Hi ankal natumai u-mzima!!
Nadhani kila mwenye macho na masikio anajua kuwa, Manispaa na majiji yetu ya kibongoMipango miji ni zero! Si Dar tu, hata Arusha, Tanga, Mbeya, Mwanza, nk.
Na sidhani kuwa kama wahusika hawalijui hili, wanalitambua fika, na kuna wakati Manispaa za Dar,Temeke, Ilala na Kinondoni kwa mfano wakaweka mpango 'niite wa kisanii' wa kupunguza kasoro hizo hasa yale maeneo ambayo kwa sasa ujenzi na makao mapya yanaenda kwa kasi ya ajabu.
Sasa cha kushangaza na cha kujiuliza hawa jamaa kweli wanataka mabadiliko ya kweli au la? Maana unaweza kuona hao wanaoitwa watu wa wanaopima na kuthaminisha/surveyors wanapita na kujaribu kuthaminisha maeneo ambayo tayari watu wamesha anza kujenga, tena kwa kuwaambia wasubiri hilo zoezi liishe/nina maana ya stop order!
Tena kuna wakati wanapita na mgambo wakukute wewe na mafundi wako mko bize na ujenzi hapa itakuwa kama mmeua vile, yaani mshimshike kamata kamata then mkamalizane mbele kwa mbele "si unajua tena inakuwa mradi juu ya mradi"!
Watapimapima na kuandika vilivyomo humo na kuchukua details za wahusika. Hapa watasema msubiri mchakato wa kulipwa na kupimwa maeneo yenu katika kipindi cha miezi mitatu. Haya wananchi wanatulia kusubiri kifuatacho kama walivyo ambiwa, cha ajabu sasa miezi mitatu itaisha hakuna jibu hata kama utafuatilia ofisi za kata wanakuambia bado hawajarudi na hawajui watarudisha majibu lini.
Ifaamike wakiwa wanatembelea maeneo ya watu hupitia katika ofisi za kata husika.Sasa hivi kwanini wahusika wasiwe na tabia ya kufanya kazi kwa kasi ileile ambayo miji inatanuka kuendana na kasi ya mahitaji ya jamii kupata makao? Mbona Madaktari/Walimu/Mahakimu/Polisi/Wanahabari huwa wanakuwepo maeneo yao ya kazi at least, sasa hawa watu wa ardhi nina maana 'Surveyors' na wapimaji maeneo yao ya kazi ni maofisini na vijiweni au huko ambako jamii iliko?
Au hayo mabadiliko wanayoyataka kwenye mipango miji ni kuchora michoro mizuri kwenye karatasi na kuwakirisha kwa mabosi zao ili waone kazi waliyofanya inavyopendeza? Lakini kwenye ground mambo kuwa tofauti? Maana wananchi watasubiri na hadi wanakata tamaa na kuamua kuendelea na ujenzi wao kwa mitazamo yao nje ya wataalamu, penye makazi wataweka bar, na maukumbi ya disco! Atalaumiwa nani kwenye jambo kama hilo? Wanataka warudi baada ya miaka mitatu na kuchora "X" na kuandika Bomoa? Eti kisa wananchi wamevamia maeneo?
Na hiyo stop order ina maana wananchi waendelee kusubiri hadi lini?
Au hao wahusika wanasubiri wananchi watumie visenti vyao ama vya kiunua mgongo/wanavyovujia jasho then wao waje na kusema mmejenga kimakosa hapo bomoa na hakuna fidia?
Ina shikitisha sana kuona sekta hii nyeti ikiwa kwenye mwendo wa kobe na ujenzi wa makazi mapya ukiwa kwenye mwendo wa roket, je kuna siku zitaenda sambamba hapo?
Mifano iko mingi tu, Kinyerezi/Kifuru/ Ila hao hao wapimaji wakiitwa na mtu yaani kwa dili nataka kupima eneo langu na kwa kuwa wanajua kuna cha juu tena kuna wakati Surveyor wa Kinondoni anakuja kufanya kazi Ilala si dili.... hapa, yaani kila kitu kitaenda fasta katika siku tatu nne utakuta wamesha mwekea hadi mawe na kumwaidi muhusika wataendelea na mchakato wa offer na baadaye hati-kama atahitaji wao washughulikie kwa haraka!!! Ina maana aongeze fungu!!
Binafsi sijui kama hilo ni sahihi au inaruhusiwa kumpimia mtu mmoja mmoja (utaingizwa hadi kwenye master plan ya eneo husika) na kama kweli mwisho wa siku 'documents' zote zinakuwa halali au la-au ndo mambo ya mjini mjini, au ndo mambo ya "changa la macho"
Muheshimiwa alikuja na mission statement ya " Ari mpya Nguvu mpya na Kasi mpya" sasa sijui hawa jamaa wa ardhi wako na 'mission statement' ipi? Au fani imevamiwa?Naomba wanajamii tusaidiane maana hilo ni tatizo tena si dogo kwani madhara yake yatachukua miongo mingi ijayo "Yaheri ya Kinga kuliko tiba"Wakurugenzi mpo? Ma-surveyors mpo? Wananchi mpo?
Wakereketwa mpo? Mjenga nchi ni Mwananchi.....!
Kila mtu awajibike na awepo eneo lake la tukio/kazi...
maendeleo hayaji kwa.............................!
Nawakirisha,
Madau/Mwanakijiji!Chimbyo........!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ankal kwa upande wangu nakubaliana na mtoa mada. Ni tatizo kubwa sana kama ambapo wanaacha kuzuia wananchi wasikate miti ovyo misuituni halafu wanawasubiri barabarani kuwanyan'ganya mkaa. Au wanavyoshindwa kusimamia sheria za barabarani halafu wanajaza matuta kibao bila kujua wanachelewesha watu makazini na kuwaharibia magari ambavyo vyote ukichanganya na matumizi ya mafuta mengi kwenye foleni ni pigo kwa uchumi na pia kuchelewesha maendeleo.

    ILA KWA HILO LA UPIMAJI napenda kuwasafisha Halmashauri ya JIJI la Mwanza kwani mpaka sasa hivi hata wananchi wa kijijini hawajengi bila kwenda ofisi za jiji na kupatiwa michoro. Labda
    Mh. Kandoro alisimamie hilo tu na jitihada zaidi zifanyike ili watu wengi washiriki katika upimaji na kulifanya jiji la Mwanza liwe kwenye mpango unaostahili. Nategemea Mwanza litakuwa jiji lililo katika mpango mzuri zaidi kuliko majiji mengi Afrika kutokana na jinsi muelekeo unaonekana.

    Mdau Juma----Mwanza.

    ReplyDelete
  2. I feel you mdau, yamenikuta huko Kwembe, hapa nilipo sijui pa kuanzia maana mawe yapo, offer nilishapata na hadi hati ninayo but jamaa wamekuja kuthaminisha na wameweka mawe yao juu ya mawe yangu. Yaani jiwe la "so called serikali" juu ya jiwe laserikali..Nijuavyo mimi ni kuwa only Rais ndio anaweza ku-revoke hati ya kiwanja..sasa sijui kama Rais wetu mtukufu ana habari na haya tunayofanyiwa wanakijiji wa Kwembe/Luguruni?
    Na naskia wamehamia Kigamboni sasa, kaaaz kweli kweli

    ReplyDelete
  3. Hongereni Mwanza, ni ukweli usiopingika Mh.Kandoro si mchezo katika uwajibikaji wake. Wewe hukumbuki alivyokuwa anayafanya kazi hapa Dar. Kwa kweli sikio la kufa halisikii dawa, mpaka leo nashindwa kuelewa huyu mheshimiwa mwenye nchi apendaye kushinda hewani na ugenini kwa nini anapenda sana wasanii kiasi cha kutuletea huyu bwana longolongo kutoka Dodoma sasa hivi mambo mengi ambayo Mhe.Kandoro alikuwa ameshaanza kuyakabili yanashindwa tena. Nina uhakika ndiyo maana hata Manispaa ya Kinondoni sasa hivi imeanza kiburi tena na jitihada za kutoa vibali vya bar na vitu vingi visivyohitajika katika makazi ya watu. Haya bwana tutafika!!!

    ReplyDelete
  4. MIMI HUU NI MWAKA WA TATU,MPIMAJI KACHOMEKA MAWE TU NA HAONEKANI TENA.HAPA NI WILAYA YA KINONDONI.KUNA WAPIMAJI AMBAO WANAENDESHA VITENDO VYA KITAPELI SANA.KESSI NYINGI ZIKO MAHAKAMAI.HII WILAYA NI CHAFU SANA.

    ReplyDelete
  5. juma hauleMarch 01, 2010

    Wilaya ya KINONDONI wapimaji wanaongoza kwa UTAPELI WA ARDHI.
    Serikali ebu watupieni jicho hawa watu.

    ReplyDelete
  6. Huyo mdau wa march 01,04:07:00PM kuweka jiwe juu ya jiwe haiwezekani kama imetokea hivyo basi hati yako itakua fake manake kama eneo lako limepimwa na umepata offer mpaka hati haiwezekani mtu yoyote kuja kukubabaisha tena

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...