Waziri wa mambo ya ndani Lawrence Masha katikati akiwa na mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta Jenerali Said Mwema(kushoto) pamoja na mkuu wa chuo cha polisi Moshi Afande Matanga Mbushi wakiwa wamesimama wakati wakipokea gwaride la heshima wakati wa sherehe za kumaliza mafunzo ya askari polisi chuoni hapo wikiendi hii
Inspekta Jenerali Saidi Mwema akisoma hotuba
yake wakati wa kuhitimisha mafunzo

Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Lawrence Masha na
Inspekta Jenerali Saidi Mwema kwenye sherehe hizo
Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Lawrence Masha
akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya polisi
kikosi cha bendera kikipita mbele ya jukwaa kuu
Kikosi cha polisi kinamama kikipita kikakamavu mbele ya wakuu
polisi pia hupata mafunzo ya karate na judo
kikosi cha huduma ya kwanza kikionesha kazi zake
zoezi la kuokoa majeruhi

zoezi la ukakamavu katika mazingira magumu
wahitimu wa FFU
FFU wakionesha wanavyopambana na fujo kiasi cha
kupewa ina la utani la 'Fanya Fujo Uone' badala ya Field Force Unit
maonesho ya namna FFU wanavyopambana na fujo
FFU wakiwasili tayari kukabiriana na fujo
PICHA ZOTE NA DIXON BUSAGAGA
WA GLOBU YA JAMII, MOSHI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. sasa mmeshamaliza mafunzo mkishapangiwa vituo vyenu vya kazi sio muanze kuonea raia na rushwa za hapa na pale fateni maadili ya kazi na sio ulaji tu! naogopa hata kuwapa hongera hao FFU wanatisha!

    ReplyDelete
  2. ready for october

    ReplyDelete
  3. safi kabisa judo tena))))
    ila mcwasahau ktk kamshahara muwape kanono..
    Jivaz- Ulaya

    ReplyDelete
  4. hi!!!teh!teh! mwe!mwe! hawa ffu wajamaa zao akina ras naniiino?walikuwapo?

    ReplyDelete
  5. busagaga vipi kaka????? moshi hapo najua pako fureshi kinoma hebu lete mambo bwana!!! kuna kale ka-night klabu flani opposite na jengo la KNCU mzee hukajui nini?? wakichaga hao kaka!!!

    Mdau wa Pajazzz+titizzz

    ReplyDelete
  6. Candid ScopeFebruary 21, 2010

    Jeshi letu la Polisi linahitaji kufanyiwa upembuzi yakinifu katika shughuli zake za kila siku.
    Kwanza vitendea kazi vyao vilivyoridhishwa tangu enzi za ukoloni vinaonyesha kama wanafanya maonyesho ya silaha za kale. Nilipokuja likizo karibuni nilishangaa kuona mtutu anaotembea nao polisi akiwa kwenye doria au lindoni ni kichekesho kwani ni lile gobole la shemeji ningoje.
    Majambazi yanatumia zana za kisasa, sasa polisi na gobole lile la meta mbili atamfukuza vipi jambazi mwenye pistol?

    Polisi hawana vyombo vya habari za kikazi vya mtandao kama computer ambavyo wanaweza pata matokea ya awali ya mhalifu hii ni kutokana na utunzaji duni wa matokea mbalimbali.Lini utapata muda wa kiutafuta jalada la kuchunguza matokeo ya awali>
    Leseni za uendeshaji magari hazina kumbukumbu za pekee za computer hivyo ye yote anaweza tu tengeneza ya kwake na hivyo polisi barabarani hawezi kuhakiki uhalali wa leseni ya dreva.

    Na mengi ila kwa leo niishie hapa kwanza waosha vinywa wengine waseme niliyofumbia mdogo

    ReplyDelete
  7. Ujambazi unazidi kuongezeka siku hadi siku. Polisi hawana vyombo vya usafiri vya kutosha kufanya doria na pia kuwafikisha eneo la tukio mapema.Matokeo yake ukivamiwa na majambazi mpaka polisi waje majambazi yalishaondoka kitambo. Waziri wa ulinzi unaliangaliaje hilo swala?
    Nashauri chama tawala badala ya kugawa pesa,ubwabwa,kanga n.k wangetumia hizo pesa ktk kuimarisha jeshi la ulinzi.

    ReplyDelete
  8. mmeshamaliza mafunzo sasa kinachotakiwa mufanye kazi sio mkaanze kuonea raia ovyo na kuwapiga hamkujifunza ouonevu huko jeshini maana mnasifa kweli nyie sijaona bongo puuuuuuuuuuuu!kooooooooh ptuuuuuuuuu!!!!!

    ReplyDelete
  9. hakuna haja ya kuwapa vitendea kazi hao jamaa. kufanya hivyo ni kuwatajirisha. No pikipiki, no pingu, no bastola, no nothing. huvitumia hivyo vifaa si kwa kazi iliyokusudiwa. wakiwa na vifaa hivyo huimarika katika kazi yao ya kuomba rushwa. samahani kwa kusema ukweli

    ReplyDelete
  10. Lo,,Hao Fanya Fujo Uone ni noma,,,laiti jeshi lote la polisi lingekuwa kama kitengo cha hao jamaa amani ingekuwa shwari,,,,big up sana wazee wa kazi,nawakubali kwa kazi yenu,,,,waongezewe mishahara yao jamani kazi yao ni nzito sana.

    ReplyDelete
  11. HARUFU YA DAMU YANUKIA JIMBO LA KIBAMBA.
    KAMANDA KOVA, PCCB NA WENGINE WOTE WANAHUSIKA, TUNAOMBA MTUNUSURU WANANCHI WA JIMBO LA KIBAMBA KUTOKA NA MIGOGORO YA ARDHI INAYOTUKABILI, KWANI SASA HALI MBAYA SANA.
    MIGORORO HIYO KWA KIASI KIKUBWA INACHANGIWA NA KIKUNDI CHA WATU 20, IKIONGOZWA NA BW. ATHUMANI MATUTA NA WENZAKE.
    KAMANDA KOVA NINAOMBA KWA NIABA YA WANANCHI WA MAENEO HUSIKA AU WATU WANAOGUSHWA NA MATATIZO HAYO, FANYA UPELELEZI WAKO KWENYE MITAA YA KINGA’ZI, MALAMBA MAWILI NA KISARAWE NA KWENYE MAHAKAMA YA ARDHI HATA KWENYE VITUO VYA POLISI VYA MAENEO HAYO ILI UGUNDUE KIPI KINAKWAMISHA KUWAONDOA MATAPELI HAYA KUENDELEA KULETA MIGOGORO YA ARDHI?
    ATHUMANI MATUTA AMEKUWA ANATUHUMIWA NA KESI TOFAUTI TOFAUTI ZAIDI YA MIA MOJA (100) ZA KUUZA MASHAMBA YA WATU AU VIWANJA KWA NJIA YA UTAPELI, HIVYO KUSABABISHA MIGOGORO YA ARDHI.
    AMEKUWA NA KESI ZA MIGOGORO YA ARDHI KWENYE MITAA YA KWEMBE, KING’AZI, MALAMBA MAWILI NA KWENGINE KWINGI TU. MAHAKAMA MBALIMBALI AMEKUWA AKISHITAKIWA KWA MAKOSA KAMA HAYO MFANO MAHAKAMA YA MWANZO KIMARA, MAHAKAMA YA ARDHI WILAYA KINONDONI, ILALA NA MAHAKAMA NYINGINEZO ZA KISARAWE. MABARAZA MBALIMBALI YA KATA KATIKA JIMBO LA KIBAMBA NA MAENEO JIRANI IKIWEMO KISARAWE YAMEKUWA YAKITATUA MIGOGORO INAYOSABABISHWA NA ATHUMANI MATUTA NA TIMU YAKE. HATA KWENYE VITUO MBALIMBALI VYA POLISI KAMA MBEZI KWA YUSUFU JINA LA MTU HUYU SIO GENI.
    HUU NI MFANO WA MIGOGORO YA ARDHI INAYOTOKEA:- ATHUMANI MATUTA NA GROUP LAKE WAMEUZA SHAMBA LA MTU MWINGINE AMBAYE (MMILIKI HALALI) KWA MTU A, MTU A BAADA YA KUPATA TAARIFA KWAMBA LILE SHAMBA AMETAPELIWA NAE ANALIUZA HARAKA KWA MTU B, MTU B NAE AKIPATA INFORMATION HARAKA ANALIUZA KWA MTU C.
    IMEFIKIA HATUA KWAMBA MTU UKITAKA KWENDA KWENYE ‘SITE’ YAKO LAZIMA MUWE SI CHINI YA WAWILI, TENA WOTE MMEBEBA SILAHA ZA JADI KAMA SIME NA MIKUKI ILI KUJIAMI NA SHAMBULIO LA WATU HAWA.
    KITU CHA AJABU NIKWAMBA HUYU JAMAA KUFANYA UTAPELI WOTE BADO SHERIA INASHINDWA KUCHUKUA MKONDO WAKE. HATA UKIMPELEKA POLISI BAADA YA MUDA MCHACHE ANAACHIWA, ANAPITA MITAANI AKIJINADI “MIMI NIMEFUGWA JELA MIAKA 18 HAKUNA MBWA YEYOTE ATAKAYENITISHA KWENYE ARDHI HII”
    KINGINE NIMEGUNDUA HAYA MABARAZA YA KATA HAYASAIDII CHOCHOTE HASA PALE KIBAMBA, WALE WAZEE WAKIPEWA SHILINGI ELFU 5000/= TU. BASI WANAPINDISHA SHERIA, HIVYO HAKUNA MSAADA WOWOTE.
    SERIKALI TUNAOMBA MTUPIE JICHO SUALA ILO ILI KUZUIA UMWAGAJI WA DAMU KAMA SEHEMU NYINGINE.
    WAKO:-
    RAIA MWEMA
    KATIKA POLISI JAMII.

    ReplyDelete
  12. HONGERA SANA WAZIRI MASHA WEWE NI MTENDAJI KAZI MZURI SANA NDO MAANA HATA RAIS ALIKUTEUA. UNA DESERVE

    ReplyDelete
  13. Hivi ile ripoti ambayo Mwema alisema atatoa baada ya wiki mbili kuhusu uhalali wa raia kumiliki pingu, ameshafanya hivyo ?

    ReplyDelete
  14. hongera sana mhe masha, wewe pajazzz hiyo club ipo juu sana Moshi inaitwa club Makumba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...