Ukitaka kuongea muziki wa dansi uliingiaje nchini ni muhimu kujua historia ya mji wa Tanga. Tanga ndipo muziki wa dansi ulipoingilia nchini. Wajerumani waliusambaratisha mji wa Tanga kwa mizinga kati mwaka 1888 na 89.
Na baada ya hapo kuujenga upya kwa kufuata mpangilio uliosababisha Tanga kuwa na mitaa maarufu kama barabara ya kwanza ya pili na kuendelea. Wajerumani walianzisha shule ya kwanza ya serikali Tanga 1892 na hapohapo wakanzisha bendi ya shule ya kwanza, pamoja na kuwa Wajerumani hawakutawala muda mrefu baada ya hapo lakini Waingereza waliiendeleza sana bendi hiyo iliyokuwa ikipiga aina mbalimbali za muziki wa kigeni.
Dansi ilianza kwanza kama klabu ambapo watu walialikana kuja kucheza aina mbalimbali za muziki wa kizungu mtindo maarufu unaojulikana kama ballroom dancing. Aina hizi za klabu zilianzia Mombasa na kuingia nchini kupitia Tanga na kisha kuletwa Dar Es Salaam na klab iliyokuwa maarufu Tanga iliyoitwa Tanga Young Comrades Club, klabu nyingine ilianzishwa ikaitwa New Generation Club ambayo ilianzisha matawi miji mbalimbali. Klabu hizi ndizo zilizozaa bendi za dansi.
Inaonekana Dar es Salaam ndio ilikuwa ya kwanza kuwa na bendi yake African Association Jazz Band, ambapo wanamuziki wengine waliihama na kuanzisha Dar Es Salaam Jazz Band, hiki kilikuwa kipindi kati ya miaka 1930 na 1940, kwenye 1950 kulikuwa na bendi maarufu Bagamoyo iliyoitwa Lucky Star jazz band ambayo ilikuwa na urafiki na Dar Jazz.
Haya na mengi mengine kuhusu muziki hapa nchini mtembelee mkongwe John Kitime wa Njenje kwanye Libeneke lake la nguvu
Huwezi kuongelea mziki wa Tanzania bila kumzungumzia Al Marhum Abbas bin Mzee wa kundi la EGYPTIAN musical club
ReplyDeletehebu nionyeshe wapi utapata nyimbo kama UNANUNIA NINI, HARUSI, YATIMA na kadhaalika?
sie wengine tushaacha hata kusikiliza the so called radio stations zinazoibuka kama uyoga na zilizojaa watangazaji wasojua Kiswahili..eti utasikia mtangazaji anasema waLIKUJAGA, wakaENDAGA na kadhalika!
hamna kitu solution ni nie wenye mitandao kuendelea kuwaenzi wanamuziki wetu pamoja na malenga wetu
Ina maana huwezi kudansi(kudensi) reggae ikipigwa, huwezi kudansi(kudensi) rap ikipigwa,ndombolo ikipigwa nk? Wanaposema ni mziki wa dansi/densi wanamaanisha nini?Navyojua aina nyingi za miziki zinadensika. Hata ile miziki ya kitaliano(opera) au ya kichina huwa inachezwa.Naomba mnieleweshe.
ReplyDeleteAnkal, hii picha imenikumbusha mbali sana enzi ya ujana wangu. Hata hivyo imenisikitisha sana kwa kuwa ndugu yetu Raphael alifariki dunia miaka miwili au mitatu ilyopita. Tunamwomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amin.
ReplyDeleteSABUNI SIKU MOJA MIAKA YA SABINI ALIKUNJWA SHATI AKAPIGWA VICHWA NA JAMAA MMOJA JANGWANI,NAKUMBUKA JAMAA ALIKUWA ANAITWA MBADEMBADE,KISA SABUNI ALIKUJA KUMFUATA MAREHEMU MARIJANI RAJABU ILI AKAJIUNGE NA BENDI YA STC KAMA MUIMBAJI,NA MARIJANI ALIKUWA NI KIPA TEGEMEO WA KAHE NA WALIKUWA NA MECHI NGUMU NA SIMBA KOMBE UWANJANI NA WALISHA TOKA SARE MARA MBILI KAHE ILIKUA OPOSITE NA DAR JAZZ KARIBU NA CLUB YA SIMBA,SABUNI JOHN,MGOGO,JAMES MKUMBO,DAVID MUSA,ROGES MRINGO,AKINA MUHUTO NA WENGIE WENGI WAMESAHALIKA KATIKA HISTORIA YA MUZIKI WA DANSI HONGERA KITIME KWA KUWEKA KUMBUKUMBU.
ReplyDelete