Maalim Seif

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad anatarajiwa kuhutubia katika mkutano wa kihistoria utakaofanyika East London leo.

Mkutano utazungumzia umoja miongoni mwa Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kwa manufaa ya Watanzania.

Watanzania wote bara na visiwani mnakaribishwa kuhudhuria mkutano huu utakaofanyika
Barking Abbey School Leisure Centre,
Woodbridge Road,
IG11 9ET,
Leo Jumamosi ya tarehe 13 Februari 2010,
kuanzia saa 1.30pm.

Train station ya karibu ni Upney station
(dakika 5 kutembea).
Kwa maelezo zaidi piga simu 07535656346.
Kwa niaba ya Maalim Abdallah (ZAWA).
Wote mnakaribishwa.
Zenjydar Community Association.
www.zenjydar.co.uk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. HAINGII AKILINI MASWALA YA TANZANIA YAJE YAZUNGUMZIWE LONDON HUO NI UTUMWA WA MAWAZO, KWA WAZUNGU WENYEWE HAWATAKI WA-AFRIKA HIVI HADI LINI TUTAWAKUMBATIA HAWA JAMAA AMBAO HAWATUTAKI, KILA KUKICHA WANAWEKA MASHARITI MAGUMU YA KWENDA KWAO, NI BORA TUWAKUMBATIE WACHINA AMBAO WANANYESHA UTU KULIKO WAZUNGU, TUTAKIWA KUJIKOMBOA NA NJIUA PEKEE NI KUPATA VIONGOZI VIJANA WENYE MTIZAMO WA KISASA TUACHANE NA HAWA WAZEE. EUROPE HATAKI WAFRIKA TUACHANE NAO KABISA NA NGOJENI DAVID CAMERON AU PM NDO MTAONA

    ReplyDelete
  2. we mdau ni mjinga mpunbavu ujui africa baada ya kuwafukuza wangu sasa kilicho baki tunazulumiana wenyewe kwa wenyewe. ujuwi kitendo cha kuwafukuza wazungu leo hii kimetugalimu sana leo hii africa kila pande nchi zina zungumzia ufisadi unao fanywa na viongozu wetu wenyewe kiongozi hajali kumuona raia wake wanakufa kutokana na uwongozi wake yeye mbovu na anaona ni bora akachukua mamilioni ya pesa kwenda kujilimbikizia mwenyewe bira kujali leo hii kira siku kuna watoto na kina mama wanakufa kutokana kukosa matibabu . kwaiyo swara la africa ni kwanza kwa sisi waafrica kujitosheleza ktk nafsi au kujiona umuhimu wako pale unapo pata nafasi ya kuchaguliwa na wana nchi wako kuliko kukaa na kuwapigia makerere wa zungu wakati sisi ndio tulio wafukuza kwetu tukijua tulikua atuna huwezo wa kujitawala wenyewe kutokana na uroo wa watu wachache kuwatawara wenzao kwa gia kua tuna baguliwa sasa leo hii atubaguliwi . we mdau unaonekana ujawai kufika ughaibuni nini ? ni vibaya kusema ni bora kutawaliwa ila si vibaya kusema ni bora kutawaliwa ukichukulia leo hii tunayo yaona viongozi wetu wanayo tufanyia kwa kusaini mikataba mi bovu ya wazungu pamoja na nahao wachina wanao panga nao matokeo ya kuwapa pasenti katika mikataba mibovu kwaiyo tukitaka kuendelea sisi waafrica ni razima kwa sisi wenyewe kujituma na kuwacha kubaguana na kujitosheleza ktk nafsi sio kuwaraumu wazungu kila kukicha na tukiamka asubui tunamkia kwenda kuwaomba chakula ukijuwa atuwataki . unajuwa unapokuja kuniomba kitu mimi ni la zima nikupangie masharti ili niweze pata faida kutokana na njaa yako na ntatengeneza mazingira ya kukunyonya na kukutumia kila siku.wewe unafikilia mchina aje hawekeze africa bura bila kupata faida . [mweu we. shwani kabisa] africa ilikua bado mda wake wa kujitawara na ndio mahana matokeo yake tuna yaona leo hii

    ReplyDelete
  3. WEWE MDAU UNAYELALAMIKA HAPO JUU NA KUMUITA MWENZIO MJINGA NA MPUMBAVU HAJAWAHI KUFIKA MAJUU, UNASIKITISHA SANA HIVI UNAWAJUWA WAZUNGU AU UNASIKIA KWENYE LUNINGA TU! HIVI NANI KWA KUAMBIA WAZUNGU SI MAFISADI, HIVI NI NANI WALIWAHONGA WATANZANIA ILI TUNUNUWE RADAR YA KIJESHI AMBAYO WALA HATUNA MAHITAJI NAYO NA WALA HATUNA NDEGE ZA KIVITA NA WALA HATUKUWA NA UWEZO WA KUNUNWA TULINUNUWA KWA PESA YA KUKOPA, WAULIZE HAO WALIO MAJUU WANAVYOISHI USIWAONE WANARUDI HOME NA NYUSO ZA FURAHA UKADHANI WANATOKA KUOGA ASALI NA MAZIWA, IT IS REAL HARD LIFE SI MCHEZO WAZUNGU WANAFIKI WATAZUNGUMZA KINYWANI LAKINI MATENDO YAO NI OVYO, UKIMUONA MZUNGU ANAIPENDA NCHI KUNA JAMBO ANALITAKA KUTOKA KWA NCHI HIYO SI BURE, POLICY ZAO NI MBAYA KWA FOREIGN COUNTRIES HASA ZA AFRICA UKITOWA ZILE WALIZO NA MASLAHI YAO UKUBALI USIKUBALI NI HIVYO NA HATA WAO NI MAFISADI KUPITA KIASI HIZI NCHI ZA KWETU WAMERIDHI HIVYO VITENDO VYAO. SO NI UJINGA NA UPUUZI KWENDA KUZUNGUMZIA MAMBO YETU KWAO HIVI UMEONA LABOUR, CONSERVATIVE, LIBRAL DEMOCRAT WAKIJA BAGAMOYO KUZUNGUMZIA MASWALA YA SCOTLAND, NI U-ALI NACHI TU. NIMEISHI SANA ULAYA NA BADO NIKO HUKO NAYAONA HAYA NINAYOYASEMA NI WATU WA OVYO TU NA NI WABAGUZI KUPITA KIPIMO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...