madansa na wanamuziki wa bendi ya walemavu ya TUNAWEZA wakitumbuiza leo kwenye bonanza la michezo na muziki la kila jumapili viwanja vya leaders club jijini Dar. habari zinasema bendi hii sasa itakuwa ikitumbuiza hapo kila jumapili pamoja na Twanga Pepeta
Bob Mazongela, kiongozi wa bendi ya TUNAWEZA akikung'uta gitaa la bezi
tumba zinapigwa na huyu dada
viongozi na wanamuziki wa bendi ya walemavu ya TUNAWEZA wakiwa na mlezi wao Asha Baraka wa Twanga Pepeta. Bendi hii inafadhiliwa na mchezaji wa zamani wa Simba SC Isihaka Kibene (wa pili shoto nyuma) ambaye ni Rais wa bendi na wa kwanza ndiye Mkurugenzi wake.video ya onesho la TUNAWEZA inaandaliwa. kaa chonjo upate masebene ya nguvu


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...