Shikamoo 'anko' Issa,
Kwanza, pole na mihangaiko na pilika pilika za kila kukicha. Bila kukupotezea muda wako, napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha Vijana kuhusu website/blog changa, Vijana FM:
http://www.vijanafm.com/
Lengo la 'kijiwe' hiki ni kuwakutanisha Vijana kutoka sehemu mbalimbali; kuwapa ukumbi wa kujadili mambo yanayojiri kwenye maisha yao. Kama wahenga walivyotuasa, "Kwenye wengi, hapaharibiki neno," kwahiyo ni matumaini yetu kuwa mijadala hii itasaidia kuwafungua macho na kuwaendeleza Vijana kwa njia moja au nyingine.
Utaona kwamba website/blog imejaa mambo ya teknolojia, hasa mtandao. Lakini tunakusanya nguvu kazi au Vijana watakaokuwa wanaongoza mijadala kwenye nyanja nyingine, kama Sanaa, Fasihi, Upigaji picha, Michezo, Burudani n.k. Bila kuwasahau watu wa Runinga na Redio. Tafadhali, Vijana, msisite kuwasiliana nasi - kwa nia ya kukosoa, kutupa mawazo au kujiunga na timu.
Wote mnakaribishwa kwa moyo mkunjufu!
Steven,
Kwa niaba ya Vijana FM

Safi sana Dr Bunga, hii kazi imetulia sana na tuko pamoja katika kuliendeleza hili libeneke...
ReplyDeleteKibangu wakilisha!!!
ebwana ndio!
ReplyDeletevijana visingizio vipungue!...ooohh tulikuwa hatujui hatukupata info.
ReplyDeleteEndeleeni jamani..nitakuwa nalicheki libeneke.
Shukrani,
Mdau