Ankal nasikia kuna upatu ka wa DECI Mwanza, na unashamiri sana ingawa ndo unaanza anza na sijui mode yake ila unaitwa mega worth. Hawa jamaa wanatumia sana MPESA kufanya hizo transaction zao. Sasa nahisi hii ni hatari. Kabla watu hawajalia hebu fanya utafiti kama iko hivyo au la.. KCB bank Mwanza unaweza anzia kama una mtu pale maana huyu mtu wangu kausikia hapo na akashawishiwa kujiunga akachomoa.
Mdau Rock City.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Bro na Mdau wa Rock City, Naomba kusema kuwa vyombo vyetu vya habari vinatumia vibaya neno UPATU wakati wanachotaka kukieleza ni Pyramid scheme au Ponzi scheme. 1.Upata ni mfumo unaotumiwa na Waswahili (wenyeji wa mwambao wa Africa Mashariki) ambapo kundi la watu kila mwezi huchanga pesa kidogo ambazo anapewa mmoja wa wanachama wa duru hiyo; halafu mwezi unaofuata mwanachama mwingini hupewa kitita hadi duru zima likamilike. Neno upatu hasa maana yake ni kisahani cha mchango kinachozungushwa katika sherehe. 2. Pyramid scheme huanza kwa watu wengi kuwapa waanzilishi wa mfumo pesa kidogo na kuwaingiza wanachama wengine wengi zaidi ambao huwapa pesa wanachama waliotangulia, n.k. hadi piramidi inakuwa kutoka, mathalan, watu 20 hadi kufika laki moja au zaidi. Katika nchi za Asia na Afrika Kaskazini mara nyingi mfumo huo hufanikiwa kutokana na mzunguko huo kusambaa na kuzunguka. 3. Ponzi scheme ni mfuko wa wawekezaji uchwara ambao wanachukua pesa za watu wanaowaamini na kujitia wanawekeza na kisha kuwapa investors faida kubwa kila mwaka. Tatizo ni kuwa brokers wao hawawekezi!!!!: wanachofanya ni kutumia pesa za wawekezaji wapya na kuwalipa wawekezaji wa zamani hadi hapo wanapogonga ukuta. Mfano mzuri wa mpango huu ni yule tapeli aitwaye Maddof aliyewatapeli wawekezaji wake USD bilioni 50. (4)Kwa hivyo ingia upatu na watu unaowaamini. Wachana kabisa na pyramid na ponzi schemes kama zile za DECI; huo ni utapeli ambao utawaliza watu. Mdau A. Hamadi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...