Lile shindano la filamu la BBC World Service lilopewa jina la My World Competition, kesho ijumaa tarehe 19/03/2010 saa moja jioni kwa saa za Africa mashariki ndIo linafikia tamati kwa BBC World Service kutangaza mshindi wa shindano hilo kupitia online www.bbcworldservice.com/myworld
Shindano hilo liloshirikisha dunia nzima kwa watu kutuma filamu fupi za dakika mbili.

Ibrahim Matukuta anae iwakilisha Tanzania kwa filamu yake yenye jina la "Somewhere in Northern Tanzania" ameingia katika tano bora, na kuwa filamu pekee iliyochaguliwa kuwakilisha Bara la Afrika katika hizo tano bora ambazo mshindi atatangazwa na jopo la majaji wa tano wa filamu wanaoheshimika kutoka katika kila bara, yaani Afrika, Americas, Asia, Oceania, na Europe. Mmoja wapo wa jaji ni Cara Mertes Director, Sundance Institute Documentary Film Program. Jumla ya filamu 500 zilipokelewa katika shindano hilo. Majaji walichagua filamu moja bora kutoka katika kila bara ili ziingie tano bora.

Kwa habari zaidi angalia
www.bbcworldservice.com/myworld

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Naomba kusahihisha kidogo.Siyo hitma bali hatma au hatima.Tusiharibu lugha yetu adhimu tafadhali.

    ReplyDelete
  2. Du! hii kali ya mwaka, asante mdau wa kwanza kwa kuona mushkeli ktk tangazo hili muhimu, maana hata Bongo tumo ktk 5 bora.

    ReplyDelete
  3. Congratulations Ibrahim...Vipaji hivyo vya kukuzwa hivyo mnaona wizara ya elimu? ....hatujui umri wake au elimu yake lakini watu kama hawa ndio wakuongezewa scholarship waende wakasomee zaidi ili waweze kujatengeneza movie zinazoeleweka......


    Hongera muzee

    ReplyDelete
  4. Mbona umewatangazia watu muda tofauti? Naona wameandika wao kuwa africa itakua saa 18.15 ingawaje miye military hours sizimind lakini kwa haraka harak naona ni kama saa 6:15 pm...au nakosea?

    Huwa natoa 12 hours ili niweze kuelewa hizi saa
    18.15 - 12 = 6.15

    ReplyDelete
  5. Hongera kwa hatua uliyofikia, kwa kuitangaza Tanzania katika tasnia ya filamu huko duniani!

    Mdau US

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...