Mkuu wa wilaya ya nanihii na wanajamii,
Kweli nilijisikia nipo nyumbani jumamosi ya 20 Jan 2010 nilipokuwa vekesheni mitaa ya kandokando ya Mto Thame karibu na Jicho la London mbele ya NATIONAL GALLERY pale nilipokutana na kibanda cha mduara kilichotengenezwa kwa kupamba picha za watu weusi, wakina mama na watoto.

Nilivutiwa kwa kuona wanafanana na waafrika nilivyosogelea nilizidi kuchanganyikiwa nilivyosikia wimbo ambao sikujua unatokea wapi kwani huoni spika wala redio kwani sauti inatoka ndani kwa ndani kwanye kuta za mduara huu, niulize basi ni nyimbo gani ilikuwa inaimbwa?

kwa kweli ilikuwa ni nyimbo inayohusu mateso waliyoyapata na wanayoyapata wakongo wakati wa vita na nyimbo hii ilikuwa inaimbwa kwa Kiswahili, niliganda hapo kwa zaidi ya nusu saa na kujisifia mbele ya wengine waliofika hapo kuwa mwimbo naufahamu na ni lugha yangu ya Kiswahili. Nadhani unaweza kupata picha upo nje ya nchi yako nchi ambayo haiongei Kiswahili halafu unakutana na nyimbo au makala au watu wanaongea kiswahili.

Wadau wanaweza kutembelea pale sina uhakika kile kibanda kitakuwepo kwa muda gani, kimewekwa na Oxfam. Kila picha inamaelezo jinsi ambavyo muhusika alipata kasheshe wakati wa kukimbia vita inasikitisha kwa kweli.

Benedict Kimbache
Skype Name: Kimbache1

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Bila shaka walikuwa wakifanya juhudi za kuomba misaada kuwasaidia hao wahanga wa vita, Je ulichangia lolote kwenye bakuli lao? Au ulifaidi tu muziki wa bure?

    ReplyDelete
  2. hapo juu ha ha haa uuwii bila shaka hakuchanga!

    ReplyDelete
  3. NI RIVER THAMES SIYO THAME

    ReplyDelete
  4. Unaekosoa kuwa ni river thames si umeelewa? Nadhani mdau hakulenga sana kuelezea huo mto; yeye alilenga zaidi ktk kujivunia uafrika wake pamoja na kuelezea furaha yake baada ya kusikia lugha yake ikitumika katika wimbo nchi na mahali ambapo hakutegemea kusikia kitu kama hicho.

    ReplyDelete
  5. Hapo juu acha hizo,aliyekuambia kuwa ni kibanda cha kuombea misaada ni nani,,maelezo yake umeyaelewa....? au unaropoka tu,,yasome upya dogo.

    ReplyDelete
  6. MI NABISHA WIMBO GANI UPIGWE NUSU SAA NZIMA? NAWEWE UMESIMAMA TUU UNAUSIKILIZA?

    ReplyDelete
  7. Wewe unaebisha wimbo kupigwa nusu saa nzima wenda hujua "repeat track" kwenye nanihiiee. Au huna hakika kuwa sometimes mtu akisema "wait a minute" unaweza kusubiri hata zaidi ya dakika tano [hata wazungu].

    All in all, mdau emejisikia raha kusikia wimbo wa Kiswahili, na pia kuona AFRIKA ikikumbukwa Ulaya... halafu mzuka wake ukapanda akatushirikisha. What a wonderful moment ....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...