Juu na chini Meli ya MV Serengeti ikiungua moto ikiwa iko nje kidogo ya bandari ya Zanzibar jana, huku wafanyakazi wa shirika la bandari zanzibar kwa kushirikiana na kikosi cha zimamoto na uokozi(KZU) wakiwa katika jitihada za kuuzima moto huo. Meli hiyo yenye namba za usajili IMO:6818796 ilikua katika matayarisho ya kwenda kisiwani pemba. Juhudi hizo zilifeli ila hakuna maafa yaliyotokea na hadi sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana. Usafiri wa kwenda na kutoka Pemba sasa umewekwa njia panda maana MV Serengeti ilikuwa tegemeo la wengi na haijulikana itakuwaje baadaa ya hapo
Wananchi mbalimbali wakishuhudia meli ya MV Serengeti ikiungua moto nje
kidogo ya bandari ya zanzibar. Picha na Haroub Hussein





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Maji si hayo mnayaona? wekeni pump mnasubiri nini?

    ReplyDelete
  2. Wapemba wenzangu tupoe maana hii meli ilikua ndio mkombozi wetu, kweli sasa sijui itakuaje

    ReplyDelete
  3. haa! ha! hicho ni kitendawili kaka mjanja hategui, sawa na mbio za panya, asante ankal usinibanie
    mdau kibanda maiti,

    ReplyDelete
  4. 1. haina insuarance

    2. hao watu pembeni wanangoja maji yapungue wazamie kuiba vitu

    3. rescue boat haikuwa na maji ya kutosha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...