Ndugu michuzi,
Pole na kazi kwa mara nyingine. Natunaini bado unaifanyia kazi meseji niliyo kutumia jana. Nina jambo jingine ningependa kukuomba tena kama lipo ndani ya uwezo wako.

Sisi wajasiria mali tuishio hapa u.k tunakwazwa sana na uhaba wa informations hasa katika kitengo cha TRA kinachohusika na ushuru wa magari. Maana mtu unanunua na kutuma kitu nyumbani bila hata kujua kikifika huko utatakiwa kulipa ushuru kiasi gani, mfano mzuri ni mimi mweyewe nimeshatuma magari zaidi ya matano na kila wakati natajiwa bei tofauti za ushuru.
Sasa sielewi ni kwamba huwa natapeliwa au ndio hivyo ushuru unabadilika kila wakati?

Ombi langu linakuja kama ifuatavyo; Kuna mtu nilizungumza nae akaniambia kwamba kuna FORMULA zinazotumika ku calculate gharama za ushuru kulingana na vigezo mbalimbali. Sasa naomba kama utaweza kututafutia hizo formula ukatuwekea kwenye Globu yetu ya Jamii kwa manufaa ya wadau wote. Nina hakika hasara tunazopata kila siku zitapungua.
Ahsante
Mdau ERIC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Ankal,
    Mshtue JK kwamba vijana wake wa Bandarini na TRA wasumbufu sana na kwa sasa wajanja wanapitishia Mombasa kuepuka nyodo wanazoonyeshwa hapo Dar.
    -Mdau
    Kiwanja!!
    Maltisizeshenishipu Oyee!!

    ReplyDelete
  2. aisee hilo swala ni la maana sana.mimi pia kichwa kinawaka pale ninapofikiria kupeleka mzigo unaolipiwa kwa kukadiria au calculation zisizojulikana kwa wateja.hili swala naomba tulikalie vizuri litatusaidia hapo mbeleni.asante mdau.mada nzuri

    ReplyDelete
  3. Kwa ujumla TRA wanafanya kazi nzuri sana na wanajitahidi sana kwenda na wakati.

    Tatizo ni kwamba kuna baadhi ya maofisa sio waaminifu na TRA wanaochafulia jina ile taasisi nyeti.

    Uchachotakiwa kufanya ni kuwa na mawasiliano na clearng agent kabla ya kutuma gari ili 'aweke mambo sawa'.Hiyo hai guarantee kwamba kila kitu kitakwend kama unavyotarajia lakini inasaidia kupunguza 'surprise' ya kodi inaoweza kupelekea mshtuko wa moyo.

    Nadhani umenielewa.

    ReplyDelete
  4. Ni kweli wajanja wameanza kupitia Mombasa. Ni bora mzungumze kodi unayotakiwa kulipa wakati umeegesha gari nyumbani kwako kuliko wakati limeshikiliwa na wazee wa bandari ya Nazir. Wanatumia storage charges kama njia ya kukukaba koo, noma sana.

    Msemaji wa TRA angejibu swali hili kupitia globu ya jamii angekuwa amecheza heko sana. Changamoto hiyo, TRA mtajibu????

    ReplyDelete
  5. Wewe usidanganyike, hakuna formula wala maziwa ya watoto. Yaani TRA ni kukisia na kumjua mtu au fedha yako tu. Formula zingekuweko wangeweka wazi long time, hazipo na ni kwa kuwa wanahitaji kujaza kwanza mifuko yao.

    Tafuta mshikaji pale TRA au elewana na hao jamaa madalali wa kutoa mizigo bandarini wao wanajua nani wa kumshikisha mshiko na wapi wauweke.

    Ukija bongo kichwakichwa utatozwa ushuru wa meli au treni kwa kikorola chako

    ReplyDelete
  6. jamani kuna waliowahi kupitishia gari mozambique? mi ningependa kujaribu huko kwa sababu najua bandari dar kwangu basi tena, wamozambique wanaonekana kama ni watu waungwana sana, wanaweza wakatufaa wengine. asante.

    ReplyDelete
  7. tembela,www.gariyangu.com

    ReplyDelete
  8. Mdau wa feb 20 09;31 umetoa site ambayo inadetailed culculcutions zote za gari. Safi sana. Nimefanya calculculations zangu na ndo gharama nilizolipia gari. www.gariyangu.com ni superb wadau tumia hiyo

    ReplyDelete
  9. FORMULAR IPO ILA BILA DATABASE YAO WANAYOJIFANYA KUWA NDIYO KIGEZO CHA PRICE YA KU-UPLIFT PRICE ZA MAGARI YANAYOINGIA NI KAZI BURE.

    NB: SWALA NI HIYO DATABASE KUWA OPEN KWA PUBLIC NA FORMULAR PIA....ITAKUWA RAHISI KWA KILA MTU!

    TATIZO:

    Formular peke yake haitosaidia kukupa kodi halisi kama wao wataongeza bei kwa kujifanya wana bei zao. Swala ni hizo bei kuwa wazi, haitakiwi kuwa siri ni haki ya jamii.

    ReplyDelete
  10. Hiyo calculator haisaidii kabisa, labda kama uwe ndugu yake nanihii. Juzi kati mtu katuma gari yake cc 2000, ya mwaka 2000, CIF $5200 kalipa kwa ecxemption T.Sh 1350000! ina maana bila excemption ingefika karibu mil 16! Kuna idara inafanya re-evaluation ya thamani ya gari (CIF au FOB price), na wanakuja na yao (sijawahi kusikia ikiwa ndogo zaidi ya uliyolipa Japan!)


    Kwa wanaojua collabo ya Maagent na baadhi ya maofisa wa TRA, kama mdau alivyosema kupitisha gari dar ni kama huku pata ugonjwa wa Moyo ni kufilisika kabisa!!

    ReplyDelete
  11. JK alitembelea bandarini nakusema anawajua wababaishaji lakini mpaka leo kimya.

    ReplyDelete
  12. unafuu wa mombasa kwenye ushuru border unabagain unatoa rushwa alafu mzigo unapita.alafu ninyi haohao mnapiga kelele ktaka maendeleo ya nchi na kuloa kodi hamtaki,hizi gari nzako nzee fanya umezingiza hapa uk ungelipa ushuru kiasi gani,serikali yoyote isiyo ksanya ushuru ni hovyo,na wasiwasi we kama ata unalipa council tax,na watu wafungwa hapa uk kama ukikamatwa umekwepa kodi na kodi ziko juu sana na ndio maana unaona watoto wetu wanakwenda shule bure.

    ReplyDelete
  13. TRA WANATUMIA KODI KAMA MTEGO WA KUANZISHA MAZUNGUMZO YA RUSHWA, UTAKAPOENDA KULALAMIKA JUU YA KODI NDO HAPO MWANYA WA RUSHWA UNAANZA, NA KAMA HULALAMIKI BASI UTALIPA HIVYO NA MARA NYINGI UKILIPA HUWA AZIFIKI KAMA ZILIVYO KWANI WANAANDIKA RISITI MBILI MOJA FAKE YA BEI YA JUU UNAPEWA WEWE NA ILE HALALI YA KODI UNAYOSTAHILI KULIPIA UPELEKWA SERIAKILI NA HUONI HII COPY YAKE UCHANWA NA TOFAUTI YAKE NDO ZINAKUWA ZAO.

    ReplyDelete
  14. www.gariyangu.com SI WEBSITE YA TRA AU SERIKALI SO IT IS ABSOLUTELY AND UTTERLY WRONG TO BASE ON IT, WE NEED INFORMATION FROM TRA OR THE GOVERNMENT ITSELF, TUNACHOFANYIWA NA WAFANYAKAZI WA TRA NI KUKOMOWANA TU NA NI DALILI YA WIVU NA WIZI KWA WALIPA KODI

    ReplyDelete
  15. Tatizo kuwa wafanyakazi hadi wakubwa wa hiyo TRA wote ni jealousy,si kwamba utarekebisha wafanyakazi tu,Huko kenya kwa sasa ukipitisha Mzigo kila gari ni dola 650 tax yake,Tumelipa ushuru Rav 4 ya 2002 Mil 4 laki 9 Moshi but TD5 LANDROVER 02 NI MIL 9 USHURU UMETUSHINDA HADI SASA HAPO HAPO KENYA,GARI COST YAKE NI 3900 PLUS 80O ZA USAFIR,CHA KUSHANGAZA HAKUWEKWI VIPIMO KUWA ENGINE KUTOKA 1 HADI 1500 CC KIASI FLANI KAMA WANAVOFANYA ULAYA ILA WAO NI THAMANI YA GARI NA HATUJUI THAMANI WANACHUKULIA KIWANGO GANI,KWA KWELI NI KUKOMOANA TU,KIBAYA ZAIDI UFUNGUO TU WA HIYO RAV 4 wa Akiba ULITUMWA KWA DHL UKALIPIWA USHURU 50,000 TZSH KWA KUWA UNA ALARM HAPO NDIO NIMESHANGAA ZAIDI

    ReplyDelete
  16. Tehe Tehe, wabongo bwana! Sasa wewe unapewa desa la kukusaidia unang'aka. Haya wasubiri TRA wakuletee hizo info.

    www.gariyangu.com ipo accurate. Nimepiga hesabu pale na ndiyo hiyo hiyo nimelipa TRA (tofauti ni exchange rate tu).

    Tatizo mara nyingi sisi tunapenda kulalama sana lakini ni wabovu kabisa wa kufuatilia na kujua tatizo liko wapi.

    Tunawalalamikia TRA lakini ukweli ni kwamba anayekukaanga ni wakala wako. Na wanawakaanga watu kweli kweli. Kuna mmoja tulikuwa tunapiga naye stori kishkaji akawa anatusimulia jinsi walivyomkamua mama mmoja mpaka wao wenyewe wakaona aibu hata kupokea kamisheni yao, wakamuacha aende. Yaani inasikitisha kwa kweli.

    Fuata ushauri uliopo www.gariyangu.com pengine unaweza kukusaidia kupunguza headache. La sivyo endelea kusubiria serikali yako ikuwekee hayo mambo online.

    TRA huwa inatoa documents zinazoonyesha unatakiwa kulipa kiasi gani. Kama hujaziona na umeambiwa tu kwenye simu na wakala wako ni kiasi gani unalipa, basi ujue umejitengenezea mazingira ya kupigwa bao baya.

    ReplyDelete
  17. TRA NI VITEGA UCHUMI YA WATU WACHACHE..NASIKU ZOTE TZ ITAKUWA MASIKINI

    ReplyDelete
  18. Naungana mkono na mdau wa hapo juu.

    Ukweli tatizo la msingi ni mawakala. Wakala uamwamini lakini yeye ndio anakuingiza mkenge, saa nyingine anashirikiana hata na jamaa wa TRA kukukaanga.

    Mfano: Wakala anaweza kukudanganya mbadilishe invoice ili bei ionekane ndogo. Halafu baadaye yeye ndiye anaenda kuwatonya wenzake walioko TRA. TRA wakishakudaka na invoice ya kugushi, wana-uplift CIF. Na hapo hutoki mwana hata uende kwa raisi, maana kwanza unakosa la kugushi. Sasa itabidi ulipe hiyo kodi ya juu, au uwape kidogodogo wakupe haueni.

    Tafuta wakala muaminifu na anayejua analolifanya.

    Mimi wakala wangu huwa akipewa uplift anazi-fight kwa hasira na kuwa anashinda. Na cases chache ambazo ameshindwa ni pale mwenye gari mwenyewe ameshindwa kutoa documents za muhimu. Unaambiwa lete nakala ya TT ili tuangalie kama kweli ulilipia kiasi hiki, unasema umeipoteza; sasa unataka usaidiweje? Mwingine mjinga kabisa anaileta wakati inaonyesha wazi kwenye hiyo TT kwamba pesa zilizotumwa ni nyingi zaidi ya anazodai yeye.

    Saa nyingine tusiwe tunalalama tu. Ni kweli wapo wezi pale TRA. Lakini wewe ungekuwa ni afisa wa TRA, na mtu anakuambia ameleta gari Land Cruser Prado ya 2008 km 22,000 na haina tatizo lolote kwa CIF 1,000 utamkubalia tuu?

    Wengi wetu tukiagiza magari tunawaruhusu mawakala wagushi documents ili tulipe ushuru mdogo. Huu ni ukweli, na hawa watu ni wengi mno. Ukifanikiwa unajiona mjanja. Ukibambwa na kupigwa uplift unakuwa mkali. Busara inasema kama ni wakala wako ndio alikudanganya mkigushi utalipa ushuru mdogo, kwa nini usianze kumlalamikia yeye pale inapo-bounce?

    ReplyDelete
  19. Ni kweli JK kapita port but up to now things are unclear anyhow just to help:
    Kama una exemption kama mfanyakazi wa serikali unalipa about 30-40 percent of original cost ambazo ziko mandatory.

    kama huna exemption inategemea gari umeichukua CIF au FOB. CIF means price iko calculated mpaka kufika bandarini alafu port charges utalipia separate. FOB inamaanisha bei ya kununulia gari bila kuisafirisha. Hivyo basi itabidi gari likifika Dar umlipe wakala bei ya kusafirisha pamoja na bei ya kuclear gari.

    Bei ya kuclear gari lazima inabadilika badilika. Inategemea na mwaka na cc na kadhalika. Kwa mfano kuna policy ya kutoagiza magari yaliliyozidi miaka kuni iliyopita. Ukiagiza gari la mwaka 1999 leo utalipia extra 1000$ penda usipende.
    Pili, Kuna kitengo cha TRA cha kuuplift. Baadhi ya watu hununua gari ambalo muuzaji kule Japan au Malaysia or wherever kadai ni la mwaka 1998 lakini in actual fact ni la miaka ya karibuni. Hii uplifting unit ikikagua products inakuta ni ya 2003 etc hivyo wataupdate bei kulingana na vile wameona products[engine seatbelts] etc zimeproduciwa.
    Kwa wastani bei inakaribia half the price uliyonunulia. Kama ni basi la $27,000 kodi inakuja almost 13-14 mil as ageneral formula baada ya hizi processes zote kuisha. Lakini huwezi kuclear gari bila kuwa na wakala. Sasa Wakala unayemchagua ndo ishu!
    sister

    ReplyDelete
  20. Jamani Wazalendo wenzangu mnaoishi nje na hamjarudi kwa muda au mlindoka mkiwa wadogo na bila kufanya kazi TZ. System ya TZ ni tofauti na nje ya TZ.
    Bongo hakuna fomula. Ukileta computers leta na umeme, ukiweka umeme basi hakikisha kuwa una contingencies zingine maana switch zitazimwa.
    We kama umeamua kufanya lako livulie nguo ulioge ....
    Hao wneyewe wanaotakiwa kuthibiti yanayoendelea wanaingia madarakani kwa kampeni za mabilioni wanazitoa wapi ..... !!!????? Ukipata jibu basi na TRA kutakuwa tambarare. Till then vumilia.
    Sio kwamba naunga mkono vitendo vya rushwa lakini believe you me me hata Takukuru wanaula itakuwa TRA? Kalaga baho .....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...