuja.

    ReplyDelete
  5. Wewe annon wa tatu una maana gani unaposema upendeleo wa watu fulani tuu, fafanua ueleweke usibanie mambo, kuwa muwazi kama nia yako ni safi katika hili sio unasema mambo kwa mafumbo. Acha chokochoko kwani kuna mengi ya msingi unayopaswa kusema na kutekeleza na si kutaka kuanzisha hisia zisizo na msingi.

    ReplyDelete
  6. namuunga mkono msemaji wa 09:57 mkuu aongeze opportunity kwani degree nyingi ziko mtaani ajira hakuna ikiwepo maslahi hakuna

    ReplyDelete
  7. graduates wanakufagilia

    ReplyDelete
  8. Tunamtakia Rais wetu safari njema na mafaanikio katika safari hizo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...