INA MUONYESHA MSAIDIZI WA BALOZI WA JAPAN HAPA NCHINI AMBAYE PIA NI MTAALAM WA MASWALA YA UCHUMI BW. YOSHIYASU MIZUNO AKISIKILIZA KWA MAKINI ALIPOFIKA OFISI ZA TANZANIA INDUSTRIAL RESEARCH DEVELOPMENT ORGANIZATION(TIRDO) MSASANI JIJINI DAR KUHUSU JENERETA AMBALO LINATUMIA HEWA KUZALISHIA UMEME.PEMBENI YAKE NI ENGINEER AU MVUMBUZI WA JENERATA HILO CAPT MSTAAFU ATHUMAN MSEKENI
DK. MMASI ANTHONY AKISISITIZA NA KUWEKA MKAZO WA JAMBO HILO
> KWA WADAU WALIOFIKA KUJIONEA JENERETA HILO HUKU MVUMBUZI WAKE KEPTENI MSTAAFU ATHUMANI MSEKENI AKISIKILIZA.

DIRECTOR WA INTERNATIONAL TECHNICIAN CONSULTANCY AND
DESIGN BW. EMMANUEL MWAMPISHI AKIWAFAFANULIA WAGENI JINSI JENERETA HILO LINALOTUMIA HEWA KUFUA UMEME KWA AJILI YA MATUMIZI MBALIMBALI AMBALO LITAWASAIDIA WATANZANIA WENGI KUJIKWAMUA KIUCHUMI NA KUEPUKA NA TATIZO LA GIZA. NA KUWASIHI WADAU WENYE MAPENZI MEMA WASAIDIE KUTOA MICHANGO YA HALI NA MALI KUENDELEZA UVUMBUZI HUO.
JENERETA LITUMIALO NGUVU ZA HEWA KUZALISHA UMEME
MTAALAMU AKIIKAGUA JENERETA HIYO
JENERETA LENYEWE
PICHA NA HABARI NA EMMANUEL JOSEPH







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. HONGERA SANA CAPTAIN MSTAAFU, NA WEWE UMEINGIA KATIKA HISTORIA YA WAVUMBUZI.
    WADAU, HUTUTAKIWI KUKATA TAMAA MAPEMA. TUJIFUNZE KWA CAPTAIN MSTAAFU, PAMOJA NA UZEE WAKE HATIMAYE AMEFIKIA NDOTO YAKE.
    NEEMA-DAR

    ReplyDelete
  2. Ha ha haaaa mjapo kaziba pua! Hilo jenereta lilikuwa linatoa hewa mkaa kwa wingi au?

    ReplyDelete
  3. Nimecheka kwa sababu imenichekesha!

    ReplyDelete
  4. Mdau asaidiwe kwanza kutengeneza na kuandikisha PATENT ya hiyo jenereta. Wadau wengine wanaweza kuiangalia teknologia yake na kuiiga fastafasta na kumuacha jamaa hana kitu... Wazo langu ni kwamba jamaa asaidiwe ili afanikishe njozi hii yenye manufaa kwa jamii nzima...upepo wa
    Mungu usiouzwa.

    ReplyDelete
  5. kimbuma kutoka kiunganiMarch 14, 2010

    hewa inazalisha umeme? hewa gani... hydrogen?;

    ReplyDelete
  6. TUWEKANE SAWA HAPA, INA MAANA HALITUMII KITU CHOCHOTE KILE KULIWASHA? NINA MAANA HALITUMII HATA KIDUCU KITU KAMA UMEME, MAFUTA YA AINA YOYOTE ILE. NI UPEPO TU? EBU TUPEANE MAELEZO YA KUTOSHA. NA LINA UWEZO GANI? LINAWEZA KU-POWER NYUMBA NZIMA NA VITU VYOTE VIKAFANYA KAZI I MEAN FRIJI, TAA, TV, KUPIKIA, PASI, HOOVERS. YAANI MASHINE ZOTE ZINAZOHITAJI UMEME ZITUMIKAZO MAJUMBANI ZINAWEZA KUWA POWERED NI HILO JENERETA?

    ReplyDelete
  7. what is needed here is to turn this thing into commercial production, wrap it up into final appealing product. Some needs to pour money into this project, and quickly obtain the partent.

    ReplyDelete
  8. Jamaa anayusanifu tu. Hakuna chakufagilia wala nn. Anaongalia jinsi gani ambavyo tuko nyuma

    ReplyDelete
  9. MICHUZI ACHA UTANI... UVUMBUZI MAANA YAKE NI KUBUNI KITU/TEKNOLOJIA MPYA AMBAYO HAIPO/HAIJATENGENEZWA. HAPA TUNAONA GENERATOR LINALOTUMIA UPEPO KUFUA UMEME, SASA SIONI TOFAUTI YEYOTE NA WINDMILL AMBAZO EUROPE ZIKO TOKA MIAKA YA ZAMANI SANA.. HALAFU HAMJAONYESHA PICHA YA KIFAA KINACHOZUNGUSHWA NA HUO UPEPO. HII HAINA TOFAUTI KABISA NA KATAUPEPO AMBAZO NYINGI KWA SASA ZIMEKUFA KATIKA MIKOA YA SINGIDA, DODOMA INGAWA ZENYEWE ZILIKUWA MECHANICAL KWA AJILI YA KUPUMP MAJI TOKA VISIMANI. NINACHOONA HAPA NI MATUMIZI YA VIFAA DUNI KUTENGENEZA KITU KILICHOKWISHA TENGENEZWA NA WENGINE, WALA SIO UVUMBUZI. NINA HAKIKA LEO UKIENDA CHINA YAKO MENGI SANA MAJENERATOR YA NAMNA HIYO KWA BEI RAHISI.

    Mzozaji

    ReplyDelete
  10. Huyu mzeee anastaili pongezi na kwa vile nawajua wajapan walivyo hawatamuacha hivyo hivyo iko kichwa cha maaana

    ReplyDelete
  11. Real "ignorance is a bliss".

    Sasa nyinyi unaojifanya mnajua "engineering design" kweli mmekwenda shule au mnaharisha midomoni mwenu?
    Mmeshaanza kupondea na viswali vyenu vya kejeli kama vile mnajua mnachosema!

    Hongera, designer, retired captain Athman kwa kazi yako nategemea utapata ushirikiano unastahili ili hiki kitu kiwe commercial success.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  12. Michuzi sina wasiwasi na uvumbuzi wa mzee wetu huyo,kinachonitia shaka ni kuwa ni upepo au hewa ya namna fulani inahitajika kama nishati kwa ajili ya kuliendesha hilo jenereta? na kama ni upepo kweli basi tumefanikiwa hatua moja ya kuelekea nchi ya ahadi,ila jaribu kulifanyia utafiti,linatumia nishati gani? nguvu yake?teknolojia yote kwa ujumla na zaidi jaribu kumuhoji mzee wetu alipata wapi wazo na inspiration ya kuvumbua mashine ya namna hiyo,pia mwahisheni pale BRELA kabla wajanja hawajala juu yake,nampongeza kwa hatua aliyofikia japo wengine wanaiona ya kishamba wenzetu walitokea huku huku..kama iko poa aionyeshe kwa wataalmu wa dra tech na chuo kikuu tafadhali.giza chungu hasa ukiwa kijijini..na ndipo tulipotoka!

    ReplyDelete
  13. Mafisadi mpo ! Hapo mkiinject vijisenti vyenu (1 million USD)kwenye projects kama hizi itakuwa ni kwa faida ya vizazi vingi sana vya watoto wetu, maana zitasaidia katika kuzalisha ajira nyingi na pia mtakuwa mmerudisha angalau vijisenti vichache kati ya hela mlizonazo kwenye jamii. Ukiichunguza vizuri hii jenereta imetengenezwa kwa scrapers tu, sidhani kama imetumia zaidi ya shilingi laki moja mpaka hapo ilipo. Kazi nzuri Captain.

    ReplyDelete
  14. kwa kuinangalia tu naona hiyo ni full kulipuka anytime...makelele je mbona hayajasemwa...anyway tumpe support auze walau mbili tatu maana tanesco tangu walaaniwe na kakobe umeme hauwaki sikuhizi

    ReplyDelete
  15. kwa mujibu wa picha naona neno AIR COMPRESSED ENGINE kwa maana hiyo mashine inahitaji mtungi wa hewa iliyogandamizwa ama kushindiliwa kwa ajili ya kuleta mzunguko wa hiyo ALTERNATOR ya gari ambayo itazalisha umeme. kwa nijuavyo mimi umeme utakao zalishwa hapo utakuwa wa VOLT 12. Kwa hiyo huyo "Mvumbuzi" amechukua teknolojia inayotumika kwenye magari ya kuchajia betri la gari ili kuzalisha umeme wa kuwashia taa na mambo mengine kwenye gari na kuweka mtungi wa hewa.

    ReplyDelete
  16. It is sad kuona watanzania wanapondea watanzania wenzao. I bet you angekuwa mzungu aaah msingetoa comment zenu za kejeli. Well, mzee anaitaji kuwa na patent/copy right ya ujuzi wake and investors ili kuweza kutengeneza generator zilizo na std ya kueleweka.

    Hongera mzee!!!!!

    ReplyDelete
  17. Hapo Mjepu ana wachekelea tu. Hata Mtoto akienda haja inabidi umpongeze.
    Vitu kama hivi ndivyo vinfanya serekali inazidi kulala usingizi mzito na nchi kuendelea kuwa masikini. Kampuni kama Tanesco zinatakiwa zije na ufumbuzi wa suala la umeme unaoeleweka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...