Washiriki wa semina ya mafunzo ya siku mbili kwa Masheikh na Mapadri kuhusu Usajili wa Ndoa na Talaka ulioanza leo katika ukumbi wa Msimbazi Center jijini Dar leo chini ya Wakala wa Usajili,Ufilisi na Udhamini-RITA.
Juu na chini ni washiriki mbalimbali wa wa semina hiyo ya ndoa na talaka leo









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Hii haijakaa vizuri,mbona hao viongozi wa talaka ni wanaume wengi?yaani mwanamke nimemuona moja tu!Women step up your game.mtakua mnaonewa kila siku.

    ReplyDelete
  2. Candid ScopeFebruary 24, 2010

    Ndo mwenendo wa dini zetu. Waislamu hawawezi fika mkutanoni na kuchanganyika au kukaa pamoja na mashehe. Kwa upande wa mapadre ni wanaume ndo wahusika katika kutatua matatizo ya ndoa za waumini wao. Vinginevyo wangeshirikishwa walei ndo mchanganyiko ungenoga vinginevyo ni mkorogo tu.
    Upembuzi yakinifu kwa nini wakristo wamekaaa upande wao na waislamu upande wao? Kwa nini wasichanganyike ili kuonyesha upendano kati yao kwani Mungu habagui na humimina neeza zake kwa kila binadamu bila ubaguzi wa rangi, dini au kabila

    ReplyDelete
  3. Semina ya Ndoa na Talaka inahudhuriwa na Wanawake 2 wanaume zaidi ya 30...!!!

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli wanawake nasi turuhusiwe kutoa talaka ikibidi lol kila siku wanaume tu. Na sisi huwa tunakosewa na tunajisikia kuacha na sio kuachwa. Tuinuke wanawake hasa wa kiislamu jamani.

    ReplyDelete
  5. Huu ni ujinga Kabisa. Yaani suala linaluhusu Waume kwa wake. Ninaona vikofia tu vya wanuame tu! Kwani Tanzania ni AFGHANSTAN AI IRAN. Tena kesi za Ndoa kwa hali yetu Tanzania ni vizuri zinapofika kwenye Mahakama zisimamiwe na mahakimu wanawake. Hili litaondoa uzandiki an uongo

    ReplyDelete
  6. KWA UJUMLA ADA ZA USAJILI WA NDOA NI KIKWAZO KWA JAMII MASKINI NA MWISHOWE NA UPOTEVU WA HAKI ZA MIRATHI NA CHIMBUKO LA MIGOGORO YA KIJAMII.TALAKA SIYO SULUHISHO KAMILI LA MATATIZO NDANI YA NDOA BALI NI MTAZAMO HASI WENYE HUZUNI NA MAHANGAIKO YA KIJAMII.ELIMU YA MISINGI YA KUDUMISHA NDOA KWA WANAJAMII NI MTAJI RASMI WA KUHIFADHI NDOA.

    ReplyDelete
  7. katika ukristu hakuna kitu kinachoitwa talaka wala wanandoa kutengana na atakayeivunja ndoa ni mungu tu pale ambapo mmoja amefariki dunia huo ndio mwisho wa hiyo ndoa hapa duniani... sasa hao mapadre wanaojifunza kuhusu talaka wanataka kutueleza kuna toleo jipya la BIBLIA (AGANO LA 3) limeisha toka? matumokhide!

    ReplyDelete
  8. Majority (if not all) are Imams & Pastors i.e. representing the Islamic & Christianity faiths. As far as I'm aware, there're very few female priests in Tz, and that's what you're seeing as a 'true' representation.

    ReplyDelete
  9. Anoni wa Wed Feb 24, 06:59:00 PM, kuna zaidi ya watu wangapi hawana kofia? hao ni wanawake?

    usitukane watu

    ReplyDelete
  10. ......just kumjibu huyo anyony anayesema katika ukristu hakuna talaka,mi nataka kumwambia kuwa KATIKA MAISHA HALISI TALAKA ZIPO NA WATU WANAZIISHI KILA SIKU,na ndio maana wameitwa mapadre hapa ambapo tunajua kanisa katoliki halita,bui talaka,ni katika kuwaambia tu kuwa talaka zipo katika maisha halisi,sasa tafuteni namna ya kudeal nazo.msituletee mambo yaleyale ya kupinga condom kwa kuwa kuna watu wamekaa Vatican na kuona kuwa hazifai wakati watu wanakufa kila siku na ukimwi........!!

    ReplyDelete
  11. Nani kasema lazima wanawake na wanaume wawe saw kwa sawa? acheni ujinga wenu wa kikekike!
    Mmesha kuwa brainwashed na wazung nyie kunguwani!

    Nendeni mkaishi ulaya, wajinga kama nyinyi hatuna shida nanyi hapa ni africa, tutadumisha tamaduni zetu zisizo na malengo ya kudhulumu wanawake

    ReplyDelete
  12. siyo madhehebu yote ya kikristo yana Mapadri sasa sijui wachungaji na mashemasi hawakualikwa. Tanzania kuna ubaguzi kweli kweli. Kama wachungaji wangealikwa mngewaona wanawake wengi zana hapo.

    ReplyDelete
  13. Huyu hapo juu anayesema wanawake waache ujinga hana nidhamu. Mjinga ni mama yake tu na dada zake. Hapa mashehe na mapadre wanataka kuweka mambo sawia.

    Pole sana ulipewa mdomo wa kuongea uchafu ukanyimwa akili ya utambuzi.

    ReplyDelete
  14. Kwa ufafanuzi mfupi ni kua hiyo ni semina ya mafunzo ya Usajili wa Ndoa na Talaka kwa viongozi wa dini mbalimbali ndani ya nchi yetu jijini Dar. Kama tunavyojua katika imani nyingi za kidini hakuna viongozi wengi wanawake sasa hao wanawakilisha hali halisi katika ngazi hizo. Kwasuala la Talaka hakuna dini inaruhusu wanandoa kuachana lakini kama serikali yetu inavyosema haina dini ila watu wake ndio wenye dini hakuna budi wananchi kufuata taratibu na sheria zilizopangwa na serikali na moja ya taratibu hzo ni suala la usajili wa ndoa na Talaka.

    Asia A.Mwita

    ReplyDelete
  15. kazi kweli kweli duh!!

    ReplyDelete
  16. BIBLIA INARUHUSU NDOA NA TALAKA.HILI SUALA LIPO WAZI KWA WANAFUNZI WAZURI WA BIBLIA.KUSAJILI NDOA NA TALAKA NI KWA MUJIBU WA SHERIA ZA JAMHURI AMBAZO KILA RAIA NI LAZIMA AZIFUATE.HONGERA SANA RITA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...