SINEMA MPYA YA KITANZANIA KUTOKA UINGEREZA MWEZI UJAO

Na Freddy Macha, London

Sinema mpya, Lovely Gamble, katika Kiswahili na Kiingereza, inatazamiwa kufanyiwa sherehe rasmi kabla ya kuonyeshwa na kuuzwa ulimwenguni, mwezi ujao.

Watengezaji wa sinema hiyo, Frank Eyembe na Baraka Baraka, ambao ni Watanzania na wakazi Uingereza, wamesema mchezo una waigizaji wa Kiingereza na Kibongo akiwemo mwanatamthiliya wetu maarufu, Steve Kanumba na ina azma ya kufungua njia mpya ya utengenezaji picha kwa Watanzania.

Walifafanua: “Miaka ya karibuni tumeona sinema zikitolewa haraka haraka, kwa mwezi mmoja, kiholela na kuuzwa mitaani. Sinema hizi huwa zinawafaidi wafanyabiashara wanaowapa presha watengenezaji wanao lipua lipua tu. Utengenezaji sinema si suala la kulipua. Ila msanii akiambiwa atalipwa shilingi hamsini milioni anaona nyingi, kumbe mfanya biashara anabaki na haki miliki. Hatuwezi kuendelea mbele kama sinema zetu zitafuata masharti na matakwa ya hawa wafanya biashara na wamachinga.”

Kampuni ya Urban Pulse yenye makao mji wa Reading inawahusisha pia vijana na wananchi wa mataifa mbalimbali na pia wenyeji wa hapa Uingereza.
Karibuni kumekuwa na msisimko mkubwa wa sinema za Kibongo nyingi zinazotengenezwa vibaya jambo ambalo limewafanya Watanzania tusipende filamu zetu wenyewe na kukimbilia za wageni mathalan Wanaijeria.
Shirikisho jipya lililoundwa miezi michache kurekebisha hali ya sinema nchini, Tanzania Film Federation (TFF) limeweka vipengelee kadhaa vya kusaidia tatizo na kati yake ni kupanga haki miliki na kuzipanga sinema katika umri takikana (certification) kusaidia watengenezaji na wasambazaji kuzingatia maadili wanapoonyesha mahusiano ya kijinsia na mapenzi.

Tazama kipande:

http://www.youtube.com/watch?v=j-fbwizJWEw
Kumpata Freddy Macha nenda:
Blog: http://www.freddymacha.blogspot.com
Web: http://www.freddymacha.com
Freddy on TV: http://www.ailtv.com
Swahili blog: http://www.kitoto.wordpress.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Haya tena issue ya lugha itarudi tena najua. Ok nafungua mjadala tena, na kwa sasa huenda ikaelekezwa kwengine............

    ReplyDelete
  2. Bravo wote walioshiriki katika kumwezesha Knumba na wenzake kutengeneza Film itakayokuwa katika ubora wa hali ya juu, na hivyo kuongeza mauzo na kujitangaza.
    KANUMBA SAFI SANA, waacha waseme wewe unajua unafanya nini Unapiga kiinglishi kama huna akili mzuri, ume improve sana sio sori ninatumaini waliokuwa wanakucheka wataacha midomo wazi.
    Mdau Ben. Kimbache-Kipatimu Kilwa

    ReplyDelete
  3. Big up Kanumba,umeimprove sana kwenye kinglishi.Dont let ppl put u down.From today onwards i will b ur number one fan.Halafu unaonekan mcheshi sana kwenye interview eti nobody hates u...lol....na kwenye interview moja niliona ya kwenye sporah jamaa alitaka kukukatisha ukamuambia..."because am talking about African figure,now u wanna talk" hahaha hicho kipande kilinifurahisha sana... waonyeshe how charming we r as Tanzanians.

    ReplyDelete
  4. Jamani wale wabaya wa Kanumba sasa semeni sijui wapi mtaanza kwani huyyu jamaa eng siyo lugha yake lakini he doing good hata kuliko Ali Kiba this how is.
    Ndambe uk

    ReplyDelete
  5. Hongera sana Kanumba, Muacheni mwenzenu Wivu tu..
    Aisee nampongeza sana huyu dada maana anasaidia sana vijana wetu kupata exposure.
    BIG UP Dada SPOLAH

    ReplyDelete
  6. Kaka Michuzi Eee, Mi nampenda sana huyu Dada na Show yake.Sasa jamani, kwanini hichi kipindi kisiwekwe bongo ??????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
    Nimaoni tu natoa, I think she is very good kwa Tanzanian generation.

    ReplyDelete
  7. Well done Kanumba, I love the whole Show.
    Asante sana dada kwa kutuwakilisha.

    ReplyDelete
  8. Kanumba Amejitahidi sana, Jamani nafurahi sana kuona Watazania wakifanya mambo kama haya.
    Hongereni wooote, hasa huyo Dada anaetuwakilisha Tanzania kwenye Mataifa makubwa.

    ReplyDelete
  9. Sio kama East African Tunachukiana, Hapana. Ni basi tu tuwagumu tu kuelewa vitu, na hatujafundishwa kushirikiana. Ila sasa naona mambo kama haya ya Sporah Show yanaanza kuweka mambo wazi, na kwasababu ni kijana mdogo, mrembo, na mwenye akili pia, naamini kabisa vijana wengi watajifunza kutoka kwake na labda kubadili mienendo yao nakuanza kusapotiana katika shughuli zao.

    ReplyDelete
  10. duh ama kweli jitihada ni nzuri duniani, kanumba kigugumizi kimeondoka thats good.

    ReplyDelete
  11. Hongera sana Kanumba, Nahuyu dada jamani Kaka Michuzi siarudi nyumbani? We need people like her hapa Tanzania. Ni hilo tu kwa leo Kaka Issa.

    ReplyDelete
  12. Kanumba Uko juu Kaka, achana na watu kwasababu woote wanaokusema ni wivu tu kaka angu.
    Sporah napenda sana show yako ila niko Bongo sina access yakuangalia zaidi ya youtube, So Jaribu kutuconsider huku nyumbani.

    ReplyDelete
  13. Naitaji msaada wenu, Mi nampenda Show ya sporah na siichi kuangalia, napenda sana anavovaa, sasa sijui niliaribu kumsifia, kama naona sikuizi boyfriend wangu nae amekua akimsifia sana, mara namkuta kwenye youtube anaangalia show za sporah, sasa ivi nimemkuta amejoin kuwa fan wa spora show. Mi jamani simuelewi ni anampenda huyu dada kwa show yake kama mimi au kuna mambo mengine, maana sanyingine roho inaniuma akiwa anamsifia sifia huyu dada, ila na mimi kweli nampenda na ninapenda sana show yake na nimejoin kuwa fan wake kwenye face book
    Jamani nisaidieni, nijitoke kuwa rafiki nae halafu nimwambie nae ajitoke, au nimwambie tu ukweli sipendi unavyomuongelea huyu dada kwenye relationship yetu maana kweli kunasaa anazidi.
    Nisaidieni maana nampenda boyfriend wangu ila naogopa kumwambia how i feel.

    ReplyDelete
  14. MMH, Patamu hapo, labda nayeye anampenda tu kama wewe. Tatizo letu sisi wasichana nao wivu. Umelikoroka mama, ulinywe.

    ReplyDelete
  15. Mimi Kama Mwanaume, ningekushauri ujitahidi kuwa na confident, maana uzuri haswa ulioko kwa huyu dada ni confident zake, na wanaume wasiku hizi wanapenda wasichana ambao wako confident.Kwahiyo hata usimuulize, we Komaa tu zidi kumsifia kpale unapoona anaitajika kusifiwa, utakuona jinsi mimacho itakavyomtoka, ataanza kukuogopa, ma mapenzi ndio yatakapoongezeka pia.
    Pole dada angu, ila Huyu dada kweli si mchezo, hata mi kunasaa anani tempt sana, ila ninaswahiba wangu.

    ReplyDelete
  16. Nyie wakina dada nanyie, ndo hivi hivi mnaachikaga, sasa wewe kama unaona huyu dada anavaa anapendeza, anaongea vizuri, si na mwinzio anaona ivoivo, we kwanini mawazo yako yanakua mabaya???
    Je na yeye angekwambia kwanini unampenda Sprah!! labda na wewe nani...iiii!!
    Jaribuni kuwaamini wapenzi wenu dada zangu.Labda mwenzio hata hafikirii hicho, sasa wewe ndio utamfanya aanze kufikiria mambo mabaya.

    ReplyDelete
  17. Eti Wanaijeria ni bora kuliko wa East Africa, what a bullshit!!

    ReplyDelete
  18. Ili suala la kupondea kwenu ni ujinga usio kifani. Hao wanageria mnaowasifia wanaongoza kwa utapeli, ufisadi, udini, ukabila, uuzaji wa madawa ya kulevya, uchoyo etc. Nyinyi wengi hamjaishi na wapopo ndiyo kusifia tu. Wanageria wamebarikiwa na mafuta, watu wengi, wasomi wengi, lakini wako wapi kiuchumi? Vita kila siku huko kwao. Wengi wanakimbilia nje kutafuta maisha, sasa nyinyi ndio mnaona mfano wa watanzania kufuata!!!!!

    Hacheni hizo, kama huwezi kuvumilia kukosolewa basi mna matatizo makubwa ktk dunia hii ya uwazi. Vile vile kumbukeni kuwa hapo mlipo ni hao hao Watanzania waliowafikisha sio Wanaigeria kwani hizo filamu zenu soko lake kubwa Tanzania.

    Sasa msianze kunyea mkono unaowalisha. Muwe makini na maneno yenu kwani mnaweza mkapata "backlash".

    Watanzania wako huru kusema chochote, lakini wewe kama msanii ongeza bidii katika fani yako na uwape burdani ya hali ya juu. Jifunzeni zaidi hiyo fani sio kila mnachofanya ni lazima watanzania wawasifie hata kama kibovu, "give us some real high quality products not mediocre ones".

    Nawaomba hata siku moja msitukane kwenu na kusifia kwa mwanzako usipojua.

    Wewe jiulize hayo mambo ya "JUJU" ya wanigeria ni ya nini kama hawana roho mbaya wenyewe kwa wenyewe??!!!!

    Wabongo hapa wamecheza filamu ya "Baby Powder" kila mtu kaisifia, sababu wamezalisha kitu kizuri ambacho hakina ubishi.

    Mr. Kanumba, ulipo-improve kiingereza chako kila mtu amesifia, kwani hicho ndicho kinachotakiwa pindi ukikosolewa wewe unaongeza bidii na kusawazisha upungufu. Hata wale wasiotaka kushirikiana watrudi kwenye mstari na kukuunga mkono bila ya kulalama.

    Mdau.

    ReplyDelete
  19. NAOMBA TOPIC YA MAMISS WA TANZANIA KUTOKA KWA DADA SPORAH. AU FILAM KUTOKA KWA KANUMBA...
    Hawa warembo wetu sasa Wametushinda, maana watoto wetu wanaiga nini???? Leo wamelewa, kesho wamegombania bwana, keshokutwa ......

    WANAUDHI MCHWIIIIIIIIIIIIIIIII

    ReplyDelete
  20. Nakubaliana na wewe, na ndio maana naomba huyu dada aje azifanyie shoo zake Bongo, yaani hapa dar hakuna kabisa role model, wasichana wanaoonekana kwenye magazeti, matangazo, maTV ni MAMISS, sasa waone hao Mamiss, ukija kwenye mainternet wasichana ndo hayohayo, jamani..
    WE NEED GOOD ROLE MODEL IN TANZANIA, hasa kwa Young girls.
    Yes namimi pia narequest Hii topic Ya Mamiss wa Tanzania kwa Sporah kama alivotoa ushauri wa Condom na Mr Blue.
    Asante sana Kaka Isa kwa Habari.

    ReplyDelete
  21. Big Up Sana Sporah, Uko Juu You are Truly an Insipiration for Tanzanian..I am So Proud of You girl, your a True Icon Keep it up the Good Work and inspire the young generation.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...