Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Jumanne Maghembe amemteua Rosemary Lulabuka kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) .
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotelewa jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Hamis Dihenga inasema kuwa uteuzi huo ulianza February Mosi mwaka huu.
Alisema kuwa Waziri Maghembe amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Elimu Tanzania namba 8 ya mwaka 2001 ilianzisha Mamlaka ya Elimu Tanzania.
Dihenga alisema kuwa kabla ya uteuzi huo, Lulabuka alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Mei, 2009 na pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Mamlaka hiyo.
Aliongeza kuwa Lulabuka amewahi pia kufanya kazi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) akiwa Mhasibu Mwandamizi.
Dilenga alisema kuwa Lulabuka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bibi Mercy Silla aliyeteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru tangu Aprili, 2009.
Bibi Lulabuka ana Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara(Master Degree in Business Administration ) na Certificate Public Accountant (CPA-T).

Dada Rose hongera sana. Wewe ni mmojawapo wa IDM Mzumbe graduates tuliokuwa pamoja miaka ile 70s ambaye unapeperusha bendera ya ex IDM students na kuzidi kukipatia heshima chuo hicho. Hongera sana. Wengine ni Ndugu Ludovick Utoh, the CAG, Mheshimiwa Anna Makinda nikiwataja wachache. Nakutakia heri kwenye wadhifa wako mpya. Well done my sister.
ReplyDeleteKwanza nakupongeza bro kwa kazi nzuri unayoifanya!
ReplyDeleteNaomba msaada wako nijulushe ni vipi naweza kukutumia habari yangu na picha itoke hapa kwenye blog yako?
Nitashukuru sana kujua.
email yangu ni joo2@hotmail.co.uk
Asante
Hongera Rosemary, sote tunakutakia kazi njema.
ReplyDeleteMichuzi, hebe soma mstari wa mwisho, maajabu! Sio Certificate Public Accountant bali ni Certified Public Accountant
ReplyDeleteWadau naomba msaada! Hivi CPA ni certificate public Accountant au ni CERTIFIED PUBLIC ACCOUNTANT? Hiyo habari hapo juu imenichanganya kidogo
ReplyDeleteIt is Certified Public Accountant na siyo Certificate Public Accountant. Kuipata hiyo unatakiwa ujipinde kweli. Ukiona mhasibu ana CPA mheshimu sana.Ninachojua wenye CPA nchi hii ni wa kuhesabu. Hakuna kufake au kuipata kiubabaishi hiyo. Masharti yake hayapandishiki.
ReplyDeleteHongera sana dada, na nyie hiyo ni typing error, all in all tunajua ni CPA tu kirefu chake mi nadhani kinawahusu watu wa accounts zaidi kuliko wadau wengine.
ReplyDeleteKeep it up ankal michuzi!!!!!!
Anonym.. feb.22, 02:07:00PM, kupata CPA ni bidii yako tu kama ilivyokuwa kwa vyeti vingine. Ila wengi wanaofanya mitihani hii wanatokea makazini, hivyo muda wa kujiandaa unakuwa mdogo. Matokeo yake ni mass failure. Wachache wanaofauru wanaonekana kana kwamba wao ni wenye akili sana.
ReplyDeleteNimekuwa nikishiriki kutunga na kusahihisha hii mitihani ya CPA, nilichokiona si ugumu wa mitihani bali maandali finyu kwa watahiniwa.