
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) Mh. Phillip Marmo (pichani) amesema kuwa serikali haitokaidi uamuzi wa Mahakama kuhusu suala la wagombea binafsi endapo Mahakama ya Rufani itasisitiza kuwa waruhusiwe kwenye uchaguzi mkuu ujao kama ilivyoamuriwa na Mahakama Kuu mwaka 2005.
Hata hivyo, Mh. Marmo amesema kuwa kutokana na mchakato wa maandalizi ya uchaguzi mkuu kufikia mbali endapo msimamo wa mahakama utakuwa ni ule ule basi itabidi uchaguzi mkuu uahirishwe ili kuruhusu utaratibu wa kubadili Katiba na kuwezesha wagombe huru na binafsi kushiriki kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu.
Pamoja na hilo Mh. Marmo amedokeza kuwa endapo itabidi Katiba ibadilishwe basi kuna uwezekano kuwa suala la mgombea binafsi litarudishwa kwa wananchi ili liamuliwe kwa kupitia kura za maoni. Akizungumza na KLHN International ambacho ni kituo cha Watanzania kirushacho matango kupitia mtandao wa Intaneti Mh. Marmo alisema kuwa hata hivyo kwa wakati huu suala la kura za maoni halipo “kwani tutavuka huo mto tukiufikia”.
Kuhusu kile ambacho kinaonekana kuwa ni mgongano kati ya serikali na mahakama kuhusu suala la mgombea binafsi Mh. Marmo alisema kuwa hakuna mgongano wowote isipokuwa hivi sasa haupo muda wa kutekeleza uamuzi wa mahakama akidai kuwa rufaa iliyokatwa na serikali ilisababisha uamuzi wa awali usitekelezeke.
Mh. Marmo alitumia mfano wa adhabu ya kifo ambapo rufaa ikikatwa basi adhabu ya awali ya kunyongwa haitekelezwi hadi rufaa iamuliwe. Hata hivyo alipoulizwa kwa kutumia mfano wa kesi ya Nalaila Kiula (aliyekuwa Waziri wa Ujenzi) na ile ya kina Nguza Viking ambapo wote licha ya kukata rufaa bado waliendelea kutumia adhabu zao Bw. Marmo alidai kuwa “kesi hizo ni za mazingira tofauti”.
http://mwanakijiji.podOmatic.com/
entry/2010-03-02T22_31_19-08_00
Sawa basi wananchi turuhusiwe pia ktk kura ya maoni, kukubali kama kuna umuhimu wa
ReplyDelete- wa vyama vya siasa kuwepo au la.
- Je Bunge lisiwepo kwa vile limeshindwa kutekeleza majukumu yake au la
- mkuu wa mkoa achaguliwe na wananchi au la.
- je sambamba na mkuu wa mkoa, je wakuu wa wilaya wawepo au la
Hii kura ya maoni iweke mambo mengi ambayo wananchi hawajaulizwa toka tupate uhuru wa Tanganyika na pia kutokana na tuliyojifunza ktk miaka 48 ya uhuru wa Tanganyika, lazima kuna mambo ya kurekebisha, kuondoa au kuyatia ktk katiba na sheria za nchi kupitia kura ya maoni ya wananchi.
Mdau
Kilimatinde.
hivi huyu mwanakijiji hana life,kazi kushabikia siasa tu,utakufa masikini wewe,mwenzako mboye unayemsapoti mjanja kwa hela,si unaona kaona akigombania urais hashindi na anazidi hasara,anaingia bungeni na yeye akazinyonye,sasa we baki kushabikia tu huko.bongo hamna siasa,ccm wanakula na wapinzani ile ni ajira ya kudumu kwao.nakushauri huu muda ya kuandika ujinga ungepumzika na familia yako na kuonesha upendo.
ReplyDeletehuyu jamaa yetu kijiji kimemshinda,anakimbizia miswada yake kwa ankal,kweli mithupu wewe ni moto wa kuote mbali,blog ya jamii haina majungu,ni news tu kwa kwenda mbela.michuzi kiboko.
ReplyDeleteI wish, tungekuwa na waandishi wa habari mia kama Mwanakijiji !
ReplyDeleteHongera Mwanakijiji,
ReplyDeleteMahojiano yalikuwa mazuri; kila Mtanzania mwenye akili timamu sasa anajua fika kuwa Serikali haikuwa imedhamiria kabisa kitii hukumu ya Mahakama.
Job Well done.
NE,
Reading, UK.