



Hapa barabara ya Ali Hassan Mwinyi rodi, karibu kabisa na AAR kuna ajali ya gari imetokea muda mfupi uliopita.
Kuna hilo lori limebeba mapumba/ mashudu yale machicha ya kutengenezea nadhani bia. Sasa lori hilo likawa limefunguka mlango wa nyuma so mashudu yanamwagika tu, hivyo limepaki pembeni.
Basi kuna hii gari ndogo imekuja ikitokea mjini kuelekea Mwenge. Kumbe yale mashudu yamemwagika tokea kama mita mia hivi toka roli liliposimama na mashudu yenyewe yanateleza basi hiyo gari ndogo ile kuyakanyaga mashudu tu ikalewa ikaanza kuyumba yumba na hatimaye kuangukia mtaroni.
Kwenye gari hiyo ndugu kulikuwa na watu wawili, dereva hajaumia ila abiria (mdada) ndo ameumia na bahati nzuri madaktari wa AAR wakaja haraka na kutoa msaada na gari la wagonjwa (ambulance) likaja likambeba abiria aliyeumia.
Kusema ule ukweli kama mwenye hilo roli angeweka alama kwamba kuna tatizo (reflectors) nadhani hii ajali isingetokea.
Mashudu yanateleza sana. Si mchezo. Niwewahi kuona magari yanateleza vibaya sana maeneo ya nyerere road pale quality plaza. kibaya gari lenyewe lilikuwa limeshayeya. Inatakiwa kuwe na utaratibu maalum wa kuyabeba hayo maulevi yenu
ReplyDeletePia barabara sio salama kwa maana hakuna kizingiti cha kukuzuia usiingie kwenye mtaro kama gari ina loose control. Barabara inapoishia tu kuna mitaro pembeni na ukiyumba tu kidogo ndo hivyo unadumbukia mtaroni.
ReplyDeleteHivyo ingesaidia sana kama wajenzi wangeweka vizingiti kuzuia magari kuingia kwenye mitaro au kwenye kona kali
Mitaro ni very Hazard. Wizara ya Usafiri inatakiwa kutafuta alternatives ya hii mitaro mfano iwekewe vizibo juu.Hii itapunguza ajali za namna hii.Sijawahi kuona nchi nyingine duniani yenye mitaro.
ReplyDeleteMitaro inasadia sana. Magari mengi huishia mitaroni na kuepusha madhara kwa waenda kwa miguu na kusababisha ajali nyingine. Hebu fikiria lori lililo kata breki pale kibo kuteremkia Ubungo! Dereva akiliingiza mtaroni, mambo shwari kwa abiria wengine. Fikiria hata hiyo gari ndogo. Huenda dereva kaliwahisha mtaroni makusudi ili kuepusha madhara zaidi, mfano kugongana na gari linalokuja kutokea upande mwingine.
ReplyDeleteIkikutokea tena hali kama hii usikanyage breki. Attention iwe kwenye usukani, nyoosha gari.
ReplyDeletePamoja na melezo mazuri na lawama kwa dereva wa kilo lori, bado ni jukumu la kila dereva kuwa makini anapoendesha gari na hasa annapoona barabara haiko kama kawaida. Hii ni sehemu ya mafunzo ya udereva "defensive driving". Nawashauri madereva wote wawe makini zaidi wanapoendesha.
ReplyDeleteni kweli madereva wengi wa bongo hawana mafunzo yoyote ya udereva. kwa vile magari ni automatic basi kila mtu ni dereva. ndio maana ajali zinakua nyingi TZ. serikali iamke na iangalie upya utoaji wa leseni vinginevyo kila siku magari yatatumbukia kwenye mitaro..
ReplyDeleteHii ndiyo raha ya Bongo bwana. ukiona gari lako limepata pancha au kioo cha pembeni kimekaa vibaya n.k wewe huna haja ya kuhangaika, paki hata katikati ya barabara kwa raha zako rekebisha. Hakuna haja ya kuweka alama yoyote ya tahadhali kwa wengine. Ukimaliza ingia ndani ya gari lako, mwendo mdundo.
ReplyDeleteMdau Mbezi kijijini
mdau mbezi umenichekesha acha tu,
ReplyDeleteweee ndo unajua moviez za barabarani maana unakuwa kichaa tu kwakweli,,,,bado kwenye mataa ndo kasheshe jamani
poleni mliopata ajali na mdada apone mapema tu aisee!