Na Ripota wetu, Kigoma.
Ankal niko Kigoma kama ulivyonituma, na mambo huku ni pouwa tu kwani mvua zinanyesha na tunatarajia mavuno. Upande wa shoto kwenye hilo la mvua wadau wanapata shida sana kwani ardhi ya huku ni utelezi sana na miundombinu ni ya kusuasua kwa maeneo mengi.
Kimsingi serikali inajitahidi sana lakini aina ya udongo wa huku hata kama barabara ikitengenezwa vizuri vipi, kama siyo lami basi mvua kidogo tu inaweza kusababisha watu wengi kushindwa kusafiri.
Katika hatua za kuondoa hayo matatizo, barabara ya kutoka Mwandiga hadi Manyovu (boda ya Burundi na TZ) inajengwa kwa kiwango cha lami na inakaribia au imefikia asilimia 50.
Barabara nyingine nayo inaendelera kutoka maeneo hayo ya Mwandiga kwenda hadi Kidahwe ambapo barabara ya Kaulu inaachana na barabara ya Uvinza. Tunaomba serikali ijitahidi kukamilisha hata kufika Nyakanazi ili kurahisisha maisha japo kama sehemu nyingine.
Kibaya katika hilo la barabara ni kwamba hawa Wachina hawatengenezi barabara ndogo za pembeni “Diversion” na wadau wanapata shida sana huku kwani sehemu nyingi wanazojenga tope ni la kutumbukia na hata mara nyingine hata Land Cruisers zinakwama.
Sasa Hiace itakuwaje? Halafu wana kiburi na hawasaidii watu kukwamua magari yao japo makosa ni ya kwao. Sasa sijui hawa wasimamizi hawalioni hilo au ni vp?
Manyovu ni kilomita kama 60 tu lakini watu mara nyingine wanasafiri siku mbili bila kufika. Hivi mikataba ya wajenzi wa barabara haijumuishi diversion?
Kwa upande mwingine Kigoma ni sehemu nzuri sana kwani mambo ya vyakula ni muswano. Wakulima hawaumizi kichwa sana kwani hata kulima nyanya au kabeji si lazima ulime pembeni yam to.
bunge la tanzania 2035 baada YA KIZAZI CHA SITA , WABUNGE LAZIMA WAWEWE WAKUJITOLEA NA WENYE UWEZO KUJIKIMU. PESA ZOTE NI KWENYE MAENDELEO. UHAI WAKO NA UTANZANIA LAZIMA UPATE GAWIWO SAWA LA KIPATO CHA TAIFA. RAISI HAMNA MKUU WA SEREKALI WAZIRI MKUU.
ReplyDeleteKIGOMA MAWESE NI MENGI MNO KIASI YANAMWAGIKA HOVYO MPAKA UDONGO UNAKUWA RANGI YA MAWESE!
ReplyDeletekwani tatizo ni nini hapo? si wangejenga mafuraiova tu tatizo kwishrinaa! huu ni uvivu wa wazi kabisa wa kufikilia. wanawasababishia wananchi foreni ya bule kabisa. wamekaria politique tu, kazi kuilala kwi bunge tu wakati wananchi inabidi wasubili mpaka saa za mangaribi ili kupita kuibalabala.
ReplyDelete