Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akiweka shada la maua juu ya kaburi la Balozi Christopher Ngaiza, aliyekuwa mdhamini wa chama hicho wakati wa mazishi yake yaliyofanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Mbale wilayani Muleba, Kagera wikiendi hii.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akitoa salamu kwa niaba ya chama hicho, wakati wa mazishi ya aliyekuwa mdhamini wa chama hicho, marehemu Balozi Christopher Ngaiza, yaliyofanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Mbale wilayani Muleba mkoani Kagera wikiendi hii. Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Grace Kiwelu, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mmoja wa wadhamini wa chama hicho, maehemu Balozi Christopher Ngaiza, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Mbale wilayani Muleba mkoni Kagera wikiendi hii.
Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki, wakihusha kaburini jeneza lenye mwili wa marehemu Balozi Christopher Ngaiza, ambaye alikuwa mdhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakati wa mazishi yake yaliyofanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Mbale wilayani Muleba, Kagera wikiendi hii.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. RIP, na pole kwa wahusika wote. Mbona siwaoni viongozi wa serikali au kwa vile aliihama CCM?. Hapo inaonyesha jisnsi viongozi wa TZ walivyo na roho mbaya, asingehama CCM wangejazana kama nini. Tuthamini michango ya mtanzania yeyoyo hata kama angekuwa na mtazomo tofauti wa kisiasa na seriksli iliyopo madarakani. Mchango wa Balozi ulikuwa mkubwa kwa taifa letu.

    ReplyDelete
  2. Pat-magazetiMarch 29, 2010

    Ninaunga mkono kwa mtoa mawazo ya juu. Hawa jamani ni First generation ya viongozi wetu wachache sana walikuwa wamelika sana na waliobaki Tanzania. Sasa huyu ni generation ya mzee wangu ambayo serikali yetu imewasahau kabisa. Wazee walioelimisha second generation ya hakina warioba na Nyanganyi...sasa CCM wangetuma Kiongozi toka serikalini kuwakilisha kwa sababu Oscar, Bomani, Nhigula, Chagula, Magombe, you name those were first Diplomats who represented our baada ya uhuru. Sasa kama Marehemu Oscar Ngaiza alifanya makosa and paid the price, mbona hawa wapumbavu wameiba over $100 millions bado wako kwenye chama. Serikali bado inawaabudu.....CCM acheni unafiki na kutokuwa na upanufu wa mawazo ya kibinadamu. Marehemu alimshauri hata baba wa taifa....Butiku huko wapi jamani...Tanzania tunaelekea kubaya sana na tumejenga tabia ya kusahau wenzetu mliofanya nao kazi katika ngazi za juu. Oscar, Peter, na mama ngaiza poleni sana.

    ReplyDelete
  3. kweli hii haikukaa vizuri hata kidogo, umoja wa kitaifa ni jambo la msingi mno, siasa za chuki na uhasama katu haziwezi kujenga nchi,Mh Rais Kikwete hii haikukaa vizur hata kidogo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...