Meya wa Jiji la Dar Mstahiki Adam Kimbisa akimkabidhi JK zawadi ya jezi namba tisa ya Timu ya Real Madrid ya Hispania inayovaliwa na nyota wa timu hiyo Ronaldo ikulu jijini Dar es Salaam leo kwa kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kukuza mchezo wa soka nchini.
Msanii Paul Ndembo ambaye amejikita katika uchoraji wa sura za watu mbalimbali hususan viongozi akimkabidhi JK picha aliyoichora wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijinji Dar leo
Msanii Paul Ndembo akimuonesha JK moja ya picha alizochora za nyakati mbalimbali za Uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Picha hiyo imewekwa katika ukuta sehemu ya mapokezi ikulu jijini Dar. Msanii Paul Ndembo ni Mhitimu katika kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda Mwaka 1970 na ni pia mchoraji mahiri wa stempu za barua Tanzania.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. Halafu tunadai kuwa tuko huru, wakati hata Rais wa nchi anathamini wa ughaibuni kuliko wetu! Nilitegemea kuwa angepewa jezi ya Haruna Moshi, Nizar Kahfan au Henry Joseph! Hakika, bado tuna safari ndeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeefu!

    ReplyDelete
  2. Katika kujipendekeza unaweza kufanya mambo yasiyoeleweka.

    ReplyDelete
  3. viongozi wetu kweli kiboko.

    sasa kwanini usingempa zawadi ya jezi ya simba kwa vile wao ni mabingwa wa soka nchini kwetu yenye jina lake nyuma?

    au kama jezi ya simba itawakera washabiki wa yanga kwa vile tumejaa majungu,kwanini usingempa jezi ya timu ya taifa yetu yenye jina lake nyuma?


    unatoa zawadi kwa mchango wake kwenye michezo,unampa jezi ya ronaldo,yeye kamsaidia nini ronaldo au soka la nje? tujaribu kujivunia chetu saa nyingine ndugu zangu.

    ReplyDelete
  4. sina mengi yakusema kwa kifupi ni hakuna lisilowezekana bongo

    ReplyDelete
  5. HUWA SIINGII KUANGALIA MAONI YA WATU, LAKINI BAADA YAKUONA HIYO ZAWADI YA JEZI YA MTU AMBAE HANA UHUSIANO WOWOTE NA JAMII YETU!!!....KWAKWELI SINA LAKUSEMA!!...YAANI HATA NINGEKUA MIMI NDO RAHISI NINGEMKANUSHA PALE PALE NA UHAKIKA ANGEKUA MWALIMU(MAREHEMU BABA WA TAIFA) ASINGE LAZA DAMU.

    ReplyDelete
  6. nlivyoiona jezi ya ronaldo nlifikiri jamaa(ronny)yuko bongo baada ya kizunguzungu cha Lyon,baada ya kusoma habari yenyewe jinsi isivyohusiana na ronaldo,I was nearly choked na lunch langu la usiku!

    ReplyDelete
  7. Naungana na wadau waliotangulia, angalau me sio mchabiki wa Simba, lakini Rais angefaa apewe jezi ya mchzaji yoyote wa Simba kuonyesha kuthamini mchango wao wa soka kwa mwaka huu. Na pia ku-promoti vijana wetu. Tanzania na Ronaldo wapi na wapi?

    ReplyDelete
  8. Na yeye angetoa ya Hashim pale (licha ya kwamba ushindi hajatuletea) au yule Martina Chambiri jamaa angegundua kwamba licha ya kwamba nchi ni sio tajiri lakini tunajivuna kivyetu vyetu

    ReplyDelete
  9. ehh kweli hiki ni kiwewe cha sifa lol huku majuu mwananchi akampe raisi wao wa nchi tshirt imeandikwa kaseja haitakaa itokee milele ila wewe mwenzetu ununda unakuzonga imebidi nicheke umelala na zawadi yako unaomba kukuche ukampe raisi zawadi !!! zwadi ni zawadi ila hii ni zawadi tata

    ReplyDelete
  10. KIMBISA UMENIACHA HOI KABISA HAPA, HATA MTOTO WA CHEKECHEA ANAWEZA KULIONA HILI, HIVI HAKUNA SHIRT YA TEAM YA MAJIMAJI UKAMPA RAIS WETU MPENDWA MPAKA UKACHUKUWE YA REAL MADRID, YA RONALDO MRENO! KWELI ELIMU NI MALI. I HAVE SEEN THIS TO VODCOM TOO ON THIS VERY BLOG, I PUT MY COMMENT THERE TOO, IT IS EXTREMELY NO BRAIN TO DO JUST SUCH THAT! WE HAVE OUR OWN TEAMS WITH OUR OWN SHIRTS, HOW ON EARTH WE ARE DOING THIS THINGS, UNBELIEVABLE, EXTREMELY BAD, SENDING WRONG MESSAGES TO OUR YOUNG GENERATION, TO OUR BELOVED KIDS.

    ReplyDelete
  11. jamani kazi za kupepea nazo ni kazi, mwacheni kimbisa wa watu anajua analolifanya. sie tunakalia madongo, mwenzetu jina lake litatajwa la kwanza katika uteuzi ujao.

    ReplyDelete
  12. siamini macho yangu, yaani roho imeniuma karibia itoke, halafu muangalie huyo Rais alivyofurahia, hata sielewi watanzania tumepatwa na nini.
    siku hizi watu hawataki tena kuongea kiswahili katika kuwakilisha nchi yao, vit vinauzwa kwa kutumia dola na hata kumbe Rais anachekelea kupewa jezi ya Real Madrid. MAKUBWA

    ReplyDelete
  13. Naona kama meya amempiga rais dongo kiaina maana tuliahidiwa Real Madrid wangekuja kucheza neshno hapo ila uchaguzi unakaribia hatujawaona Real Madrid. Kihalali rais alipaswa kupewa jezi ya Taifa stars yenye jina lake au kama ni jina la mchezaji basi mchezaji aliyestaafu ambaye hawezi kuleta kashfa baada ya kumaliza muda wake kuchezea timu ya taifa mfano Mecky Maxime au Peter Tino.

    ReplyDelete
  14. mtoaji + mpokeaji = guiness world records

    ReplyDelete
  15. mrs drogbaMarch 17, 2010

    kumbe Ronaldo ni mtanzania! nimefurahi kweli nilikua nazania ni wa ulaya kumbe ni mmatumbi mwenzetu! hongera sana kaka yetu ronado!

    ReplyDelete
  16. We have long way to go, that is all that I can say !

    ReplyDelete
  17. Jamani hiyo ni zawadi imetolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Timu yoote ya wataalamu hapo Ikulu wakaina iko OK na washauri apewe Rais. Kwa kweli hii ni kudhalilisha Ofis kubwa kama hiyo...jamani lets be serious.....yaani bora zawadi yenye uhusiano hata na Afrika basi kama hatuipendi nchi yetu. hata timu yeyote ya Afrika inayocheza FIFA 2010 basi ingeleta maana...lakini hii jezi mimi sielewi something is wrong somewhere....Ankal next time habari kama hizi weka kapuni zinatuletea huzuni sana.

    ReplyDelete
  18. Wadau kuna mtu ananamba ya Adam Kimbisa.. kweli ningependa kumuuliza ni nani alimpatia hiyo tshirt, hata kama mheshimiwa ni shabiki wa real madrid basi si amepongezwa kitaifa.. kwanini basi tusijivunie team zetu au wachezaje wetu lukuki.okay kama nisipoipata nitamuuliza mheshimiwa mwenyewe.si twajua kampeni zi karibu. nikimkosa hapo basi mpaka nipate nauli..

    ReplyDelete
  19. KWAKWELI SINA LA KUONGEZA - YOOTE NILIYOKUWA NAFIKIRIA MUMEYASEMA HAPO JUU NA NINA UHAKIKA MENGINE YANAKUJA..

    ReplyDelete
  20. Jamani Rais angepewa jezi ya nahodha wa timu yetu ya Taifa na si Ronaldo ambaye umaarufu wake hautusaidii chochote, hapo mmechemka kwa kweli Watanzania tupende vya kwetu jamani

    ReplyDelete
  21. Du nafikiri rais hakupewa muda wa kufikiria vizuri. maana nae wamekuwa wanambambikia tu vitu. lakini Kimbisa umeonyesha ni jinsi gani usivyotumia akili.Jezi ya Real Madrid. au hujui kwamba madrid ni jiji huko hispania na wana meya wao. Halafu wewe ni meya wa Dar. hizi ni akili au matope, wewe una timu ngapi hapa kwenye jiji lako? mpe hata ya Twiga Stars. Heeeee jamani nimechoka kabisa. Nahisi hata tukiwa tunasali Mungu anajiuliza SASA HII MIJITU NIISAIDIAJE WAKATI HAINA AKILI HATA KIDOGO.

    MICHUZI EHH MAKE SURE RAIS NA KIMBISA WAKE WANASOMA HIZI COMMENTS.

    ReplyDelete
  22. Kingwendu Jr.March 17, 2010

    Siku zote nawaambia tuna Safari ndeeefu ya kwenda sisi jamani, hayo mnayosema kuwa tz inapiga maendeleo ni viinimacho na mnatathmini msiyoyajua, jamani hao viongozi wetu ni kama vile hawakwenda shule!!!!!

    ReplyDelete
  23. Kwanini jezi ya Ronaldo badala ya jezi ya simba , yanga, n.k. And it is sad kuona kwamba viongozi wenyewe mtoaji na mpokeaji wako happy tu na kukenua meno yao kwenye picha. Well, ni sana na twanga pepeta wanavyovaaga tops zenye bendera ya jamaica!!!! huwaga sielewi.

    Tanzania wake up!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  24. ina maana raisi yuko kwenye facebook?? babda ni rafiki mkubwa wa ronaldo jamaa amegundua hilo akaona alete na zawadi ya tshirt kabisaa

    ReplyDelete
  25. KAMA MIMI NINGEKUWA KIKWETE NINGEIKATAA HIYO JENS HAPO HAPO.

    ReplyDelete
  26. Kikwete naye bwana!!

    Kwani nini hakumtolea uvivu Kimbisa kama alivyofanya kwa yule mkurugenzi wa halmashauri ya Loliondo ambaye alikwenda kupokea gari ya halmashauri nyingine?

    Hapa angemuulize, bwana hii jens ni ya timu gani? je huyu mchezaji ni wa Tanzania? Sasa kukuza kwangu mchezo wa soka hapa nchini kuna uhusiona gani na huyu mchezaji?

    Sasa hii zawadi naikataa.

    Lakini cha kuchangaza jamaa amepokea tena kwa furaha kubwa.

    ReplyDelete
  27. Tukumbuke miezi michache baada ya kuchaguliwa kuwa rais JK alienda Madrid anataka timu hiyo ije nchini kucheza uwanja mpya.

    Sasa hatawezi kujua mambo yaliotokea. Labda Madrid kupitia kwa JK inatoa mchango wa kuinua soka nchini. Mshahara wa Maximo na hela zingine za kuendesha soka zinaweza zikawa zinatoka Madrid.

    Kwa hiyo sisi yetu macho tu basi, undani tunaweza tusijue

    ReplyDelete
  28. Nazani Michuzi ndo hajafafanua vyema hii habari...Hiyo jezi imetolewa na timu ya Real Madrid officially kama zawadi kwa rais wetu,ila Kimbisa yeye katumiwa tu kuiwakilisha kwa prezidaa....kwa mujibu wa vyanzo vyengine vya habari

    ReplyDelete
  29. Jamani tusiwe sana negative, labda Madrid kwa kupitia JK inachangia maendeleo ya soka nchini.

    Msharaha wa Maximo, kulete Ivory Coast na mambo mengine tusioyajua.

    Hivyo hapo Madrid na JK wanapongezwa.

    ReplyDelete
  30. amakweli unapojipendekeza ni rahisi sana kujiaimbisha, duh! yaani mshikaji amechemshaaaaaaaaaaa! jamani waliopo karibu na mayo wamtonye basi, na hao wasaidizi wa JK mko wapi hata hamwezi kumpiga kipepsi mkuu mkamwambia "hii mzee acha NOMA"........... BONGO TAMBARARE!!!

    ReplyDelete
  31. Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote, ......... nilalapo raisi amevaa jezi ya ronaldo, niamkapo kavaa ya Drogba mama heeee, Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wate

    ReplyDelete
  32. Hata Ze Komedy wasingeweza kubuni kitu kinacho chekesha kama hiyo picha ya kwanza

    ReplyDelete
  33. Real Madrid kihistoria inahusishwa na Dikteta Jenerali Franco. Historia na misingi ya timu ya Real Madrid siyo nzuri hivyo.

    ReplyDelete
  34. VIONGOZI WETU HAO HAPO JUU WANAHITAJI MAOMBI !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...