ustaadh akipiga chabo kwa mbali kwani tofauti na alivyozoea safari hii kakuta mkwara mbuzi kwenye stendi ya magazeti mjini Iringa karibuni, kwa mujibu wa kaka Maggid Mjengwa ambaye taswira zake hizi zinatoa hali halisi ya mambo yalivyo bongo. Hongera Maggid kwa taswira hizi



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. pao imetuliaa,dezo dezo katafuteni maktaka,
    nimefurahi sana na tangazo hili kwa sababu mijitu bibaba mijitu mizima inapenda kusoma magazeti bure bure wakati wenzenu wanahangaika na biasha kutafuta kula yao na family yao.

    mdau kutoka New York
    nilikuwa muuzaji wamagazeti kabla sijapata zari ya kuja huku utumwani.

    ReplyDelete
  2. kwa mkwara huo lazima ustadh apige breki za mbuzi kwanza asikilize kwa mbali

    ReplyDelete
  3. Hahaaah Ustadhi anaona duh leo Hakuna Cha Bure kusoma nitaenda kusoma wadau kwa Ankal Inshallah. Seif.

    ReplyDelete
  4. Ustaadh naona anakivutia uradi hicho kibanda ili akifika pale yule muuzaji asimshtukie.haha ahah ahaha imetulia sana.

    USTADHI KAFANYA USTAARABU YEYE KAELEWA KWAMBA KWAMBA GAZETI LA MEZANI NDIO UNATOZWA SH 2,000 KWAHIYO ANASOMA YALE MAGAZETI YALIYOKUWA KWENYE KAMBA YA KATANI HAHAHAHA. PAZI.

    ReplyDelete
  5. Hii kali sana....Ustaadhi naona katia pozi la kutia uruma ili muuzaji amwite..."njoo soma chapu chapu alafu uondoke kabla ya watu kujazana hapa..." Halafu hii barabara bado iko kwenye ujenzi au ndio imeshakamilika hapo?
    -Mdau Wakudumu

    ReplyDelete
  6. ..KWELI KABISA USTAADHI NI MJANJA SANA.. ANASOMA MAGAZETI YALIYO JUU YA KAMBA, TANGAZO LINATIA MKWARA KWA MAGAZETI YA MEZANI. HAPO HAWEZI KUMSTAKI WALA NINI . ILA LAKINI NAYE ANA MACHO! HIYO DISTANCE NI TISHIO KUONA MAANDISHI... DUH

    ReplyDelete
  7. Hata ukiwa umejikalia bar au ndani ya daladala unasoma gazeti lako, unaona mtu aliyekaa jirani na wewe naye ananyoosha shingo kusoma. Hii ni tabia mbaya sana. Yaani mijitu mingine sijui ikoje

    ReplyDelete
  8. hahahhahahaaaa kazi kweli

    ReplyDelete
  9. From paris to ny jhb to london same story kama upo ktk public transport unasoma gazeti watu watasoma kinyemela tu sio Africa tu

    ReplyDelete
  10. Duh ustazi ananiua alivyo simama mikono nyma tumbo mbele saaaana.Inaonekana alikua ametoka kupata dinner ya mchana.kashiba kufa mt.

    ReplyDelete
  11. teh teh teh..kusoma pale pale buku 2,kununua mia 4.hahaha.next week ustaadhi atatumua "kiona mbali".atakaa mbali na "kigoda" chake then anakula chabo "kistelingi" kama Chuck Norris ktk Missing In Action.

    ReplyDelete
  12. Michuzi hii picha ya Ostaadhi imenikumbusha enzi zile miaka ya 1980-90 ukipiga picha za matukio mitaani. ulikua unakuja kwenye Daily/Sunday news na picha kama izi. mtu anapigwa picha bila kujijua, anashtukia yupo gazetini na tukio analofanya.Siku hizi umepanda lank na picha za mitaani hatupati tena.
    Ongera Mr Mjengwa kwa nice pic.

    ReplyDelete
  13. twiiii tweeeee... hii babu kubwa.... inabidi na kwa hair dressers hiyo iwepo manake kuna mijitu inaenda kupinga upepo wa feni tuu... hahhaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...