Heshima yako Ankal Michuzi,
naomba msaada wako kuweka haya machache katika Globu yetu ya Jamii tuweze kupata jibu toka kwa wadau amabo nafurahi kuna wataalamu wa mambo kibao tu...

Jamani mimi ni mpenzi wa michezo, huwa napoteza muda mwingi kuangalia hii michezo ya olympic. Sasa kila ninapotazama wachezaji, wanariadha, tufe..nk. Sioni hata mchezaji wa Tanzania hata mmoja.
Kila nikitoa macho wakenya, waethiopia, wajamaika inaniuma ninajiuliza hivi sisi tupo wapi? Mpaka vitu hivi tushindwe kwanini wao waweze wananini na sisi tushindwe tuna nini. Inakera kila wakati kenya na waethiopia tuu nisaidieni au wanatumia nini?
Mdau Mosha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mdau Mosha,
    Wabongo wengia hawachukulii michezo kama riadhaa ni profesheno. Michezo hii inataka mazoezi na maandalizi ya muda mrefu.Mfano ni kwamba mimi nilikuwa nasoma chuo kikuu hapa marekani ambopo kulikuwa na wakenya waliokuwa na fulu skolashipu kwaajili ya kukimbia mbio za mashindano ya vyuo hapa marekani. Wabongo mlioko bongo hasa vijana jitahidini kujiweka katika ramani ya michezo ambayo hasa yanahitaji tu mazoezi na maandalizi ya muda mrefu kama kutoka baruti. Hii michezo ni dili sana hapa Marekani katika vyou vikuu.
    Mdau, Loscow.
    U.S

    ReplyDelete
  2. Mdau unaangalia winter olympics au vipi manake ndo olympics zinazoendelea hivi sasa? Michezo ya barafu na wabongo wapi na wapi. Kwenye olimpiki ya ukweli huwa tunatuma misafara. Viongozi kumi na wanamichezo wawili. Sema wanamichezo wawili waliofanya maandalizi ya zimamoto huwezi kuwaona. Kama kwenye mbio wanakuwaga mwishoni, lamda we unakuwa ushaacha kutizama.

    ReplyDelete
  3. Wewe uliyeuliza unafanya mchezo gani? Au ndo kuuliza tu wenzako kama vile wew si mtanzania na wala huhusiki katika kuhitajika kujihusisha na mchezo wowote. Kama wewe huchezi basi jibu unalo.

    ReplyDelete
  4. Bwana Mosha,

    Maelezo yako ni kweli, marathon za London,Berlin, Rome, Tokyo, Frankfurt,Madrid,Chicago, Boston, Los Angeles, New York na Rotterdam washindo kwa mwaka 2009 washindi 8 walitoka Kenya, kwa nini? Wanajituma na pia uongozi wao ni sio mzuri sana lakini wanajituma zaidi halafu shule za sekondari kuna mwamko mkubwa kuwa huko Marekani kuna scholarship za riadha.
    Suleiman Nyambui na Filbert Bayi walileta medali kutoka kwenye Olimpiki ya mwaka 1980 huko Moscow, sidhani kama tutapata medali yoyote kwa miaka mingine 20 ijayo.
    Je, tutafanye nini sasa? Chama cha Riadha lazima kiwe mbele kuendeleza vijana huko mashuleni, Olimpiki ijayo ni mwaka 2012 hapa London, Tanzania hakuna maandalizi.
    Ethiopia na Kenya timu zao za Juniors kwa upande wa wanawake na wanaume zimawatia jasho wazungu ambao ni wakimbiaji senior.
    Wizara ihusikayo ingeingilia katika itafute sababu, pia viongozi wa chama cha riadha na Olimpiki Tanzania ambao wameshika uongozi kwa miaka zaidi ya 20 waachie ngazi ili wengine wachukue hizo nafasi tuone watafanya nini.
    Ulaya ukiwa kocha timu yako ikashindwa unatimuliwa, Tanzania hakuna hilo !!

    Sasa tuna uongozi wa serikali awamu ya NNE, Riadha bado tuko awamu ya KWANZA. Ipo kazi!!!

    ReplyDelete
  5. Na hiyo wizara ya michezo ni bora hata isingekuwepo kwa sababu hatuoni wanachokifanya.

    Mchezo unaopewa kipaumbele ni soka ambayo inaendeshwa sana kisiasa. Viongozi wa vyama vya michezo wanatumia nafasi wanazopata kuendeleza mambo yao binafsi kama vile kusafirisha dawa ya kulevya.

    ReplyDelete
  6. Bwana mosha unaonekana ni mpenzi sana wa taarab naona umeshindwa kujizuia mpaka umeimba wimbo wa mzee usufugas

    ReplyDelete
  7. Anony 02:16 umenichekesha mana hapa sina mbavu.ila umejisemea kakejeli kaukweli.

    ReplyDelete
  8. eee bwana weee wacha tuu sie viongozi wetu wameshughulika na ufisad na sie wametulewesha hiyo pombe kali mbaka tunasahau hayo kwani wewe una riyadha gani unafanya au wewe sio mtanzania a

    ReplyDelete
  9. Ndugu Mosha.Napenda kukufahamisha kuwa uwezo wa kutoa wachezaji wazuri wa kutuwakilisha na kuleta ushindi wapo na wanaweza kupatikana ila tatizo liliopo ni uandalizi.Riadha ni mchezo ambao unahitaji uvumilizi ,maandaliziya muda mrefu,lishe bora,uangalizi wa afya kila mara.Nakwa kuwa huu mchezo ni mtu binafsi its not a team work like football,netball,basket n.k.Inabidi kujituma hasa.Na michezo hii huanza toka age ndogo lakini kuanzia9-10 hapo unaanza kama kocha-kufundisha watoto kwa kutumia njia ya kucheza kama kukmbia distance fupi mfano60m,kkutupa mpira-hii yote nikuanza kuangalia uwezo au kipaji kiko wapi.13yrs na kuendelea hapo ndio unaanza kutoa zoezi kwa kuzingatia umri.uwezo.sasa kwa ufupi ilituweze kupata cream ya wacheza wawakilishi kwa kweli michezo inatakiwa ianze shule za msingi na kupanda mpaka juu.Na yote haya pia watumiwe makocha wenye upeo mzuri wa mchezo huu kwa kuzingatia kuwa mazoezi wanayoyatoa yanalingana na umri wa mcheza ili tusiwaume ki uwezo kabla hawajafikia malengo ya juu.(Scientific treining)Kwa hiyo ni maandalizi ya muda mrefu na yanahitaji pesa kwa ajili ya kusaidia na ufuatiliaji.tatizo lingine lililopo ni kuwa tuna wachezaji wazuri lakini kutokana na kuwa mbio za siku hizi ni pesa basi baadhi ya wachezaji wamejenga ubinafsi na kiburi kwani wakipata chance ya kupata mio nje wakishinda huja kuwaunganisha ndugu,rafiki-wanafanya zoezi na kushiriki sana mbio za mialiko ya pesa.sasa inapokiua Olympic nk.miili ishachoka.Na kingine kwa kuwa wameshajua njia ya kutengeneza pesa inatawala jeuri.Kocha anakuwa hana sauti maana mcheza ndie ana power.Nyambui,Bayi na wachezaji wa miaka ya 70-80 walikuwa na nidhamu sio sasa.Sprints,Mitupo,Miruko ni michezo inayohitaji vifaa vingi tofauti na marathon.Na michezo hii haileti matunda kwa kipindi kifupi nimpango wa muda mrefu.Pia Tz riadha haithaminiwi kama mpira.Kwa taarifa riadha ni mchezo ambao umeifanya Tanzania itambulike baada ya Bayi kuweka redi ya dunia lakini mpaka leo ni wachache sana wanaofuatilia mchezo huu.Serikali ingeupa kipaumbele mchezo huu na kutoa changamoto,Riadha inaanzia toka shule za msingi.Jamani Riadha Juu Juu Kabisa.

    ReplyDelete
  10. bwana we kwa sasa hivi huku canada ndo kuna winter olympic game na hii kitu haihusiani na sie manake hatuna hayo masnow labda watu waanze ku ski mount kilimanjaro ili olympic nyingine washiriki vinginevyo watu wanashiriki saana tu kwenye hiyo olympic nyingine sema ndo hatushindagi tu hayo magold masilver bronze medal lakini tunaendaga sana tuuuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...