ankal akiwa katika ofisi za Quality Machinery and Truck Commercial Ltd ya mji wa kusoma ambako alikutana wakurugenzi wake Mohamed Hijja (aliyekaa) na Athumani Mloka (kuume). Shoto ni mdau Gardol. hawa wadau ni mabingwa wa kusafirisha aina yoyote ya magari makubwa na matrekta na magreda na hata meli na treni popote duniani. wanapatikana katika email ya qmtcommercial@bconnect.com
na namba ya simu ya chap chap ni +441 1895 98614

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. wapi anuani yao ya Mtandao(internet)maana unaweza kuta hawa ni wasanii wa Ukerewe.Tupatie hiyo anuani kama ipo we are serious in supporting diaspora.

    ReplyDelete
  2. Ankal wadau wa mji wa kusoma hawajakutendea haki, Inakuwaje hawajakupelekea T_shirt yetu ya jamii kwa drai klina?
    hadi unavaa T-sheti hazieleeki bwana

    ReplyDelete
  3. wizi mtupu!!!

    Sasa mkuu unakagua ofisi, haina hata kiti? meza nyeupeeeeeeeeee, zaidi ya ka-laptop kamoja.

    Haya kamanda wa diaspora-2, wakilisha baba yake

    ReplyDelete
  4. Hii!!! umeshiba ile mbaya wangu

    ReplyDelete
  5. "NAMBA YA SIMU YA CHAP CHAP...." SI USEME TUU MICHUZI KUWA NI NAMBA YA MOBILE. OFISI ZA MKONONI!

    Mzozaji.

    ReplyDelete
  6. haya bwana mabingwa hawana hata web site?wanatoa cm ya chap chap na email?

    ReplyDelete
  7. michuzi mkuu mheshimiwa mbona unatuchengua siku hizi zamani katika blog yako picha kibao sasa hivi picha za jana hata huzioni unaziondoa kwa nini watu tunataka kusoma issue za dispra uliyokwenda huku ukerewa leo hii natafuta hata siioni mkuu vipi tena unafuta futa picha haraka na unaweka zile unazozitaka na ziko long time hizo unazozitaka..

    acha hizo mkuu watu tunataka kuona picha zote ulizoposti tuzisome na kusitolea comment

    ReplyDelete
  8. we mdau uliyesema hawana website usidhani kutoweka website hapo ndo hawana. Usilolijua usiku wa giza ukitaka jua website yao nenda kwenye webpage ya michuzi juu kabisa utaona adverts yapili ni yao pamoja na maelezo imeandikwa reading na full address usione kila mtu tapeli kabebe box we acha wenye vijitambi vyao waketi.

    ReplyDelete
  9. PETER NALITOLELAMarch 31, 2010

    MIMI NAWASHANGAA WATANZANIA SANA HASA WALE AMBAO WAHASOMA CHUO KIKUU CHA MUZUMBE UNIVESITY CHA KULE MOLOGOLO. HAWA JAMAA CHOKA MBAYA, UFISI YENYEWE HAKUNA KITI. BWANA MSITUZINGUE SANA, MIMI NDO MIMEMALIZA MASTAZ YANGU KULE OFKODI YA KULE KWA US BULOGA NA MUTU HAWEZI KUDIGANYANYA UTAFIKIRI MIMI NI MTOTO. HAWA NI WASANNII WANAOTAFUTA NAULI YA KURUDI BONGO HUKU WANATUDANGA'YA HETI MAJASIRIMALI. MAJASIRIMALI MAKALIO YANGU? WABEBE BOXI KWA AMANI. MIMI NARUDI MUZUMBE KULA NDONZOZZZZ ZA PHD, YA UCHUMI ILI NABII ASILETE ZAKE ZA KUNIZINGUA HETI SIJUI UCHUMI

    ReplyDelete
  10. Munaodai website wacheni ushamba.

    Warren Buffet tajiri nambari 2 duniani hana hata computer kwenye meza yake na anafanya biashara.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  11. ofici zingine zinatishaa kaa za jela vile.hamna simu ya mezani ,printer,scanner na photocopy fax nk.laptop haina hata ile waya lesi modem hapo neti hinhaa.hii hapa itakua ofici bubu tuuu. kichwa changu cha scania kitafika kweli bongo africa au ndo yale yale ya bandarini dar

    mdau cardiffu kwa bibi zabbeti

    ReplyDelete
  12. Ofisi ya laptop

    ReplyDelete
  13. mboga saba sema naona umekaa tu na laptop nini punguza tumbo hilo mabaga hayo

    ReplyDelete
  14. Baba UbayaMarch 31, 2010

    watz umaskini ushatimua netiweki kinoma ktk vichwa vya wengi.hao jamaa wameamua kufanya shughuli zao kihalali lkn wengi roho zinawauma na kuanza kutoa kashfa ba kasoro kibao.
    hata hao mabilionea walianza mdogo mdogo na baadae wakafika walipo.kwanza karne ye2 ya sasa hata ukiwa na cell phone inatosha kufanya biashara zako na sio mpaka uwe na mazagazaga yote yaliyotajwa.pia kuna All-in-One(Printer,Scanner,Copier & Fax) ambayo haihitaji nafasi kubwa.
    Wadau wa Mji wa Kusoma endelezeni libeneke lenu and Jah Bless u all.
    some peeps need 2 grow up!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  15. We anon wa 01.47pm, unasema jambo usilolijua nisawa na usiku wa giza...mbona unajisema mwenyewe. Swift freights uk ltd ni tofauti na hawa jamaa,hata addresses nitofauti moja london nyingine mji wa kusoma. swift niya Abuu Faraji ambaye alikuwa mwenyekiti wa Tz uk.
    Kama una-advertise biashara website ni muhimu kwenye tangazo kuliko email.Kwasababu Website inakuwa na email.

    ReplyDelete
  16. Mswahili ni mswahili tu, hata azaliwe ulaya WAZIMU MTUPU!!!!!badala ya kutoa hoja za maana, mnamsagia mtu na afya yake mkomeni,yuko ktk kujitangaza kibiashara.

    ReplyDelete
  17. wewe anon wa Wed Mar 31, 08:12:00 PM ni walimu wako wangapi wamepata kichaa wakijaribu kukuelimisha wewe? hebu tazama hapo juu ya hilo tangazo la swift kuna tangazo gani? au labda huoni vizuri dodosa basi "hillview family company"

    ReplyDelete
  18. Kaka zangu Mwenyezi Mungu azidi kuwapa nguvu zaidi za kujiendeleza, tatizo wabongo mnapenda Watusi wanaoiba sio wanaohangainga na jasho Lao km jaws kaka zangu wanaojituma wenyewe ,inshallah maneno ya wakosaji ,wabongo mmezoea wale majambazi wa epa km wakina liumba na wenjine wote walioiba kuingusha nchi. We will alys support u brothers,hija,mloka,gardo.office itakuwa juu tu kwa uwezo wa mola. Office ya abu faraji inahusu nini na hii kila Mtu ana maisha Yake na anafagiliwa ma watu wake.brothers well done. Love sister jade pinker

    ReplyDelete
  19. Hapo Salamander

    ReplyDelete
  20. mimi siyo mboga saba nitatoa hiyo picha yangu

    ReplyDelete
  21. Wadau nijuze, mboga saba maana yake nini?

    ReplyDelete
  22. halo halo Anon 12.25 umenikuna maana umempashua sawa sawa huyo Anon 12 kwakutojua kusoma wala kufungua macho yake sawasawa halooooo nilitaka nimpeshua yake lakini umemaliza big up tuko pamoja wenye wivu wajinyonge. Yeye kaona tangazo moja tu la London la Reading hajaona.

    Mdau mpenda maendeleo ya watu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...