Ankal hilo ndio squad zima la Sweet Noise Band iliyo na maskani yake Iringa kutoka mbele kushoto ni Mwimbaji Steve, Boutross mpiga drums na Mwimbaji Felly Kano. kuoka nyuma kulia ni Nicco mpiga Kinanda na Shedrack "mzee wa viloba".

Sweat Noise huwa inafanya maonyesho yake kila siku za Jumatano na Jumapili Club VIP, Ijumaa na Jumamosi Luxury Pub.

Bendi hii ilianzishwa kwa lengo la kuwaburudisha wakazi wa Manispaa ya Iringa ambao kwa muda mrefu sasa walikosa burudani ya muziki wa Dansi kwa kila wikiendi. Mara nyingi walikuwa wakitegemea Bendi za Dar es salaam ambazo zilikuwa zikitoza kiingilio kikubwa sana na hivyo kupelekea baadhi ya mashabiki kushindwa kumudu gharama za viingilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. acheni kupotosha watu iringa, dodoma tangu lini yamekuwa majiji?

    ReplyDelete
  2. Ankali naunga mkono juhudi za hawa "wanyalukolo" kuanzisha bendi kwa ajili ya kutoa burdani huko Iringa. Unajua ankali mimi nilikata nondo zangu huko Iringa na kweli kulikuwa kumezubaa kidizaini na sasa hivi mji huo umekuwa kibiashara na hata katika sekta nyingine kama vile elimu. Nawaunga mkono hawa "wanyalukolo" na nadhani mji utachangamka sasa....

    ReplyDelete
  3. awa watu mbona wame pozi kama wachekeshaji??? mi nilizani ze comedy

    ReplyDelete
  4. jamaa wamenikumbusha jiji la iringa.Nakumiss sana makanyagio,isoka,mtwivila,gangilonga...ndo majina ya baadhi ya vitongoji vya iringa...makorongoni,mwembetogwa,mlandege,..mto mchambawima..KIHODOMBI....

    MDAU WA ILALA PRIMARY SCHOOL,ENZI HIZO TUKIWA NA AKINA MWL.MWAMBENE,LUMBIRA,MWAKYEJA,AMBWENE NA KAKA MKUU EZRA MBWILO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...