Kaka mi ni fan wa blog yako bwana.
Sasa kuna issue imetokea usiku wa leo maeneo ya salender bridge one of my friend kapata big problem pale. Ucku mida ya saa 6 hivi, gari imemfia mahali pale, wakatoka vibaka porini mle wakamvamia wakampora kila kitu na wakamkata mapanga mwilini . Kiukweli its too bad wamemuumiza sana wamemvunja mguu.
Dah! inatisha kwa kweli, cjui Tanzania tunaenda wapi? Mana pale pembeni kuna kituo cha polisi lakini bdo maeneo yale yamekuwa ni mazuri ya vibaka na hii si mara ya kwanza kutokea vitu vya namna hyo. WADAU WENZANGU TUFANYAJE JAMANI?? TUTAFIKA KWELI??
The guy is in a bad condition, yuko hospital.
NAWAKILISHA
MDAU
The guy is in a bad condition, yuko hospital.
NAWAKILISHA
MDAU
pole sana ndugu yetu kwa mtihani liomkuta..hapo salenda bridge sisemi mengi lakini kweli panatisha..kwa serekali ni aibu tupu sehemu nyeti kama ile wanashndwa kuweka hata kamera zikawa zina operate tena karibu na kituo kikuu cha polisi...hivi ni kitu gani ambacho serekali wataweza kufanya.....tena kama mnavosikia kwenye vyombo vya habari eti kuna wabunge kwa miaka mitano hawajatoa mchango wao bungeni...tujiulize wanafanya nini au wanawakalisha nani..?any way ni aibu sana kwaserekali sehemu kama ile haina facilities kama hizo.....inabidi watambue kuwa siku zinavyosogea mbele crimes inazidi na hii inasababishwa na mambo mbali mbali ikiwemo uenevu na umasikini.....wewe angalia jangwani sehemu moja ina taa ni pale mwanzoni tena sio ya serekali ni ya matangazo...sehemu iliyobakia hadi magomeni hamna kitu...
ReplyDeleteJamani pale mahali sio mara ya kwanza mambo hayo kutokea. Vijana wanajificha kwenye ule msitu na wanatoka na silaha na kukuvamia. Wakati mwingine nyakati za mchana kama kuna foleni sana wanachomoa simu au hata vioo vya pembeni vya magari wakati gari linatembea kidogo kidogo na halafu wanakimbilia kule msituni.
ReplyDeleteSwali la kujiuliza, je Halmashauri ya jiji haioni kuwa ile miti inaficha majambazi. Wanashindwa kuipunguza ili eneo lile lionekane? Kuna siri gani ya kung'anga' nia kuwepo kwa msitu mkubwa kama ule? Hebu safisheni eneo lile uone kama atabaki jambazi.
Alikuwa ametoka wapi usiku huo...aaahhh mambo mengine ya kujitakia mnataka sirikali!!!!HOW???yaani sirikali ifanye kazi zote kwa nini asitumie common sense nakukimbilia kituonni???wabongo banaaah wavivu kwa kila kitu!!!!yaani sirikali ifanye kila kitu??TUMECHOKA NOW NA ISSUE ZENU ZISIZO NA MIGUU WALA KICHWA....kila kitu ooohhh sirikali.
ReplyDeleteMdau wa UK
Hayo ni madhara ya ubinafsi na ufisadi.
ReplyDeleteweee hapo juu tumia kichwa kufikiri na co nguvu,mtu ana haki ya kutembea muda wowote anaotaka na WAJIBU WA SERIKALI KUMLINDA,na ww unaishi uk ya ulaya cjui au uk ya tz,make km ni huku ulaya mbona watu tunatembea mpaka usiku sana,sasa unataka saa 12 jion watu walale??,jaman hawa serikal na polis wao mambo ya kipuuz ndo wanahangaika nayo kweli lkn ya muhimu km hayo walaaa!,utaskia bungeni wanataka kuongeza majimbo na wabunge wakati shule hazina madawat,hospitali hamna vitanda na ulinz kwa raia wake hamna kbsaa!
ReplyDeleteWewe Anon wa 01:06 usiwe unaongea vitu kama ZUZU kwani hujui mjini kuna nini? Labda anatoka kazini Late Shift na unaambiwa gari limemzimikia, Mbona watu wengine wapumbavu sana, yaani ni ili mradi upate kuongea tu. Jaribuni kuongea vyenye maana siyo kila kitu unadakia na kutoa ujinga. Ankal na wadau samahani kwa lugha ni kutaka kumfikishia ujumbe huyo Juha.
ReplyDeleteWatu wengine wana roho za ajabu kweli hata pole kwa aliyeumia unaanza tu umetoka wapi? wewe inakuhusu nini huku ulaya tunapokaa hata hakuwasaidii chochote bado mnakuwa na mawazo ya maporini tu. Roho mbaya tuuuu!!!!
MWESHIMIWA ULIYELETA HII HABARI MPE POLE SANA HUYO MTANZANIA MWENZETU TUKO NAYE PAMOJA KWENYE SALA MWENYEZI MUNGU ATAMJALIA AFYA NJEMA NA KURUDI KUENDELEZA SHUGHULI ZAKE ZA KILA SIKU. SISI NI WAJAMAA KAMA KUNA LOLOTE UNAONA TUNAWEZA KUSAIDIA USISITE KUTULISHA KUPITIA HII BLOGU YETU YA JAMII KWANI TUPO WENGI WENYE MOYO WA KUSAIDIA JAPO HIKI KIDOGO TULICHONACHO TUTAGAWANA IWE FWEZA AMA MAWAZO. MUNGU AMBARIKI SANA. AMEN
MDAU WA BUCKINGHAMSHIRE-UNITED KINGDOM
MAJIBU KWA PROF.J. MBELE HAYO SASA VIJANA WAMETOKA VIJIWENI MADHARA MNAYAONA SASA? JOKE ASIDE!!!
ReplyDeleteMPE POLE SANA MUUNGWANA HUYO NAJUA WATAKUWA WAMEMRUDISHA NYUMA LAKINI ASIFE MOYO MUNGU MWENYE REHEMA ATAMJALIA AFYA NJEMA NA ATARUDI KWENYE MAPAMBANO NA ATAMZIDISHIA MARA 10 YA HAO VIBAKA WALIVYOCHUKUA.
TUTAMWEKA KWENYE SALA ZETU MUNGU AMPATIE BARAKA ZAKE ILI AWEZE KUPONA HARAKA NA AWE MWENYE AFYA NJEMA.
MDAU BRANDS HILL
Wewe mdau wa UK unayemshutumu aliye shambuliwa na majambazi inabidi ufikirie kabla ya kuandika. Nafikiri hujui hata jukumu la serikali ni lipi. #1.Kuhakikisha usalama wa raia na mali zao. Sasa kwa akili zako unataka kila mwananchi awe anatembea na panga au kisu kujilinda nafsi yake? Hiyo ni kazi ya serikali kuhakikisha usalama wa raia. Nafikiri hata huko UK ndio utaratibu unaofatwa na wananchi na serikali yao. Sasa sisi kulalamikia serikali yetu wakati raia wema kishambuliwa na waovu kosa liko wapi?
ReplyDeletePole sana nyote mliofikwa na uovu huo unaondelea hapo. Hawa watendaji wa serikali ya jiji wamelala usingizi fofo wakati wananchi wanateketea.
oyaa hiyo sehemu wala msisumbuke nayo saaaana...mimi yashanitokea hayo tena mapema sana ilikuwa mida ya saa tatu hivi...
ReplyDeleteUkweli ni kwamba kile kituo cha polisi pale si kito cha polisi bali cha vibaka,ninaamini kabisa polisi wanawafahamu wale jamaa ila ndio hivyo tena wanakula wote.
Cha maana ni kumuomba mungu tu usiharibikiwe pale ...Polisi ni mradi wao ule..poleni wadau.
wewe anoni wa feb 11, 1:16:00 am,wewe mpuuzi nini, mbona unaongea pumbaa?? nafkiri wewe ni mmoja wa hao mafisadi.... sasa kazi ya kulinda wananchi ni ya nani kama sio serikali?? sasa unaambia wa2 wamemzunguka na mapanga atakimbilia vp polisi unamegwa nini.... hayajakukuta bado ndio maana unachonga ngoja yakukute ndio utayajua punguani wewe....
ReplyDeleteTanzania tuna uhuru wa kuwa na silaha. Kwa kuwa polisi na serikali haina programu yoyote ya kutatua swala la ujambazi, naamini kuwa wananchi peke yao wanaweza kuyatatua matatozo ya ujambazi kwa kuomba vibali vya silaha. Wakiona wananchi wana silaha, wao wenyewe watakimbilia mbali na kukuacha. Dukani kwangu nina askari kanzu binafsi sita nje kila siku, na kila meneja ana silaha, nasubiri kwa hamu kuvamiwa. Sitapeleka jambazi hata mmoja hai polisi, nitawaua hapo papo.
ReplyDeleteI am not surprised, it's a familiar story especially for that place.
ReplyDeleteUshauri wa bure tu na kwa nia njema. Kama huna uhakika na ubora wa gari lako kwa mida kama huo uliyoutajwa ni vizuri ukawaomba police pale kituoni wakupe escort.
Emergencies kama flat tyre keep on driving until you reach a safe place where you stop and change your tyre.
Mshauri mwenzako ambaye hawezi kuaccess habari hii.
Pole sana. Lakini kwa ushauri tu, tupunguze safari za usiku zisizo za lazima.
ReplyDeleteKama ni muhimu bora kupita njia yenye watu wengi..wanaopitapita
Kama mtu una mgonjwa bora msindikizane watu kadhaa hata kuomba kwa jirani..kama mliopo hamtoshi (hio inasaidia sana). Lakini peke yako kwenye gari usiku wa manane mh! kwa hapa Dar ni risk sana maana gari ni kifaa utakuta ghafla limekuzimia popote.
Mara nyingine watu wanawekwa kazini hadi usiku wa manane bila utaratibu wowote wa kuwa sindikiza nyumbani kwao si haki kwa hali halisi ya vibaka hapa Dar...
MDAU WA UK (UKONGA) Thu 11, 01:16:00AM NI MMOJA WA HAO VIBAKA AMBAO HUFANYA UHALIFU HAPO KISHA KUKIMBILIA UKONGA KWENYE MAFICHO YAKE. HUYU AMEKUWA AKISHIRIKI KWENYE UPORAJI HAPO NYAKATI ZA MCHANA LICHA YA KUJIFANYA KUWA HAJUI KAMA UHALIFU HUO HUFANYIKA NYAKATI HIZO; TUSHIRIKIANE KUMTAFUTA ILI TUMKABIDHI POLISI.
ReplyDeletePole kwa aliyejeruhiwa. Mdau wa Uk ondoa uvivu wa kufikiria ujue kuna Madaktari na wauguzi wanafanya kazi hadi usiku, Walinzi na waongozaji club za usiku na sehemu za burudani pia huwa wanafanya kazi mpaka usiku wa matisa. Afu wasiilaumu serikali kwani kodi yao anachukua nani? Waache kutoza kodi tuajiri walinzi wetu binafsi kama vipi. Ulinzi usipoimarishwa ndo ivo kauchaguzi kanakuja tujaribu mwinginelabda atatulinda.
ReplyDeleteWee limbukeni wa UK acha ushamba huwezi ukauliza eti mtu sa6 usiku katoka wapi hapa mjini kazi ni nyingi na swala la kuilalamikia serikali ni hake yake ndo maana hatoi kodi kwa mtu yeyote zaidi ya serikalini. Hivi unajua swala la ulinzi wa raia ni la serikali na si mtu yeyote hebu endeleeni kufanyishwa kazi za ndani huko UK na kulala kwenye vibaraza.
ReplyDeletewe mdau watatu wa u.k mambo ya tz kama huyajui yaache endelea na ya huko u.k tuachie sisi wenyewe wa tz tunauelewa huo msitu sio tu usiku hata mchana kweupee watu wanaibiwa.tena kwenye foleni.kuhusu swala la anatoka wapi usiku haikuhusu kwani wewe hujawahi kuwa barabarani mida ya sa sita?shame on you,and you just close your big big mouth.
ReplyDeleteSEREKALI INAPASWA KUWEKA ULINZI KILA MAHALI, JAMANI SI SALENDA TU. HATA SEA CLIFF HOTEL. KUNA NDUGU YANGU ALITOKEA SEA CLIFF ANAELEKEA MJINI MIDA YA SAA MBILI USIKU, BAHATI MBAYA GARI IKAKOROFISHA MAENEO YA KARIBU NA SEA CLIFF HOTEL, WAKATI ANASHUKA KWA AJILI YA KUFUNGUA BONET, AKATUPA JICHO KWENYE SITE MIRROW YAKE, AKAONA VIBAKA WANAKUJA KWA KUNYATA TENA WAMESHIKA MAPANGA , YEYE ALIWEZA KUKIMBIA WANAMKIMBIZA WAKARUSHA PANGA AKAKWEPA (HAWA NADHANI WALITAKA KUUA KABISA) BAHATI NZURI ALICHOMOA FUNGUO ZA GARI HIVYO ALIBONYEZA ALAM HUKU ANATIMUA MBIO HIVYO GARI ILIPIGA MAKELELE, VIBAKA WAKAKIMBIA LAKINI WALIMUIBIA KILA KITU. MAANA GARI ILIKUWA WAZI.
ReplyDeleteSEREKALI (VYOMBO VYA USALAMA): HII NI AIBU NA NI MBAYA KWA USALAMA WETU NA WAGENI PIA. MNAFANYA KAZI GANI. KUNA SHIDA GANI KUPELEKA ASKARI KULINDA MAENEO KAMA HAYO. NA KWANINI MAENEO KAMA HAYO MNAONA KABISA KUNA VICHAKA KWANINI HAMVITOI NI VYA NINI?
Hv mdau wa Uk unaakili kweli wewe!
ReplyDeleteau haujui kusoma vizuri?
umesikia gari limeharibika pale ulitegemea akimbilie polisi kivipi? na unajua vizuri lile eneo likoje hjata kama kukimbia utakimbia mpka wapi.
Kumbuka maeneo yale kuna shughuli nyingi hospitals, homes etc sasa kusema amejitakia mwenyewe ni upungufu wa fikra
Nakutakia kila la kheri na ishu zako zenye migu na kichwa, as i cn see uko very perfect.
Kikubwa ni uzembe tu, matukio mengi kama hayo yameripotiwa eneo hilo lakini hamna angalizo lolote liliofanyika.
wewe 01:16:00AM, siamini ulichoandika? alikuwa anatoka wapi usiku? kweli inawezekana wewe pia uanfanya kazi za ujambazi na ni muuwaji, how can write such a stupid post mtu kaumizwa na ni wajibu wa serikali kulinda wanaanchi wake kwa kuhakikisha wako salama, alafu of all pipo you should have known better kwa kuwa umejidai uko UK, labda kama uko UK D. kweli akili zako ziko matakoni.....serikali isipo weka usalama unataka aweke baba yako? your such a nit wit!!!
ReplyDeletePole sana ndugu yetu kwa mkasa huu. kwa mawazo yangu ya kawaida tu hapo mahali nahisi kama ni mradi wa IGP na RPC wake wa kanda maalum kwa maana sii rahisi kuwa na maficho ya vibaka mbele ya kituo cha polisi.
ReplyDeleteAnkal kama kunauwezekano muhamasishe Kova na mwema angalau wasome mavituzz kwenye blog ya jamii
Ankal
ReplyDeleteHuyu mdai wa tatu kanikera kweli! Dhamana ya ulinzi ni ya nani? huo muda kweli unaweza kuuliza mtu alikua anatafuta nini? hizi kejeli anazitowa wapi? Vp kaokota box lina viji pound ndio maana ana maneno ya hovyo hovyo!?.......wacha niache najisikia mzuka unapanda.....!
POLISI WAKOBIZE KUSHUGHULIKIA MASHWARA YA JERRY MURO
ReplyDeletewewe unayejiita mdau wa UK acha upuuzi wako,kuna tatizo gani kuendesha gari usiku?kwa akili yako usiku vibaka ni halali,dawa ni kuwatega tuu hawa vibaka siku mnabeba machine zenu za kutosha then mnajifanya mmeharibikiwa gari,na wengine wanakuwa wamejificha kwenye buti la gari na zana kamili(bunduki)wakitokea ni kuwamwaga ubongo wote bila huruma(i mean kuwaua),nakuhakikishia hiyo tabia ya kukaba watu itaisha siku hiyo hiyo,ni ukatili lakini ndio dawa yao once and for all,na kwanini wasichukue wanachotaka mpaka wamkate mtu mapanga...hawa dawa yao ndogo na inakuja soon mtasikia.
ReplyDeletemtoa maoni 01:16, nadhani hujawahii kufikwa na shida siku ikikufika nawe utajua usiku wtau huwa wanatoka wapi jaribu kufikiria kama ingekuwa wewe ndo umekutwa na tukio hilo.
ReplyDeletepole sana ndugu kwa tukio lilompata mwenzio hii ndo inji yetu.
Wewe mtoa maoni namba tatu ujui usemalo, na inaonekana kuwa ni mgeni na mji huu.suala sio alikuwa anatoka wapi!! suala hapa ni kuvamiwa na majambazi!! iwe anatoka kazini ama kwenye starehe. hiyo sehemu ni mbaya sana kwa taarifa yako hata wewe inaweza kukukuta. salender pana vibaka wengi sana na ajabu ni kuwa kuna kituo cha polisi na majengo ya ubalozi wa uk, na urusi ambayo yote yanalindwa na FFU. lakini ni jambo la kawaida kabisa hata saa 4 asubuhi unaweza kukabwa na kuporwa kila kitu. muwe na tahadhali sana katika sehemu hii kwani inaonekana hata asikali wameshindwa.
ReplyDeletendugu watanzania ni kazi ndogo sana vibaka dar nzima au nzima haizidi elfu moja wakati watanzania tuko milion 4o.
ReplyDeletecha kufanya nia kuanzisha kikosi cha usalama sisi wenyewe vijana na kuwafuata hao wahalifu kila kona na kuwaeleza kundugu wakome maana la sivyo simu kuiba itamfanya kupoteza maisha. haina haja ya serikali maana imelala.
kuna sehemu mie nakaa nimeanzisha inaitwa ndala ilikuwa majizi wa silaha sasa tumeweka ulinzi wetu.
jamaa tumewafunsha kutumia mishare na mikuki hpia ikifika saa 4 hamna mtu kutembea ilikuwa kila siku shida sasa mwaka hamna.
maana nimewafundisha wakisikia bdunduki lala chini na tumia mshale au mkuki maana hatari ya risasi ni kusimama ila ukisikia lala halafu rusha mshale tena usifanye haraka wacha wao waoigi risasi halafu ifuate sauti wananch karikbu hamsini sasa ni shwari.
inasikitisha watanzania tumekuwa wapumbavi leo basi zima linatekwa na panga moja na ndio maana haya majizi yanapata moyo maana watu wamelala.
Kwanza kabisa mwenzetu pole kwa mkasa wa ulomkuta rafiki yako. lakini mimi naweza sema kuwa hao vibaka wa hapo salender kutakuwa na connection na askari wa kituo cha polisi. maana ni kwamba matukio ya hapo yamekuwa mengi yakiripotiwa hila hayapewi kipaumbele kushughulikiwa. Polisi hao hao wanashindwa vip kupadhibiti mahali hapo?
ReplyDeleteHuo ni mradi wa mapolisi wa salander bridge, ndio maana hao vibaka hawawezi kuisha. Nilishasema hapo awali kuwa, tatizo lisiloisha ktk nchi yetu huwa ni mradi wa vigogo na mapolisi wakiwemo......
ReplyDeleteMdau wa UK una akili timamu? Alikuwaanatoka wapi muda huo? Hujui watu wengine wanakuwa ofisini kujuenga taifa hadi usiku? au kama katoka hospitali je? Hata kama katoka kujirusha haihalishi kufanyiwa uhalifu huo. Anyway natoa pole kwa janga hili na kutoa wito kwa vyombo husika kuona hata aibu kidogo na kuamua kufanya kazi
ReplyDeleteKwa kweli nimesikitishwa sana na huyu mwenzangu hapo juu. Si ajabu na yeye akawa mmoja wapo wa hao vibaka. I'm certain hata huko UK ulipo umejilipua. Mtu kavamiwa, kaumizwa na kuibiwa and thats all you can say!! Sasa utakimbia vipi ndugu yangu watu wamekuvamia. And what makes you feel kwamba hakujitahidi kujiokoa kwa kukimbia. Na when asked kwamba usiku wote huo alikuwa anatoka wapi, wewe huko UK kazi yako unafanya saa ngapi. I'm pretty sure hauna kazi ya 8am-5pm but rather kazi ya shift. What you said had so much on your shallow thinking.
ReplyDeleteOn the other hand, inabidi uelewe kuwa majambazi wakubwa hata Tanzania ni Polisi na Askari. As a matter of fact uendapo kutaka haki katika vyombo hivi ndipo utapoteza haki zaidi.
Pole sana kwa ndugu yangu aliyelazwa hospital kwa majiraha na matatizo yaliyo kukuta. Mungu anakusaidia upone mapema.
Na kwa wewe mbeba maboksi pole sana kwa mawazo yako finyu.
WATANZANIA LAZIMA TULIULIZE JESHI LA POLISI KWANINI NAMBA YA SIMU 112 (SOS) HAIPATIKANI, NAMBA HII UTUMIAPO NI BURE NA HAIHITAJI SIMU KUWA NA SIM CARD KWA MUJIBU WA UTARATIBU WA NAMBA ZA IMEJENSI. INAWEZEKANA INAHUJUMIWA NA POLISI ILI VITENDO VYA UHALIFU VIFANIKIWE. MIMI BINAFSI NIMEKUWA NKJARIBU SANA KUITUMIA BILA MAFANIKIO KITU KINACHONIFANYA NISHINDWE KUTOA TAARIFA ZA IMEJENSI.
ReplyDeleteAcha hizo wewe usijifanye mjuaji! kuna kazi zingine ni za shift kwa hiyo acha uzushi anatoka wapi maana yake ni nini?? hapa tunahitaji ushauri na si mada ya kujua person issue. Serikali inatakiwa kusafisha lile pori na si vinginevyo.Na vibaka wa pale si usiku tu ata mchana pia juzi kuna shost wangu wamemwibia pochi palpale mnamo saa saba mchana kwa hiyo issue si kurudi usiku issue inabaki palepale vibaka wanajificha kwenye lile pori linatakiwa liondolewe. hata hivyo ina maana wananchi sasa tunatakiwa tulale saa kuminambili kama kuku???? mshamba wewe!!
ReplyDeleteWe mdau UK acha hizo. Ujui kuwa shida yaweza tokea wakati wowote na mtu ukatakiwa kusafiri hata saa tisa usiku????!!!!! Siendelei kuandika kingine maana michuzi ataibania lakini*&^())(+_)()_*&*£"!!¬&^ yako
ReplyDeleteJamani hii ni soooo na watu wa eneo lile tunalipa 3000/= kwa mwezi kwa ajili ya ulinzi shirikishi.... tooo much... polisi mfanyekazi jamani
ReplyDeletemmezidi ulevi na kupenda starehe usiku huo alitoka wapi,kama ni night shift angekuwa anatoka asubui bia mpaka jmatatu ndo maana,sasa serikali ifanyaje wakati duniani kote usiku ni hatari
ReplyDeletePigia kura CCM, watamaliza matatizo yoooote hayo.
ReplyDeleteHANG ON MY FRIEND,WENYE MAGARI TUOMBE VIBALI VYA PISTO FULLSTOP.
ReplyDeleteNi Salender au Selander??
ReplyDeletePili, nampa pole huyo aliyekutwa na majanga!! Kwa tunaoishi hapa Tanzania hizi ni symptom za tatizo kubwa ambalo liko katika nchi zetu na bara letu (Sub-Saharan Africa). Na kwa TZ hiyo ni "trela". Hali isiporekebishwa kwa haraka naogopa kusema kitakachotokea. Hivi hizo division zero na failures wengine wanamezwa wapi kwenye mfumo wa kiuchumi??
Tuache masihala tuliangalie hili kwa marefu na mapana yake. Na ni wajibu wa kila mtu, sio wanasiasa wala polisi wala mgambo au sungusungu.
we mdau wa uk mpumbavu mkubwa ucye na haya jambo kama hilo unaongea pumba, au kwasababu cyo wewe wala ndugu yako? fikiri kisha utajua ulichoongea ni ulimbukeni yaani kwasababu wewe uko uk ndo unongea rubish, je? angekuwa mama yako ungeuliza alikuwa anatoka wapi ucku, koma, tena ukome kweli, shwaini we, jifunze kuongea nalabuuku!
ReplyDeleteKILA mtu na dini yake mradi siku moja wamkute Ridhwani mbona hata daraja la Manzese kutapitika?
ReplyDeleteUnashangaa kuporwa jirani na kituo cha polisi wakati Polisi wenyewe ndo vibaka
ReplyDeleteleooo mdau wa uk domo lako na wewe limezidi kuharishaaa maana kila mtu anakusema wewe uwe unaangalia vitu vya halafu unachekecha akili yako kisha ndo uandike ok huo ulioandika ni pumbless ukome siku nyingine ina maana wewe bongo umetoka kitamboo au ashuo lako basi kama umeisahau usitie neno ok!!ok pole sana dada ulie pata matatizo wamekutia ulemavu wa bure maskini kama serikali imelala inabidi watu wajaribu kupambana nao tena wawepo wengi na silaha na mguu wa kuku usikosee wanahakikisha wanatoa utumboooo na kuupelaka palepale kituo cha polisi loh kama wanalaana vilee jamani!!!ok god bless u mgonjwa usijali utapona get well soon!!!
ReplyDeleteyaleyale . Bongo huduma za jamii si nzuri, usalama hakuna ....LAKINI TAMBARARE .
ReplyDeleteNamwombea mgonjwa apate nafuu haraka .
polisi wenyewe wanasubiria kwa hamu hizo mali zinazoibwa ili wagawane, saa ngapi wataimarisha usalama. ikiwa mkuu wa kituo naye anasubiri share yake kwenye rushwa tunazotolewa barabarani saa ngapi usalama utaimarishwa jamani, wakale wapi? nchi imeshaoza hii, wenye kuozesha ni hawa hawa viongozi wetu. tusingekua wanafiki, watanzania wote tungeweka mgomo, hakuna raia kupiga kura, mpaka haki zitendeke kwa kila mwananchi.
ReplyDeletemichuzi usinibanie tafadhali
salender bridge ni hatari sana kuliko hata huko uwanja wa fisi ishu hii hadi imfike mtoto wa mkuu wa nchi ndo patashughulikiwa fasta si mnakumbuka pale a-port walilamba begi lake moja wakati anatoka safari wala hakusumbuka saaana kama kina sie alimtwangia mkuu tu lol dakika ishirini nyingi sana begi na kila kitu hivi hapa na apologize kibaao yani salender narudia tena pale ukiharibikiwa hata saa moja usiku funga gari kimbilia pale kituoni manake ukisubiri msaada mauti yanakufata! pole mdau kwa tatizo lililokufika iko siku yataisha tuu ila lini hatujui hadi nani azaliwe wa kuitokomeza adha tunazopata lo!
ReplyDelete