£ovely Gamble is a soon coming film to your small and big screens starring Steve Kanumba geared towards your maxmum entertainment. Brought to you by Urban Pulse Media with Afro Euro Management Enterprise
Watu Ohhh maimuna....ooh hajui Kiingereza....ooooh sijui nini. Sasa waliokuwa wanambeza watakoma kulinga, tuache kukatishana tamaa na kutoa kashfa sisizokuwa na maana, ni umasikini wa mawazo na wivu tu.Kiingereza sio lugha mama, haiingii akilini pale mtu anapomcheka anayejitahidi kuongea kiingereza eti hafahamu kuongea vizuri, atafahamu vipi kuongea vizuri wakati anajifunza? nisawa na mtoto mdogo anapoanza kushika neno moja moja mpaka anafikia hatua ya kuchanganya.Bravo Steve Kanumba , kwani ameweza ku improve kwa kiwango kikubwa na kuwapita hao wanaomdhihaki, na ninaimani kadri muda unavyopita ndivyo atakavyo weza kuongea vizuri zaidi.
SINEMA MPYA YA KITANZANIA KUTOKA UINGEREZA MWEZI UJAO
Na Freddy Macha, London
Sinema mpya, Lovely Gamble, katika Kiswahili na Kiingereza, inatazamiwa kufanyiwa sherehe rasmi kabla ya kuonyeshwa na kuuzwa ulimwenguni, mwezi ujao.
Watengezaji wa sinema hiyo, Frank Eyembe na Baraka Baraka, ambao ni Watanzania na wakazi Uingereza, wamesema mchezo una waigizaji wa Kiingereza na Kibongo akiwemo mwanatamthiliya wetu maarufu, Steve Kanumba na ina azma ya kufungua njia mpya ya utengenezaji picha kwa Watanzania.
Walifafanua: “Miaka ya karibuni tumeona sinema zikitolewa haraka haraka, kwa mwezi mmoja, kiholela na kuuzwa mitaani. Sinema hizi huwa zinawafaidi wafanyabiashara wanaowapa presha watengenezaji wanao lipua lipua tu. Utengenezaji sinema si suala la kulipua. Ila msanii akiambiwa atalipwa shilingi hamsini milioni anaona nyingi, kumbe mfanya biashara anabaki na haki miliki. Hatuwezi kuendelea mbele kama sinema zetu zitafuata masharti na matakwa ya hawa wafanya biashara na wamachinga.”
Kampuni ya Urban Pulse yenye makao mji wa Reading inawahusisha pia vijana na wananchi wa mataifa mbalimbali na pia wenyeji wa hapa Uingereza.
Karibuni kumekuwa na msisimko mkubwa wa sinema za Kibongo nyingi zinazotengenezwa vibaya jambo ambalo limewafanya Watanzania tusipende filamu zetu wenyewe na kukimbilia za wageni mathalan Wanaijeria.
Shirikisho jipya lililoundwa miezi michache kurekebisha hali ya sinema nchini, Tanzania Film Federation (TFF) limeweka vipengelee kadhaa vya kusaidia tatizo na kati yake ni kupanga haki miliki na kuzipanga sinema katika umri takikana (certification) kusaidia watengenezaji na wasambazaji kuzingatia maadili wanapoonyesha mahusiano ya kijinsia na mapenzi.
Tazama kipande:
http://www.youtube.com/watch?v=j-fbwizJWEw
Benedict Kimbache
Kwenye movie wana klemu lines tu ...Jean clade van dam ....jackie chan wote hawawezi kuongea ki english...lakini angalia wanavyoongea kwenye movie
ReplyDeleteKimbache,
ReplyDeleteAcha kumhariba Kanumba kwa kuamsha marumbano yasiyo na kichwa wala miguu. Wengine tulimshambulia na kumuasa aache kulia na aende kujifunza Kiingereza. Kama kajifunza na sasa anaongea vizuri, kwa nini asije kusema asante kwa ushauri wenu? Unachoandika wewe ni sawa na kuanza kumtengenezea maadui na kwa muuza sura kama yeye hiyo si nzuri kabisa.
Homeboy Kanumba, wewe sema asante kwa ushauri na endelea kufanya vitu vyako. Usiingie kwenye marumbano milele. Kama ni kuwaonyesha kuwa si Maimuna, wewe ongea na watu watapata habari yao ingawa nina wasiwasi kama watakumbuka. Una kipaji na anza kufikiria mbali ya mipaka ya Africa na UK. Kipato chako kinaweza siku moja kutoa ajira kubwa tu kwa Watanzania.
Hongera kwa picha, endelea na kazi na kumbuka huwezi shindana na watu. Wee fanya kazi zako na hilo ndiyo litakuwa jibu kwako. Mengi tuliandika na itakuwa upuuzi kurudia. Noyaga, Sikonge.
MZEE KANUMBA, MKUU UNATISHA. SASA MBONA SIJAMUONA SWAHIBA WAKO KWENYE MOVIE ZAKO ZA HUKO ULAYA?? MIE JOHN MASHAKA NAMUONA TU KWENYE MICHUZI BROG. NASIKIA WEE NDO WAZILI KWENYE BALAZA LA 2015 LA MICHEZO NA UTAMADUNI?? . WAKUU KAGOMBEENI URAIS ILI TUPATE KUJA BONGO KULA MARAAZ IKULU
ReplyDeleteTETETEEEE
KANUMBA OYEEEEE
Mdau umeongea sana ungekuwa na akili na busara zilizo timu usingetia hoja - usibishane na watu bana kwa mambo kama haya just let nature ichukue mkondo wake - ooh mtakoma kulinga ivi ni kulinga au kuringa unaona mpaka unachemka mwenyewe?
ReplyDeletewe uliyetuma hii habari unaelekea ni mtu wa visasi sana uswahili mwingi nani akome kuringa?? kila mtu na ishu zake we vip bwana ebo!! hakomi mtu
ReplyDeleteKanumba BIG UP, nani kama Kanumba? mimi siwaelewi, hakuna cha ku improve wala nini, tangu mwanzo Kanumba anaongea english saaaafi sana. gramma iliyotulia na lafudhi ya kitanzania. ujinga wenu mnaomkandia ambao mnadhani kuiga lafudhi ya wazungu ndio dili. Kanumba unatesa kijana, hakuna anaekufikia kwa kuigiza, i am proud of you. keep it up WABONGO ROHO MBAYA TU NA WIVU TELE CAUSE MBONA HATUWAONI? KANUMBA UNATESA KAZA BUTI TUPO NYUMA YAKO.
ReplyDeleteacheni hizo anavyofanya kanumba sawa tu anaongea kiswahili then sub hitle wanaandika kienglish sisi tuiombali na nyumbani tukiangalia ktk dstv ukisikia kiswahili unafarijika kuna movie za kinigeria wamecheza kiingereza ila kwa kujishtukia watu hawawezi kuwaelewa wanaongea nini nao wanaweka maandishi ya kiingereza kanumba wewe endelea na muda wa kuzipiga ndio huu ukizubaa uzeeni ni kutumia tu
ReplyDeleteUkweli kabisa bila kinyongo na mtu Tittle Lovely Gamble is a goof, a blunder! Ukimwuliza Kanumba why lovely Gumble atakueleza kile wengi tusichokitarajia hii inatokana tatizo la direct translation! To gamble is to take a risk in hope of favourable outcome! Lovely ni kitu adorable, Loverable, appealing! Hebu jaribu kutafuta muunganiko wenye kuleta maana maana ambao si lazima uwe ni wa maneno hapo juu lakini hata ile general conception! Mimi nimeshindwa! Matatizo ya direct translation! Sijui Steve ulikuwa na maana gani! Hebu dadavua Bro!
ReplyDeleteLabda alikuwa anamaanisha, "Love Gamble?" Uchukue risk ya mapenzi? Unajua chizungu tena. Wapiga debe wanasifia tu bila mpango. Maana hata hilo tangazo lenyewe lilitakiwa liandikwe kama hivi, "£ove Gamble will be coming film to a theater near you soon, (It could be a movie or home theater). Starring Steve Kanumba, the movie/film is geared towards (or just for) your maximum(not maxmum, little proofreading is helpful, hey) entertainment. Brought to you by whomever.
ReplyDeleteNaona hata mimi nimechemsha. Hiyo ingekua, "Love Gamble is a film that will be coming to a theater near you!" Unajua mambo ya kucopy na paste, inaleta uzembe!
ReplyDeleteMpenda chizungu
Swali la Kizushi...kujua Kithungu ni kusikia, kuzungumza au kuandika
ReplyDelete