NAIBU KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA , DK. ASHA-ROSE MIGIRO AKIFUNGUA MKUTANO WA 54 WA KAMISHENI YA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU HALI YA WANAWAKE, MKUTANO HUO PAMOJA NA MAMBO MENGINE UTAFANYA TATHIMINI YA UTEKELEZAJI WA TAMKO LA MKUTANO WA NNE WA WANAWAKE ULIOFANYIKA BEIJING MWAKA 1995. RASI WA MKUTANO HUO ALIKUWA MHE, GETRUDE MONGELA AMBAYE NAYE ANAHUDHURIA MKUTANO HUO.
SEHEMU YA WAJUMBE WANAOHUDHURIA MKUTANO WA 54 WA KAMISHENI YA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU HALI YA WANAWAKE. (PICHA NA TAARIFA KWA HISANI YA UBALOZI WA TANZANIA UMOJA WA MATAIFA


Ikiwa ni miaka kumi na tano sasa tangu kupitishwa kwa Tamko la Beijing kuhusu Hali ya Wanawake, imeleezwa kuwa pengo la usawa wa kijinsia kati ya mwanamke na mwanaume bado ni kubwa. Na kwamba hali hiyo ipo katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua mkutano wa 54 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake.

Ajenda kuu ya mkutano huo kwa mwaka huu, pamoja na mambo mengine, ni kufanya tathimini ya Tamko la mkutano wa nne wa Beijing na mpango wake wa utekelezaji. Mkutano uliofanyika mwaka 1995 rais wake walikuwa alikuwa Mhe, Getrude Mongela ambaye hivi sasa ni mbunge wa jimbo la Ukerewe ni mmoja ya washiriki wa mkutano huu.

Mkutano huo wa wiki mbili umeanza siku ya jumatatu na unafanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, na kuhudhuriwa na wanawake akiwamo makamu wa rais wa Ghambia ambaye ni mwanamke, mawaziri, wabunge, makatibu wakuu na makundi kutoka asasi zisizo za kiserikali.

Akitoa mfano, Migiro anaeleza kuwa bado idadi kubwa ya maskini ni wanawake kuliko wanaume, wasioujua kusoma au kuandika wengi ni wanawake kuliko wanaume, hata wanaofanya kazi katika mazingira magumu, kwa ujira mdogo na bila kinga au bima yoyote ni wanawake zaidi kuliko wanaume.

Kama hiyo haitoshi, Naibu Katibu Mkuu anabainisha kuwa hata mtizamo kuhusu masuala ya wanawake bado ni hasi ingawa kuna mwamko kidogo, na kwamba utekelezaji wa mambo mengi bado unamtizamo wa kibaguzi. Huku kukiwa na utofauti kati ya upitishwaji wa sheria na utekelezaji wa sheria hizo.

Anasema Migiro. “ Bado wanawake wengi ni maskini, wanaofanya kazi ngumu au za majumbani ni wanawake na watoto wakike , robo tatu ya wanawake hawajui kusoma wala kuandika na hali hii haijabalikia kwa zaidi ya miaka 20 sasa“.

Kuhusu nafasi ya uwakilishi katika vyombo vya kutunga na kupitisha sheria, Migiro anasema kasi yake si ya Kuridisha kwani hadi mwaka 2009 ni nchi 25 tu ambazo zimeweza kufikisha lengo la kuwa na asilimia 30 ya wabunge wanawake.

Kwa upande wa huduma za afya ya uzazi, Naibu Katibu Mkuu, anaeleza kwamba, bado ni eneo ambalo halijawa na nafuu yoyote, idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi bado ni kubwa. vifo ambavyo siyo tu havipashwi kutokea lakini pia vinaweza kuzuilika.

“ Kwa hiyo, wakati tunaona kuwa kuna dalili zuri za mafanikio mbalimbali kuhusu hali ya wanawake miaka 15 baada ya tamko la Beijing, ukweli ni kwamba bado hakuna mabadiliko ya kuridhisha na kujivunia.

Pamoja na mapungufu hayo, Naibu Katibu Mkuu ametumia fursha hiyo kuwapongeza na kuwashukuru wanawake, katika nafasi zao mbalimali kwa kazi kubwa wanaoifanya ya ubinifu wa kuzishinikisha na kuziwajibisha serikali zao zitekeleze sera, sheria na mipango inayolenga kuleta usawa na uwezeshwaji wa wanawake.

Akasema jitihada zao hizo zimeweza kulete mwamko na uelewa miongoni mwa viongozi wanawake kwa wanaume ya kuwa suala la usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wa mwanamke na mtoto wa kike si jambo la kupita na badala yake ni moja ya nguzo muhimu katika upatikanaji wa maendeleo endelevu, ukuaji wa uchumi, amani na usalama.

Akasema yeye na Katibu Mkuu Ban Ki Moon wamedhamiria kuhakikisha kwamba Umoja wa Mataifa unaweka mazingira bora yatakayoziwezesha serikali na asasi za kijamii kuhakikisha kuwa masuala ya usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake yanaingizwa katika Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs).




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ankal, mie nina mawazo tofauti kidogo na wakereketwa wa haki za wanawake, kwa maoni yangu nafikiri watu wote tunatakiwa kupinga kunyanyaswa kwa wanawake na vitendo vya kikatili dhidi yao, kama vile kubakwa, kutopelekwa shule n.k, hii mimi ninaiunga mkono, ila hapa ukiangalia agenda ya wazungu si kuwasaidia wanawake wa kiafrika, bali ni kutuletea tamaduni zao, kwani kwa kawaida ukitaka kumtawala mtu mfanye apende tamaduni zako, basi akakopi kila kitu toka kwako na atakuwa nyuma yako milele, hawa wazungu wanatuletea usawa ambao kwao umefeli kabisa, kwa mfano uingereza wastani wa ndoa zilizodumu mpaka kifo ni chini ya asilimia thelathini, wakati afrika hapo awali kabla ya kutuletea hizi tamaduni zao ndoa zilikuwa zinadumu mpaka kifo kwa zaidi ya asilimia tisini, sasa wewe mwenyewe tazama ndoa za siku hizi hapa afrika baada ya watu kuanza kufuata tamaduni za kimagharibi, ni aibu vijana wanaachana miezi sita tu ya ndoa, kwenye nyumba hajulikani nani ndio kiongozi, mwenye pesa au mdomo ndio anakuwa kiongozi, jamani tuwe makini, maisha si kuiga kila unachokiona bali ni kutafakari kila ufanyacho.
    Ahsante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...