Mkuu wa libeneke,
naamini una tarifa juu ya uporaji wa mikoba kina dada ulioibuka kwa kasi hapa jijini. Kwa busara yako jaribu kuifuatilia gari aina Toyota rangi ya kijivu hasa maeneo ya masaki.
Jana jioni mida ya saa 12 jamaa wamewaliza
watu na wakatokomea kwa kasi ya ajabu..
Mdau!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Inaonyesha kasi ya maisha imeongezeka na maisha yamekuwa magumu mpaka mbinu za aina hii zinatumika. "maisha bora kwa kila mtanzania" imeshindwa kutekelezeka........Tufanyenini sasa wa Tz? Maoni..

    ReplyDelete
  2. Binafsi nimewahi kuona pale Chole road karibia na ofisi za madini mdada mmoja akiporwa begi lake lenye Laptop akapiga ukelele na kuokota mawe nakurusha wakati salon ikitokomea kwa kasi ya formula one.Kuna haja hawa wakawekewa mtego na watakatwa tu

    ReplyDelete
  3. Siyo saloon tu. Hivi sasa matukio haya ni ya kawaida hapa Dar Es Salaam. Watu wanalizwa na wahalifu wanakimbia. Kuna wakati nilishuhudia uporaji huu nikawa nawakimbiza nikiwa kwenye gari aina ya ESCUDO. Nilijaribu kupiga simu polisi na namba za dharura zilikuwa hazipatikani kabisa. Nikaamua kwenda kutoa taarifa kituo cha Urafiki, Nilipofika nikaelezwa kwamba uwezi kupata utasumbuka bure. Nikauliza ni kwanini simu ya dharura haipatikani wakasema ni mtandao wa ZAIN tu ndo watumia namba hiyo nikaachwa hoi.

    Hivyo polisi hawana msaada bali wananchi tuungane kupambana na tabia hii kwa kuweka mitego

    ReplyDelete
  4. Ujumbe kama huu uwe unachujwa. Hasa mnapoupitia nyinyi wataalam. Anataja gari bila namba na details zingine! wadau tunahoji huhalali na ukweli wake.

    Angalia messages zinazotumwa na wajumbe tafadhali.

    ReplyDelete
  5. Weka Registration number. Usionee haya uporaji!

    ReplyDelete
  6. Hii habari uncle Michuzi haieleweki kabisa, ni too general kwa jiji kubwa km Dar es Salaam, Unaposema toyota ya kijivu zipo ngapi na kuna aina ngapi za toyota hapa Dar ? Ni vema habari ingezungumzia ni toyota ya aina gani na kutaja namba zake za usajiri. Habari km hizi ziwe za kina sio juu juu hivi.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  7. Hukutaja namba....sasa ole wako nipatiwe usumbufu kwa corolla yangu kuwa na rangi ya silver......PATACHIMBIKA!....mwenyewe umeona umezungumza point...kumbe umechemka tuu.

    ReplyDelete
  8. hao watu si Masaki tu na maeneo mengine ya jiji na sina uhakika kama ni walewale au ni kikundi tofauti. Kuna dada mwingine walimwiibia Mwenge. Hawa walikuwa na baloon rangi sifahamu. Inatisha kwani walimshikia kisu, huku wengine wakijifanya wanazungumza nae ili kuwachanganya wapita njia wasifikirie kama kuna uhalifu unatendeka. Polisi inafahamu kwani haya matukio yanaripotiwa na inaelekea yanazidi kuongezeka. Naomba hii tahadhali itolewe kwenye vyombo vya habari na mkuu wa jeshi la polisi kama anavyotangaza wanapokamata wahalifu au silaha n.k. waathirika wakuu wamekuwa akina Mama. Nawasilisha.

    ReplyDelete
  9. Hiyo Taxi pia inazunguka na kuwapora wanawake mitaa ya Regent mpaka kairuki Hospital

    ReplyDelete
  10. Huu wizi umeenea sana, hasa mitaa ya Oysterbay na Masaki, wanawavizia watu wakiwa wanatembea kwenda kwa jirani au wanatembea mazoezi alafu wanawapora chochote, kuanzia mobile n.k.

    Kwakuwa mtu anakuwa mtaani anakuwa na amani maeneo ya nyumbani hivyo hata mtu akishuka kwenye gari anajua tu labda anashughuli zake, ila ghafla inakuwa hivyo!

    ReplyDelete
  11. ni kweli kaka hawa jamaa wanaliza sana watu, hasa laptops na wanapenda kuzungukia maeneo ya masaki na ostabey. na huwa wanabadili magari leo hili kesho hili.

    sema wadau wenye gari ndogo za namba private wawe makini na watu wanaowakodishia, hawa jamaa wanakodi gari zenye namba za njano na kwa siku wanakulipa 30,000. sasa unaweza mkodisha mtu kumbe baadhi yao tunawajua . wanaudhi sana

    ReplyDelete
  12. NI HIVI KAKA, SIYO GARI HIYO TU NI MENGI. NGOJA NIKUPE HIKI KISA KILIWAKUTA WADOGO ZANGU. WAO WALIKODI TAX MWENGE WAKIELEKEA MBEZI BEACH. BAADA YA KUINGIA NDANI DEREVA FUNGA MILANGO, ALIPIGA GARI MOTO MPAKA PORINI AMBAKO KULIKUWA NA WENZAKO WALIWAPORA, KILA KITU, BAHATI NZURI NDUGU ZANGU WALIWEZA KUSHIKA NAMBA ZA GARI. MUNGU BARIKI ILE TAX BAADA YA MIEZI KAMA 7 TULIIKAMATA SINZA CHA KUSHANGAZA POLISI WALITHUBUTU KUSEMA KUWA TUMALIZANE NA MWENYE GARI. KWA KUWA DEREVA AMEKIMBIA, HIVI NINANI ANAWEZE AKACHUKUA GARI AMPE MTU AMBAYE HAMJUI! POLISI WAKO WALISHAMALIZANA NA MWENYE GARI KESI IMMEISHA, SASA ANATAKA MWENYEGARI TUMALIZANE NA SISI HIVI KWELI UNAWEZA KUKAA MEZA MOJA NA JAMBAZI MMALIZANE! KESI IPO POLISI KIJITONYAMA GARI LIMEACHIWA TAX NAMBA AAZ 556 TOYOTA COROLA HUWEZI AMINI LAKINI NI KWELI NA HII KESI IPO POLISI KIJITONYAMA MABATINI. HII NDIYO TANZANIA BWANA. NILITAKA KUNJIBU HUYO MTU HAPO NAMBA SIO TATIZO SISI NA NAMBA TUNAIJUA NDIYO HIYO HAPO JUU NA KESI NDO IMEISHIA HIVYO. NA NDIO MAANA VITENDO HIVI HAVIISHI! NINACHOJUA MIMI ASKARI KAZI YAKE NI KULINDA RAIA NA MALI ZAO SASA SIJUI HIYO HAKI YA RAIA YA KULINDWA NA POLISI IPO WAPI. ROHO INANIUMA SANA!

    ReplyDelete
  13. Kwa kweli hapa mjini kwa hivi sasa hii ni kero kubwa kuliko hata kupatikana na pingu.

    Wadau tushirikieni kuwadhibiti hawa jamaa ni rahisi tukishajua gari wanalolitumia.

    ReplyDelete
  14. Kaka umekosea ni grey siyo silver,

    ReplyDelete
  15. wa-tz wenzangu sio masaki tu bali dar nzima dada kaporwa Changombe kalia ka mtoto lakini ipo cku

    ReplyDelete
  16. Hii hali inakatisha tamaa!ni kweli wizi huo upo ila jamani tusiangalie upande wa gari peke yake,iwe ya kijivu au tofauti,lamsingi ni kunoti plate namba inaweza ikasaidia kuripoti na hatua zikachukuliwa.Ila pia raia wema kuweni makini pia kuna wizi kama huo ila wanatumia pikipiki,tena unakuta ni mtu mmoja tu anakwapua kisha anakuachia vumbi tu na pikipiki,nimeshuhudia hilo maeneo ya Mabibo hivi karibuni.

    ReplyDelete
  17. MDAU WA JUU, HATA UKIJUA GARI WANALOTUMIA NI KAZI BURE KWANI KILA SIKU WANABADILISHA GARI. DAWA YAO NI KUWATEGA NA KUWAKAMATA NA KUTOA FUNDISHO LA NGUVU SANA IWE ONYO KALI SANA KWA WENGINE..
    WIKI HII TUNAANZISHA MTEGO MAENEO YA MASAKI NA MIKOCHENI MTASIKIA MATOKEO YAKE.

    ReplyDelete
  18. Kwakweli nasononeka saana kama Tanzania yetu ndo inakuwa hivi. Mie nataka kwenda likizo Tanzania natamani ningejua jinsi ya kutengeneza bomu nikaliweka katika mkoba na nikadunda nalo huku nikiwa na remote control, wakininyakua mkoba tu wakapanda katika gari mie nalipua na hakuna atakayepona katika gari basi tungewamaliza hivyo hata wengine wangeogopa maana najua wako weengi ni group la watu weengi.Ila ukisema uangalie namba za gari unajisumbua maana wanabandika namba feki wanapofanya uhalifu huo.

    ReplyDelete
  19. hii ishu ni kweli jamani. hapa Chukwa Road, barabara ya kwenda Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki na Hospitali ya Mikocheni, ambapo pia pana nyumba za Mawaziri na vigogo wengine, kuna uporaji mkubwa wanamna hiyo. matukio yanaanza majira ya saa 11 jioni hivi. wahanga ni wote wanaobeba mabegi. wanafunzi zaidi ya 6 wamekwishashughulikiwa, na wananchi kadhaa pia. inasemekana baadhi waliripoti polisi Oysterbay,but walijibiwa kuwa ikitokea tena wapige simu polisi.

    ReplyDelete
  20. sio magari tuu.. sasa hivi wanatumia hata pikipiki na ni mchana kweupeeeee...wiki mbili zilizopita nje ya gate la hospital ya Kairuki jamaa alikuwa na pikipiki tena kapakia mtoto wake wakaja jamaa nao wakiwa kwenye pikipiki wakampiga risasi ya mkono uliokuwa umebeba mkoba wenye laki sita na docs za ofisi ....wakachukua ilikuwa majira ya saa nne za asubuhi baada ya hapo wakapiga risasi gari iloyokuwa inakuja mbele yao wakidhani kwamba inawafuata kumbe jamaa alikuwa anawahi safari zake

    ReplyDelete
  21. U.S. Embassy
    Dar es Salaam, Tanzania
    Warden Message - Security Notice – Snatch and Grab Incidents
    February 3, 2010


    Over the last month, there have been several reports of snatch and grab type robberies in Dar es Salaam. In the most recent occurrences, occupants of a passing vehicle have grabbed bags, purses, and backpacks from pedestrians and bicyclists traveling on the side of the road. Many of these reported robberies occurred on the Msasani Peninsula on Yacht Club Road, Chole Road, and Haile Selassie Road.

    At least three of these robberies occurred after the victims visited the Barclay’s bank in Slipway. U.S. Embassy Dar es Salaam Embassy reminds American citizens to be aware of your surroundings at all times and to be especially alert to individuals paying an undue amount of attention to your activities. U.S. Embassy Dar es Salaam also strongly advises against carrying bags or purses while on foot or bicycle. If unavoidable, carry the bag in front of you or on your side furthest away from traffic. Also, it is recommended that the bag should be nondescript, even worn or dirty in appearance, so as to make it less appealing to criminals.

    It is advisable to walk facing oncoming traffic. Doing so increases your chances of recognizing the approaching danger and allows for the opportunity to take evasive measures.

    If you are the victim of a snatch and grab, you are advised to release your belongings to avoid physical injury. Hanging on to your belongings increases your risk of being dragged down the street (as has happened already), or getting caught under the rear wheel of the car.

    In the event of an incident, contact local authorities and the Consular Section of U.S. Embassy Dar es Salaam at 255-22-266-8001. Your cell phone should never be carried in a bag for this reason; carry it in a pocket or elsewhere on your person.

    The Consular Section of the U.S. Embassy in Tanzania can be contacted by telephone 255-22-266-8001 and fax 255-22-266-8247. You may also contact the U.S. Embassy in Tanzania via email at drsacs@state.gov. After hours American Citizen Emergencies should call 255-22-266-8001

    ReplyDelete
  22. du kweli Tanzania imekwisha,nchi inameoza na inanuka.Uamuzi wangu wa kuja kuishi Nchi za Scandinavia ulikuwa wa maana sana.Hapa hakuna hofu za mtu kuvunja nyumba yako usiku au kukukwapua mkoba wako ukitembea barabarani.Sasa ninaondoa ndugu zangu siku hadi siku na kusahau hayo matatizo.

    ReplyDelete
  23. du kila sehemu shida ulaya baridi kali maisha magumu hata ubebe box labda mbinguni pengine

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...