kikosi cha Simba
kikosi cha Yanga

Afisa ubalozi amekubali mualiko kuwa mgeni rasmi kwenye kindumbwe dumbwe cha Simba na Yanga,mechi inayozungumziwa mjini Washinngton na vitongoji vyake,

Mpambano huo wa kukata na shoka utachezwa jumapili April 4 kwenye wanja jipya la 1417 Kalmia St,Nw,Washington Dc,kambi zote zipo shwari na zinaendelea vizuri na mazoezi.

Simba inaonekana imejiimarisha zaidi baada ya wachezaji wengi wa mikoani akiwemo Francis Makalaa aliyewahi kuichezea Simba miaka ya Nyuma kuthibitisha kuwepo kwenye mpambano huo,Kuhusu Nteze John bado viongozi wa Simba wanaendelea kumtafuta kwa udi na uvumba,Nteze anaishi Washington State alisahawahi kua mchezaji wa kutumainiwa Simba na Timu ya Taifa.kabla hajajiunga na Simba,alikua mchezaji wa Pamba ya Mwanza.

Kambi ya Yanga imekua kimya Kocha Yasini Randi amesema Simba wacha waongee,msema ukweli dakika 90,sisi bwana tupo tunaendelea vizuri na kambi yetu,sisi tunaingia uwanjani kama YANGA IMARA KUFUNGWA DAIMA MWIKO.

Jumamosi April 3 kutakua na mechi nyingine ya Stars na Maryland untd,itakayochezewa 18031 central park circle,Boyds,Md,20841,uwanja # 20

mechi hii ni moja ya mechi za kujinoa ya Stars kwa safari ya kuelekea Sweden july mwaka huu,mechi nyingine ya Stars ni April 24 mjini Boston itapambana na Zambia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Yanga kumdondosha Mnyama ni ngumu...kwani mwaka huu wachezaji wooote simba watakuwepo.Mwakajana Mlituvizia wakati wachezaji wetu wengi wapo kwenye mashindano ya college.

    ReplyDelete
  2. Wabongo tungependa sana kwenda Sweden, lakini kitendawili cha makaratasi bado ni kigumu.

    ReplyDelete
  3. kaka mbona matokeo ya man u siyaoni broo kuna watu wa london tunataka maoni yao kuhusu mechi.

    ReplyDelete
  4. ankal bwana yaani umeshindwa kuweka picha za champion league unavunga na hao wauza sura...

    he he he jana sijaona yale manjonjo ambayo mtu anafanyaga akiwa mgongoni... hee heee kumbe mbeleko ilikuwa hakuna... hee hee kitu mimba mshikaji kuja kupona miezi tisa...

    ReplyDelete
  5. KWA NIABA YA CHAMA LA YANGA MJINI HOUSTON,TEXAS......TUNAWATAKIA MAFANIKIO YANGA,DC KATIKA MPAMBANO HUO MKALI,WEMBE NI ULE ULE....
    MKEREKETWA NA MCHEZAJI WA YANGA,HOUSTON,TX
    ANDREW SANGA AKA BABA ZOE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...