The Rector of Fatih University in Instabul, Turkey, Professor Shariff Ali confer upon President Jakaya Mrisho Kikwete a honorary Doctorate Degree (Honoris Causa) in International Relations during a colourful ceremony held at Fatih Univesity in Instabul Turkey Friday evening
President Jakaya Mrisho Kikwete prepares to deliver his acceptance speech shortly after he was conferred with Honorary Doctorate Degree in International Relations yesterday at Fatih University, in Instabul, Turkey Friday evening. Photo by Freddy Maro.
Rais Kikwete atunukiwa
shahada ya falsafa ya udaktari
. Yeye asema anaitunuku kwa Watanzania wote

Na Mwandishi Maalum,
Istanbul, Uturuki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Februari 19, 2010, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Falsafa ya Udaktari katika Masuala ya Kimataifa na Chuo Kikuu cha Fatih cha Istanbul, Uturuki.

Mara baada ya kuwa ametunukiwa shahada hiyo, Rais Kikwete ametangaza kuwa naye anaitunuku shahada hiyo kwa wananchi wa Tanzania ambao wamechangia mafanikio ya utawala wake katika miaka minne iliyopita.

Akizungumza kabla ya kutunuku shahada hiyo, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Sharrif Ali, amesema kuwa uongozi wa chuo hicho kwa ushauri wa Baraza la Seneti la Chuo hicho umeamua kumtunukia Rais Kikwete shahada hiyo kwa sababu ya mchango wake mkubwa katika masuala ya kimataifa.

“Katika nafasi zako zote ulizozishikilia katika maisha yako yote, hasa ulipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ulisimamia kutatua migogoro mingi katika eneo la Maziwa Makuu ukiwamo ule wa Burundi, na zaidi uliposhika urais umeendelea kusuluhisha migogoro mingi,” Profesa Ali amemwambia Rais Kikwete.

Profesa Ali ameongeza kuwa kwa kutoa shahada hiyo ya falsafa kwa Rais Kikwete, Chuo Kikuu cha Fatih kimepata mwakilishi, mtetezi na msemaji wa chuo hicho siyo tu katika Bara la Afrika bali duniani pote.

Rais Kikwete anakuwa mtu wa tatu kutunukiwa shahada ya udaktari na chuo hicho. Wengine ambao wamewahi kutunukiwa shahada ya namna hiyo, tokea kuanzishwa kwa chuo hicho cha sayansi, mwaka 1996, ni Rais wa Azerbaijan, Mheshimiwa Ilham Heydar Aglu Aliyev na Waziri Mkuu wa Uturuki, Mheshimiwa Recep T. Edorgan.

Akizungumza baada ya kuwa ametunukiwa shahada hiyo ya falsafa, Rais Kikwete amesema kuwa naye kwa heshima kubwa anaitunuku shahada hiyo kwa “Watanzania, kwa mke wangu na kwa familia yangu” ambao kwa pamoja wamemsaidia katika kutekeleza majukumu yake.

Katika hotuba yake ya kupokea shahada hiyo, Rais Kikwete ameelezea jinsi Bara la Afrika lilivyobadilika na kuwa Bara bora zaidi katika miaka ya karibuni iwe katika kujenga demokrasia na kujenga mataifa ya Bara hilo.

“Yapo mafanikio mengi yanayojionyesha katika Afrika leo tofauti na ilivyokuwa wakati wa Uhuru miongo mitano iliyopita. Mambo mengi mazuri yametokea katika Afrika yakiwamo kuboreka kwa maisha ya wananchi wa Afrika,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Afrika siyo Bara la ovyo ama Bara lililo gizani kama baadhi ya watu wanavyopenda kuliita. Badala yake, Afrika ni Bara lenye kushamiri, lililojaa matumaini, na ambako mambo yanabadilika na kuwa mazuri zaidi. Afrika inapaa kuelekea kwenye mafanikio ya kiuchumi kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya. Hii inajionyesha na kujithibitisha katika Bara zima la Afrika – kutoka Cape Town hadi Cairo, kutoka Dakar hadi Dar Es Salaam.”

Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa bado Bara la Afrika linakabiliwa na changamoto nyingi. “Kuna changamoto za kisiasa, kijamii, kiusalama na kiuchumi. Lakini changamoto kubwa zaidi ni ya kiuchumi, hasa katika kuongeza kasi ya kukua kwa chumi za nchi za Afrika na kuwainua Waafrika walio wengi kutoka kwenye umasikini.”

Ameongeza: “Nchi 38 kati ya nchi 49 masikini zaidi kwenye dunia hii wanaishi katika Afrika, na wengi wao wanahemea wakiishi kwa kiasi kisichofikia dola moja ya Marekani (sawa n ash. 1,300) kwa siku.”

Rais Kikwete pia amezungumza hali ya kisiasa ya Afrika, hali ya kiuchumi katika Afrika, umuhimu wa nchi za Kiafrika kuongeza ushirikiano katika masuala ya kiuchumi na uhusiano kati ya Afrika na Uturuki.

Leo usiku, Rais Kikwete na ujumbe wake, ameandaliwa chakula cha jioni na Gavana wa Istanbul na Chama cha Wafanyabiashara wa Uturuki kwenye mgahawa wa Feriye.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Nawewe Mithupu Dr. of Philosophy haiandikwi PHD ila inaandikwa PhD. Sijui unajua ulikosea au hujui kabisa...I hope uta-post hii comment yangu maana lately umekuwa adui yangu mkubwa...hakuna posts zangu unazozituma kwa miezi kama miwili sasa..sijui nimekufanya nini...!! Si uliweka globu mwenyewe kwahiyo tuna haki ya kusema?

    ReplyDelete
  2. Mtoa maoni hapo juu Anonymous (Sat Feb 20, 01:03:00 AM),nawe hauko sahihi, ni Ph.D., katika kiingereza neno likfupishwa huwekewa nukta. Ph.D. ni kifupi cha Doctor of Phylosophy.

    ReplyDelete
  3. Congrats Mr. Prez!!!

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  4. Dah! ubatani tambarare sasa watanzania kuingia bila viza.

    ReplyDelete
  5. wote mmekosea ni Doctor of Philosophy na si Phylosophy khaaah!

    ReplyDelete
  6. Mtoa maoni namba 2 yuko Ok ila Ph.D imefupishwa kutoka neno la kilatini "Philosophie Doctor (Ph.D), meaning "teacher of philosophy". ila mara nyingi huandikwa bila kuweka hiyo nukta...

    Pia naomba mtoa maoni namba moja usimshanmbulie mithupu..atafanya uhariri wa habari ngapi na kuzirusha hewani sometimes mimi naona hizi human editorioal error ni OK tu ili mradi watu hawatukani wala maana haipotei...
    Naona watoa maoni mko makini...Hongera President kwa Ph.D sasa tutamwita "H.E. President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete" siyo au tutamwitaje Anko Misupu

    ReplyDelete
  7. ...haya na wewe Ka Kazi philosophy siyo phylosophy...kisha Anonymous yuko sahihi ni PhD siyo Ph.D

    ReplyDelete
  8. Hello Dr J. M. Kikwete..!!

    Congratulations Mr President.

    Network Engineer (NE),
    Reading, UK.

    ReplyDelete
  9. ADILI NA NDUGUZEFebruary 20, 2010

    Na wewe Ka Kazi umekosea. Haiandikwi "Phylosophy" bali Philosophy

    ReplyDelete
  10. A PhD in international relations no one can urge that, bag it - well done!!

    ReplyDelete
  11. Wee Ka Kazi hapo juu - PhD au Ph.D is an 'essentialist argument' Pili, umekosea spelling za P. Mwisho, JK HONGERA SANA, angalao watanzania sasa wanaogozwa na daktari mfilosofia.... tunasubiri kuona hizo busara kwenye DUAL NATIONALITY... JM, PhD

    ReplyDelete
  12. kaka michu kwa kweli umetuacha katika mataa sanaa tu, mie ningependa kujua hasa yule jamaa uliemtoa juzi amehukumia miaka mingapi jela au amehukumiwaje. Napia Jerry Mulo naye pia ishu yake imekwenda vipi. Nakupongeza sana kwa kuwa mwana habari na mwana blog number moja tz, mi ni mkenya hata pale kenya hakuna kama wewe sasa twasema ungemaliza kabisa habari ulizo tupa ingekua sawa kabisa. kama unakua unatoa nusu nusu kwa sie machalii tunaopenda blog yako, tunaona kwamba haki zetu unatunyima kidooooogo. Kwavile haumalizii ulichokua unatueleza. Naipenda sana tz kwakua hamna ukabila ila naona kama wewe ni mjaluo vile na mimi ni mkikuyu sasa unaninyima haki yangu makusudi, au wewe chailii wangu unaona vipi sasa. TAFADHALI MHESHIMIWA NAKUOMBA. MALIZA KAZI YAKO SOTE TUKUELEWE. UNATUFANYA KUKUFIKIRIA VIBAYA WAKATI ISIVYO. HESHIMA KWAKO KWA HABARI SAHIHI SASA MALIZA BASI.PALE NAIIII WANGE WEKA SIRI KILA KITU ILA WABONGO MKO KWA JUUU SANA. KAMA BAHARI HAINA MWISHO, LAKINI HABARI ZOTE HUWA NA MWANZO PIA NA MWISHO.
    WATAKA KUNIFANYA NII CHUKULIE POA EAST AFRICA YOTE, MAANA MI NILITAKA KUISHI BONGO NIKIRUDI AFRIKA ATI.

    MDAU UK.
    SASAAA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...