Pole ankal na shughuli mzito ya kulisukuma
gurudumu la maendeleo la globu yetu ya jamii.
Sasa bana mimi nilikuwa naomba msaada kwenye zebampu. Kuna nyimbo 5 nimezitunga ambazo ziko kwenye manjonjo ya bongofleva. Sasa bana nimejaribu kuwasiliana na baadhi ya masupastaa wa bongofleva nchini, lakini naona wanadengua mno.
Wengine hata kunisikiliza hawataki. Nimejaribu kuwauliza kama wana meneja ili nikaonane nao, lakini ndo hivyo tena midenguo miiingi. Kuna mmoja nilijaribu kumsihi tukutane nae ili angalau aione kazi tu. Lakini akanijibu kwa maringo hivi, “ahsante kwa kushoo lavu, lakini hapana sina muda huo.” Nikabaki nacheka tu!

Kusema ukweli, wala siwalaumu. Kwa sababu kwanza hata hawanijui, na wala hawajahi kuona kazi zangu. Kwa hiyo, pengine wanafikiri mimi ni chokoraa au mwandishi wa magazeti ya udaku nafuta habari ya kuuza gazeti.
Au pengine ni kwa sababu wasanii wengi hawa bado hawajajua kwamba kuna watu wanaitwa “song writers” ambao kazi yao ni kuandika nyimbo na kuwapatia/kuwauzia waimbaji.

Sasa basi, mimi nataka kuzigawa hizi nyimbo bure kabisa. Tena naweza kuwatafutia hata beats zake. Sharti pekee ambalo ningependa kuwapatia ni kuwa waitambue kazi yangu na waweke wazi kuwa hizo nyimbo nimetunga mimi. Yaani maana yake ni kuwa wasithubutu kunitupa kapuni, na kujifanya kama wao ndio wametunga hizo nyimbo.


Majina ya nyimbo zenyewe ni kama yafuatavyo:
*Bongofleva 4 life – nimeutunga kwa ajili ya msanii wa kiume. Na huko katika manjonjo ya hip hop.
*U tayari kwa pendo langu – msanii wa kike. uko katika manjonjo ya soul.
*Njoo kwangu – msanii wa kike. uko katika manjonjo ya R&B.
*Forbidden love - uko kwa kiingereza, na unafaa msanii wa kike. Huko katika manjonjo ya soul.
*Jogoo la shamba – msanii wa kiume. uko katika manjonjo ya hip hop.


Ningeweka dondoo ya ryrics,
lakini naogopa kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Sasa kama kuna wasanii wowote ambao wangependa kukutana nami ili waone kazi, basi wasisite kuwasiliana nami kupitia 0655 712751

Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. kaka michuzi mail yako kwenye blog twaipata vipi?

    ReplyDelete
  2. Jay dee atakusaidia....wasiliana naye...!!!

    ReplyDelete
  3. HIP HOP LONGTIME-UKMarch 18, 2010

    USHAURI WA BURE WE SONGWRITER,NAJARIBU KUKUSAIDIA KAMA MTU MWENYE EXPERIANCE KIDOGO KWENYE GAME,NILIWAHI KUWA MSANII WA HIP HOP MIAKA YA TISINI ILA KWA BAHATI MBAYA AU NZURI KIPINDI KILE MUZIKI ULIKUWA UNAONEKANA UHUNI TU NA SIO TU HILO VILE VILE ULIKUWA HAUNILIPI KITU UKICHANGANYA SABABU HIZO MBILI NA SHINIKIZO LA WAZAZI KUTAKA NISOME NIKAACHA KABISA MUZIKI WEZANGU WENGINE SASA HIVI HAPO BONGO WANA MAJINA MAKUBWA TU,KUTOKANA NA EXPERIANCE NILIYOKUWA NAYO KATIKA MUZIKI NATAKA NIKUSHAURI KITU KIMOJA HIZO NYIMBO ZAKO ZIPELEKE KWENYE CHAMA AU BARAZA LINALOHUSIKA NA MUZIKI UKAZIANDIKISHE KWANZA MAANA UKIMUONYESHA MTU KABLA YA KUFANYA HIVYO UTASIKIA BAADHI YA MANENO KWENYE NYIMBO ZAKO YANAIMBWA AU HATA WIMBO MZIMA,NAKUAMBIA HIVYO MAANA KUNA WASANII NA MAJINA YAO WAMESHACHUKUA NYIMBO ZANGU ILA HATA NIKIWAAMBIA WATAKATAA KATA KATA KWA SABABU WAMEPATA MAJINA NA MIMI HAKUNA ANAYENIJUA KWA SABABU SIKUWAHI KUSIKIKA,LASTLY MUZIKI TANZANIA IS NOT A REAL THING NASHAURI WATU WASOME,VIJANA SOMENI MIMI NISINGE SOMA NINGEKUWA KAMA BAADHI YA WASANII UCHWARA BONGO.WATOTO WANAACHA SHULE KISA HIP HOP ETI ANUNUE TOYOTA CHASER WAKATI WATU WANAWAZA MARA MIA YA HIYO.NI KWELI UNAWEZA KUWA NA KIPAJI ILA KIPAJI BILA YA MISHIKO NI UJINGA BORA UKAZANE NA MAMBO YATAKAYOWEKA MISINGI YA MAISHA YAKO IMARA.NI HAYO TU

    ReplyDelete
  4. Pole, bahati mbaya kutokana na elimu duni ya music industry hapa kwetu wasanii wengi wanaona ni kudhalilika kutumia tungo ya mtu mwingine, wakifanya hivyo basi hawataki kabisa kumtambulisha mtunzi. Japo wangejua kuwa wao wana kipaji cha kuimba au kughani tungo, na kuna watu wenye vipaji vya kutunga tu, na wakiungana matokeo huwa mazuri sana kwa sababu una kuwa na the best kwa kila upande. Kwa kuwa media ni darasa Michuzi fanyeni kazi ya kuelimisha hilo. Hongera kwa jitihada zako mtunzi dont give up

    ReplyDelete
  5. Mimi nakushauri nyimbo hizo umpatie dada MARTINA CHAMBIRI. I'm sure kipaji bado anacho na kwa tungo zako potentially atalitoa taifa kidedea kwa mara nyingine kama hapo awali (utotoni) alipotu-surprise na wimbo wake wa Tanzania eeee, Tanzania aaaa huko kwa kina Mheshimiwa Chibiriti!!

    ReplyDelete
  6. Nashauri uende kwa Lady Jay Dee, she is really something, atakutangaza vilivyo na hata akiimba nyimbo zako atakubali kua hakutunga yeye na atakurusha kua wewe ndo umetunga nyimbo...ila utunzi kwa wenzetu wa nje ni kazi kbsa yenye kipato cha kutosha, andikishana na yeyote ataechukua wimbo wako mkataba wa % fulani kwani hiyo mtu wangu ni kazi kbsa km nyingine.All the best.

    ReplyDelete
  7. POLE SANA ILA HIZO NYIMBO NINAUHAKIKA HAZITA TAMBA, BONGOFLEVA FOR LIFE NDIO NINI? AF JOGOO LA SHAMBA HIYO SIO NYIMBO YA MOROGORO JAZZ? WE TAFUTA SHUGHURI NYINGINE YA KUKUPATIA UMAARUFU KAKA NYIMBO ZAKO ZINA MAJINA YA MOVIE. U TAYALI KWA PENDO LANGU? DIWANI YA MLOKA AU MALENGA WAPYA??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...