Mheshimiwa Michuzi,
Nami naomba kuchangia kuhusu mada ya Diaspora.
Mimi kwa upande wangu ningependa tuliangalia swala hili kwa upande mwingini Who set it ? and whos interest...
Kama Diaspora anataka kutuma pesa kwao you do not need dual citizenship, you can have a permant stay visa and still contribute to your countries and perform well in your country of residence.

Tatizo la dualcitizenship kwa nchi zetu changa kuna mengi. tukiangalia matatizo mengi kwenye bara la Africa na dunia kwa ujumla ni Diaspora... ndio hao mara nyingi wakisha nunuliwa wanachochea conflits nyingi na kusupport machafuko kwenye nchi zao mfano DRC , Eritria, etc. Matatizo mengi huko yamesababishwa au yamekuwa funded na Diaspora ambao wana tumiwa na watu wa huko walipo.

Kabla swala hili halija fanyiwa kazi ni vizuri kuwa na wataalamu wa maswala haya na kuliangalia kwa undani. sababu Diaspora sio hao tuu wanaongea kiswahili kuna diaspora ambao waliondoka nchini for more than hundred years 3 to 4 generations wanaweza ku claim citizenship as well!

Kwa upande wangu Si lazima Diaspora warudi nyumbani kama kuna mechanism ambayo ita wa accomodate ili waweze ku contribute kwenye nchi.
Diasporas who demands dual citizen hawana imani na nchi zao if you are Tanzania and you have confident with your country ,why dual citizen ship??Maana ni kwamba unataka kubaki uko ulipo na hutaki kuwa permantly Tanzania,(...) do we need those Tanzanians??(watalii)

Ushauri wangu ni kuongeza kitengo cha Diaspora kwenye foreign ministries ili kuweza kulifanyia kazi hili suala kikamilifu, kama wale ambao wananataka kurudi nyumbani ku walink na sehemu za kazi, kuwasaidia na kutoa ushauri mbali mbali kwa Diaspora ambao wako tayari kurudi na kusettle! (sio watalii)Balozi ziwaamasishe watanzania kuwa na umoja wa watanzania ili kuweza kuwa karibu na kuongelea maswala haya kwa undani kuna baadhi ya nchi zimekuwa passive kabisa kwenye swala hilo.Maana kuna watazania walisha ukana Utanzania (kujilipua) kabla hawajachukua passport za nchi nyingine lakini nao ni watanzania pia(...).
Mheshimiwa tungependa kupewa fursa ya kuchangia kuhusu swala hili kwa kirefu.
Mdau EU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Looking at this response, I must conclude that DUAL CITIZENSHIP is inevitable.

    I really couldn't understand a thing, I must say it reminds me of BRAINSTORMING session while I was in early years of my college.

    Anybody could say anything for attention, even if it entertaining the ideas from aliens.

    ReplyDelete
  2. Kwanini wachangiaji wanaopinga dual citizenship wana upeo mdogo? Mtazamo wenu uko kwenye kutumia pesa familia tu, na mnasema hatuitaji uraia wa tanzania kutuma pesa au kuwekeza kwa sababu wapo wachina, wapakistani, wazungu na wahindi wanawekeza na sio watanzania.

    Jibu kwanza sisi sio wapakistani wala wachina, sisi ni watanzania. Pili hao wote wanawekeza nakupeleka pesa kwao hawa retire hapo Tanzania. Sisi hivyo ndivyo tunafanya huku tuchume tuwekeze huko na kulala milele huo Tanzania. Sasa kama sina haki nitawekeza vipi? Unachotakiwa kuelewa, kama sina haki huko itanibidi niwekeze ambapo watoto zangu watapokuwa na haki kurithi jasho langu. Kumbuka kama haujanipa haki mimi ina maanisha mtoto wangu ndio hana haki kabisa Tanzania.
    Kwa upande wangu mimi nina uwezo wa kununua nyumba huko na ningependa ku adopt watoto yatima huko at leat wawili ili kulea watoto wanne ukijumlisha wawilinilionao. Je unaona sisi wengine mchango wetu utakavyokuwa.
    Mntakiwa muanze kufikira deep sio jujuu tu halafu mnajiona mnapoint. Bilashaka sisi tutatoam mchango mkubwa tu katika sehemu tofauti.

    ReplyDelete
  3. Mfano wa viongozi wetu waliotangulia;
    Kwame Nkruma, Julias Nyerere baada ya kutapa elimu yao walirudi nyumbani katika mazingira maguma na kusaidia kuikomboa Africa hakuwomba dula citizenship au kuchukua uraia wa uingereza kwanza.

    Sasa basi kama Diaspora wanabaki nje ni ruhusu kupewa support kama AU ilivyotangaza kama Africa Diaspora as A sixth Region of African Union.
    si dhani kama hao second or third generation za Diaspora will be going back to their countries of origin, mifano tunayo kama Turkey ambao wali settle germany after 2rd world war, hakuna aliyerudi kwao mpaka sasa.
    Kama wewe umesjindwa kurudi hataweza mtoto wako you must be joking!!
    Mwenye nia ya kurudi na kusaidia kuleta maendeleo haitaji Dual Citizenship.
    Balozi zote vifanye uchunguzi kwa kina kuhusu swala hili kabla ya maamuzi yoyote yale kufanyika tufanyike analysis.

    ReplyDelete
  4. Anayepinga uraia wa nchi 2 ana matatizo yake. hakuna tatizo kabisa vinginevyo kuna kawivu tu kinawanyemerea.

    ReplyDelete
  5. wewe umeshachokoza uanja subiri vijana waamke utapewa usahuri na majibu mazuri,wengine wamelala na wengine wako makazini sasa subiri kidogo tu jibu utapewa mi sisemi kitu nawachia vijana

    ReplyDelete
  6. Life has many choices, and every choice we make has a price to pay. Unfortunately, some of the choices we make are seriously wrong, and we end up paying hefty price in the future. Example, the chaos we have in the mining sector. As a result the victims tend to force others to pay the price of the wrong choices they have made. Dual citizenship is an excellent idea but Tanzania (Tanzanians) is/are not prepared well not only to introduce it, but also to faciliate it's effective implementation, especially in dealing with smart and sophisticated criminals/countries that will take advatantage inefficency system of our country. More time is needed to get organised. let's avoid a tendecy of embracing an idea because others are doing it.
    People, you have made your choice to become diasporas, live with it!

    ReplyDelete
  7. Mdau wa EU,

    Mimi napenda kutembea duniani kote, kikazi na kistarehe. Hii ni sababu namba moja ya kuchukua uraia wa Marekani. Leo nikitaka kupanda ndege kwenda ulaya, napaa leo leo. Wewe mwenzangu kama una pasi ya Bongo, inabidi ujitayarishe miezi sita kabla ya safari. Huu ndio ubabe wa pasi ya nchi tajiri.

    Pasi mbili au moja, sisi tulio nje tutazidi kuwasaidia ndugu zetu nyumbani. Leo tu nimepeleka dola 7000.

    ReplyDelete
  8. Mie hapa naona kuna watu ambao tayari wanajifanya kuwa ni watanzania wapo hapa tanzania na huenda ni matajiri tayari hivyo wanaushawishi kwa viongozi wa nchi na hao ndo wanataka uraia wa nchi mbili.

    ReplyDelete
  9. Natumaini huyu Bwana kipaji chake cha kuongea kina unafuu kuliko uwezo wake wa kuuandika!

    ReplyDelete
  10. Huu mjadala unatakiwa uanzie na uishie kwenye manufaa Vs. hasara na sio hizi pumba za kutumia pesa ndugu. Ndugu wanakuja na kuondoka kila siku ila umaskini sugu wa nchi upo palepale. Kwenye huu mjadala tujiulize kwa makini sana nchi zinazoruhusu hili swala (dual citizenship) zina hamasishwa na nini? Huu uswahili wa NGOJA kidogo! unauwa watu.

    ReplyDelete
  11. Tupo madiaspora wengi tuu ambao kwa manufaa ya Tanzania hatutaki Tanzania iruhusu dual citizenship. Ingawa kuna watu huko bongo mnadhania kwamba kila diaspora anafagilia swala la dual nationality. As a diaspora "danish by passport Tanzania by nature" everytime I visit Tanzania I find that I have more rights in Tanzania than Tanzanians in Tanzania.

    ReplyDelete
  12. Naunga mkono Mdau EU althoung ujajieleza vizuri but i see the point.

    Ukitaka kuridi nyumbani ruksa, ukitaka kuwa Diaspora ruksa!!

    Hawa dispora wanataka kuja ku beep Tanzania and not to settle! na ndio hao hao kazi yoa kupoint fingers and do nothing....about it

    Tatizo lenu nyinyi mnaojihita manabii wa kusingizia mnataka kula UKO na UKU!

    if your r a serious Tanzania rudi nyumbani upambane kama wengine mmesha kuwa sophisticated you can not even fit in the society ya bongo!ilichobaki ni kutafuta popurality na kuuza sura tuu.

    ReplyDelete
  13. Huyu mdau aliyeleta hoja ameongelea swala la Diaspora kutuma pesa nyumbani. Swala niko uku napiga kibarua nje na napata mshahara mzuri, ndugu zangu wako Tanzania nikituma pesa wakajenga nyumba faida ya nani kama si ya nchi, nikisomesha ndugu zangu wakapata elimu faida ya nani, ninunu vitu tuseme gari au mashine za kuwekeza faida ya nani kama nchi haikusanyi kodi. Kutuma fedha za kigeni zinakwenda wapi kama siyo kwenye akiba ya foreign currency ya nchi yetu.
    Anaongelea kuwa wenye dual citizenship wanachochochea migogoro, naomba atoe mifano inayoeleweka kwa mfano fulani alichochoea mgogoro mahali fulani siyo anaongea tu mradi tu anataka kuongea. Inakuwa kama vile Chama fulani kilivyokuwa kinasema kuwa watu msikubali vyama vingi penginepo tutaingia kwenye vita, matokeo yake tumeona michango ya wabunge wa upinzani wanavyotoa hoja zenye nguvu na nyingine Chama tawala kimechukua.
    Watanzania mara nyingi tunabaki nyuma kwa sababu ya woga na kujifanya tuko sana wazalendo kumbe uzalendo wenyewe ni kuujumu nchi.
    Mfano mzuri yule anayesema njoo ufanye kazi Tanzania utakuta mshahara wake ni laki tano au pungufu lakini mtu huyo ana gari zuri, nyumba nzuri na watoto wanasoma international schools. Jiulize pesa katoa wapi kama siyo mwizi wa mali za umma na bado anakwambia Tanzania ni nchi nzuri ya kufanya kazi. Ukiangalia mchango wake kulingaanisha na Diaspora ambaye anatoka jasho na kutuma pesa Tanzania na yule anayebaki nchini na kuibia nchi utaona nani anajenga nchi.
    Watnzania acheni woga na uzalendo uchwara

    ReplyDelete
  14. duhu fazaa ulayaa umeleza swafi sana yaani.diaspora wa nchi nyingine ndo hao hao makaburu huatumia kuvuruga amani za nchi zao africa.cheki kaa hii ya warundi waishio ulaya kuuuza nduguzao kisaa nini mshiko watu wengine kuchapa kazi hawataki wanataka miela veri izee

    mdau ulayaa almere kwa wauza ndugu zao majuuu

    ReplyDelete
  15. Wapinga dual citizenship watakuwa ni wachache wenye uwezo na wanaotaka kulinda maslahi yao. Sana sana watakuwa ni mafisadi au corrupts wenye kutaka utaratibu uliopo uendelee.
    Hofu yangu msitake kuifanya nchi yetu iendelee kuwa masikini kwa vizazi vingi vijavyo kwa manufaa yenu. Can you imagine nchi nzima wananchi wanatumia prepaid phones kwa mawasiliano?
    Imeshadhirisha utamaduni wa nchi kama za kwetu sio kutetea na kuhifadhi kizazi chake. Ukiwa nje usitegemee sana balozi kwa msaada wowote, watu wanasaidiana wenyewe. Saa nyingine haya mambo ya jumuiya za watanzania inafanya balozi zina lala.
    Umasikini ni kitu kibaya.

    ReplyDelete
  16. wacheni upuuzi nyie,minilikua bongo na kabla sijaondoka nilishasikia mtanzania anasema bora niwe mbwa wa clinton marecan kuliko kuishi hapa leo nimepata zari nipo KIWANJA napata uraia wa usa unaniambia nikatae kwa ajili ya tanzania?HELL NO!Kwa taarifa yenu DUNIANI HAPA KUNAVITABU VITATU TU, BIBBLE, KURUANI NA AMERICAN PASSPORT AMBAYO ITANIPELEKA SEHEEMU NYINGI DUNIANI BILA KUSUBILI VISA KWA MIEZI SITA.

    KAMA MNAKUMBUKA NYERERE ALISEMA KUTENGANA NI UKABURU,NCHI ZILIZO ENDELEA ZINAUNGANA E.G USA,EURO ETC.NA NCHI ZILIZO ENDELEA ZINA DUAL CITIZ,SEMBUSE BONGO?ANGALIA GERMANY,ENGLAND,AMERICA,CANADA ZOTE HIZI ZINA DUEL CITITZ.HII NI DUNIA YA UTANDAWAZI....DUAL CITIZENSHIP IS UNSTOPABLE IN TZA.

    VAMOS VAMOS, ADIOS

    ReplyDelete
  17. Mdau Hansen, KobenhavnFebruary 17, 2010

    Faida za kuwa diaspora. Ulaya, america, canada

    1) Kuishi katika nchi ambayo hakuna mizengwe ya ukitaka kung'oa jno hospitalini basi lazima dentist ashikishwe kitu kidogo, na wala huwezi kufanywa jerry muro mpaka uwe muhalifu ki-kwelikweli.

    2) Ukiishi safi na usipokuwa mpumbavu, kamwe hautapigwa hata kibao/kofi na polisi.

    3) Ukifanya kazi yoyote ile, basi una uwezo wa kumiliki gari, nyumba na kuwawezesha watoto wako kupata elimu. (Ukiwa mvivu na kuamua kuishi kwa vouchers au benefits; hasara watapata watoto wako)

    4) Ukitaka kusafiri kwenda sehemu karibu zote duniani unachohitaji ni pesa yako na pasipoti yako tuu, na huna muda wa kuamka alfajiri kuwahi foleni ya viza.

    5) Una uwezo wa kuishi sehemu zingine duniani (zaidi robo tatu ya dunia) bila mizengwe

    6) Kama upo ulaya (isipokuwa england) watoto wako wana uwezo wa kusoma darasa la kwanza mpaka phD bila ya kulipa fees.

    7)Ukiachishwa kazi, serikali inakupa pesa ya kuishi katika muda ambao unatafuta kazi

    8)Ukienda bongo unapewa haki kuliko wabongo wanaoishi bongo. Wakishakujua tuu kama wewe ni mtu wa kiwanja basi utakuwa wa kwanza kupewa huduma kabla ya wazalenzo wanaoishi bongo, na hata mwalimu wako wa kike wa zamani atakukaribisha kitandani kwake, wakati amekulea yeye mwenyewe.

    9)Unaweza kumiliki mali kama gari, nyumba na shamba ndani ya bongo kama m-bongo mwingine yoyote yule

    10)Kuishi katika nchi ambayo kama umeelimika basi elimu yako inashabihiana na maisha unayoishi.

    11)na kadhalika.....

    Hasara za kuwa diaspora

    1) Sometimes unakuwa homesick, hii mara nyingi ni kwa wale ambao hawaja-establish familia huko wanapoishi

    2)Huwezi kugombea ubunge Bongo, au kuwa mwanasiasa ili kupata "ulaji, wizi, ufisadi" (na ndo maana kuna diaspora wanataka dual nationality)

    Kwa kuangalia faida na hasara za hapo, mimi kama diaspora nasema kwamba "I don't need dual nationality". Ukizingatia kwamba naweza kuingia, kutoka, na kuishi bongo ninavyotaka.

    Kama wewe unakubali au unakataa jambo la "duality" basi hakuna sababu ya kukashifiana, badala ya kujadiliana kwa hoja zenye kueleweka.

    Naipenda Tanzania kuliko watu wengi tuu wanaoishi Tanzania, na kamwe siwezi kuihujumu Tanzania. Ingawa siishi Tanzania, ninachangia maendeleo ya Tanzania kwa kiwango cha kuridhisha tuu, kuliko watu wengi tuu wanaoishi Tanzania. Sina pasipoti ya Tanzania, lakini mimi ni mtanzania na nitabakia kuwa mtanzania ingawa nina pasipoti ya nchi ya ulaya. Hivyo basi, nyie mnaodhania kwamba eti diaspora wote wanajuta kuuchukua uraia wa nje, au eti wote tunataka "duality"; just keep believing your own lies if that keeps you happy.

    ReplyDelete
  18. Mdau mwingine mwenye kutaka kuwapotosha watanzania kwa madai yake ya ajaabu. Unaongea bila facts, eti matatizo mengi kwenye bara la Africa na dunia kwa ujumla ni diaspora! Unataka kusema matatizo ya magonjwa, ukosaji wa maji safi ya kunywa, njaa, upungufu wa zahanati na huduma bora kwa wananchi na kadhalika zinasababishwa na diaspora?! kwasababu hayo ndio matatizo makubwa yanyoikabili bara la Africa na dunia kwa ujumla. Unazungumzia conflicts ambazo unadai zinasababishwa na diaspora, hujatupa mifano hai unazungumza kwa ujumla tuu...tupe facta tupe mifano hai. Hata kama diaspora iko responsible for conflicts, tukizungumzia Africa peke yake, unafahamu ni nchi ngapi zenye conflicts...nchi 15, fanya utafiti utapata jibu. West Africa, ni Cote d'Ivoire, Guinea, Liberia, Nigeria, Sierra Leone, and Togo. East Africa, ni Eritrea, Ethiopia, Somalia, Sudan, Uganda. Central Africa, ni Burundi, Democratic Republic of the Congo, Rwanda. North Africa, ni Algeria na South Africa, ni Angola and Zimbabwe. Kwa ujumla africa ina nchi 54. nchi 15 katika nchi 54 zina conflict ya aina moja ama nyingine amabayo ni asilimia 27 tu. Kwahiyo hata kama madai yako ni ya kweli diaspora imesababisha conflicts katika asilimia 27 tu ya nchi za Africa, je hii ni sababu ya msingi ya kuukataa u dual citizenship? Kwani nikitaka kuanzisha zali bongo, kutokuwa na passpoti ya Tanzania kutanizuia vipi wakati nina mkoba wa Marekani na kja bongo ni bwelele...visa nagongewa bila shaka airport hapo? Unamaanisha hutaki watu wasafiri nje ama unmaanisha nini kwa madai hayo? unadai oooooh matatizo mengi barani africa yanasababishwa na diaspora ...your ignorant!!

    Tena unatujumuisha wote kwa kusema hatuna imani ya nchi yetu, nani mwenye imani ya nchi ambayo kupata haki za msingi lazima uzungushwe ama uhonge wakati watu wachache wanzidi kutajirika, hamna mtanzania mwenye kupenda hali hii ila hatuna jinsi. Mtanzania gani mwenye uwezo wa kupata maisha bora atachagua maisha duni? Wewe mwenyewe unaongea pumba ukiwa EU.

    Watanzania hatuko pabaya kwani tuna uwezo wa kuziangalia nchi ambazo zimeruhusu urai wa nchi mbili, kwanini tusiziangalie hizi nchi tukajifunza mema na mabaya ya mfumo huu (maanake hakuna jema lislo na kasoro, Watanzania tunaogopa nini? Njia hii haina kiza, kwanini tusiwaangalie waliotutangulia? Inachosikitisha ni kwamba itachukuwa muda lakini DUAL CITIZENSHIP IS ON IT's WAY. Kwanini because it is the right thing to do, we are living in a global village..the longer we wait the further behind we will get.

    Mdau Kichugo

    ReplyDelete
  19. Ukitaka uraia wa nje kwa haraka basi OWA au Mzalishe mtoto wao na jitahidi awe Mweupe (kama uko West). Na ukishapata makaratasi basi wee ishi zako salama. Ukijisikia vipi basi nenda Tanzania na uowe kibinti fulani hivi. Tanzania unaweza kuwa na wake wengi. Na kama umetoka Ulaya basi watakupapatikia wee hata kama una miaka 60. Ukishaowa mchezo ni uleule wa kuanza kupata makaratasi na kusubiri tu kufa.

    Hivyo msitutishe na eti hatutaki uraia wa nchi mbili. Kwanza nafanya mpango nipate gamba la huku Gabon. Nikilipata basi ntahonga wasininyang'anye gamba langu la Tanzania. Mbona ze utamu ana UK na Tz Passport? Nawafahamu watanzania wengi tu wana magamba mawili na wanayatumia yote. Nyie kalaga baho na umbumbumbu wenu wa kufikiri mnawazibia wenzenu ila ukweli ni kwamba mikono yenu ikiziba matiti, basi sehemu nyingine mnaacha wazi.

    ReplyDelete
  20. mimi kidogo naona nijitose katika huu mjadala baada ya kusoma maoni ya baadhi ya waandishi nimegundua na kujifunza mengi ya maana na yasioingia akilini,maoni yangu kuhusu hili suala la uraia wa nchi mbili au saba linaweza likaleta faida sana au hasara kubwa yote itategemea na utekelezaji wake na mazingira gani tutayaweka katika kuukubali mfumo huu kwa mnufaa ya taifa sio ya watu binafsi au kikundi cha walio nje ya nchi kwani kila mmoja ambae anatetea mfumo huu ambae ana urai wa nje huenda ana ajenda "in mind" nzuri au mbaya na wale wanaokandia mfumo huu walioko bongo huenda wana sababu zao za msingi au za ovyo katika kukubali au kulikataa suala hili nimetumia neno huenda kwa makusudi kwa sababu sina ushahidi wa kisayansi wa kuambatanisha na haya madai yangu huenda nikawa mimi niko wrong.
    sasa tatizo jengine tanzania tuna ukomunisti uliokithiri ambao hata yugoslavia hauko ingawa tulikuwa nao katika mfumo wa siasa za nchi zisizofungamana na upande wowote hawa viongozi wetu wengi na wachangiaji wa mjadala huu ingawa mawazo yao yamebadilika kiasi fulani na upeo wa siasa zao umekuwa polished kwa mageuzi yaliyotokea eastern block na ulimwenguni kwa ujumla lakini bado kizazi cha nyerere na kilichofuatia sio rahisi kukubali mabadiliko au kuwa na mawazo ya wazi"open minded" katika kutafuta ufumbuzi wenye manufaa bila kuwa corrupted na ideology za kijamaa ambazo tutakufa nazo.
    mimi nina umri wa miaka arubaini hivi nafikiri mjukuu wangu akizaliwa kwani hata uja uzito bado akifikia umri wa miaka thelasini wao wataweza kulichukua taifa letu tunakotaka lifike kwa sababu kizazi hicho kitakuwa na upeo wa kuyatafakari maamuzi ya nchi kwa mtizamo wa wakati huo na faida ya nchi zaidi kwa vile matatizo ya kikomunisti tuliyosomeshwa na kuishi nayo mpaka leo yatakaribia kikomo ndio maana mimi binafsi kwa mawazo yangu utumaji fedha kwa ndugu na hawara huko nyumbani sioni kama ndio kigezo cha kuruhusu,kama tunaruhusu basi iwe tunafanya hivyo kuondoa usumbufu kwa wenzetu hawa na kuwavutia katika kuwekeza zaidi kwenye miradi na biashara zenye kuweka vitega uchumi kwani sote tunaelewa kwa mgeni kuwekeza tanzania mfumo uliopo sasa ni bora ukawekeze katika sayari za anga za juu utafanikiwa kirahisi kuliko kukutana na urasimu wa nchi yetu ambao upo kwa nia moja tu kuimarisha rushwa ndio solution ya kuweza kuvuka viunzi hivyo ndio maana hatushindi vita hivi.
    kwa kufungia tu mimi bado nalitafakari hili sijafikia uamuzi kama linafaa au la kwa hiyo tulijadili zaidi.
    asanteni.
    billdulla.

    ReplyDelete
  21. Wengine wanataka urahisi wa kuingiza na kutoa biashara zao haramu tu, hawana lolote. Watanzania wasomi wenye maisha mazuri nje kutokana na kazi za maana ni wachache sio majority na wengi wao wanashiriki kwa kiasi kikubwa kuchangia maendeleo ya nchi kwa kushirikiana na Taasisi zilizopo kama za akademia na afya, na wala hawajakwama kisa hawana passport za TZ. Wengi wanaolilia dual citizenship ni wenzangu na mimi ambao tunahisi kama tukiingia TZ hatutaruhusiwa kutoka.

    Labda niseme kitu kimoja, WaTZ wengine wana passport mbili na biashara zao za ajabu ajabu na jinsi wanavyozitumia wanajua wenyewe na faida yake wanaijua wenyewe. Subirini mtaona matokeo.

    ReplyDelete
  22. Mdau UK, kama huoni haja ya dual citizenship, basi wewe binafsi unafanya nini UK. Si urudi hapa TZ tu. kwani hata hapa TZ vyuo viko vingi tu na sio lazima ukasome huko UK. Kama kazi basi hata hapa TZ zipo na sio lazima huko UK.
    Watu kama nyinyi ndo hata hatukutaka toka mwanzo mpate visa mwende nje kwa kuwa bado mna ukasumba wa hapa Tanzania.
    Ukasumba wa kwamba ohh mimi sifanyi kazi hii au ile, mimi familia yetu ina hela, kwetu pale, mjomba wangu fulani na mimi najulikana na nafanya kazi ya maana ofisini.
    Ulipoenda nje hayo yote ya misifa ya unafiki hukuyakuta hapo UK, sasa una jazba na roho mtima nyongo kama kifuu.
    umewazibia watu manufaa waliotaka kwenda nje na kukabiliana na mambo walioyategemea toka wakiwa TZ. Yaani kutokuchagua kazi na kujua wao ni wageni na watakuwa wageni tu katika nchi za watu.
    kama hata uraia wa nchi mbili ukianzishwa watapata tu wale walio huko nje na wenye document za huko.
    Hii itakuwa chachu kwa wewe usiye na Docs kuona umuhimu wake kuzipata na kama huzitaki basi rudi TZ leo hii ukajenge nchi na sisi hapa, na sio kuandika pumba.
    Ok point zako wewe mdau UK na Fredrick Mboma, zimehuzu fedha na mmesema mifedha yao inayotumwa ni dola/pound kidogo, kumi na 15 hata kama ni hizo fedha mbuzi wanazotuma hao jamaa walio huko nje wawe na makaratasi au hawana unajua ni clean money zinasaidia sana hapa TZ, hata kama ziwe pound 10 au dola 15 au dinar 20. Kidogo kidogo kwa mwaka 2009 hao jamaa wameiingiza USD millioni 450 sawa na Tsh 604,575,000,000.00/ Billioni 600 za kitanzania bado kidogo kufikia karibu Trillion 1 kila mwaka.
    Elewa mdau UK hizi ni fedha zinazoingia hapa TZ na sio zinazotoka nchi.Hizi japo zinatumwa 10 au 20, kidogo kidogo kwa ujumla zinasaidia kuendeleza nchi na kama watu wake wasingetoka kwenda nje basi tungekuwa maskini wa kutupwa.
    Nakushauri mdau UK, Fredirick Mboma na Professa Mbele ni bora mungebaki hapa hapa TZ, kwa kuwa hakuuna maana ya nyinyi kwenda nje na kubaki na mawazo ya ujinga ambayo hata sisi tulio hapa tunayaona ni ya kijinga.

    ReplyDelete
  23. ILANI:
    WABONGO, TAYARISHENI MAOMBI YA VISA, MTA ZIHITAJI SANA KUKIMBIA NCHI BAADA YA UCHAGUZI!

    ReplyDelete
  24. dual citizenship=ugumu wa maisha utokako=kufanya lolote ilmradi tu upate pesa ya kuishi life la majuu (mf.kuuza madawa,kufadhili vita,kuoana na vizee/ill terminated pple nk)

    yangu maoni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...