Miss TZ 2009 Miriam gerald

Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald 22 pamoja na rafiki yake wa kiume, Kennedy Victor, jana walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kujeruhi na kuharibu mali katika ukumbi wa TPDC uliopo Mikocheni jijini Dar.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa na mwendesha mashtaka Nassor Sisiwaya mbele ya hakimu, Kweye Rusema, alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo katika ukumbi wa TPDC, Mikocheni.

Rusema alieleza mahakama kuwa tukio hilo mbali ya uharibifu wa mali, mmoja wa watu waliokuwepo ukumbini hapo, Shaban Moshi alijeruhiwa na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Mbali ya kujeruhi, vurugu hizo zilisababisha kuvunjika kwa amani na utulivu ukumbuni hapo. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka vurugu hizo zilizoanzishwa na mrembo huyo na rafiki yake na kusababisha uharibifu wa vyombo vyenye thamani ya sh. 720,000.

Baada ya kusomewa mashtaka, Hakimu Rusema alisema kuwa dhamana ipo wazi kwa watuhumiwa wote huku kila mmoja akitakiwa kujidhamini kwa 1,000,000. Hata hivyo wahusika walishindwa kujidhamini na kwenda katika mahabusu hadi Februari 25 kesi yao itakapotajwa tena.

Huyu ni mrembo wa pili kufikishwa mahakamani ambapo machi mwaka jana Miss Tanzania 2006/07 Wema Sepetu katika mahakama hiyo kwa kosa la kumfanyia vurugu mwigizaji wa filamu nchini, Steven Kanumba.
Wakati huohuo Mwenyekiti wa kamti ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga wakati akizungumza na kituo cha Radio Clouds jana jioni kuhusiana na tukio hilo alikiri kupata taarifa za mrembo huyo kufikishwa mahakamani.

“Juhudi za kumuwekea dhamana zilishindikana kutokana na muda kuwa mdogo lakini juhudi zinafanyika ili siku ya jumatatu tuweze kumtoa kwa dhamana” alisema anko Hashim.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Ama kweli, dont judge a book by its cover, haya yote ni kulewa usuper star na kubweteka, for my opinion, kwa mtu yeyote anayefahamika especially in a community kind of roles, ni vizuri awe makini na vitendo vyake hasa vile ambavyo vinaweza kuharibu image yake, kwa huyu Miss sasa hili ni doa tayari! na huyu mwanaume nadhani ndiye aliyeplay part kubwa manake men are always vishawishi.

    ReplyDelete
  2. unafuata nyayo za wema sepatu. du tutafika kweli

    ReplyDelete
  3. Hivi hawa ma miss wanamatatizo gani? yaani kama huyu ckumdhania kabisa kuingia kwenye matatizo ya kijinga hama haya, too low on her.

    ReplyDelete
  4. dah! hii kamati ya miss tz sasa inabidi wawe na kazi za ziada za kujua tabia za washiriki..
    ni kwanini wanashindwa kubehave kama
    warembo wengine waliotangulia??
    kwanini wasione fahari ya kuheshimika kama warembo wengine waliotangulia?
    ushauri wangu kwa hawa warembo wajaribu kufuata nyao za warembo wenzao walitangulia kama wakina angel damas, faraja kota, nancy sumari, hoyce temu, happy magese, na wengine wenye sifa na tabia nzuri kama za hawa!!
    ni aibu hata miezi 6 bado tayari Miss TZ keshaanza skendo, kila kukicha hawakosekani magazetini.. lol.. jamani inaboa.. mi binafsi hizi kero zimenichosha...
    jamani embu jirekebisheni.. lol..

    ReplyDelete
  5. Huyu ni ushamba tu utakuwa unamsumbua!
    Kamati ya miss Tz inabidi iwe makini zaidi, hawa viumbe huwa wanawakilisha Taifa sasa tunapata picha gani? AIBU TUPU!!
    Nadhani ungekuwepo utaratibu wa kuwavua mataji Ma-miss wanao missbehave wakati ana hold title. USA waliwahi kufanya hivo kwa Vanessa.
    Mshaulini arudi Mwanza, Jiji limeshinda.......

    Mdau H.

    ReplyDelete
  6. mimi naomba avuliwe taji, na gari ichukuliwe iuzwee pesa zikasaidie watu wasiojiweza kwenye jamii. ametukosea watanzania adabu. alaa.

    ReplyDelete
  7. Kaaazi kweli kweli.

    Umaarufu usio na malengo ni mzigo.

    Is it me, au Watanzania wamekuwa wepesi sana kwenda kushitaki Polisi siku hizi??

    NE,
    Reading, UK

    ReplyDelete
  8. jamani mimi sijui mahesabu lakini shilingi 1,000,000 ni sawa na paundi ngapi?

    ReplyDelete
  9. ..yaani na umaarufu wote wamekosa Tsh 1millioni tu ya kujidhamini??...hahah...kumbe umaarufu bongo ni wa sura tu na sio kwenye accounts...wangekuja kwangu pedeshee joji niwadhamini.!!

    ReplyDelete
  10. mbona mambo jamani hawa mamiss nahisi akili zao si nzuri loh mara hii na huyu kashaanza kashfa ya kuwekwa rumande loh wazazi mna kazi nao hao watoto ukiona hivo tu anaanza kasoro mapema mbona mamiss wengine hawana vituko vya ajabu loh!!!sijui ni kitu gani ok sifa za kijinga nahisi si bure loh!ok wanafundisha nini jamiiiiiiiii.

    ReplyDelete
  11. Ndio tatizo la kuchagua mamiss wazuri alafu low profile,
    Pia kwa wadada ni tatizo kubwa sana kudate preeeeeeeeeeeeeety boys,nendeni kwa michuzi jr mkamuone,atakuwa amemfumania Boyfriend wake ndio akamfanyia fujo,na kutokana na mwanaume wake kuwa nae na tabia za kichokoraaaaa kama uzuri wake unavyomvimbisha kichwa akakubali kuachia hali ya fujo na mrembo.
    Warembo msiangalie suru zitawatesa jamani,kwanza likaka lenyewe linaonekana limezoea kulelewa kwa kifupi mfumo wa ki Big mama boy kazi kuumiza na kuwapanga wadada wa watu

    ReplyDelete
  12. Hapana jamani naomba tuwe positive kidogo. Kwa hili mie nadhani huyu miss anaupendo wa kweli na jamii yake ndio maana akafanya kila njia ili aoneshe upendo katika sikukuu ya wapendanao akiwa rumande na mahabusu Na hiyo ni ili kuonesha upendo na kushiriki shida na Watanzania wenzetu waliopo huko. Hongera kwani hakika unaupendo wa kweli mama.

    ReplyDelete
  13. lazima tuelewe hawa bado teenagers akili zao bado hazijakomaa utoto bado mwingi hilo ndo tatizo linalowasumbua, pale wanapobahatika kuwa super stars basi wanafikiri kwamba wanaweza kufanya lolote kwani wapo juu ya sheria! Inabidi vijana hawa waende shule itasaidia sana kufuta ujinga. Tuwasamehe bure kwani sasa hivi ndo wanaingia kwenye real world na dunia inafundisha kwa mtingo huu. Ni aibu kubwa sana na imeweka doa kubwa kwenye kwa taifa.
    Sorry!!

    ReplyDelete
  14. BRO MICHUZI MAMBO VIPI ASANTE SANA KWA KUWEKA HII HABARI HAPA INATUWEZESHA NASISI KUTOA RAI ZETU. MIMI NADHANI KAMATI YA AKINA LUNDENGA INASTAHILI KUJIUUZULU HARAKA IWEZEKANAVYO KWA KUWA IMESHINDWA KAZI YA KUWALEA IPASAVYO HAWA MA MISS KUANZIA YULE WA MWAKA JANA NA HUYU ALIYEMPOKEA. NI KWELI KAMAWANGECHUKUA HATUA MUHIMU WAKATIN YA ISSUE YA WEMA SEPETU HIII ISINGETOKEA KWA KUWA WAO NI WALEZI WA HAWA WAREMBO KWA MFANO WENGEWEKA WAZI KWAMBA KWA MREMBO ATAKAYESHINDWA KUWA NA TABIA NZURI KWA JAMII BASI ATAKOSA SIFA YA KUENDELEA KITWA MISS TZ NA KUNYANG'ANYWA KILA ALICHOPEWA NA HII INGEKUWA FUNDISHO KWA VIZAZI VIJAVYO. KWA MTAZAMO WANGU MIMI NADHANI KUITWA MISS TZ NI HESHIMA YA JUU SANA NA INAPASWA KUHESHIMIKA MAANA KILA MTU ANTAKA KONA NI JINSI GANI UNAKUWA BALOZI MZURI KWA JAMII HUSIKA NA NCHI KWA UJUMLA UKIZINGATIA NA UWAKILISHI WAKE KWA NCHI .KWANZA PAMEKUWEPO NA MAKOSA MENGI YA WAZI SANA KUHUSU HAWA MAMISS WANAVYOPATIKANA NA MBAYA ZAIDI AKINA LUNDENGA WAO WAKO KIMYA KANAKWAMBA HAWAJUI KINACHOENDELEA .NA MWISHO NI WASHAURI HAO WADHAMINI WNAGALIE SEHEMU NYINGINE ZA KUDHAMINI NA WAACHANE NAQ HII BIASHARA YA KUDHAMINI WATU WASIO KUWA NA TIJA KWA NCHI NA JAMII KWA UJUMLA MDAU FINLAND KAMA KAWA KWA JINA DANI MWANA WA MKUCHU

    ReplyDelete
  15. Niwakati wa kamati ya Miss Tanzania kuwa makini zaidi na mchakato wa kuwapata warembo hawa. Mawakala wamekuwa wakiangalia muonekano tu wa mrembo bila ya kuangalia nini ambacho mremo anabeba kichwani mwake. Kwa kuangalia tu naamini warembo wanashikana nafasi ya pili ama ya kwanza kwa kufanya vitu vya kijinga, sasa huyu mtoto muda mfupi huu ameshafanya ujinga. Najua watu wanaweza anza sema lbda kaonewa but the issue ni kwamba amesomewa mashtaka that means alijiweka katika mazingira ya kushtakiwa. Brother Hashim amini Miss Tanzania itazidi kudharaulika na hata nyinyi kudharaulika, maana mtu akiwa Miss Tanzania tunaamini ni bora kwa kila kitu na bora kwa warembo wote walioingia Miss Tanzania. Tatizo nchi yetu imeingiwa na Usanii wa hali yajuu, vitu vingi tunafanya kisanii then baada ya muda picha nyiiingi kwenye blogs eti huyu ni fulani, Tanzania inasikitisha inako elekea!

    ReplyDelete
  16. Umefika wakati sasa Kamati ya miss Tanzania kuanza kuwasainisha mikataba hawa warembo njaa ya miaka miwili kuwa
    1. Akipatikana na kosa lolote liwe la jinai aua madai basi U-miss wake unakuwa revoked na kutakiwa kurudisha zawadi zote walizopata kwa kuwa washindi

    2. Akionesha tabia iliyo nje na maadili ya Kitanzania kama kugombewa na mabwana au ikibainika ana bwana au mpenzi zaidi ya mmoja ndani ya kipindi cha U-miss Tanzania yaani 1 year basi Kamati ina mamlaka ya ku-revoke ushindi huo na kutangaza kuwa mwaka huo hakuna mshindi. Maan wakipendekeza mshindi wa pili apewe watakuwa wanawindana.

    ReplyDelete
  17. tehee heee heee. Wadau mnawalaumu kamati ya miss tz wakati wao wanatengeneza pesa tu.
    Marehemu mchonga aliona ujinga huu akaupiga ribiti. Mtoto akililia topaz au okapi mpe.

    ReplyDelete
  18. Nawaomba niwaulize wooote mnaomshutumu huyu dada swali moja tu : JE, MAHAKAMA IMEKWISHAMHUKUMU NA KUMKUTA NA HATIA na nyinyi mmewasikiza mashahidi wangapi kabla ya kufikia "hukumu" yenu hiyo ya kipanya??? Tukiwa na ujinga huu wa kutoheshimu utawala wa sheria (innocent until proven guilty, tutafika kweli????????

    ReplyDelete
  19. Huyu Kennedy Victor mwaka jana alikuwa Dereva wa aliyekuwa Miss Tanzania 2008 sasa cha kushangaza sasa anaendesha /anatoka na Gari la Miss Tanzania 2009 Mmmh

    ReplyDelete
  20. hii habari iko too general fafanua vizuri asa,,,yani miss uyu aliazna tu vurugu na kuharibu mali???

    hapana ebu mtujuze fresh

    nb:ivi kumbe miss world ilishafanyika alikua wa ngapi uyu binti??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...