Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania Suleman Nyambui akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano wa wadhamini kutangaza zawadi zitakazotolewa kwenye mbio hizo, wengine kwenda kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, Afisa Udhamini wa Vodacom, Ibrahim Kaude, na Meneja Udhamini wa Vodacom Rukia Mtingwa Zaidi ya Sh. Milioni 22 kushindaniwa Kilimanjaro Marathon
Kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 22 zitatolewa kama zawadi kwa washindi wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2010 zitakazofanyika tarehe 28 Februari 2010. Fedha hizo ndio kiwango kikubwa zaidi cha zawadi kuwahi kutolewa katika shindano lolote la mbio ndefu nchini Tanzania.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema jana kuwa “zawadi za washindi wa mbio ya kilomita 42 kwa wanawake na wanaume ni shilingi milioni 7.5 na jumla itakuwa ni shilingi milioni 15.
Washindi wa mbio za kilomita 42.2 kwa wanaume na wanawake watajipatia shilingi milioni 3 kila mmoja, washindi wa pili watajipatia shilingi milioni 1.5 kila mmoja na washindi wa tatu watajipatia shilingi 850,000 kila mmoja. Washindi wa kilomita (nusu marathon) watajishindia shilingi milioni 1.5, washindi wa pili watajipatia shilingi 750,000 na washindi wa tatu watajipatia shilingi 425,000 kila mmoja.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kutangaza zawadi jijini Dar es salaam leo, Kavishe alisema kuwa lengo la kuendelea kutoa zawadi za kuvutia ni kutokana na ukweli kwamba dunia nzima wanariadha wanalipwa vizuri.
“Tunaishi kwenye dunia ambayo wanariadha wa mbio ndefu wanastahili kulipwa vizuri, kama ilivyo kwa wanamichezo kwenye fani nyingine. Kilimanjaro Marathon ni mbio za kimataifa, lazima tuwe na zawadi zenye kuvutia wanariadha wazuri. Tumeona jinsi gani ushiriki wa wanariadha mbalimbali maarufu ulivyoleta msisimko mkubwa katika mbio hizi, lazima tuendelee kuboresha,” alisema.
John Addison, Mkurugenzi wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo amesema mbio za Kilimanjaro Marathon 2010 zitakuwa na mvuto wa aina yake kwani kutakuwa na wanariadha wanaokimbia kushinda zawadi na mataji, washiriki wanaokimbia kujifurahisha na kutakuwa na burudani mbalimbali. “Mbio hizi pia zitarekodiwa na baadae kurushwa kwenye kituo maarufu cha SuperSport kwa vipindi tofauti katika muda wa mwaka mzima,” aliongeza.

Waandaaji wanatarajia kuwa idadi ya washiriki itaongezeka na mashindano yatakuwa makubwa na bora zaidi. Takribani watu 3,500 walishiriki mwaka jana, “Tuna hakika mbio hizi zitawavutia washiriki wengi zaidi. Ni lengo letu sisi pamoja na washirika wetu Riadha Tanzania kukuza mbio hizi hadi ziwe kubwa zaidi hapa Afrika Mashariki,” alisema Bw. Addison.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...