Miss TZ 2009 Miriam Gerad akiondoka mahakamani leo baada ya kesi yao kuahirishwa

Miss Tanzania 2009/10 Miriam Gerald na rafiki yake Kenedy Victor ‘Kenny’, leo wamepandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni kwa mara nyingine, ambapo kesi yao ya kushambulia na kuharibu mali na vyombo vya muziki vya bendi ya Volcano Sound, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki saba ilitajwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 21
na washtakiwa hao wanaendelea kupeta kwa dhamana.

Kenny na Miriam walitinga mahakamani hapo majira ya saa 3 asubuhi, wakiwa katika gari moja aina ya Harrier yenye namba za usajili T 178 BDV na baada ya kuingia walianza kushangiliwa na mahabusu waliokuwa wakifika mahakamani hapo wakiwa katika mabasi ya Magereza.


Kenny akiondoka mahakamani leo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Haiwezekani kesi ikawa tarehe 21 Machi, 2010 kwani itakuwa siku ya Jumapili. Ofisi za serikali ikiwemo Mahakama TZ hazifunguliwi jumapili

    ReplyDelete
  2. Hakimu kasoma kalenda ya mwaka jana...hahah!!
    -Mdau Wakudumu

    ReplyDelete
  3. Au ni wewe ISSA ndiye umechemsha kunakili? Wadau wako makinii na issue!Hawadanganywi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...