Vodacom Tanzania imezindua maduka matatu ya kisasa yatakayotoa huduma za Vodafone M-PESA Jijini Dar.

Vodacom pia, itazindua maduka zaidi ya 100 nchini kote yatakayotoa huduma za Vodafone M-PESA kwa wateja wa huduma hiyo wapatao milioni tatu kwa sasa--- huduma hizo zitatolewa katika mazingira bora na yenye usalama zaidi.

M-PESA ni huduma ya utumaji na upokeaji fedha inayotolewa na Vodacom Tanzania, huduma hiyo inamuwezesha mteja wa Vodacom Tanzania kutuma pesa kwa kutumia simu yake ya mkononi mahali popote katika Tanzania kwa na mteja wa mtandao wowote uliopo hapa nchini.Pia ina muwezesha mteja kulipia bili za huduma mbalimbali kama vile umeme, maji na DSTV.

Mkuu wa Mauzo wa Vodacom, Franklin Bagalla alisema, “ ili kukabiliana na ongezeko la kasi la wateja wa huduma ya M-PESA, ambapo sasa wamefikia milioni 3 , hatuna budi kuyaboresha mazingira ya utoaji huduma zetu za M-PESA, yawe bora na yenye usalama.

Alifafanua kuwa Vodacom siku zote imekuwa ikijidhatiti kutoa bidhaa na huduma zake katika kiwango bora.


Maduka yaliyozinduliwa yako katika mitaa ya Msimbazi (Kariakoo) Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Sinza Kijiweni, baada ya wiki tatu maduka mengine yatazinduliwa katika maeneo ya Kibaha, Mwenge Kigamboni feri Jijini Dare s Salaam.

“Maduka haya yamebuniwa ili kuwezesha kufanikisha utoaji wa huduma ya M-PESA. Ni benki halisi ya M-PESA na yamewekwa katika maeneo ambayo ni rahisi kufikika”

Maduka kama hayo tayari yameshazinduliwa katika mikoa ya Kilimanjaro (Moshi Mjini)
na Arusha, hadi sasa kuna mawakala wa Vodafone M-PESA zaidi ya 2000 nchini kote.

Alisema duka la Msimbazi litatoa huduma zake kwa masaa 24

“Tunatambua kwamba Kariakoo ni eneo lenye shughuli nyingi za kibiashara. Watu wengi wanaofika hapo wanatoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu kununua bidhaa na huduma mbalimbali.

Alisema kutokana na uhalisia huo, huduma ya kifedha ya masaa 24 ni muhimu sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. son of landless peasantFebruary 11, 2010

    well done,voda hii itavutia watu wengi kujiunga,ila my observation ni kwamba maeneo ya kinondoni watumiaji ni wengi ila tatizo hamna kituo kituo kituo kilichopo maeneo ya studio hakifai kabisa kwa sababu yule mdada anaekiendesha hana kauli nzuri kwa wateja,personal nilienda kujiandikisha,ila nilivyokuwa treated ni kama mtoto,mwisho nikachaniwa hata na zile form nlizokuwa na jariwa nikatupiwa,na kwenye kitabu zikachanwa,kwa kweli ilinisikitisha sana kwa kuzingatia nilitoka mbali kwa ajili ya zoezi hilo,na nilipoteza mda wangu na gharama zangu za nauli,hadi pale,ikabidi niende mlimani city,thanks them kwani walinipatia huduma nzuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...