basi lililogonga treni
basi lililogonga gari la mafuta

gari lililopopoa embe
Habari za leo Ankal,
Katika siku za hivi karibuni nimekuwa nikiogopa kuangalia taarifa za habari na wanangu kwa kujua kwamba habari ya kwanza itakua inahusu ajali na zitaonyeshwa picha za maiti na majeruhi. Kwa hesabu za haraka haraka, nafikiri idadi ya watu waliofariki kwa ajali za magari mwaka huu hapa nchini hazipishani sana na idadi ya watu waliofariki dunia kwa tetemeko la ardhi huko Chile.

Kinachonistua mimi zaidi ni Serikali yetu kutoonekana kuwa na mkakati mzuri wa kupunguza au kuondokana kabisa na ajali hizi. Kwa muda huo wote nilikuwa najaribu kutafuta suluhisho la majanga haya kwa kuwa najua katika kila ajali kuna familia zinapoteza mzazi, mkuu wa familia au mtoto na Watanzania kwa ujumla tunapoteza nguvu kazi muhimu. Katika ajali hizo pia kuna wanaopata majeraha makubwa na kupoteza viungo na hivyo kupungukiwa na uwezo wa kujiendeleza kiuchumi.

Mara nyingi habari huwa ile ajali yenyewe na vifo vilivyosababishwa na ajali hiyo. Kinachotokea siku na miezi baada ya ajali hakipati nafasi tena katika vyombo vya habari. Huwa hatujiulizi, je, ajali ile ilisababishwa na makosa ya nani? Je, majeruhi wote walipona na wale waliopoteza viungo walipata msaada gani? Je, waathirika huwa wanalipwa fidia yeyote au kila mtu na lwake? Je, wamiliki wa mabasi hukata bima zinazowalinda abiria?

Maswali ni mengi lakini kwa sasa naona ni muhimu kupata ufumbuzi wa tatizo lenyewe. Katika kujaribu kutatua tatizo hili nadhani vitu kadhaa inabidi vifanyike

Leseni zote daraja C zisimamishwe matumizi yake kuanzia Julai 2010 mpaka hapo dereva husika atakapohudhuria mafunzo maalumu yatakayoratibiwa na NIT na VETA ambayo yatamfundisha dereva kuwa makini awapo barabarani, jinsi ya kutoa huduma ya kwanza, uhusiano mzuri na mteja na jinsi ya kukagua gari lake.
Wahitimu wa mafunzo hayo watapewa “smart card” ambazo zitaingizwa kwenye mtandao. Kwa kuanzia Jeshi la Polisi linaweza kushirikiana na mashirika ya NSSF na PSPF kutoa kadi hizo, kuhifadhi picha, alama za vidole pamoja na habari zote za mhusika kwenye mtandao wa kompyuta. Mashirika haya yana uwezo huo kiteknolojia na yana ofisi nchi nzima.
Kila dereva wa gari la abiria atatakiwa kuvaa kitambulisho hicho (smart card) muda wote atakaokuwa kazini.

Nakala ya kitambulisho hicho (A4) itatakiwa kuwepo nyuma ya kiti cha dereva sehemu ambayo abiria ataweza kuiona. Dereva mmoja ataruhusiwa kuendesha gari si zaidi ya masaa 11 kwa kipindi cha masaa 24.
Jeshi la polisi likishirikiana na SUMATRA lianzishe kikosi maalumu cha barabara kuu (highway patrol) ambacho kitakuwa na jukumu la kuorodhesha madereva wote watakaokuwa wanafanya kazi katika barabara hizo. Kikosi hicho kitapewa uwezo wa kutoza faini za papo kwa papo pamoja na kupunguza pointi za dereva kila atakapofanya kosa.
Kila kosa litakuwa na pointi yake na dereva akifanya makosa mengi katika kipindi cha mwaka mmoja leseni yake itasitishwa.

Kampuni za simu zisaidie kampeni kwa kutoa namba za simu motomoto (hotline) ambazo zitaandikwa kwenye bodi za mabasi kwa ajili ya wananchi kuripoti madereva watakaokiuka sheria.

Mabasi yote yatatakiwa kuwa na namba za kuyatambulisha (Vehicle Identification Number - VIN) itakayochorwa ubavuni mwa basi ili kulitambulisha basi hilo kiurahisi.

Basi litakalopata malalamiko mengi zaidi kutoka kwa wananchi litafuatiliwa kwa siri na wakaguzi maalumu kutoka SUMATRA (Highway Marshals) ili kuthibitisha madai ya wananchi.

SUMATRA iwe na kikosi maalumu cha uokozi chenye vifaa vya kisasa na mafunzo maalumu. Gharama za uokozi zaweza kufidiwa baadae na kampuni za bima.
TBS ikishirikiana na wataalamu wengine wa nje na ndani ya nchi watafute jinsi ya kupima bodi za mabasi na kuthibitisha usalama wa matumizi yake.
Inawezekana kuwa hatua hizi zikasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa sana ajali barabarani.
Bila shaka, zitategemea sana mabadiliko kwenye muktadha wa kuendesha shughuli za barabarani kwa wadau wote. Kupita yote, hatua hizi zitakuwa na tija pale tu ikiwa suala la rushwa barabarani litatokomezwa kabisa, na wananchi watashirikiana ipasavyo na vyombo vya usalama.
Mdau Che Geuvera

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Ankal!
    Hili nalo ni neno. kAMA KUNA UWEZEKANO UMTUMIA IGP MWEMA ASOMO NA NINAHAKIKA KUNA ATAKACHO PATA. Ni muhimu kumtumia maana sidhani kama kwa binadamu wa TOLEO lake na CHAPA yake wanauwezo wa kujua blog ni kitu gani zaidi ya kukujua wewe kama michuzi. Kwa kuwapatia hawa ama yeye ni mwanzo wa yeye kuwa na ufahamu na huensa akawa ni miongoni mwa watu 90,906 waliobakia kutimiza watu 8M ili ajishindie ze fulanazzzz na pia awe amepata nenozzz zuri. Ila nakuomba utayarishe size itakayo mfeet kamanda kombezzzz xxxxx6 itamfaa wakati anasoma makala hii

    ReplyDelete
  2. good idea my friend lakini hao akina Sumatra wapo tayari kwa ushari kama huu wakati wanajua haowenyewe ndio wahusika wakuu kwa sababu wana magari ya daladala,mabasi ya mikoani na malori itakuwa ngumu wao kutekeleza hilo ndilo tatizola wa-tanzania walio wengi.

    ReplyDelete
  3. Ajali kwa Tanzania au sub-saharan Afrika zinatokana na kiwango kidogo cha kustaarabika. Iweje penye magari machache ndipo penye ajali nyingi?? Sijui kwenye ubongo wetu kuna kitu gani kimewekwa humo?? Nje tunaonekana smart, suti safi, utanashati. Lakini ndani Mwenyezi ndio anajua!!

    Kuanzia watu tunavyopata leseni, kuja mpaka watu tunavyoendesha magari, hata vibarabara vyenyewe (eti ni highway), traffic lights zilizozimika, hata zinazofanya kazi haziheshimiwi, watu tunaruhusiwa kutuma sms wakati tunaendesha magari, ...and nobody cares!!

    Utaarabu wa kuwa na hizi mashine (yaani magari) bado hapa Afrika. Kila mtu anahusika kwa hili. Hata anayetumia daladala anachangia vurugu zilizoko barabarabini. Kwa nini uombe kupandia au kushukia kituo cha msaada??

    Suluhisho ni kuanzia kwa mtu mmoja mmoja, angalia ustaarabu wako ukoje unapokuwa barabarani.

    Ripoti ya shirika moja la kimataifa inasema kuwa, hivi karibuni watoto wanaokufa kwa ajali za barabarani itazidi vifo vitokanavyo na malaria au kifua kikuu, kama watu tutaendelea kuwa machizi na wendawazimu "behind the wheel"!!

    ReplyDelete
  4. kaka hayo uliyosema ni ukweli mtupu,naaamini wanaohusika watachukua moja mbili tatu.
    kingine,ningependa kusema,hata barabara zetu hazina alama za barabarani.
    hakna hata stop signs,wala hata taa pale zinapohitajika,muda mwingine nawaza tanzania tunaendeshaje magari maana sasa nipo USA naogopa hata kuendesha home nikienda.
    hli suala linabidi lishughulikiwe kwa haraka,ni kweli tunapoteza watu na nguvu kazi kwa ajili ya uchumi.
    ni hivyo tu.

    ReplyDelete
  5. si Tanzania, Tanzania ni kufa tu. sheria zitawekwa lakini sheria hizo ndizo zitakazowapa watu kula, yaani dereva akikamatwa na kosa moja rushwa elfu 50 kila kosa. watu watashiba sisi tunaendelea kufa. NI HERI MFUNGWA ULAYA KULIKO RAIA MWEMA WATANZANIA.

    ReplyDelete
  6. Mdau Che Geuvera maoni yako ni muafaka kabisa na ya kizalendo. Ankal, unaweza kuprint na kusaidia kuwasogezea akina afande Mwema, Sumatra, na hata kule Magogoni, kama walikuwa bado hawajafikiria mamabo kama haya pengine wanaweza kuopoa moja au mawili na kuyaingiza katika ILANi ya Uchaguzi!!

    ReplyDelete
  7. Mdau solutions zako zitaleta usumbufu tu kwa abiria kwasababu wewe ume assumed ajali zina sababishwa na madereva tu. Lakina unashindwa kuelewa barabara zetu zina itaji kuboreshwa katika maeneo yote ambayo ni hatari kwa ajali vivile na wa invest ku enforce existing road traffic laws.

    ReplyDelete
  8. ninakubaliana na maoni ya mtoa maada hii,pamoja na hili pia ninamchango kidogo kuhusu tatizo hili. nikweli kwamba ukitizama ajali nyingi vyanzo huwa vimejikita katika maeneo mawili tu:-
    1.dereva kahusika kiuzembe.
    2.gari haliko katika hali muafaka ya kuwa barabarani.
    KUHUSU UZEMBE,kwa tanzania siwezi kusema ajali nyingi zinasababishwa na ulevi,hilo sidhani kama ni chanzo,bali mara nyingi huwa ni ujinga wa dereva,ama kazidisha mwendo,ama anamzuia mwenzie barabarani,ama ana overtake mahali pasipo stahili n.k, na kwa kiasi kidogo magari kuwa katika hali isiyo stahili kuwepo barabarani kabisa,na KUTOKUKIDHI VIWANGO VYA USALAMA ENDAPO INATOKEA AJALI ILI KUPUNGUZA MADHARA KWA ABIRIA.
    ninge shauri,ili kupambana na sehemu ya kwanza,ni kufanya LESENI ya udereve ipatikane kwa KUIENDEA SHULE YA NGUVU na kuisotea miaka kadhaa kama 3 hivi,hili litasababisha anayeipata kuthamini kikwelikweli na kutotaka kuipoteza, na kama POINT zitashuka kwa 50% basi alazimike kurudi shule ili kupata tena LESENI.UJANJA UJANJA WA RUSHWA UKOME KTK MAISHA YA WATU.
    pili nashauri viendeshwe vipindi katika redio na TV inavyo husisha watu walio athirika na matokeo ya ajali na kupoteza viungo,uwezo wa kazi,ndugu,nk katika ajali. hii itasaidia kliweka tatizo katika jamii kiuwazi zaidi ili watu wasiishie katika kusikia tukio la ajali tu bsi inaishia hapo.
    tatu madereva lazima wapimwe kisawa sawa ili kuhakikisha kuwa wapo katika hali inayoruhusu kupata leseni ya kuendesha gari,na kila siku kabla ya kuendesha magari ya abiria na mizigo,lazima pia wapimwe halizao kama zinaruhusu. natambua sio rahisi lakini hii inafaa ifanywe PILOT PROGRAM kama miaka 5 hivi tuone matokeo yake.madereva wengine wanakuwa na vifafa vya namna tofauti,sio lazima kuanguka chini,lakini akiwa katika mwendo kasi anaweza kupoteza fahamu sekunde 20 na hii inaweza kusababisha ajali mbaya sana tu!!!
    na wengine anaweza hata kuona illusions (maluweluwe)barabarani ambayo kiukweli hayapo na akasababisha ajali pia,hivyo swala la kupimwa dereva ni muhimu sana!!!
    kuwekwa speed governor ni muhimu pia,kupunguza mwendo kasi. katika nchi kama hapa pia wanatumia viffaa flani ambavyo vinapima pombe katika hewa anayopumua dereva,na ili kuwasha gari dereva anapaswa apumulie hewa katika kifaa ambacho ndicho kinawasha gari,kama knywa pombe gari aiwaki,na kila baada ya dk45 gari inazima na inabidi apumulie tena ili kuwasha. ukitumia pump ya hewa swichi haiwaki mana pumzi ya binadamu ina mchanganyiko tofauti na hewa ya pump.
    mwisho kuhusu uokoaji,nikweli kinahitajika kikosi maalum kiundwe na kiwe na vifaa,SUMATRA kwa kushirikiana na wadau tofauti watafute angalau HELIKOPTA moja kubwa yenye vifaa,na kikosi maalum cha madaktari wa upasuaji na resuscitation waweze kufikishwa eneo la tukio ilikupunguza idadi ya vifo kutokana na kuchelewa kufikishwa hospitali.ikitokea ajali wanapigiwa simu kwa hotline wanafika kwa haraka na kusaidia kuokoa maisha palepale.
    mungu ibariki tanzania.
    mdau

    ReplyDelete
  9. Mdau Che nakubaliana na wewe , ila nataka kuongezea kidogo ,nilikuwa nyumbani mwaka jana nilisafiri kutoka Dar kwenda Tabora kwa basi, kupitia Singida na Nzega , barabara ni nyembamba sana na zinajengwa kienyeju mno .Hata kabla barabara haijamalizika kujengwa kuna sehemu nyingine zimeshaanza kuharibika. Kuna kipande ambacho ni katikati ya ya Singida na Nzega kilikuwa kimemalizika lakini kuna sehemu ya kipande hicho katika milima ya sekenke kilikuwa kimeshaanza kudidimia . Ingawa sheria zikifatwa zitasaidia lakini serikale lazima iwajibike katika kutoa contracts za miradi ya barabara , na vilevile kuwe na mikakati ya kujenga barabara imara na za kisasa . Jinsi nilivyona nyumbani sisi sio masikini na tuna uwezo wa kuwa na barabara za kisasa kuunganisha mikoa yote. Tatizo ni rushwa , ubadhirifu , na mikataba duni .Kwa mfano nilichukua taxi kutoka southern sun kwenda mikocheni ambapo si zaidi ya maili 5 ilinichukua karibu masaa mawili . Sasa ukijumlisha wakati wangu , wakati wa taxi driver na mafuta yaliyotumika ukizidisha na mamia kama sio maelfu ya wakazi wengine ambao walipoteza wakati na mafuta , haya ni mamilion ya pesa kila siku yanapotea , ni kama vile tunachoma moto pesa na nguvu za watu.City planner lazima wawajibike, tokea miaka ya 80s hakuna pans zozote za kudhibiti msongamano wa magari, au hatuna planner ?. Kwa upande mwingine hawa wausika wangekuwa wanaplan a freeway (two way) kutoka Dar-Kigoma , Dar-Mbeya , Dar-Arusha,Dar-Mwanza, Dar-Mtwara. If this is done will not only cut the accidents ,but will reduce traveling time. And that will have rip o effect in business , hence job creation and all that good stuff . And in less than 10yrs you will have a lot of investors and the cost of the road construction will be paid for . Superior Infrastructure is the backbone of development , hence it is always a good investment .

    ReplyDelete
  10. ajali ya basi likua watu sita arizona tumetangaziwa hapa siku nzima na ni big deal.....Ila hata huku tulipo ajali zipo ila haziuwi kama huko.

    na huku fidia zipo..kwanza ukipata ajali uko kwenye mapasi au matrein yao hata kam hujaumia wanakupa hela haraka haraka ili usiwasue wakapata kazi ya kwnda mahakamani


    Bongo mpaka atolewe jino kiongozi mmoja ndio watashtuka na kuona wao sio foolproof

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...