Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh I ssa Shaabani Simba akiwa katika picha ya pamoja na Sheikhul-Azhar (GRAND SHEIKH OF AL-AZHAR) Pr. Dr. Muhammad Sayyed Tantawyi katika Ofisi zake za Masheikhatul-Azhar zilizopo Darassa.
Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaabani Simba katika Mazungumzo na Sheikhul-Azhar Pr. Dr. Muhammad Sayyed Tantawy Katika ofisi yake Masheikhatul-Azhar iliopo Daraasa Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa S Simba akiwa pamoja na katibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi wa Kitaanzania wasomao Nchini Misri (T.S.U) na Mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Al-azhar Cairo Nd,Ghalib Nassor Monero katikati Sheikhul-Azahar Baada ya Mazungumzo katika ofisi za Sheikhul-Azhar Daraasa Cairo.
Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaabani Simba yupo nchini Misri Akihudhuria Mkutano Mkuu wa 22 (The 22nd General Conference: Under the Title The Objectives of Shariah(Islamic Law)And Issues of the Contemporary Age. Mkutano huo ambao ulianza siku ya 22-25 February 2010 sawa na 8-11 Rabi Al-awwal 1431H. Mkutano huo ulifanyika Katika Hoteli ya Conrad, Cairo, na ulijumuusha Masheikh na Viongozi wa Wakuu wa Nchi mbalimbali.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hello,
    Mimi nina swali.. Je kama unaijua kurani- Quaran ina maana kuwa unaweza kuongea kiarabu fluent?
    Mdau Ottawa, Canada

    ReplyDelete
  2. Muulizaji wa 1st.

    Kuweza kusoma Quran haimaanishi kujua kiarabu fluently.

    Karibu Waislamu wote wanaweza kusoma Quran lakini si wote wanaweze kuongea fluently.

    Waumini husoma kiarabu kwa ajili ya universality ya dini na baada ya hapo kila mmoja anaweza kusoma tafsiri kwa lugha anayofahamu.

    ReplyDelete
  3. WATU WENGI WANAOSOMA QURAN NI KWAMBA WANAKARIRI MAANDIKO, NI KAMA VILE MTOTO UNAVYOMPELEKA SHULE NA KUJIFUNZA KUSOMA, UNACHFANYA NI KUKARIRI TU, KINACHOSAIDI KWA MFANO KAMA UNAKARIRI KUSOMA KISWAHILI NI MANENO HAYO HAYO UTAYATUMIA NYUMBANI NA FAMILIA YAKO NA UTAKUMBUKA ALAAAA KUMBE NILICHKARIRI SHULE NDO HICHI NAKIONGEA HAPA NYUMBANI, LAKINI KUKARIRI MAANDIKO YA KIGENI NI VIGUMU KUJUWA UANONGEA NINI, NI SAWA NA KUAMBIA SEMA GOD IN ENGLISH LAKINI HUJUWI MAANA YAKE KIKWENU, SO MANY PEOPLE HATA KIJIJINI KWENU MIAKA HIYO YA 60 KULIKUWA NA MASHEIK WAZURI SANA WASOMA NA KUFUNDISHA QURAN LAKINI WALIKUWA HAWAJUWI KUITAFSIRI KWA KISWAHILI NA WALA WALIKUWA HAJUWI KUONGEA KIARABU NA NINAHISI HADI LEO IKO HIVYO UNLESS MTU AMESOMA LUGHA YA KIARABU. NA JAMBO LINGINE NATAKA KUJUWA MBONA WANAFUNZI KARIBU WOTE EWANAOSOMA NCHI ZA MISRI, TURKEY AND THE LIKE NI WA DINI MOJA TU SIJASIKIA ANNA ROBERTS KWENYE LIST ZAO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...