Mzee wa Chama Serve Malai (wa pili shoto) akiwa na vijana wake wa Pazi walipozuru Marekani enzi hizo. Mzee Malai, aliyekuwa chachu kubwa ya basketball nchini kwa mapenzi ya makubwa ya mchezo huo atakumbukwa daima kama baba wa basketball nchini. hadi leo hajatokea kama yeye. Taswira hizi zote ni kwa hisani ya Vitalis Gunda anateishi marekani sasa.
wachezaji nyota Thomas Shempemba na Mbaga Mwamboma wakila kuku Marekani
Patrick Nyembela (shoto, sasa ni kinara wa EATV sports) na Abeid wakiwa Marekani
vijana wa Pazi wakiwa Marekani
njiani kuelekea marekani
kulikuwa na kipupwe cha nguvu
kabla ya mchezo
vitalis gunda ( wa pili kuume) akiwa na wenzie. anaiweka taswira hii kama kumbukumbu ya kumuenzi hayari Dr. Hamesh Shaba (wa tatu shoto)
Pazi Basketball Club katika michuano ya ubingwa wa taifa mwaka 1990, uwanja wa Jamhuri stadium Morogoro. Toka shoto ni Yasin, Abeid, Moddy Siu, Kwame Makame, Runner, Harold Kida, Emma "magic"Nighula, Andreson Kailembo,Thomas shempemba,Sidi Kikenya,Vitalis Gunda, Abbas Mansour, Mbaga Mwamboma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Mbona hujasema mwaka na sehemu waliokua. Ni wale walifika Iowa mwaka sijui 95 au 96? Tulienda kuwaona wachezaji wakicheza sijui ilikua ni college gani vile? Lakini ilikua Iowa.

    RIP

    ReplyDelete
  2. Nakumbuka Pazi ilipokuja tulienda kuwaangalia pale Wartburg College Iowa wakicheza na team ya shule ya pale. Bahati mbaya walipgiwa bao.

    ReplyDelete
  3. Vitalis inabidi hii timu ifanye re union na icheze mechi mtukumbushe enzi za akina magazeti,tiger,tom,abdallah aboud etc this will be very good tribute for the father of basketball i Tanzania

    ReplyDelete
  4. Enzi ya Pazi basketball namkumbuka Marehemu Yusuf Omari (1985) wachezaji mahari sujui kama mchezo huo unaendeleshwa nchi kupitia makocha hodari kweli tunaweza sana kufika mbali kimataifa ukihamasishwa .

    ReplyDelete
  5. wewe patrick embu nitafute

    ReplyDelete
  6. Duuuh, hii picha imenikumbusha mbali sana. Pazi ni timu ambayo ilitikisa sana miaka ya 90 and natumai mpaka sasa inatesa (siko sure as sijafuatilia basket baada ya kuwa mvivu kwenda Taifa). Kuna jamaa mmoja hv mzaire alifariki miaka hiyo ya 90, jina lake limenitoka kidogo, alikuwa soo mbaya. Patrick Nyembela mzee wa Channel 5 enzi zake ilikuwa balaa tupu. Mbaga Mwamboma, Vitalis (umekimbia kabisa bongo) tunawapa saluti kwa kuibeba pazi enzi zenu. Mzee Serve Malai, RIP. Tunakukumbuka sana, kwa mchango wako kwa vijana hawa wa Pazi, wengi wametoka shavu kwa sasa, kutokana na efforts zako.

    ReplyDelete
  7. 1. hii ndi trip ambayo abbas mansour na marehemu tambwe walinyimwa viza.
    2. hii ndio trip ambayo shabani kazumba alipata klabu. lakini akataka aje dar kwanza 'wamwone'. matokeo yake, nauli tu ya kurudi marekani ikawa mzozo.
    3. mzee malai kuna siku akawaambia pazi, hivi mlitaka niseme, "wewe baki, wewe baki, wewe baki". yaani timu nzima ilirudi!!!

    ReplyDelete
  8. tunaomba location ya walipovisit walipokuja huku..!!

    ReplyDelete
  9. michuzi nisaidieni niweze kupata taarifa za nyuma,,,natafuta ile news ya RADAR malipo yaliyorudishwa tanzania

    ReplyDelete
  10. nimekumbuka zamani sana!
    enzi hizo nakwambia tunaenda kuangalia basket zanaki, basi wavulana walikuwa wanajiona keki! kina Gunda walikuwa wanasoma sijui azania, kina Delphinus,Marehemu Hunter.......Shempemba nikikumbuka!
    it was so fun, at that time wengine wanacheza basket, wengine wanatukuza bangi, kina shetani Tambaza!!

    ReplyDelete
  11. Daa sio siri yaani machozi yamenitoka hasa nikiangalia hizi picha...Hii ilikuwa pazi iliyokuwa inaishia ishia.hivi hawa jamaa wapo kama Thomas Shempemba,Patrck,huyo Abbas Mansour naye yupo jamani mara ya mwisho nolisikia yupo Austaralia.wapi kissoky?yaani kuna watu hata majina nimewasahau plz mdau mwenye kum´wakumbuka atupe majina zaidi.
    mdau Uswidi.

    ReplyDelete
  12. Hii ndio Pazi ya Mzambarauni, pale jirani na Movenpick Hotel. Nakumbuka entry ya uwanjani ilikuwa kwenye kona ya barabara ya Ohio na Ghana Avenue!. Wakali wa wakati huo, Tom Shempemba(Yellow Man), Sidney Kikenya, Abdallah Aboud (Kocha), Hassan Kange, Pacheli, Hassan Tiger, Grace Magoti(RIP), Mary Njohole, Namsifu Mndeme, Conso Henry, Vitalis Gunda (Mpongos), Patrick Nhigula (Magazeti), bila kumsahau mzee wa viroja na porojo, Teacher, mzee wa Kuzacha Worriors!

    ReplyDelete
  13. Kwa kweli inatukumbusha mbali sana!Aziz Kateta yuwapi jamani.Angeanzisha ze komedi angekuwa BOMBAAA!He had a wild sense of humour!Nakumbuka kina Patrick Nyembela, Hassan Tiger,Vitalis na wenginewe wasio warefu sana waliulizwa kama wao wamesindikiza timu au wanacheza.Lakini waliopoona dribble zao na defense wamarekani na utall wao walitoa macho.Walifungwa ndiyo lakini they played a good game.
    REUNION JAMANI!Zonga upo,Tom upo,Abdallah upo,Patrick upo na wenginewe pia...

    ReplyDelete
  14. kuna mchizi mmoja tulikuwa naye TAMBAZA anaitwa ADAM"KATOSHA" huyu nae alienda hii safari...huyu mchizi anaongea kama rediooo..alivyorudi mwezi mzima anaongea yeye tu pale tambaza.....
    KATOSHA uko wapi we mchizi???

    ReplyDelete
  15. Hi vitalis Gunda nimefurahi sana kukuona.Ni siku nyingi zimepita.
    kila la kheri ya maisha may God Bless you and your family. msalimie Rahaba.
    Baby.

    ReplyDelete
  16. Picha hii yanikumbusha mbali sana (1985-91) na machozi yanitoka.

    L. Ind
    UK

    ReplyDelete
  17. mdau ulie uliza Aziz Kateta huyo jamaa kweli alikuwa ni The komedi.Aziz anafanya kazi Tazara na yupo upande wa Zambia.Patrick Nyembela Yu wapi??
    Mdau Uswidi.

    ReplyDelete
  18. wapi Shaaban Kazumba?

    ReplyDelete
  19. Patrick NhigulaFebruary 12, 2010

    Patrick Nhigula-Magazeti,
    Hii ilikuwa historia kwa timu ya mpira wa kikapu ya Tanzania kufanya ziara Marekani. Hii safari ilikuwa nzuri sana na kama Vitalis una picha tulizopiga pale Chicago kwenye Hotel ya Michael Jordan weka basi kwenye mtandao. Mzee Malai alikuwa "Baba wa Basketball Tanzania" kwa nini BMT na Tanzania basketball association wasiwe na "Malai Cup" au Kimario "Cup". Sisi tupo Columbia, South Carolina na Ongera Pazi na tutaijenga upya.

    ReplyDelete
  20. BJ Hammer, simuoni hapo, au alishaanza enzi hizo?.

    ReplyDelete
  21. Vitalist naomba tuwasiliane kwa namba ya simu +255 712 240042 msalimie Rahaba na Rehema mimi uncle Elikana

    ReplyDelete
  22. Duuh nimefurahi saana kukumbushwa enzi zile,ligi inapigwa railway gerezani mimi ndo nilikuwa secondary lakini nilikuwa sipitwi na mechi.Ndugu zangu wa city bulls vijana mpoo,tupeni zenu tukumbuke wa wakati ule.Nakumbuka hizo zama, ukiwa unacheza basket ball basi mademu wa upanga,o-bay,chan'gombe maduka ma2,unajichukulia tu

    ReplyDelete
  23. RIP Hemish we miss you boy !

    ReplyDelete
  24. Mzee Malai,Yusuf Omar na Ray Ndanshau RIP.Hizi picha zimenikumbusha mbali,enzi hizo tunakwenda kuangalia mazoezi na mechi za basket pale kona ya Ohio/Ghana avenue viwnaj vya Gymkhana.Dar ilikuwa nyingine kabisa...!Sasa hivi nasikia giza likiingia kidogo tu hakupitiki kwa vibaka!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...