JK na mwenyeji wake Raıs wa Uturuki Abdukkah Gul wakıkagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya Rais Kıkwete kuwasili katika ikulu ya nchı hıyo iliyopo jijini Ankara leo asubuhi.
Rais wa Uturuki Abdullah Gul na mkewe wakiwakaribisha ikulu ya jıjını Ankara JK Mama Salma leo asubuhi
JK akifafanua jambo wakati wa mkutano n a waandishi wa habari mara baada ya kufanhya mazungumzo rasmı katıka ikulu ya Ankara nchını Uturukı leo asubuhi.Pembenı akımsıkılıza nı Rais wa nchı hiyo Abdullah Gul.Raıs Kıkwete yupo katıka zıara ya kikazi nchini Uturuki
Pıcha na mdau Freddy Maro

Na Mwandishi Maalum
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo 18 Feb, 10 anaanza ziara ya siku tatu nchini Uturuki kwa makaribisho rasmi ambapo Rais wa Uturuki Mheshimiwa Abdullah Gul atamkaribisha Rais Kikwete katika kasri ya nchi hiyo.

Mara baada ya makaribisho hayo, viongozi hao wawili watafanya mazungumzo rasmi ya kiserikali na kushuhudia utiaji saini kwa mikataba mitano kati ya nchi mbili hizi shughuli ambazo zitafanywa na mawaziri.


Mchana wa leo, (18.2.10) Rais na ujumbe wake utakutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyid Erdogan kabla ya kukutana na kufanya mazungumzo na spika wa Bunge la Uturuki Mheshimiwa Mehmet Ali Sahin.

Rais Kikwete pia atakutana na kufanya mazungumzo na Umoja wa Wafanyabiashara wa Uturuki na baadaye kukutana na mabalozi wa Nchi za Afrika waliopo Uturuki na baadaye jioni hii Rais Kiwete na ujumbe wake watahudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Duh Urais ni madaraka makubwa sana. Jamaa anakagua gwaride la waaarabu(former colonial masters). Woow!

    Mke wa rais wa Uturuki nae. MMhhh!

    ReplyDelete
  2. Kumbe JK anaweza press conference, mbona bongo hafanyagi hivi?, anaita wahariri tu. Inatakiwa kuwe na utamaduni wa kuwauliza maswali wanasiasa wetu ili kuwaweka busy katika masilahi ya wananchi. Maana kama huwezi jibu maswali basi ujue kuwa utaonekana huwezi kazi.

    ReplyDelete
  3. JK naomba ukirudi uniletee koti hilo make kwetu Iringa baridi kali sana pl'se mpiga kura wako 2010 kilimo kwanza.

    ReplyDelete
  4. sisi tumesoma zamani naomba tukumbushane hivi Uturuki inaongozwa na Rais ama inaongozwa na Waziri Mkuu?

    ReplyDelete
  5. We anon wa kwanza hapo aliyekwambia waturuki ni waarabu nınanı nadhanı una upungufu wa elimu ya kıgeographia .Waaarabu watu wengine na Waturuki watu wengine kabisa kama walivyo wa İranı.Taifa likiwa la kiislam aina maana ni Waarabu.İnaonesha jinsi gani elimu ilivyo mgogoro.

    ReplyDelete
  6. First Lady wetu Mama Salma umependeza sana na hiyo outfit yako, tunakushukuru kwa kutuwakilisha vizuri Watanzania huko ughaibuni.

    ReplyDelete
  7. Mona Mama Salma Kikwete havai Hijab?

    ReplyDelete
  8. mama kikwete mzuri na anaonekana mwanamke mwenye akili,sio limwamke unakuta leupe miwanja kibao umaimuna kibao.

    ReplyDelete
  9. Anonymous wa kwanza

    Waturuki sio Waarabu. Labda kama ulikuwa unamaanisha wao walikuwa wanawatawala Waarabu...

    ReplyDelete
  10. Mama Salma Kikwete is really pretty. Anavaa vizuri. Ila hapo atakuwa anapigwa na kabaridi manake hali ya hewa sasa hivi ni baridi...si unamcheki mumewe kavaa koti zito, sijui kwa nini hawakumshauri na mama Kikwete avae nguo ya joto

    ReplyDelete
  11. karibu ubatani mheshimiwa rais JK

    ReplyDelete
  12. gwaride la waarabu...????????? wewe mdau ulietangulia bado upo miaka ya 1953???????? mijitu mingine bwana haijui hata inaongea nini na wala haijui dunia tupo wapi kumbuka tupo 2010.

    ReplyDelete
  13. Mama wa kwanza hivyo ndo unatakiwa uvae utoke ki-Tanzania si maushungi ushungi tu, from now on that is how it should be, and how to wear as our first lady.

    ReplyDelete
  14. Mungu abariki safari ya Rais wetu ili tufunguliwe katika mambo fulani si misaada tu bali hata nafasi za kujifunza viongozi wetu kupitia wenziwao.Mdau

    ReplyDelete
  15. Mijitu mengine inabidi kupigwa vibao hawana akili Soon watasema Marekani ni Africa wakimuona Obama. Na Compton. Ndio hii hii inadanganywa na manchi mengine kwa habari wanazoziona kwenye TV. Masawe

    ReplyDelete
  16. Mama Kikwete unajua kuvaa! sasa hiloo baridi,nina uhakika saa zilikuwa haziendi!

    ReplyDelete
  17. we anonims hapo juu unayesema mashungi jaribukuwa mstaarabu kumbuka huyo mama kafuata dini yake na kitabu chake kinavyomwambia nafkiri na wewe ungeshika time yako ukafanya yanayokuhusu naomba nikushauri kitu kimoja kumbuka katika dini zote hakuna dini ilosema mtu atembee uchi sasa akili kichwani kwako.

    ReplyDelete
  18. Anon wa 06:50 Cha msingi si kufunika kichwa (nywele)? na nadhani amefanya hivyo.

    ReplyDelete
  19. acheni kujifanya waswalihina wakati hamna lolote! kamwene hapo juu umenia kwa kucheka lol

    ReplyDelete
  20. WW KIJANA UNAESEMA MAMA KIKWETE ANAPIGWA NA BARIDI HUJUI UNACHOSEMA NI KWAMBA UKIWA NDANI YA JENGO HUWA KUNA HEATING SYSTEMS HIVYO UNAWEZA KAA ATA TUMBO WAZI HAKUNA BARIDI,,, TEMBEA UONE KIJANA...KUTALII NI ELIMU PIA SIO UNAKAA TANZANIA TU TEMBEA UFUMBUKE...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...