ANKAL Salam!! Natumai uko salama!!

Sasa ankal naomba unirushie kijiswali changu hichi wadau wenye kufahamu au waliowahi kuexperience hii kitu wanifahamishe. Mimi nimekuwa nikiishi hapa kwa Bibi (UKerewe) muda kidogo yapata kama miaka Nne hivi.

Muda wote huo nimekuwa nikitumia simu kwa mtindo huu wa PAYG (pay as you go system) ambao ndo mtindo pekee ulioko huko nyumbani Tanzania. Lakini hivi juzi kati nimeamua kujiingiza katika contract (pay monthly) na kampuni ya Orange nikachagua simu ya kisasa kabisa aina ya apple aiphone kama ionekanavyo hapo juu pichani.

Kwa sasa ninataka kwenda Tanzania kwa rikizo isiyopungua miezi miwili. Sasa Ankal swali langu kwa wadau nilitaka kujua (sababu simu hizi za contract ziko locked) je nikii-unlock hii simu nikaenda nayo nyumbani kwa lengo la kutumia kwa muda huo nitakaokuwa huko

1. kule itaweza kupiga mzigo kama kawa au jamaa wameziwekea security flani kupunguza wimbi la foreigners kuingia nazo mitini??
2. Je Iwapo jibu la swali la kwanza hapo juu litakuwa 'itawezekana kutumika bongo', nini kitatokea iwapo ndani ya muda ambao nitakuwa likizo watakosa kipande chao cha kila mwezi??
3. Je iwapo mtu ataamua kuchikichikia nayo mojakwamoja huwa wanawezaje kuwapata watu kama hao?

Nitafurahi kwa wenye jibu fasaha maana yake kama itashindikana basi itabidi ninunue simu nyingine kwa lengo la kutumia miezi 2 tu nitakapo home. Nitafurahi hasa kwa jibu la swali la kwanza manake hilo ndo hasa lililonifanya kuomba msaada huu.
nb: i prefer anonymity ankal usirushe email yangu!
Cheers man nitashukuru kama utarusha
swali langu na nikapata feedbacks nzuri

Mdau wa iPhone

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 47 mpaka sasa

  1. Kwanza kabisa, simu namna hiyo zipo Bongo, na uki unlock utaweza kuweka local simcard na kutumia, ingawaje sijui kama utapata facilities zote kama upatavyo ukerewe. Hii itategemea network provider utakayemtumia e.g. Tigo, Zantel etc.

    Katika miezi miwili unaweza ku-negotiate na network provider wako ili usilipe full monthly rental au unaweza kupewa 'likizo' ya kutolipa kabisa - nayo hii inategemea na provider. T-mobile kwa mfano mwaka wa 2001 walinipa likizo katika muda wa wiki saba - muhimu uwataarifu kabla hujaondoka.

    Ila wajanja wakiikwapua, basi tena umeula, ukiipata una bahati!

    Kazi kwako.

    ReplyDelete
  2. hiyo idea yako haitafanya kazi.na wao hadi wamekukubalia hiyo contact ya kulipa kila mwezi ni baada ya kuonyesha proof kuwa utaendelea kuwepo UK kwa muda fulani,otherwise ungekuwa na tourist Visa ,sidhani kama wangekubali kuingia mkataba nao.

    ReplyDelete
  3. TUNAOMBA KWANZA UTUPE MODEL YA HAKO KA IPHONE KAKO KWANZA TUTAKUPA MAJIBU NI IPHONE GANI 2G,3G,3GS?JAIL BREAKING INAWEZEKANA ILA.....ILA HIZI ZILIZOTOKA JUZI JUZI MMMH NAONA ITAKUWA NGUMU KIDOGO MAANA ZIMEPIGWA PINI LA AJABU.UKIINGIA NAYO MITINI NI RAHISI SANA KUI TRACE HIYO SIMU SEMA TU WADHARAU KUKUFUATILIA MAANA MTU HAWEZI KUTUPA POUND 100 KWA AJILI YA POUND 300 UPO HAPO?.UKISHAIFANYIA JAIL BREAKING HAKIKISHA UKIWA NAYO VUMBINI KULE(BONGO) HAUINGII NAYO KWENYE MITANDAO KAMA YA APPLE NA KU DOWNLOAD SOFTWARE NA VITU KAMA HIVYO MAANA POSIBILITY NA KUPIGWA PINI TENA NI KUBWA ILA HII INATEGEMEA NA GENERATION YA IPHONE.

    ReplyDelete
  4. Kitendawili kingine unachotakiwa kupatia jibu ni kuhakikisha frequency za simu zinaendana na zinazotumika bongo. Wataalamu watafafanua mambo ya GSM 850/900 MHz nk. Ingia google uone mambo ya quad band nk

    ReplyDelete
  5. Kweli wabongo tunamatatizo makubwa, wewe ndugu yangu umepewa simu kwa mkataba maalumu wakuilipia taratibu, sasa unataka kufungua PIN au uingie nayo mitini. Huo ni wizi wa kijinga na unaweza kugharimu wabongo wenzako wasiaminiwe kwa sababu ya watu wenye tamaa za kipumbavu kama za kwako. Wewe wasilina na waliokupa simu watasimamisha makato muda utakao kuwa safarini. Bongo utanunua simu ya kichina kwa bei poa ukisha maliza likizo tupa ukifika majuu uendelee na simu yako ya mkopo.

    ReplyDelete
  6. Pambavu we wacha kuzarau kwenu... eti sijui kama haka ka iphone kangu katafanya kazi tz..**#%@?|";!!!.....
    kwa taarifa yako mpaka vibaka wanazo zinauza kwa mafungu kama nyanya tena original na siyo mchina, mpaka makonda wa daladala wanazo!
    Halafu huo mtindo wa monthly payment (contract) au malipo ya baada (post paid) mpaka mahouse girl wanapata huduma hiyo! Upo hapo?? usiwe mjinga na kuzarau kwenu eti kisa umekaa ulaya vimiaka vi4. Haya endelea kubeba mabox's.
    halafu we michu unabaniaga comments zangu wakati mwenzio nataka kuikomesha hii tabia...

    ReplyDelete
  7. mdau wa iphone!
    hiyo ni simu ya kawaida sana wala isikutishe na zipo nyingi na nzuri zaidi ya hiyo,nikianza kuzitaja hapa globu ya jamii itajaa simu kwa wiki nzima.
    Nije kwenye swali lako,kwamba huku home mtindo pekee ni PAYG.....siyo kweli hata huku home kuna contract as well.
    Swala la simu kuwa locked,hiyo ni kawaida sana kwa contract phones,ila kufunguka unapokuja huku hilo swala halina uhakika,kuna zinzofunguka na zingine hazifunguki.
    Malipo yao itakuaje utakapo kuwa nje ya ukerewe? most contract phone usipotumia kwa mwezi mzima wataku-bill na mothlhly charges kama zipo applicable kwenye contract yako.

    Njomba
    Asante

    ReplyDelete
  8. Kama alivyokueleza huyo mdau hapo juu apple iphone inaweza kuwa unlocked au kufanyiwa jailbreaking ambapo utaweza kutumia baadhi ya features zake. Tatizo kitendo cha kufanya hivyo kitaitowa simu kwenye warranty, si unaiona hata kubadilisha battery huwezi so ikipata issue ngumu kufix mwenyewe, utakuja kuishia kulipia contract wakati huna simu, so sikushauri u unlock. Kama unayo simu yako ya zamani bora ukienda bongo tumia hiyo nyengine hadi utakaporudi.

    ReplyDelete
  9. The model of your phone does not matter, gimmie a day and i can unlock it, jailbreak it, n u can use it as if it was new...

    Just check ur firmware version, the latest one is 3.1 which apparently if u have installed that one, its not easy to jail break.

    oh by the way if u must know, so many ppl are sing iphones in tz.... stop bitching about it thinking u are the only one with the latest phone, dickhead!!!

    ReplyDelete
  10. sikia huyu eti anadai hakuna system ya contract Bongo!!! we vp? Nini kaipo TZ.? hela yako tu

    ReplyDelete
  11. Ndugu yangu , kama iphone yako ina base band ya 3.1.3 hatawekana kufunguliwa kwa sasa( jail broken) lakini kami ina baseband 3.1.2/ 05.11.07 na kwenda chini in rahis kufunguliwa na ni bure ukisha fungua usiewe na wasiwasi haitajifunga mpa wewe upgrade mwenyewe kwenda 3.1.3 kwa kutumia itunes cha maana ila wakati unapoingia itune ukipata messege to up grade wewe dinie the request , kampuni yako ya simu haitajua kama ume ifungua na hata wakijua kwa sheria hawanahaki ya kukufanya chochote simu ni mali yako ikipotea hapo huna lako ila kama unataka ukijiunga na (mobile me) ya apple wao wantumia gps kulocate simu huwa inafnaya kazi mahali ambako kuna GPS signal tu wanweza kuilock na kuipiga hatakama imezimwa huwa inalia lakini kwa bongo sidhani kama hii service itafanaya kazi maana GPS signal zao sijui kama zipo bongo mimi ninayo hapa marekani na ni dola $ 100 kwa mwaka
    Kusu kuto lipa wasiliana na kampuni yako ya simu wambie unaenda bongo kwa miezi hiyo watakupa off kwa hiyo miezi na kwa kisheria wanatakiwa kufanya hivo kama wakikataa omba kuongea na supervisor wao insist on that
    web site ya kufungulia iphone ni hii hapa www.blackra1n.com , unganisha simu yako halafu chagua aina ya computer , mac or window halafu bonyeza maki it rain suburi kidogo simu itajireboot halafu mambo yote yataakuwa tayari in five minute usimepe mtu pesa kukufanyia haya mambo ni bure ndugu yangu make sure simu yako ina baseband 3.1.2 kwenda chini nakutakia safari njema
    yours,
    Alex in USA

    ReplyDelete
  12. jibu la kwanza, ndio inawezekana kuiflash na ukatumia kama kawa, ila itabidi uwe muangalifu unaingia iphone isije ikajiupdate....
    jibu la pili, unaingia contract malipa yanakuwa katika system ya direct debit, kwahiyo fweza zinakuwa zinatolewa kutoka kwenye account yako kil amwezi hata kama haupo n akma zccount yako itakuwa haina mkanja basi utapigwa fine....
    jibu la tatu, kam amtu unafkiria kuchikichia utakuwa unajitaftia matatizo, kumbuka kabla ya kuingia contract uliacha details zako zote pamoja na passport copy yako kwahiyo itakuwa si kazi kwa nchi kam ahii ambayo technolojia ipo juu kukutrace....
    nadhani nimejitahid kukujibia, wakatabahuuuuuuuuuuuuuu....
    mdau bwawa la maini....

    ReplyDelete
  13. Huyu jamaa wa huko kwa BIBI ni muongo sana maana simu za contract(monthly pay) huwa hazijafungwa(siyo SIM card locked)zina kuwa free kabisa maana wanajua kuwa unalipia kila mwezi na huwa wanauhakika wa wapi watakupata kama ukiingia mitini.kwa kifupi ni kwamba kama huna permit ya muda mrefu katika nchi husika hupati huduma ya monthly pay. utaishia kununua prepaid simu tu!!!.Mimi huu ni mwaka wangu wa 9 sasa niko katika huduma hiyo ya monthly pay na kila baada ya mika miwili(inapoisha contract) na renew na kuchagua simu mpya niipendayo mimi na zote huwa zinafanya kazi niwapo TZ.(zinakubali SIM card yoyote)

    ReplyDelete
  14. Hiyo miaka 4 tu...............hujui kama bongo kuna simu za contract.......

    ReplyDelete
  15. Acha wizi dogo, simamisha contract for 2months, ukifika bongo nunua ya mchina ya elfu 10 then unapoondoka itupe ukaendelee na mkataba wako wa kufagia vyoo huko uk ooh sory mkataba wa monthly pay. By Mwanyika

    ReplyDelete
  16. HII SIO BLOG YA WEZI NI YA JAMII SWALI HILO MUULIZE BABA YAKO FISADI. UTASAINIJE MKATABA KISHA UTOROKE NA MALII YA MTU MWIZII WEEE. TAMAAA MBELE MAUTO NYUMA

    ReplyDelete
  17. Ujanja ujanja mwingine hata hauna maana - wizi tu even on trivial things.

    Why can't honour your contract?

    ReplyDelete
  18. Ukisoma hizi comments,hakika nyingi zinaelezea uhalisia wetu wa Tz; Ujanja ujanja,wizi wizi kupenda vya rahisi bila kutoa jasho, ndoto za Alinacha na mengineyo kama hayo.

    ReplyDelete
  19. mzee wa bunjuMarch 05, 2010

    IPHONE!!!!???? BULL SHIT, TZ KIBAO WALLAHI HATA MLINZI WETU HAPA OFFICINI ANAYO NA KAMA UNATAKA NIKUPE NA NAMBA ZAKE ZA SIMU ILI UMPIGIE AKWAMBIE YEYE MWENYEWE,

    HAPA TZ KUNA MAPAKA SIMU ZENYE CHOO NA BAFU NDANI, NYIOE VIPI??? BEBENI MABOX LAKINI ACHENI KUKASHFU KWENU KWA WAZAZI WENU , KWENYE CHIMBUKO LENU, ETI VUMBINI!!!! AMA KWELI HIZO NI NI AKILI ZA KI......GA


    Mzee wa bunju

    ReplyDelete
  20. Dear Bloggers!

    Huyu jamaa anahitaji msaada,kwanza nataka ujue kwamba Tz haipo nyuma sana kitekinojia,usije ukaja na vitu vyako vya kuokota huko Ukerewe ukadhani utauza,ndugu yangu utatumia mwenyewe.

    Back to your request-Tafadhali wasiliana na provider wako(Orange) kama ana mkataba na Voda au Zain katika huduma ya roaming/kuzuru TZ kwa wateja wa malipo baada(postpaid.Kama wana roaming agreement na wakaridhishwa na proof kuwa utarudi Ukerewe basi hiyo sio issue hela yako tu.Kwani ukirudi Ukerewe utaletewa bill yako ukiwa TZ.
    Mfano,Voda TZ wana roamig agreement na makampuniya nje zaidi ya 200,kwa hiyo wateja kama wewe wanasafiri nje ya nchi wanaenda kutoa taarifa ili waunganishwe ktk huduma hiyo.sometime kuna hela ambayo unalipa kabla ya kuondok is like caution money ukirudi baada ya kulipa unarudishiwa hela yako.
    sasa hivi unaweza ku-roam na huduma za data pia,
    Kama mbeba box na sio mwaminifu njoo nayo ili wasanii waku-flashie simu yako japo hutopata huduma zote kwwnye simu yako.
    NB-iPhone,apple 4nes zipo bwerere bongo jamaa wanaenda China asubuhi jioni wanarudi nazo.

    TZ is like Ukerewe pesa yako tu ,

    ReplyDelete
  21. Wabongo bwanak.Mtu hawezi kuuliza swali la maana Online akajibiwa kistaarab.Jamaa kauliza swali la maana mmeanza kuchonga midomo "ooh unadharau bongo,blah blah".Matatizo ya kutokuelewa dunia nyingine inavyokwenda yanawapeleka puta baadhi ya watu.Cell phones sio kama land phones cell phones zinatumia different frequency na kila nchi ina frequency yake.Mtu kama huna la kuchangia acha kupiga domo.

    ReplyDelete
  22. Huku Tanzania, simu za Contract (yaani Post-paid) zilikuwepo kabla hata mtino wa vocha (Pre-paid) haujaanza kupatikana. Hadi leo, mifumo yote miwili inaendelea kushamiri, kwani mfumo wa contract unatumika sana kwenye makampuni au mashirika makubwa.

    Kwa mtu anayeomba ushauri kuhusu mambo ya nyumbani, si vema uwe unatoa maneno ya dharau kuhusu nchi iliyokuzaa...

    ReplyDelete
  23. Tumia roaming

    ReplyDelete
  24. Kama mdau Ahmed anavosema hapo juu, usii-unlock simu yako. Ukii-unlock, utakuwa umetoka kwenye warrant. Afadhali ununue simu nyingine au u- roam. Ila ujye ukirudi utakuta bonge la bill linakusubiri. Pia ni afadhali uwaambie in advance kuwa hutakuwepo kwa kipindi fulani ambapo itasababisha wewe kuchelewa kulipa. Hii inasaidia kuonyesha uaminifu.

    ReplyDelete
  25. wewe swali lako ni la 3 tu tushajua,
    mbongo mbongo tu!

    ReplyDelete
  26. hebu wadau mnifahamishe juu ya hii contract phone maana sijawapata,ni kwamba mtu anakopeshwa simu na kampuni husika ama vipi na jee huruhusiwe kuhamia kwa provider mwingine?au hii contract phone ni kama simu za mezani TTCL?

    ReplyDelete
  27. Bongo ukiwa na contract unapewa simu ya bure???

    ReplyDelete
  28. http://www.quickpwn.com/2009/10/jailbreak-and-unlock-iphone-3-1-2.html
    Ikamue kwanza Bongo utapeta kama kawa!

    ReplyDelete
  29. Wabongo wanapenda kujifanya wako juu sana na maneno mengiiiii. Lakini ukirudi huko Bongo hakuna lolote la maajabu. Wabongo wanadharau sana na kujifanya wanajua sana, lakini ukifika huko unakuta "simu za kichina". Ukiwa nje ya nchi usidanganywe na wababaishaji ukaacha kitu chako kizuri. Ukifia Bongo utaambiwa Bei yake mara 10. Ukilalamika wanaanza kukukandia kuwa wewe mchovu!! Ukifika bongo unaambiwa kuna "feki na orijino" kweny kila unachoona dukani!! Usidanganywe. Bongo wanajifanya kujua wakati wengi wao wanaishi kwa utapeli tapeli tu. Unamwona mtu ana Range Rover baada ya siku mbili unamwona central police kumbe ni "anaishi mjini kwa utapeli". Acheni kukandia msichokijua!!!!

    ReplyDelete
  30. kutokana hairuhusiwi humu ndani ila tu Michuzi mambo ya maana unayabana,sasa mtu anauliza swali la kijinga ati nini kitatokea kama sijawalipa hiyo hela yao?Sasa uliposaign contract hujasoma kabla ya kusign nini kitatokea?Acha upumbavu sim zenyewe hapa UK unalipa kuanzia 10 pound kwa mwezi halafu ulipochukua contract ulitoa Bank account yako hata usipolipa hasara ya nani? si Unakua overdrawn wewe tu na kila overdrawn ni 20 pound charge plus 15 pound eachday until you pay.halafu hayo maswali sijui itatumika sijui haitumiki ungewauliza company sio hapa na hayo yote yamo kwenye mkataba,Bongo mtandao kwa sim wameanza voda long time sio,bahati mbayamwenzangu ndio kwanza unapata juzi ulaya.Michuzi bana na hii pia.

    ReplyDelete
  31. jamani wachimba mihogo, jamaa ameuliza swali hili ajue. Ukiwa na majibu mpe usipokua nayo endelea kuchimba mihogo. Jazba zitumieni kwenye kuchimba mihogo mingi. Just remember ukibahatika kutoka Tanzania, uwezi kupanda nayo ndege.

    ReplyDelete
  32. 1.inawezakana ku jail break all the iphones kwa sasa
    2.ukichikichia nayo hawana njia yakukupata zaidi ya thamana uliotumia kukupa contract kama ndo umesepa mazima ni vyema
    3.ukisha jail break usijerudi nayo ukerewe wanajua jail broken firmwares so utakuwa utatani kidogo kwani SOME countries ni illegal anyway karibu nyumbani pole kwa kushambuliwa ts wat we call inferiority complex ya wenzetu

    ReplyDelete
  33. MJOMBA SIMU YA AINA YOYOTE ILE UNAWEZA KU-UNLOCK NA UKATUMIA NETWORK YOYOTE ILE MAHALA POPOTE PALE DUNIANI. LAKINI KAMA UNARUDI TENA UKEREWE WALA HUNA HAJA YA KU-UNLOCK UNAWEZA KUTUMIA HIVYO HIVYO NA NETWORK PROVIDE WAKO HUYO HUYO ILE UTALIPA ZAIDI KIDOGO KULIKO UNACHOLIPA SASA, NINA MAANA UTAKATWA PESA ZAIDI, UNAWEZA UKAENDA KWA NETWORK PROVIDER UKAMWAMBIA MIMI NAENDA NJE YA NCHI NATAKA KUENDELEA KUTUMIA SIMU NIKIWA KULE WATAKUBADILISHIA TARIF YAKO KUTOKANA NA NCHI UNAYOENDA. KUHUSU KUINGIA NAYO MITINI NI WENGI TU WANAINGIA NAZO MITINI NA HAKUNA KITAKACHO TOKEA NDO MAANA HUWA WANA TARIFS KUBWA NA INSURANCE KU-COVER VITU KAMA HIVYO

    ReplyDelete
  34. acheni matusi, wizi, na kupenda vitu feki vya kichina. radiation . kansa itawaua. nawewe unaetaka kuiba sim ya orange acha ushamba. very little thing, its not worth it. thanx. bidada hapa.xx

    ReplyDelete
  35. WEWE UNALIPAJE, VIA PAPER BILL ASU DURECT DEBIT, KAMA DURECT DEBIT WATAENDELEA KUCHUKUWA CHAO KAMA PAPER BILL WAKIONA KIMYA HUENDI KULIPA BANK WATAKUKATIA LINE NA WATAKUSAKA KUPITIA DEBT COLLECTORS KWANI NI MKATABA, CHA MSINGI NENDA UKAONGEE NAWO UWAAMBIA UNAENDA MAHALA WATAKUWEKA TARIF INGINE AU WATAKADIRIA KWA MIEZI MIWILI INAWEZA KUWA KIASI GANI UKALI IN ADVANCE HIVYO VYOTE VINAWEZEKANA NA NIMESHAFANYA HIVYO, UKITAKA KUCHIKICHIA NAYO UNAWEZA PIA, LAKINI UNAJENGA FILE LAKO BAYA INTERNATIONALLY UNAWEZA KWENDA CANADA, USA UKANYIMWA FACILITIES KAMA HIZO KWA HISTORIA YAKO YA KUCHIKICHIA NA VITU VYA WATU. VYOTE ULIVYOELEZA VINAWEZEKANA, KUCHIKICHIA NAYO, UNLOCK, AU KNEGOTIATE NOW. UKITAKA UNLOCK UNLOCK HAPA HAPA

    ReplyDelete
  36. Naona wewe hujipendi. Tabu yote ya nini? Mimi nikienda bongo naenda kibanda cha TIGO nanunua kasimu ka Tsh. 35,000 naweka card nakatumia muda ukiisha nampa bibi yangu kule kijijini zawadi. Sasa ukiibiwa hiyo iPhone si utajilaumu tu? Au unataka kwenda kuwaonyesha watu wa kijijini kwenu kuwa ume-make kwavile una iPhone? Lol...wala hawataelewa ni nini...! Ubaya ni kuwa features nyingi hazifanyi kazi bongo...!!

    ReplyDelete
  37. Naona mmemsema mtu wa watu wakati yeye anaomba ushauri tu. Aliku hana contract before....alichoomba ni jibu. Mambo mengine na gubu zenu acheni.

    Yeye amekaa miaka minne ...miye nilikaa miaka miwili tu kurudi mara ya kwanza vitu vilikua tofauti sana....kuuliza si ujinga.....

    Wapigie provider wako uwaambie unakwenda nje ya nchi wataifungua ....no problem hapo kabisa. Halafu ukiwa huko nunua sim card local utumie itakua cheap. Ila kama ni GMS band itafanya kazi kama ni CDMA haiwezi kufanya kazi bongo.

    Ukiwaomba wasimamishe bill kwa miezi miwili huku USA makampuni mengi yana sheria tofauti. Yangu huwa nalipa $9.00 tu kwa mwezi nikiwa nje.

    Halafu kama unataka kukata contract ili uchukue hiyo simu ni dola $175 huku nilipo. Ulizia huko ni $ ngapi. Ila siku hizi wameshtukia wanaangalia una muda gani umekua nayo na ni ya bei gani. Mwanzoni watu walikua wanachukua simu ya $700 halafu wanaterminate the contract na kulipa back $175 tu hapo wanakua wametengeneza faida ya haraka haraka. Sasa hivi kama una muda mfupi wanakuambia urudishe simu yao. Na ukiingia nayo mtaani hivi hivi si utapelekwa kwenye credit report? Ujiengezee matatizo. labda kama hutaki kurudi huko uliko. REMEMBER CONTRACT MEANS TRUST. Na usipoirudisha wakiiblock haitafanya tena kazi kwenye hiyo network yako huko ulipo...Ndio unasikia simu ina Bad ESN ila nasikia kuna watu wanajua kuflash halafu inafanyakwenye network nyingine.

    Ila kuliko kukimbia nazo mbona zipo za kumwaga kwa eBay siku hizi. Sio lazima ununue simu na contract mpya. Zipo simu bei rahisi sana kwa eBay na ni new model....Kuliko kumwachia hiyo yule old girl friend mchukulie nzuri tu on eBay ambayo ipo unlocked she will grin from ear to ear.

    Ni hayo tu

    ReplyDelete
  38. hey mjomba nasi kitika kuona kwamba una ona hiyo sim kitu cha mana sana hivyo vitu vime jaa bongo una tutia aibu wabeba mabox acha wizi beba box zako ulinde mtaji wako mtindo wa kwenda na tu sim kuji o nyesha bongo ulipitwa na wakati.

    ReplyDelete
  39. duh, waTZ noma, either tunatabu ya kuelewa au tunajifanya wajuaji. huyu jamaa kauliza:
    kwanza kama simu yake ya iphone(aiphone, lol!) ambayo iko locked inaweza fanya kazi bongo, jibu ni ndio ila inabidi ui.unlock kwanza ili uweze kuweka simcard za kibongo.
    Pili, simu yake ni ya contract je wataendelea kumcharge wakati yupo nje ya nchi (kwa wasio elewa, contract ni kwa ajili ya service tu na sio kwa ajili ya simu/handset yenyewe). jibu wapigie hao service provider wako uone kama wanaweza kuacha kukucharge kwa wakati upo nje ya uk.
    Tatu, ikiibiwa itakuaje, well, kwa uk sijui, ila hapa us, service provider wengi wanatoa pia insurance ya simu, for a fee of coz, kwa hiyo simu yako ikiharibika au kupotea, unapeleka madai, na watakutumia nyingine au wata fix kama mbovu. kwa hiyo ikiibiwa ukiwa bongo, itabidi labda usubiri ukirudi uk upeleke madai yako, ila nafikiri itabidi useme imepotea hapo hapo uk au sio!?

    anyway, wabongo wakati mwingine tunakera sana, kama mtu hujaelewa kitu sio lazima uongee, kaa kimya tu. afu ujue hupatai point zozote kwa kuongea humu coz hamna anakujua wewe nani anyway!

    ReplyDelete
  40. Mbona simu yako inasema Cingular?

    ReplyDelete
  41. Waosha vinywa, mbona huyu mwenzetu ambaye ni muuliza swali hajatoa maneno yoyote ya kukashifu nchi yetu?Kwa nini mnamvamia na matusi na kujeli wakati yeye ameuliza swali mili asaidiwe juu ya namna ya kuitumia simu yake akija huko au haiwezekani.hayo madai kwamba anadharau nchi yake mumeyapata wapi?Au ndiyo ninyi wala vumbi la bongo mnaona wivu tu?

    Kutoelewa ni jambo la kawaida kwa kila mtu.Pia unaweza kuwepo TZ na bado usijue jinsi mitandao au simu zinavyofanya kazi.Msaidieni jama kama wengine walivyofanya si kumtuzi pasipo sababu zozote.

    ReplyDelete
  42. We Kweli Mshamba umekaa kwa bibi miaka 4 lkn ujui roaming ni kitu gani? Msikilize francis kakwambia nini,fanya roaming utumie cm yako fresh ili uwaringishie wamatumbi kijijini kwako huko sitimbi...

    ReplyDelete
  43. Kaka Michuzi naomba kumsaida huyu Mdau,
    Ni hivi watu wote wenye simu zao za mikataba ya mwaka au miezi huko majuu,-ulaya, marekani, aisa nk mnaposafiri kwa muda nje ya mtandao wa simu yako..kama inatumia teknolojia ya GSM(yaani kama ni sim card) unatakiwa kuwasiliana na customer care wa kampuni yako ya mawasiliano na kumwomba akupatie "unlocking code" kwa kuwa unasafiri nje ya nchi/mtandao huo. watakutumia kwa sms au email kutegemeana na njia yako ya Mawasilianao then una-itumia hiyo "unlocking code/password" then ukitua Bongo unaweka "sim card" ya mtandao wowote unatwanga mawasiliano. Ukirudi huko ughaibuni unarudisha sim card yako na mambo yanaenda kama kawaida.
    Kama wewe iko pesa ya kutosha omba "roaming service"
    NB: Utaratibu huu hauko kwa "CDMA" technology/simu zisizo na "sim card"

    ReplyDelete
  44. Mara nyingi kama ni Contract vitu vinakua vigumu, ushauri wangu ni kuwa waage jamaa na kisha ukija bongo hapa utashangaa mwenyewe nini Iphone kuna Blackberry smart phone na inatumika kama kawa.

    ReplyDelete
  45. please give me a break!wat is iphone?mbona tz hapa ni combine tayari?lkijana acha ushamba!kila kitu kikitoka nje na nyumbani pia watu wenye mapenzi na vitu hivyo wananunua tu nyumbani!hahhaha
    umenichekesha kweli so una icho kisim unajiona uko juuuuuu
    mbona mimi naziuza hapa home 50$?nazitoa kwenyewe kabisa!
    njoo nayo kijana utatumia hadi spare zake zinapatikana na usb cables!thankx mdau

    ReplyDelete
  46. hahhahah!kama ulidhani utafunika hapa bongo na iyo iphone yako umechemka!zimejaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
    kibaoooooooooooooooo!
    hahahhahahhahahahhahahahhaha
    unajua zile cm za touch?zilivyokua common?iphone likewise!

    ReplyDelete
  47. kuna watu wengine wametoa mawazo mazuri sana tu,wengine wametoa pumba tu.swala ni kuwa mheshimiwa ameomba ushauri ,na kama ni kutumia maneno kama ukerewe au la ni kufurahisha baraza,sio kuwa anakukandia bongo,ni nani asiyekupenda bongo ,labda ni huo uhayawani wa uongozi wa kijinga.wengine wanadai eti kila simu inaweza kufanya kazi,kwa kuwa unlocked...jamani msidanganye umma, jiulize hivi simu toka japan(wenye docomo, softbank etc) unaweza ku unlock simu zao zote ?? je simu za kutoka korea je ? hizo CDMA toka china tu huwezi ku unlock,kazi kudanganya umma. ukweli kila nchi na freequency zake,na bongo tumebahatika kuwa ni sehemu rahisi ya kutumia simu karibu zote.mwisho naomba ndgu zangu wadau tusahau mambo ya kutukanana au kurushiana maneno ya kebehi, tuelimishaneni ili tujue mengi,kwani wengine pia tumepata majibu hapa hapa.eti iphone hata madereva wa daladala wanazo,jamani huyo ni mchina sio mwenyewe iphone wa kweli.sio kazi ndogo jamani, huko ulaya kwenyewe watu bado wanatumia hizo kwenye contracts,na hawajalipa bado ...embu aulizwe mtu wa japan kasheshe la kuwa na iphone, unalipaje? mwisho napenda kuwasilisha! samahani kama nimemkweza mtu,au nimemchukiza mtu ,ni wazo tu.
    ni mtanzania mwenzako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...