Kijana huyu mzaliwa wa Tanzania anayejitambulisha kuwa ni raia wa Uingereza akiwa chini ya ulinzi baada ya kudakwa katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar akidaiwa kutaka kusafirisha madawa ya kulevya aina ya Cocaine maarufu kama bwimbwi pamoja na Bangi ambavyo inadaiwa alivificha katika vinyago na pindo za suruali.
Kamanda wa kikosi cha polisi uwanjani hapo, Afande Mwajuma Kiponza alisema Maunga alikamatwa baada ya kukaguliwa katika mashine ya kawaida wakati akiingia uwanjani na akafanikiwa kupita.
Alisema baadaye polisi walimtilia shaka na kuamua kumkagua zaidi maungoni na kumkuta akiwa na pipi 69 za dawa za kulevya aina ya Cocaine na gramu 610 za bangi.
Kamanda Mwajuma alisema Maunga (35) alikamatwa juzi saa 1.30 asubuhi wakati akiwa njiani kuelekea Ungireza, ambapo alikuwa abiria wa Shirika la ndege la Uingereza na paspoti yake ilikuwa na namba 10948353, iliyotolewa mwaka 2007 nchini Uingereza.
Baada ya kumtilia shaka askari walimpekuwa kwa njia ya kumpapasa maunguni mwake ndipo walimkuta amehifadhi pipi 16 kwenye upindo wa suruali aliyokuwa ameivaa.Kutokana na kukutwa na pipi hizo alipekwa kituoni pamoja na sanduku kwa ajili ya ukaguzi zaidi ambapo ndani ya sanduku hili kulikutwa vinyago vitatu, viwili vilikuwa na taswira ya binadamu vikiwa na pipi 39 aina ya kokein pamoja na bangi.
Katika kinyago kingine ambacho kilikuwa na umbo la mfano wa kifaru ambacho kilikuwa kimechongwa kwa ndani na kuwekewa mfuniko kilikuwa na bangi.“Hii njia iliyotumika ni mpya hivyo ci changamoto kwetu kwani kutokana na jinsi vilivyokuwa vimehifadhiwa mashine hazikuweza kugundua na mzigo ulikuwa umeshapita katika ukaguzi,” alisema.
Mwajuma alisema mbali na kuhifadhi katika vinyago hivyo pia pipi nyingine 14 walizikuta zikiwa zimehifadhiwa ndani ya pindo la suruali iliyokuwa kwenye sanduku la mtuhumiwa huyo.Kwa mujibu wa Kamanda, awali Maunga alikuwa raia wa Tanzania kabla ya kubadilisha aliingia nchini wiki mbili zilizopita na alifikia Kijitonyama kwa jamaa zake.
Kamanda alisema mtuhumiwa alipokamatwa aliulizwa kama alikuwa ametumwa na mtu kusafirisha mzigo huo alikanusha na kudai ni wa kwake na alikuwa akiupeleka Uingereza. Alisema thamani ya madawa hayo haijafahamika na mtuhumiwa anatarajia kupelekwa katika mahakama ya kisutu leo.
Kamanda Mwajuma alisema hilo ni tukio la kwanza kutokea tangu kuanza kwa mwaka huu, na kuongezea kuwa kikosi chake kiko macho sana na matukio kama hayo.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar, Afande Mwajuma Kiponza, akionesha 'bidhaa' alizokutwa nazo Maunga


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

  1. hii kali,
    sasa mi sikatai kwamba unaweza ukayapitisha madawa hapo,DAR na akifika Uingereza atapitaje,manake pale lazima wamnase...manake huwa wanasachi tena,hawatilii mkazo sana kwa ndege zinazotoka NorthAmerica,Australia,Schengenstates,Uswiss.

    Kijana tayari ana makaratasi,sasa ataenda kunyea debe Bongo,ndio maana napachukia Bongo

    ReplyDelete
  2. serikali inabidi kufanya juhudi za ziada vijana wengi wameingia kwenye wimbi hili la kutoa madawa Tanzania na kupeleka Uingereza,askari wawe makini sana na vijana wanaosafiri na direct flight toka Dsm hadi Uk.hasa British Airwayz. na Kenya Airways.pia kuna genge la wanawake wanabeba madawa hayo.hao waliopata pasipoti za Uingereza watizamwe sana.na wanafunzi wanaosoma Uk

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha kuona polisi wetu leo ndo wanangundua njia hii ya kusafirisha madawa yakulevya. Njia hii imeanza kutumika tangu mwaka 2001.

    ReplyDelete
  4. Ama kweli...

    MSAFARA WA MAMBA, KENGE HAWAKOSEKANI.

    Pole Kaka, Jiandae kuvuna ulichopanda..!!

    Network Engineer (NE),
    Reading, UK.

    ReplyDelete
  5. tobaaaa yarabi, mungu wangu yesu kristo..... sasa wala vumbi wamepewa rungu... diaspora mtakomaaaaaaa.....

    ReplyDelete
  6. Msameheni! Anatafuta maisha huyoo!

    ReplyDelete
  7. watu kama hawa ndo wanaotuharibia majina sie watanzania ambao ni UK citizens,, what the hell was he thinking?? he wouldnt even go further than that na vipipi vyake kwenye suruali in UK airports,,, security is more advanced now, im sure huyo Maunga haangalii news and he is not a frequent flyer,,

    Im sure he will enjoy the rest of his precious time that he was dreaming of in the cells of Tanzania,,,Aibu tupu!!

    ReplyDelete
  8. Ayaaaaaaa Si Bora ungebeba Box tu kuliko kujitesa na kulazimisha Utajiri? Subiri tu Wakuweke Banged Up Abroad UK TV au Locked Up Abroad US TV. Pole Kaka Eh ndio Haramu ya Usafiri huo. James.

    ReplyDelete
  9. ajali kazini , pole mshikaji,na wacha ugumu ungelitoa kalaki tu hapo nina uhakika ungepita bila kusachiwa,mimi nimekatiza saba hapo, hapo ni pesa kuanzia mlangoni mpaka unaingia kwenye ndege hata kama huna unga! na ukiwapa mpaka hand laggage watakubebea mimi ndio nawa pendea hapo tu,umepita siku na saa mbaya. asubuhi kila mtu kaamka na kisirani chake

    ReplyDelete
  10. Duh! mbona soo. Ila ndo mambo ya dual citizenship hayo,kama angekuwa na passport ya Tz wala wasingemtilia shaka kwani alikuwa keshasevu kwenye mashine.

    ReplyDelete
  11. wanataka pesa za haraka ili waje hapa Tz kutia nyodo asanteni polisi kwa kazi nzuri mlio ifanya kabla ya kijana kutoka katika anga ya Tz kwani angekutikana na manyago hayo kule Uk ingekuwa aibu kwa nchi kama ilivyoaibika Nigeria hususana ukiangalia sisi tunawahitajia waingilishi katika bajeti zetu za nchi

    ReplyDelete
  12. Haya tena Diaspora ndio hiyo.

    ReplyDelete
  13. POLE SANA MAUNGA SASA HAPO NDIYO UMEFIKA . KWANZA UTAFUNGWA KIFUNGO CHA MAANA NA PILI WATAKUKUNGUTISHA NA TATU BANGI LAKO WATALIVUTA WENYEWE HALITUPWI HILO NA NNE UNGA WAKO WAATAUUZA KWA HAO JAMAA ZAKO WALIOKUCHOMA. NA MWISHO HIYO NDIYO BONGO!!

    ReplyDelete
  14. OOh sasa nimeishapata majibu, ndio maana jamaa wanalilia "dual citizenship"!!!!!!!!!

    Hapo angetumia passport yake ya Tanzania hata wasingemjua kuwa ni raia wa Uingereza, na angelifungwa au hata pengine angepata dhamana tu angetoroka kurudi kwao Uingereza kwa kutumia passport ya Uingereza, kwani passport yake ya TZ ingekuwa confisticated na vyombo vya dola.

    Hivi serikali itaweza kweli kumonitor hii "dual citizenship"? Au tunataka kuwapa wahalifu mwanya?

    ReplyDelete
  15. Yes I can......What about you?February 17, 2010

    Je kesi kama hiyo atakula mvua ngapi hapo??Wabongo bana sasa huyo atafungiwa huko uingereza au bongo??

    ReplyDelete
  16. ah wangemuacha tu usawa huu sio wa kulostishana watu wanatafuta maisha jamani bongo yenyewe nyie mshaiharibu haikaliki sasa mnataka watu wakale polisi???
    ha'fu mngemrudisha nchini kwake UK atashtakiwa hukuhuku.
    misifa tu nyie mbona mmejaa rushwa kila upande ah!!

    ReplyDelete
  17. Yaani huyu jamaa jina lake "Maunga" hahaha kiboko. Ndio maana tunasema wapeni watoto wenu majina mazuri. Sasa "Maunga" anaishia kuuza "Unga" aka "Maunga"

    ReplyDelete
  18. Angelikamatwa Uchina au Iran, Thailand ndio ingekuwa mwisho wa maisha yake. Ni kweli itakuwa wenziwe walimchoma maana inawezekana kawazima watu pesa zao au "kamkopa" demu kamlostisha ataondoka naye kisha kamuacha solemba!

    Na nyie mnaosema eti anatafuta maisha, maisha hayo ndio ahatarishe uhai wa wenzie? Hivi mmeshakuwa na ndugu ambaye ni addicted mkaona tabu yake? Uhai wa watu kibao uliopotea kwa madawa ya kulevya, huyo ni sawa na terrorist huyo, ndio hatakaa akanyage tena UK maana watamvua huo uraia wao, mbona kunyang'anywa uraia ni rahisi tu!

    ReplyDelete
  19. hatupwe jela tu.kosa lake limedhibitishwa,kidhiti kamatwa nacho,isichukue muda mrefu apigwe miaka tu.

    ReplyDelete
  20. U do da crime do da time.

    ReplyDelete
  21. huyu itakuwa amechomwa na wenzake kama alipita kila sehemu na mashine hazikujua.itakuwa kuna watu kazulumiana nao wamemchoma.

    lakini serikali iwe makini na watu wanaotoka Brazil na wanaotoka UK kuja kwa wiki mbili au tatu.vijana wengi Uingereza ni wauza unga.hata kina dada wako wengi kwenye biashara hii.

    vijana wanaosema wanakwenda kupiga muziki ulaya watizamwe sana.kuna mabondia wanabeba unga kwa kisingizo wanakwenda Uk kupigana ngumi.

    kuna vijana wenye asili ya Zanzibar wako Uingereza ni vinara wa genge hili. inatia aibu wenzetu wakipata fursa hizo wanatumia kupata elimu na fursa zingine sio kuuza unga.Tanzania hivi sasa iko juu kwenye biashara hii.

    ReplyDelete
  22. Mnapiga kelele za nini? Mbona waingereza wenyewe original kibaooo wako lupango Thailand, hongkong na juzijuzi wachina wamemdedisha mmoja . Jamaa kateki risk na mnaongea sababu kadakwa je angepenya je? Nakwataharifa yenu hapo bongo mzigo unapita vibaya mno jamaa dizaini atakuwa hajakamilishiana vizuri na askari.

    ReplyDelete
  23. HUYU NI KIDAGAA ANATAFUTA RIZIKI YAKE YAKO MAPAPA NA NYANGUMI,YALIOANZISHA KULETA MABASI YA MARCOPOLO KUTOKA KWA RONADINHO NA KILA BAADA YA MIEZI SITA SPEA ZINASHUSHWA BANDARINI DAR KUTOKA BRAZIL NA MPAKA WAKUU WA VITENGO WANALIJUA HILO.LAKINI KAMA MTU ANACHNGIA MILIONI 600 YA KAMPENI YA CCM ATAKAMATWA HUYO?WE ARE NOT SERIOUSLY BWANA,POLE DOGO NAWEWE WENZIO WANAKULA WE UNAWEKA KWENYE PINDO LA SURUALI, UBONDIA UNAUTAKA LAKINI UNAOGOPA MANUNDU.

    ReplyDelete
  24. DA HUYU JAMAA KAKOSA MSHAURI MZURI,INAELEKEA HII SIO SHUGHULI ZAKE KABISA NA HATA KAMA NI SHUGHULI ZAKE BASI HIZO MARA ZA MWANZO ALIKUWA NA BAHATI KWELI,KUBURUZA SIKU HIZI HAMNA MPANGO KABISA NA HATA KAMA UNABURUZA WATU WANAKUPA RAMANI SASA YEYE NA VINYAGO VYAKE ALIKUWA CONFIDENT KWAMBA ATAPITA KWA MWALIMU NA HEATHROW PUMBAVU SANA.HATA KAMA ANGEPITA KWA MWALIM KWA MAMA WANGEMDANDIA KWANI HATA KUPAKI KWAKE KWA KISHAMBA.VIJANA ACHENI TAMAA PIGENI BOX HII MICHEZO SIKU HIZI IMESHASTUKIWA EEEH,NA HATA KAMA UNAFANYA USIFANYE MICHEZO YA KITOTO KAMA HIYO HAKIKISHA UKIPIGA MOJA UNAYATOA KISAWA SAWA,SIO NUSU MFUKO UNAKWENDA KUKUNYESHA DEBE.

    ReplyDelete
  25. nyie mnacheza sana wote kadakwa huko bongo ndo kapeta huyo kuliko angedakwa nchi za watu huyo atatoka tu bongo tambarare maisha kokote ndo uanaume kaka usijali watu wanauza hayo mambo wengine wana miaka 20 na hawajaenda jela na matajiri kwelikweli maana kazi nyingine zaumiza zinazeesha na kuchosha ndo maana ukaona ujaribu bahati yako ila kuna mtu kakuchoma tu kaona ukifika utawin loh ndo maisha hayo bongo ankalaaaa tu kuna magwiji hapo bongo yanauza na yanakamatwa na yanatoka ukizimwaga ankala tu upo uraiani na kurudi uingereza!

    ReplyDelete
  26. DUAL CITIZENSHIP!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  27. AHENI UJINGA NYIE MANOZUNGUMZA DUAL CIIZENSHIP..LOWASA ALIYEKUTIENI HASARA MAMILION MBONA HAMZUNGUMZII NA MWISHO MTAMPA KURA ZENU MULIVYOKUWA WAJINGA...KILA MTU ANA TAMAA..JAMAA ANATAMAA KAMA WALIVYOKUWA WENGINE...TENA MULIVYOKUWA WAOGA HATA KUANDAMANA MNASHINDWA MNABAKIA KUPIGA MIYOWE MLETEWE MISAADA TU MUTIE NDANI...FANYENI KAZI KWA BIDII ZOTE MUONE MUNGU KAMA HAJAKUPENI...NA HUYU JAMAA NI MJINGA TAMAA IMEMPONZA LAKINI NINA AMINI HABARI HII NUSU NUSU.....NAOMBA KAMA KUNA MTU ANAMJUWA HUYO UINGEREZA AJITOKEZE???na haimanishi akiwa na briish passport ndio ya halali....aulizwe kwanza ni ya halali isije ya kule dubai...waliomuuwa kiongozi wa hamas....

    ReplyDelete
  28. watu wengine bwana. heti anatualibia jina letu la tz kwa waingereza, kwani wale waingereza wanajeshi walio mfanya kitendo cha ajabu na kimua yule dada yetu mtz na kwenda kumtupa kule bahari bech wamewahalibia waingereza wote. yule kakamatwa na na ujinga wake na atamalizianao na police wa tz na tz itamaliziana na serekari ya uingereza sio kunyoshea vidole vikundi furani ndio vinavyo fanya shughuli hizo wakati hapa uk kuna watu wengi tunawajua walikua wanafunzi na leo hii wako ndani kwa sababu ya kuuza unga au ni wa geni na hapa uk. mtu yoyote ambae yupo hapa toka miaka ya 90 hawezi kusema hivyo. japokua tz ndio inayo hiitaji uingereza kuliko uingereza inavyo hiitaji tz, kwaiyo uyo jamaa atakufa na msaraba wake tu . msiwe mnazungumza ujinga kuna watu tunawajua na wanahuusiano na wauza unga hapa uk.

    ReplyDelete
  29. jamani kama mmeshidwa kubeba maboksi si mrudi kisarawe mapori yako kibao mkalime mlifikiri ulaya maisha ni che shame on u

    ReplyDelete
  30. Hizi sheria za madawa ya kulevya ni za kibaguzi.

    Binaadamu anatakiwa awe na uhuru wa kufanya analotaka kwenye mwili wake na akili zake . Anayetaka kubugia bwimbi iwe ruksa, anayetaka kujinyonga iwe ruksa.

    Watumia bwimbwi tunaonewa.

    ReplyDelete
  31. Huyu jamaa atafungwa kidogo tu then atarudishwa kwao...hahhahahah Bongo Tambarare....

    ReplyDelete
  32. TATIZO HAYO MACOMMENT YOOOTE MLOTOA HAWEZI KUYASOMA WALA KUYAONA KWAHIYO HAIWEZI MSAIDIA KITU...BORA TUSHAURIANE SIE TULOBAKI NJE KWAMBA TUFANYE KAZI ZA HALALI HASA TUKIPATA HIZO NAFASI.

    ReplyDelete
  33. HIVI KWA NINI MAAFANDE WENGI WANA MAJINA YA ABDALLA, SAID, MWAJUMA OMARI, BAKARI NA WANAVYEO VIKUBWA TU KWANI NINI?

    ReplyDelete
  34. KUMBE EAPOTI KUNA POLICE? MBONA WANASHINDWA KUKAMATA WANAOTUIBIA MABEGI YETU TUKIJA KUWASAIDIA KULA VUMBI?

    ReplyDelete
  35. huyu jamaa hajanaswa na polisi ila amechomwa tu na watu roho mbaya,Kwanza hayo madawa sio haramu kwa kuwa wazungu wanatunyanyasia ndugu zetu sana mfano kule Palestina na kwengineko wameleta mfaruko kila sehemu na hii ndio njia pekee ya kuwamaliza wao wanatumia marisasi si tutatumia njia hizi tu kuwamaliza maisha yao tutawauzia hadi watie akili (ugiriki)

    ReplyDelete
  36. Okay, kijana kashikwa mimi nadhani sasa Mheshimiwa Kova afanye kazi ili huyu kijana asema ameyatoa wapi siyo kucheckelea tu, kwa jinsi ananvyooneka na mbinu alizotumia ingawa inawezekana ndiyo njia ya kisasa zaidi badala ile ya kumeza, huyu Maunga lazima anatumiwa sasa huyu aseme hata ikiwezekana apelekwe ikulu huyu akaseme hao watu huko...tumechoka vijana wanathirika mtaani

    ReplyDelete
  37. michuzi kwanza nakupongeza kwa kazi nzuli sana unayofanya mungu akubaliki kwa kweli watanzania hivi sasa wanatia aibu sana kwa madawaya kulevya apa uk tunawekwa kwenye black list kwa ajili ya wapumbavu kama awa muuza unga na muuaji akuna tofauti naomba tanzania kazeni buti kilo kibao zinapita hapo kuja uk aliemchomea nampa pongezi alikua anakuja kuua sasa akanyee debe jamani pelekeni majina wapo wengi apa uk

    ReplyDelete
  38. MICHUZI BIG UP TUNASHUKURU SANA KWA KAZI YAKO NZULI UYU MAUNGA KWA KWELI AMECHOMWA AIRPORT BONGO NA ALIKUA HANA PESA WANGEMSINDIKIZA NDANI YA NDEGE WANATUWEKA WATANZANIA KWENYE BLACK LIST HAPA UK SASA HIVI SASA ANAENDA KUOZA SEGEREA AMESHAPATA BTSH PASS BIASHARA NYINGI TU ZA KUFANYA UTAJILI WA HARAKA HAKUNA SASA HIVI WATU WAANZE KUWATAJA MIUZA UNGA TUSIARIBU JINA LA TANZANIA JAMANI WANAWAKE WENGI WANAFANYA SASA HIVI APA UK IT IS TIME TO STOP THIS SHIT

    ReplyDelete
  39. MITHUPU PONGEZI KWA KAZI YAKO ILIYOTUKUKA UYU MUUZA UNGA MAUNGA APIGWE MIAKA 30 AKILI ZAKE SIO NZULI NA WAKO WENGI SANA WANAPITA HAPO AMECHOMWA NA AKUWA NA PESA POLISI AIRPORT DAR ES SALAAM POCHI LAKO TU KIKUBWA KWANINI WANAFANYA NI UUAJI KABISA WAKO WENGI SANA APA UK MAPOPO WAMESHAACHA HII KAZI SASA VICHAA WAMEPEWA LUNGU WAKIPATA PAPER BADALA KUSOMA LONDON DAR UNGA AMKENI JAMANI TUMIENIPAPER ZENU VIZULI

    ReplyDelete
  40. HAHAHAH MDAU HAPO JUU UMENIFURAHISHA SANA ETI!! EAPOT KUNA POLISI,JAMAA KACHOMWA VINGINEVYO INGEBAKI KUWA VILE VILE EAPOTI HAKUNA POLISI,KUDADEKKK BONGO TANBARAEEE HAMSHIKI MTU.... MPAKA ACHOMWEEEE POLISI GANI NYINYI.

    ReplyDelete
  41. Huyu na uraia wa huko keshaupotesha....Kama passiport kaipata 2007 hivyo hakuzaliwa huko....hivyo ukiwa naturalized citizen ukafanya felony crime ...gado ikisema guity tu basi wanakurudisha nyumbani kwenu ulikozaliwa....

    Muulizeni Baloon boy momma (Mayumi) kwanini aliplea guilty haraka haraka aishie na mistedomina charges tu. Wangeendea na soo wangemkuta guilty basi angerudishwa kwao....NATURALIZED CITIZEN TUNAISHI HUKU LAKINI TUNATEMBELEA KWENYE KAMBA...VERY THIN LIKE....

    ReplyDelete
  42. Hellow Tanzania... Endeleeni hivo hivo wanangu.

    Marketing Officer
    TBC.

    ReplyDelete
  43. my boyfriend what????

    imekuweje tena jamani uwiiiiiiii,sasa paper zetu jamani tuzopata 2007 ndo yaweje tena mwezio sijui nifenyeje apa!!

    ReplyDelete
  44. wee unaeuliza majina ya polisi eti abdala,mwajuma,said nk

    hahahahahaaaaaaaa huna jibu jamani?grow up tizama kwa jicho la tatu

    hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  45. ujinga wake huyu mjoba uwezi kuweka pipi kwenye mapido ya suruali....je uingereza angepita wapi???
    mdau money uk

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...