Hello bro Michuzi,
Kwanza kabisa asante kwa blog yako nzuri inayotuwezesha kujua mambo yanayojiri hasa nyumbani kila siku na kuwafanya hata watanzania waishio nchi za nje kujiona kama wako nyumbani kwa njia moja au nyingine.
Ebwana nimekutana na hii habari ya zain kuwa katika mchakato wa kuuza mitambo yake ya afrika isipokua nchi za Sudan na Morocco kwa kampuni ya India iitwayo Bharti Airtel Ltd
Sasa kinachonipa maswali hapa ni kwamba kwenye hii habari tunaambiwa zaidi ya nusu ya faida ya zain kwa mwaka uliopita ilitokana na wateja wa afrika.Sasa jamaa wanataka kuuza kivipi?Au ndo yaleyale tuliyozea kuyasikia?
with regards!
mdau gegk.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. mdau gegk,
    hivyo ndio biashara inavyokwenda.
    kama Bharti Airtel wako tayari kutoa 10.7 billion wakati Zain investors kwa mwaka wanapata 7.4 billion kutoka mitandao yote ya zain (afrika na mashariki yakati) kwa upande wao hii ni bingo, huo ni mshiko ambao wakitaka kuupata kwa faida ya kuendesha mitandao (ya afrika peke yake) inabidi wadundulize zaidi ya miaka miwili ndo wafikishe hilo fungu la 10.7,

    hii sio mara ya kwanza zain (zamani Celtel) kupigwa mnada, hawa wa-kuwait walinunua Celtel kwa 3.4 billion na sasa wanaiuza kwa 10.7 billion, hata ukiangalia kwa upande huu bado ni bingo kwao

    mdau - dar

    ReplyDelete
  2. http://in.news.yahoo.com/48/20100215/1238/tbs-airtel-in-10-7-bn-talks-for-zain-afr.html


    gonga hapo pia utainona!!

    ReplyDelete
  3. lakini ukweli unabaki pale pale kwamba wawekezaji wa kigeni wanatumia mwanya wa grace period wa miaka 3 bila kulipa kodi na wanauza na kulala mbele.

    Sheria hiyo ktk uwekezaji wa ICTs lazima ibadilishwe la sivyo tutaendelea kuibiwa. TIC mnafanya nini??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...