Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Mtendaji wa Kata ya Urambo Mjini, Stella Riwa Pikpiki ili aweze kufanya kazi yake vizuri, kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Urambo akiwa katika ziara ya mkoa wa Tabora, Februari 26, 2010. Kuahoto ni mkewe Tunu na watatu kushoto ni Spika wa Bunge na Mbunge wa Urambo, Samwel Sitta.
Wasanii wa kikunid cha ngoma ya kisukuma ya Bugobogobo kutoka kijiji cha Muungano wilayani Urambo, wakitoa burudani uwanjani katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkkuu, Mizengo Pinda Mjini Urambo leo

Wasanii wa kikundi cha ngoma ya Kisukuma ya Bugobogobo kutoka kijiji cha Muungano wilayani Urambo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Urambo akiwa katika ziara ya mkoa wa Tabora,



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Duh! nikiwaangalia hao jamaa wa Bugobogobo na wanakijiji wananikumbusha miaka 30 iliyopita.

    Nami nilikuwa na na mawazo na akili kama hizi, Yaani akifika kiongozi wa Taifa unajitahidi kwelikweli kucheza gwaride mpaka mguu kichwani, baada ya hapo mnaalikwa Ikulu ndogo kula wali wa pilau na Soda, Kiongozi akiondoka ndiyo imetoka hiyo. Mnakaa na kuomba mungu arudi tena.

    Maana kipindi hicho cha Nyerere Mkoa kama Tabora tulikuwa tunachukuliwa na maroli ya mchanga kwenda Airport ya Masimba kumsuburi nyerere na matawi ya miti mpaka yanatunyaukia mikononi. Kila ndege inayotua mnaanza kujiuliza labla ni ya rais(Ilikuwa aina ya Foker tulikuwa tunaiita "JET TAIFA". Mnasubiri six to seven hours, na akifika hata Dk 5 hachukui anarukia gari huyooo, hapo sasa Kazi inaanza kuparamia malaori maana ukikosa nafasi ujue utatembea Km 30 mpaka mjini kwa mguu maana hayarudi tena kama ambavyo yalivyokuwa yanachukua watu tripu hata tano tano kuwapeleka Airport.

    Duh! Tumetoka mbali sana maana hata barabara zilikuwa zikichongwa kipindi cha Rais akikaribia kufanya ziara.

    SASA HIVI HAWANIPATI NG'O, NASHUKURU MUNGU NIMEWEZA KUFUMBUKA MACHO, ILA WATANZANIA WENGI BADO WAKO KARNE ILEEEEE YA NYERERE HASA VIJIJINI KISA NI UKOSEFU WA ELIMU. NINA HAKIKA KUWA KADIRI WANANCHI WANAVYOELIMIKA NDIYO VIONGOZI WANAPOPATA SHIDA KUONGOZA. NDIYO MAANA WANAIMINYA SERA YA ELIMU LOL!

    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  2. Furaha iliyoje kuona ngoma ya gobogobo.Inanikumbusha miaka ya 69.zamani ngoma hizi zinakuwa paformed na wana tribe siku hizi ni biahara.Ni vyema tunaendeleza jadi na utamaduni wetu.Ninauliza jamani watu wa tabore jirani zangu mie mtu wa Shinyanga ila kwa muda niko mbali kidogo nahangaikia maisha.Jamani je ile ngoma ya "UGOYANGE" ilikuwa inachezwa na kina mama wakiwa wamekaa chini hapo unaona tu rotetion ya mabega jamani iko? kama haipo jamani ifukuke kwani hiyo ni special,Ngoma ya wazee wakiwa wamevaa white kanzu ,fimbo ,na mwamvuli wana shy iko bado hiyo ngoma?Nilikuwa mdogo na hizi ngoma bado ziko kichwani.Ngoma za jadi zidumu.Mungu ibaliki Tanzania.Mzawa Shy mjini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...