Ankal na wadau wa Globu ya Jamii,
habari za kazi na poleni kwa juhudi zenu za kuwahabarisha watanzania kwa njia ya mtandao. nawatumia link hizi kuonesha hali halisi ya raia wa kigeni wanaokuja kutafuta maisha saudia jinsi wanavyofanyiwa. hatua hii imetokana na mimi mwenyewe kuwa nipo katika matatizo haya lkn mbaya zaidi kuona kuwa walionileta kutoka huko tz wanaendelea kukusanya vijana wengine kama mimi na kuwadanganya kwa kuwaahidi maisha bora wakifika huku saudia.
link hizi ni za vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikiripoti manyanyaso haya sio tu ndani ya saudia bali pia nje ya saudia lakini kwa makusudi serikali ya hapa inafumba macho na kujifanya kuwa inatenda haki. wapo waliouwawa, waliopata ulemavu wa kudumu, nk na daima makosa huwa ni ya wageni. wasaudi hawana kosa hata kama wataua au kumpa mtu ulemavu. nchi nyingine za asia zimeanza kuzuia raia wao kuja kufanya kazi hapa kutokana na hali hiyo.
vyombo vya sheria ndio kabisa kuanzia polisi hata mahakama. kwanza ukifika kulalamika utaambiwa hatujui kiingereza zungumza kiarabu kama hujui ukatafute mwanasheria. sasa mshahara wenyewe riyal 500 hadi 800 (riyal 1 ni tsh 300) utamlipa mwanasheria gani? pili huyo jamaa unayemlalamikia ni bilionea hivyo hata polisi hafiki utasikia unajibiwa huu ni uzushi msaudi hawezi kufanya hivi nenda zako. hapo kesi imeisha.
naomba musambaze taarifa hizi kadri muwezavyo hata kutumia magazeti, redio na tv ili vijana wenzangu watz kama mimi wanaotafuta kazi za udereva, uhouse girl, kuuza maduka, kwenye viwanda na makampuni nk wasidanganywe na kuja kupata mateso kama yaliyonikuta mimi hivi sasa.
tafadhali pokea link hizi.....
http://www.migrant-rights.org/2009/11/28/abusive-saudi-employer-keeps-his-filipino-driver-in-jail/
http://arabnews.com/saudiarabia/article23575.ece
http://www.mideastyouth.com/2009/10/07/abuse-of-domestic-workers-in-the-gulf/
http://gulfnews.com/news/gulf/saudi-arabia/tortured-maid-in-serious-condition-after-amputation-of-her-limbs-1.201123
http://information-hub.ofw-connect.com/OFW_Articles/migrant_workers_abused_in_saudi_Arabia
http://www.migrant-rights.org/2009/05/03/indonesian-maid-suffers-horrific-abuse-in-saudi/

INAWEZA IKAWA KWELI, ILA KWELI NCHI KAMA SAUDIA ARABIA INA MAHAKAMA ZA KISHERIA NA UTAWALA WA KISHERIA UNATAMBULIKA KABISA KIMATAIFA KAMA SHERIA ZAKENI KALI KABISA KWA UNYANYASAJI,UONGO.UWIZI .NK
ReplyDeleteMUJUE MUNGU NDIYE ANAJUWA UKWELI WA WATU HAO WANAOSEMA WANANYANYASWA.
michuzi naomba kutoka kwako mambo mawili.
ReplyDelete1 kwanza hizi link zilizotajwa hapa ziwe active yaani mtu aweze kuclick hapa na kuunganishwa na ukurasa husika. naomba ufanyie maboresho post hii ili tuweze kujisomea kama mtoa hoja alivyoomba.
2. mtoa hoja pia amemtumia chemi che mponda post ambayo katoa details za hawa jamaa wanaofanya upuuzi huu huko bongo. napendekeza kuwa ile post ya chemi si vibaya ukaiweka hapa katika blog ya jamii ili watz wote ulimwenguni wakawajua hawa jamaa wanaoshirikiana na waarabu kuwatesa wenzao watz. nimeona kule kwa chemi kuwa genge moja linaendeshwa na jamaa anaitwa BUNGIRE huyu jamaa yupo ilala na genge jengine linaitwa MADINA lipo mtaa wa uhuru. naomba michuzi tuwekee wazi hawa jamaa wakamatwe mara moja.
KWENYE MIAKA YA 80 KUNA KESI YA MWANAMKE WA KIFILIPINO AMBAYO ILKUJA ILKUJA KUCHUKUA SURA YA KIMATAIFA NA SHIRIKA LA KUTETERA HAKI ZA KIBINADAMU LILINGILIA KATI BILA MAFANIKIO.ILIKUWA NI KAWAIDA YA WASAUDIA KUTUMIA MAWAKALA NA KUAJIRI MA HOUSE GIRL TOKA NCHI MASIKINI.HUYO MAMA ALIKUWA ANABAKWA MFULULIZO NA TAJIRI YAKE WAKATI MWINGINE KINYUME CHA MAUMBILE.SIKU MOJA TAJIRI ALIKUWA AMELEWA NA KUANZA KUMBAKA BINTI AKAKIMBILIA JIKONI JAMAA AKAMFUATA AKIWA JUU KAMA ALIVYOZALIWA BINTI AKAONA KISU KARIBU AKAMPIGA NACHO CHA MGONGO NA YULE BANA KUFARIKA POLISI NA UCHUNGUZI WAKIDAKTARI ULITHIBITISHA KUINGILIWA SIKU ILE ACHILIA MBALI KUHARIBIWA KINYUME CHA MAUMBILE,NA CHPA ZA WHISKY TUPU ZIMEKUTWA NDANI YA NYUMBA.AMINI BINTI YULE ALIHUKUMIWA KUNYONGWA MPAKA UN IKAINGILA SWALA HILO,WASAUDI NI BINADAMU KAMA BINADAMU KAMA WENGINE NAO WANA MABO YAO YA AJABU.MWEZI WA RAMAZANI NENDA BANGKOK AIR PORT UONE WASAUDIA WANAVYO MIMINIKA KWA MAPUMZIKO MAFUPI HAKUNA WANACHO FUATA BALI WANAWAKE WA MADANGURO NA POMBE INGAWA SIO WOTE LAKINI MIMI NIMEKUWA NAURAFIKI WA KIBIASHARA MIAKA HIYO WACHO LALAMIKA NDUGU ZETU NI KWELI BORA KUBEBA BOX KWA WAZUNGU KULIKO SAUDIA WANAJIONA WAO NI BORA KULIKO MTU YEYOTE MZUNGU WANAMUHESHIMU SAUDIA AWEZI KUWA SAUDIA YA KISASA BILA WAZUNGU WANALIJUA HILO.
ReplyDeletemichuzi hakika inasikitisha na ikiwa ni hivi kwanini issa usitume open letter kwa raisi ili hatua za kitaifa ziweze kuchukuliwa na wananchi wakarudishwa nyumbani. ni wajibu wetu sisi tulio nje tusaidie ndugu zetu. ila inashangaza kuona mambo haya yanatendeka open bila dunia kulaani. kazi kwako issa ndugu na MUNGU ATAKUBARIKI AMEN MAANA MUHIMU ACTION IWE MARA MOJA NA HAO WANAODANGANYA KWANINI SERIKALI ISICHUKUE SHERIA NA KUWATIA NDANI MARA MOJA. NASHANGAA HUKU OMAN NA DUBAI SIJAONA UNYAMA HUO MAANA WATANZANIA KILA MARA TUNAKUTANA PAMOJA NA BALOZI WA TANZANIA HAPA DUBAI NA KWA NINI SAUDI ARABIA BALAOZI WA TANZANIA ASIFANYE KUWA ANAKUTANA NA WATANZANIA HATA MARA 3 KWA MWAKA. WASALAMU MPENDA HAKIA
ReplyDeleteKwanza ninaomba kutuma pole kwa wote ambao yamewakuta haya mambo kwani hawa jamaa wana kawaida hiyo kutesa watu au kunyanyasa ingawa sio wote wenye tabia hii lakini haya mambo yapo kwa hiyo kwa kukomesha haya mambo pia tunatakiwa kuchukua hatua muhimu na kwanza kupitia kwa balozi kwani kitu kama hichi anatakiwa asaidia Raia wake sio kukaa tu .
ReplyDeleteJamani kuna haja ya elimu kwa umma. Nadhani kaka Michu akishirikiana na vyombo vingine vya habari hili swala litawafikia wananchi wengi zaidi kwani naamini wapo wengi ambao hawana hizi taarifa kwa kuwa sio wote wenye kutumia mtandao. Wanahabari wa redio, magazeti, TV nk. walichukue hili.
ReplyDeleteKuna haja pia ya idara husika za serikali kulifanyia kazi ili kuwashughulikia wahusika wa hayo magenge, naamini Serikali ina wajibu wa kulinda raia wake dhidi ya mambo mbali mbali ikiwemo uonevu na manyanyaso kama hayo
ninyi wenzetu wa Dubai na Oman mko peponi balozi anazo taarifa na tumemuomba taarifa hizi azifikishe mbele ili tupae msaada,niko muda mrefu hapa na ata paspoti yangu sija badilisha yani kudai pasipoti kwa tajiri niliwekwa ndani mizi 7 nimetolewa na bado namtumikia tajiri yuleyule,kuna mwenzetu anatokea mitaa ubungo maziwa alirudisiwa paspoti yake na ndio alikua na vielelezo na ushahidi wa utumwa wetu kwa bahati mbaya kufika nyumbani akafariki kwani aliondoka hapa kwa ajili ya ugonjwa na ndio maana waka mruhusu.nawaonea huruma hawa wanakuja sasa wengine wanasema wameuza viwanja ama mabanda kutokana ta taarifa potofu za mawakala,bwana michuzi ubarikiwe tuna imani kwa njia hii ya blog yetu ya jamii na wewe maisha unayajua endelea kututolea kilio chetu iko siku mwenyezi mungu atatuona.ni kweli kuna mwanamke alibakwa akajitetea lakini akanyongwa mwenye haki hapa ni msaudia asili na sio vinginevyo.
ReplyDeletekama mnataka michuzi asidie kubadili tabia na sheria za saudi basi mjuwe kuna wengi wakubwa wa dunia wameshindwa, wakaamuwa kukubali.
ReplyDeletekama mnataka michuzi asidie ndugu hawa warudi, hii inawezekana. Cha kushangaza unaweza kukuta ndugu hawa hawataki kurudi bali kubadili nchi, wajuwe wanamapinduzi woote walipoteza maisha na hawakufanikiwa malengo yao isipokuwa wachache kama MLK Jr.
METHALI YA LEO: 'UMASKINI NI NUSU YA UKAFIRI'
waarabu wenyewe wanakimbia uarabuni na kwenda ulaya na marekani huku wamejaa wengi kweli je kwanini wewe unaenda tena uarabuni wakati wenyewe wanakimbia na kwenda kutafuta haki kwa wazungu?
ReplyDeletendugu zangu watanzania kuna nchi hapa duniani sio za kwenda hasa china na arabuni
ReplyDeletewaarabu wana adhabu kali sana kwani wanatumia kurani hata mwanamke akizaa mtoto nje ya ndoa adhabu ni kupigwa mawe hadi afe
ReplyDeletepole sana mdau huko hata wanawake hawaruhusiwi kuendesha magari hebu fikirieni kwanza kabla hamjaenda huko
ReplyDeletenani kasema saudi arabia kuna utawala wa kisheria kama wakikamata mwizi wanamkata mikono?
ReplyDeletejamani huko kuna neema ya mafuta tu lakini mambo mengine mmh ni hatari kama unasikiliza vyombo vya habari vya kimataifa kama dw au bbc
ReplyDeleteMdau uliyetoa mada nakupongeza sana kwa kuwa jasiri wa kuelewesha jamii ili waepuke unyama huo wa waarabu. Pole sana kwa yanayokupata mungu atakusaidia mkataba ukiisha urudi nyumbani salama. Una moyo wa jasiri ingekua mtu mwingine angekaa kimya, angetuma picha kuwaletea ndugu na marafiki jinsi anavyotanua kama kawaida ya watanzania wengi, lakini wewe ni jasiri na mzalendo halisi. Hongera sana Kaka umeokoa wadogo zako wengi sana kwa habari hii.
ReplyDeleteUjumbe kwa Watanzania wenzetu mnaoishi nje ya nchi muwe mnatueleza ukweli wa nchi mlizopo kama mwenzetu alivyofanya, hii tabia ya kupiga mapicha na kutuma Tanzania mkionyesha mnavyotanua majuu na wakati mnajua kabisa sio kweli muache kwani mnapoteza wenzenu. Uliyetoa ujumbe huu mungu akubariki sana.
ReplyDeleteMichuzi nakuomba hizi habari na maelekezo ya watu hapa uyakusanye na kuyachapisha kwenye magazeti huko nyumbani Tanzania,utawasaidia wengi sana na kuokoa maisha ya watu huko.Hii inatisha na inasikitisha sana.
ReplyDeleteUkatili unaofanywa na waarabu kwa wafanyakazi wa kigeni kutoka East Africa ni kweli.unaweza kusikiliza kipindi cha mbiu ya mnyonge kutoka BBC.open link
ReplyDeletehttp://www.dwelle.de/popups/popup_single_mediaplayer/0,,4128461_type_audio_struct_11596_contentId_2901744,00.html
NDUGU WAPENDWA, WATANZANIA, WAAFRIKA...NI jambo la kawaida sana kwetu kuteteana kwa sababu tuna zile imani 10 za Mtanzania...! "Binadamu wote ni sawa na kila mtu anayo haki..."
ReplyDeleteHaya mambo yanayozungumzwa hapa ni ya kweli na yanatokea hata leo hii mwaka huu 2010. Angalia huyu binti MKENYA hapa katika link hii: http://www.nation.co.ke/News/-/1056/840238/-/vp9oc4/-/index.html